Ilikuwa Jumamosi. Nilifika nyumbani kwangu saa moja jioni. Tangu nistaafu miakamiwili awali sikupenda kuchelewa Taarifa ya Habari. Mwezi mmoja...

      

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.

Ilikuwa Jumamosi. Nilifika nyumbani kwangu saa moja jioni. Tangu nistaafu miaka
miwili awali sikupenda kuchelewa Taarifa ya Habari. Mwezi mmoja ukawa umepita tangu nipewe pesa za kiinua mgongo. Mwezi mmoja mzima nilikuwa katika shughuli za kulipa deni hapa na kulipa karo huku. Kuwekeza kwenye mradi ule na kununua hili. Sasa shilingi laki mbili tu zilikuwa zimesalia katika benki. Watu wengi walinishawishi nijaribu kilimo cha mahindi. Bei ilikuwa imeanza kuimarika. Katika taarifa ya habari jioni hiyo, Waziri wa Kilimo alitangaza bei mpya. Shilingi 1,500 kwa kila gunia. Nami nilikuwa naanza kuumakinikia mradi huu. Baaada ya taarifa, nilikoga, nikala na nikaenda kulala. Kwa sababu ya uchovu, usingizi ulinichukua mara moja.. Usingizini niliota. Katika ndoto niliutekeleza mradi wangu. Msimu huo wa kilimo nilitenga ekari kumu za shamba langu. Wataalamu walinishauri kuwa wakati mzuri wa kulima ni wa kiangazi. Mwezi wa Januari ulipoanza tu nilitafuta trekta na kulima. Malipo yalikuwa shilingi 1,200 kila ekari. Katikakati ya mwezi wa Machi, nilitafuta trekta la kutifua shamba tena kwa gharama ya shilingi 15,000 ekari zote kumi. Kufuatia ushauri wa manyakanga wa kilimo, nilipa shilingi elfu kumi na tatu kupiga shamba lote haro. Mwishoni mwa mwezi huo, nilienda mjini kutafuta pembejeo. Kwanza, nililipa shilingi 20,500 kwa magunia 15 ya mbolea. Kisha nilinunua magunia manne ya mbegu ya mahindi yenye uzani wa kilo 25 kwa shilingi 3,300 kila gunia. Mwezi wa Aprili ulipotimia tu, niliamua kupanda. Ili nipate mazao bora, nilipanda kwa tandazi. Gharama ilikuwa shilingi 1,000 kila ekari. Mvua ilinyesha vizuri na baada ya siku saba mahindi yalianza kuota. Ilifurahisha kuhesabu mistari ya kijani iliyonyooka. Hali hii iliwezekana tu baada ya kuajiri vijana wa kuwafukuza korongo na vidiri ili wasifukue mbegu mchangani. Baada ya mwezi mmoja, hatua ya kupalilia ilifika. Nilitafuta vibarua wa kupalilia. Malipo yalikuwa shilingi 700 kila ekari. Kumbe kupalilia kulichochea mtifuko wa mahindi. Punde yakawa yananifikia magotini. Hii ikawa ishara kuwa yanahitaji kumwagiwa mbolea ya kunawirisha iitwayo ‘amonia.’ Gharama yake ikawa shilingi1,300 kila gunia. Hivyo, nikalipa shilingi 19,500 kwa magunia kumi na matano.. Mahindi yalibadilika kimiujiza. Ghafla tu yalirefuka na kunenepa mashina. Yalibadilika rangi yakapiga weusi. Shamba liligeuka likawa kama msitu wa rangi ya kijani iliyokolea. Wapita njia waliajabia mimea na juhudi zangu. Shamba langu sasa likawa kielelezo. Maafisa wa kilimo wakawa kila siwanawaleta wakulima wengine kujifunza siri ya ufanis wangu. Hapo nikaanza kuhesabu mavuno nitakayopata kukadiria faida. Nilipuuza kabisa ushauri wa wahenga kuwa ‘Usikate majani, mnyama hajauawa.’
Bila taarifa wala tahadhari mvua ikatoweka. Hayakupita majuma mawili mahindi yakaanza kubadilika. Juma moja baadaye mahindi yalinyauka. Badala ya mahindi, shamba likageuka la vitunguu vilivyochomwa na jua. Makasio yangu ya faida yaliyeyuka jinsi ufanyavyo moshi. Lakini ‘Muumba ndiye Muumbua.’ Siku moja mawingu yalitanda na mvua ikanyesha. Muda is muda mahindi yalianza kunawiri. Kumbe tukio lililonivunja moyo lilikuwa laja. Siku moja mvua kubwa ilinyesha. Asubuhi nilipotoka nje nilipigwa na butwaa. Barafu ilitapakaa pote. Shamba lilikuwa limetapakaa barafhuku majani ya mahindi yamechanika kama nyuzi. Niliugua. Baada ya wiki moja, nilipata nafuu. Nilipotazama upande wa shamba nikaona dalili za majani mapya ya mahindi yakianza kuchomoza. Maumbile ni kitu cha ajabu kweli. Muda si mrefu mahindi yalirudi hali yake tena, kisha yakakomaa. Harakati za kutafuta watu wa kuyakata na kuyakusanya zilianza. Gharama ya shughuli hii ikawa shilingi 5,000. Kuvuna, kusafirisha kutoka shamba na kukoboa kwa mashine magunia 200 yakachukua shilingi 20,500. Kufikia hapo nilikuwa nimetumia takribani shilingi 192,700. Gharama nyingine zilikuwa za usafiri, gharama ya dharura na usimamizi, usumbufu wangu binafsi, gharama ya magunia na kadhalika. Mahindi yalipokuwa tayari kwenye magunia nilifunga safari kwenda mjini kutafuta soko. Niliposhuka tu niliona gazeti. Habari motomoto siku hiyo ilikuwa: ‘MAHINDI GUNIA 900/=.’ Niligutuka usingizini.


Maswali:
a) Andika kichwa mwafaka kwa kifungu hiki cha habari.
b) Msimulizi alikuwa na kiasi gani cha pesa katika benki baada ya mradi kukamilika?
c) Taja matatizo matatu yaliyotisha mradi wa msimulizi wa kukuza mahindi.
d) Eleza maana ya methali zifuatazo:
(i) Usikate majani, mnyama hajauawa.
e) Eleza mambo mawili yaliyosababisha msimulizi asipate faida alivyotarajia.
f) Kwa nini msimulizi alisema maumbile ni kitu cha ajabu?
g) Eleza maana ya:
(i) kiinua mgongo.
(ii) manyakanga wa kilimo.

  

Answers


Maurice
a) Mashaka ya kilimo cha mahindi.

b) Shilingi elfu saba na mia tatu.

c) i) Tisho la korogo na vidiri kufukua mbegu.
ii) Kiangazi.
iii) Mvua ya barafu.
iv) Gharama kubwa.

d) i) Haikua vizuri kufurahia faida kabla kuuza mahindi.
ii) Mungu anao uwezo wa kuleta barafu na kuangalia kustawisha mimea.

e) i) Kiwango cha chini cha mvua.
ii) Kushuka kwa bei

f) Mahindi aliyodhani yameangamizwa na kiangazi au barafu yalinawiri tena.

g) i) Malipo ya kustaafu.
ii) Wataalamu wa kilimo.
maurice.mutuku answered the question on October 4, 2019 at 05:33


Next: Andika sentensi hii katika usemi wa taarifa" Nitampokea mjomba iwapo nitampata," Rehema alimwambia shangazi yake.
Previous: Sahihisha sentensi ifuatayo: Mwalimu mwenye ako nabidii amepeana mazoezi katika darasa yetu.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions