Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Ufisadi ni uhalifu unaohusu kuzitumia njia za ulaghai kujipatia pesa, mali au vitu hasa vya umma. Nchini Kenya ufisadi hujitokeza...

      

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.

Ufisadi ni uhalifu unaohusu kuzitumia njia za ulaghai kujipatia pesa, mali au vitu hasa vya umma.
Nchini Kenya ufisadi hujitokeza kwa njia mbalimbali na kila mojawapo ina athari zake. Kwa mfano kuna maafisa wa serikali wajipatiao pesa kwa kuuza stakabadhi za serikali kama vile pasi, vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya kumiliki mashamba, vitambulisho n.k. kwa raia, kuna hatari kubwa kwa sababu watu wasio raia wa Kenya wameweza kusajiliwa kama wakenya na kuendeleza uhalifu kama ugaidi, wizi na ulanguzi wa dawa za kulevya.
Wengine hujipatia vibali vya kufanya kazi na kuajiriwa kazi ambazo zingefanywa na wakenya. Hii imechangia ongezeko la uhaba wa kazi nchini.
Watumizi wengine wa umma huuza mali ya serikali kama vile magari nyumba na ardhi na kufutika pesa za mauzo mifukoni mwao. Wengine wao hujinyakulia na kufanya vitu hivyo kuwa mali yao. Ufisadi wa aina hii umegharibu serikali kiasi kikubwa cha fedha. Serikali imelazimika kununulia maafisa wake magari baada ya muda mfupi, kulipia wafanyi kazi wake kodi za nyumba na kukosa viwanja vya upanuzi na ujenzi wa shule hospitali, vituo vya polisi na taasisi zingine maalumu.
Baadhi ya wataalamu kama madaktari huiba dawa kutoka hospitali za umma kupeleka vituo vyao vyaafya. Pia hutumia wakati wao mwingi katika kazi zao za kibinafsi na kuwaacha wagonjwa katika hospitali za umaa wakihangaika. Sio madaktari tu, kuna masoroveya, whandisi, mawakili, walimu na mahesibu ambao hukwepa majukumu yao serikalini na kufanya kazi za kibinafsi.. Wengine wasio wataalam huendesha biashara za aina tofauti, na huku wanaendelea kupokea mishahara.
Wanafunzi wanaotaka kujiunga na vyuo na shule bora za umma na hawakuhitimu wakati mwinginehulazimika kusalimu amri na kutoa hongo hili wapate nafasi za kusoma. Kiasi cha pesa kinachohitajika huwa kikubwa hivi kwamba ni wachache humudu hizo rushwa. Wale wasiojimudu kifedha hubaki wakilia ngoa. Kuna wazazi ambao hutumia vyeo vyao na ‘undugu’ kupata nafasi zilizotajwa, jambo ambalo huwanyima wanafunzi werevu kutoka jamii maskini nafasi ya kupata elimu. Matokeo huwa ni kuelimisha watu wasiostahili na ambao mwishowe hawaziwezi kazi wanazosomea wakihitimu na kuanza hudumia jamii.
Ufisadi umekita mizizi na kushamiri katika sekta za umma za kibinafsi kwa upande wa kuajiri wafanyikazi. Ni vigumu kupata kazi ikiwa hujui mtu mkubwa katika shirika linalohusika au uzunguke mbuyu. Matokeo ni kuajiri wafanyikazi wasiohitimu na wasiohitimu na wasiowajibika kazini.
Vyeo na madaraka katika baadhi ya mashirika hutolewa kwa njia ya mapendeleo na ufisadi. Kwa hivyo, wafanyikazi wenye biddi hufa moyo kwa sababu hawasaidiwi ipasavyo. Badala yake wale wasioleta bidii hupandishwa vyeo na kuwaacha palepale.

