Amenivunjia mlango na kuniibia.
sharon kalunda answered the question on October 4, 2019 at 05:16
- Onyesha mofimu katika:
kilichopewa(Solved)
Onyesha mofimu katika:
kilichopewa
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Zingatia picha ifuatayo kisha ujibu maswali.(Solved)
Zingatia picha ifuatayo kisha ujibu maswali.
(a) Tambua kipera cha fasihi simulizi kinachowakilishwa na muktadha wa picha hii.
(b) Toa sababu mbili za jawabu lako katika swali la (a).
(c) Jadili sifa zozote tano zinazotambulisha kipera hiki.
(d) Jadili udhaifu wa kipera hiki katika jamii ya kisasa.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Kamilisha jedwali (Solved)
Kamilisha jedwali
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Bainisha kiima na chagizo katika sentensi ifuatayo.
Walimu hao walifanya kazi yao kwa bidii.
(Solved)
Bainisha kiima na chagizo katika sentensi ifuatayo.
Walimu hao walifanya kazi yao kwa bidii.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Eleza matumizi ya “na” katika sentensi ifuatayo.
Wageni na wenyeji walikimbiliana.
(Solved)
Eleza matumizi ya “na” katika sentensi ifuatayo.
Wageni na wenyeji walikimbiliana.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia jedwali.
Ouma alianguka mtihani ila Kamau alifuzu vizuri.
(Solved)
Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia jedwali.
Ouma alianguka mtihani ila Kamau alifuzu vizuri.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Ainisha vielezi katika sentensi zifuatazo.
(i)Jaribu kujitahidi kisabuni usianguke mtihani.
(ii)Wachezaji wote wameingia uwanjani.(Solved)
Ainisha vielezi katika sentensi zifuatazo.
(i)Jaribu kujitahidi kisabuni usianguke mtihani.
(ii)Wachezaji wote wameingia uwanjani.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Eleza maana mbili za sentensi ifuatayo.
Wanafunzi waliandikiana barua.
(Solved)
Eleza maana mbili za sentensi ifuatayo.
Wanafunzi waliandikiana barua.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Unda nomino mbili kutokana na neno "kudhulumu".(Solved)
Unda nomino mbili kutokana na neno "kudhulumu".
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Ainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo
Juma alimchinjia mamake mbuzi mzuri kwa kisu.
(Solved)
Ainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo
Juma alimchinjia mamake mbuzi mzuri kwa kisu.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Andika katika usemi wa taarifa
“Nitawatuza watahiniwa wote watakaopita mtihani mwaka huu”. Mwalimu aliwaahidi wazazi.(Solved)
Andika katika usemi wa taarifa
“Nitawatuza watahiniwa wote watakaopita mtihani mwaka huu”. Mwalimu aliwaahidi wazazi.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Andika sentensi yakinishi kutokana na sentensi ifuatayo.
Utawala mkubwa wa meya haukuzuilika.
(Solved)
Andika sentensi yakinishi kutokana na sentensi ifuatayo.
Utawala mkubwa wa meya haukuzuilika.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Andika kwa ukubwa na udogo
Sahani zote zimepelekwa nyumbani
(Solved)
Andika kwa ukubwa na udogo
Sahani zote zimepelekwa nyumbani
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Bainisha aina za vishazi katika sentensi hii
Watoto walioachwa mayatima wamesaidiwa
(Solved)
Bainisha aina za vishazi katika sentensi hii
Watoto walioachwa mayatima wamesaidiwa
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Ainisha viambishi na mzizi katika kitenzi
Hawakunichokoza
(Solved)
Ainisha viambishi na mzizi katika kitenzi
Hawakunichokoza
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya jedwali.
Sisi tulipokuwa shuleni tulisoma kwa bidii.(Solved)
Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya jedwali.
Sisi tulipokuwa shuleni tulisoma kwa bidii.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Eleza tofauti ya kisarufi ya maneno yaliyopigiwa mstari.
i)Hiki ni kitabu cha mwalimu
ii)Hiki ni cha mwalimu(Solved)
Eleza tofauti ya kisarufi ya maneno yaliyopigiwa mstari.
i)Hiki ni kitabu cha mwalimu
ii)Hiki ni cha mwalimu
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Andika sifa mbili mbili bainifu za sauti.
i)/e/
ii)/n/(Solved)
Andika sifa mbili mbili bainifu za sauti.
i)/e/
ii)/n/
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- MUHTASARISoma kifungu kifuatacho cha habari kisha ujibu maswali yanayofuatia.Watu wengi, wanaamini kwamba kufundisha watoto nyimbo shuleni ni kupoteza wakati unaofaa kwa masomo ya maana....(Solved)
MUHTASARI
Soma kifungu kifuatacho cha habari kisha ujibu maswali yanayofuatia.
Watu wengi, wanaamini kwamba kufundisha watoto nyimbo shuleni ni kupoteza wakati unaofaa kwa masomo ya maana. Lakini muziki nyumbani na shuleni una manufaa mengi.
Muziki ni kitulizo kikubwa sana cha moyo wa binadamu. Muziki una njia ya kipekee ya kuwasiliana. Baadhi ya ujumbe hauwezi kupitishwa kwa njia nyingine ila kwa muziki.
Muziki umetajwa kumsaidia mtoto kwa mambo yafuatayo:
Kuendeza hisia nzuri, za kuburudisha na kuzuzua. Muziki humsaidia mtoto kuweza kukabiliana na tajriba mbaya nazo. Unampa fursa ya kutoa moyoni simanzi na dhiki yake na hivyo kumrejeshea raha tena. Liwazo la muziki ni dhahiri wakati mtoto anapolala pindi anapoimbiwa bembelezi.