Hata hivyo, mbio za sakafuni huishaia ukingoni. Serikali imetangaza vita dhidi ya ufisadi. Tayari tume kadhaa zimeteuliwa kuchunguza visa vya ufisadi uliotekelezwa hapo mbeleni. Mojawapo ya tume hizo ni Tume ya Kuchunguzavisa vya ufisadi uliotekelezwa hapo mbeleni. Mojawapo ya tume hizo ni Tume ya kuchunguza Kashfa ya “Goldenberg” ambapo pesa za umma (mabilioni ya shilingi) ziliporwa na mashirika na watu binafsi kwa njia siziso halali. Watakaopatikana na hatia ya kushiriki ufisadi huo watahitajika kurudisha pesa hizo.
Serikali pia imeunda kamati ya kupikea malalamiko kutoka kwa wananchi waliohasiriwa na mawakili walaghai ambao hupokea ridhaa kwa niaba ya wateja wao na kukosa wakalipa, au wakilipwa kuwatetea mahakamani wanakwepa jukumu hilo ilhali wamekwishalipwa. Ni matumaini yetu kuwa ulaghai huu utaangamizwa kabisa kwani hakuna refu lisilokuwa na ncha.


1. Eleza aina nne za ufisadi zilizotajwa katika kifungu ulichosoma
2. Kulingana na kifungu ulichosoma, ufisadi umeathiri nchi yetu kwa njia gani?
3. Serikali inafanya jitihada gani ili kukomesha ufisadi?
4. Kwa maoni yako, unafikiri ufisadi husababishwa na nini?
5. Toa msamiati mwingine wenye maana sawa na rushwa
6. Eleza mana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa kifunguni;
(a) Majukumu
(b) Kashfa
(c) Shamiri
(d) wakilia ngoa
(e) Waliohasiriwa
(f) Kita mizizi

  

Answers


Maurice
1. Wizi wa wa mali ya umma
- Vyeo na madaraka kutolewa hivi hivi tu
- Uuzaji wa stakabadhi za serikali
- Kuiba madawa
- Kuhonga ili kupata nafasi za kusoma
- Kuhonga au kutumia undugu ili kupata kazi
- Kutowajibika kikazi
- Kuiba madawa


2. - Kufilisisha serikali
- Kunyima wagonjwa matibabu
- Kuzorotesha maendeleo na huduma muhimu
- Kuelimika watu wasiohitimu na kuacha walio werevu
- Kupandisha vyeo watu wasiostahili
- Kazi kufanywa vibaya bila uajibikaji


3. - Kuunda tume na kamati za kuchunguza visa vya ufisadi
- Kurudisha mali iliyoibiwa
- Kuwashtaki wahalifu


4. - Uhaba wa kazi
- Uozo wa maadhili katika jamii
- Kuongezeka kwa umaskini
- Tamaa ya anasa na starehe
- Uongozi mbaya wa kitaifa
- Kukosa huruma na uajibikaji
- Kukosa uzalendo


5. Hongo/ kuzunguka mbuyu/ chai/kadhongo


6.(a) Kazi walizopewa
(b) Ufunuo wa siri ya jambo la aibu
(c) Kuenea kwa jambo au habari
(d) Ona wivu
(e) Waliodhuriwa/ walioumizwa
(f) Umeshikilia
maurice.mutuku answered the question on October 4, 2019 at 06:40


Next: HADITHI FUPI DAMU NYEUSI NA HADITHI ZINGINEZO (KEN WALIBORA NA SAID A. MOHAMED) Mwana wa Darubini (Kristina Mwende Mbai) “Ulijuaje alikuwa anaangalia kwetu? a.Eleza muktadha wa dondoo hili. b.Hadithi...
Previous: Define the term disposal of fullness

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • HADITHI FUPI DAMU NYEUSI NA HADITHI ZINGINEZO (KEN WALIBORA NA SAID A. MOHAMED) Mwana wa Darubini (Kristina Mwende Mbai) “Ulijuaje alikuwa anaangalia kwetu? a.Eleza muktadha wa dondoo hili. b.Hadithi...(Solved)

    HADITHI FUPI
    DAMU NYEUSI NA HADITHI ZINGINEZO
    (KEN WALIBORA NA SAID A. MOHAMED)

    Mwana wa Darubini (Kristina Mwende Mbai)
    “Ulijuaje alikuwa anaangalia kwetu?
    a.Eleza muktadha wa dondoo hili.
    b.Hadithi hii inaonyesha matatizo ya kijamii. Fafanua.
    c.Eleza yaliyotokea baada ya mazungumzo haya.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Kimya changu kimezidi, navunja yangu subira,(Solved)

    Soma shairi ifuatayo kisha ujibu maswali yatakayofuata.
    Kimya changu kimezidi, navunja yangu subira,
    Marejeya ya miradi, kuhitimisha dhamira,
    Kukejeli sina budi, niwafunze utu bora,
    Nani aali zaidi, Wakenya au vinara?