Inaaminika pia kwamba muziki unakomaza akili ya mtoto na ni nyenzo muhimu sana katika hafla yake ya kujifanya mambo, hasa kwenye miaka yake ya mapema. Muziki huhitaji umakinifu ili kutambua miondoko na maneno halisi ya wimbo huo na mambo haya humfanya mtoto kuhamisha umakini huu kwenye masomo mengine darasani. Inaaminika pia kwamba kupitia kwa muziki mtoto anaweza kujifunza mbinu ya kukumbuka mambo anayofunzwa masomoni.
Watoto ambao hujifunza muziki mara kwa mara hujipatia mbinu za werevu shuleni haswa kwenye somo la hesabu na werevu wa mambo mengine kwa jumla. Utafiti umeonyesha kwamba watu wazima ambao walijifunza muziki kabla wafikishe umri wa miaka 12 huwa na utumizi mzuri wa maneno magumu na msamiati kuliko wale ambao hawakujifunza kuimba.
Muziki pia husaidia watoto walio na kasoro za kuzungumza au walio na ulimi mzito wa kuzungumza.
Watoto au watu wazima walio na shida ya kigugumizi huweza kujieleza kwa ufasaha kwa kupitia muziki na jambo hili huboresha kujiamini kwao kwa kibinafsi. Watoto kama hao huweza kujifunza na kuelewa mila na tamaduni zao.
MASWALI
a) Bila kupoteza maana iliyokusudiwa na mwandishi, fupisha aya ya kwanza hadi ya tatu.
(maneno 40 – 45)
MATAYARISHO
NAKALA SAFI
b) Dondoa hoja muhimu zinazojitokeza katika aya ya nne na ya tano. (Maneno 45 – 50)
MATAYARISHO
JIBU
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- UFAHAMUSoma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.Mojawapo kati ya misingi na nguzo za maendeleo uliwenguni ni viwanda. Viwanda ni muhimu kwa kuwa ndivyo vinavyoigeuza malighafi inayopatikana...(Solved)
UFAHAMU
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
Mojawapo kati ya misingi na nguzo za maendeleo uliwenguni ni viwanda. Viwanda ni muhimu kwa kuwa ndivyo vinavyoigeuza malighafi inayopatikana na kuwa bidhaa zinazoweza kutumiwa na watu. Katika nchi zinazoendelea, ambazo hazina uwezo mkubwa wa mitaji viwanda vinavyoimarika ni vile vidogo. Hivi ni viwanda ambavyo huhusisha amali za mikono. Kuimarika kwa viwanda hivi vidogo kunatokana na sababu mbalimbali.
Nchi zinazoendelea huwa na masoko finyu sana kwa kuzingatia uwezo wa ununuzi wa wanaolengwa na bidhaa za viwanda . Katika msingi huu viwanda vikubwa vitawiwa ugumu kufanya biashara katika mazingira ambako masoko yake ni finyu au utashi wa bidhaa zake sio mkubwa. Viwanda vidogo pia vinao uwezo wa kuwaajiri wafanyikazi wengi hasa kwa kuwa havina uwezo wa kugharamia mashine. Uajiri huu wa wafanyikazi wengi ni muhimu katika maeneo mengi ambako tatizo la ajira ni mojawapo wa matatizo sugu. Tofauti na mataifa ya kitasmia (yenye viwanda vingi) mataifa mengi yanayoendelea hayana mifumo imara ya kuwakimu watu wasiokuwa na kazi. Utegemezi wa jamaa wanaofanya kazi kwa hivyo unakuwa nyenzo ya pekee ya kuyamudu maisha.
Kuanzisha viwanda vidogo vidogo hakuhitaji mtaji mkubwa tofauti na viwanda vikubwa. Hali hii inasahilisha uwezekano wa watu wengi kujasurisha shughuli yoyote ile. Sambamba na suala hili ni kuwa ni rahisi kujarisha bidhaa mpya kwa kiwango kidogo cha kiwanda kidogo. Ikiwa mzalishaji yeyote atazalisha bidhaa mpya kwa mapanu, kwa mfano kama ilivyo kwa viwanda vikubwa, pana uwezekano wa kupata hasara kubwa. Huenda utashi wa bidhaa hiyo uwe mdogo ukilinganishwa na ugavi wa bidhaa yenyewe. Majaribio mazuri huwa ni kwa kiwango kidogo.
Kuwepo kwa viwanda vidogo huwa chocheo kubwa la usambazaji wa viwanda hadi maeneo ya mashambani. Hali hii inahakikisha kuwa nafasi za ajira zimezambazwa nchini hali ambayo inasaidia kuhakikisha kuwa pana mweneo mzuri wa kimapato nchini. Mweneo huo wa mapato unachangia katika kuboresha uwezo wa kiununuzi wa umma. Huu ni msingi muhimu wa maendeleo. Upanuzi na ueneaji wa viwanda vidogo vidogo ni msingi mkubwa wa kujitegemea kiuchumi. Aghalabu viwanda vikubwa huegemea kwenye mitaji ya mashirika ya kimataifa na huwa msingi wa kuendelezwa kwa utegemezi wa kiuchumi.
Maswali
a)Kwa nini viwanda ni muhimu?
b)Ni nini kiini cha matatizo ya uuzaji wa bidhaa katika nchi zinazoendelea?
c)Eleza faida zinazotokana na kuwepo kwa viwanda vidogo vidogo.
d)Usambazaji wa viwanda katika maeneo ya mashambani una faida gani?
e)Fafanua maana ya msamiati huu kama ulivyotumika katika kifungu.
i)Kujasurisha
ii)Amali
iii)Utashi
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)