    Serikali bila hadi, ndo kiini cha madhara,
    Yanopiga kama radi, isokuwa na ishara,
    Yamini kuwa gaidi, wakitupora mishahara,
    Nani aali zaidi, Wakenya au vinara?

    Wamejifanya hasidi, wasopatana kifikira,
    Wana yao maksuudi, kijisombea ujira,
    Wakilenga kufaidi, tumbo zao za kichura,
    Nani aali zaidi, Wakenya au vinara?

    Nchi yetu kufisidi, ni jambo linonikera,
    Tangia siku za jadi, ufukara ndo king‘ora,
    Kutujazeni ahadi, nyie mkitia for a,
    Nani aali zaidi, Wakenya au vinara?

    Maskini watozwa kodi, wapwani na walo bara,
    Kwa uvumba na uudi, mwawalipa kwa hasara,
    Hamudhamini miradi, mejihisi masongora,
    Nani aali zaidi, Wakenya au vinara?

    Mesema kazi ni chudi, basi sirikali gura,
    Nafsi zenu mzirudi, mkubali kuchakura,
    Makondeni mkirudi, muondoe ufukara,
    Nani aali zaidi, Wakenya au vinara?

    Ujanjenu umezidi, demokrasia bakora,
    Debeni takaporudi, michirizi kwenye sura,
    Kuwachuja a! muradi, kwa za mkizi hasira
    Nani aali zaidi, Wakenya au vinara?

    Maswali
    a) Toa anwani mwafaka kwa shairi hili.
    b) Ainisha shairi hili kwa jinsi tatu huku ukitoa sababu.
    c) Onyesha Mbinu mbili za lugha katika shairi hili.
    d) Bainisha matumizi matatu ya uhuru wa mshairi katika shairi hii.
    e) Andika ubeti wa nne katika mtindo tutumbi.
    f) Fafanua maudhui matatu yanayojitokeza katika shairi hili.
    g) Taja mpango mmoja unaotajwa kama njia ya kutatua matatizo ya nchi.
    h) Eleza muhudo wa shairi hili.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • USHAIRI Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali: Hakika siku ya leo, ni siku ya majivuno Basi pasiwe na choyo, na usonono Tulekezane yaliyo, unawiri Muungano. Tuzisafisheni nyoyo, pasiwe na...(Solved)

    USHAIRI

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali:

    Hakika siku ya leo, ni siku ya majivuno
    Basi pasiwe na choyo, na usonono
    Tulekezane yaliyo, unawiri Muungano.

    Tuzisafisheni nyoyo, pasiwe na miguguno
    Yaongoke tutakayo, kusiwe na mabishano
    Mbegu hii tupandayo, ilete mema mavuno.

    Tufungulie upeo, Mola usiye mfano
    Pa kitasa na komeo, tupite bila kinzano
    Tupitishe njia hiyo, pasina masongamano

    Twakuomba uumbao, mkono vyanda vitano
    Tushikane hii leo, tuwe moja tangamano
    Tupendane kwa pumbao, hali na maridhiano

    Aliye ana machukiyo, adui wa Muungano
    Naazibe masikiyo, asisikie maneno
    Kisha awe kibogoyo, asiwe na moja jino.

    Ya Ilahi ujalie, juu wetu Muungano
    Nuru yake izagae, na nguvu za mapigano
    Hasidi mpe hakie, mateso yaso mfano

    Watamati komeleo, kuimba kwangu hukuno
    Nataka maendeleo, yasiyo na malumbano
    Daima tuwe ni ngao, palipo msagurano

    (i) Lipe shairi hili anwani yake.
    (ii) Liweke shairi hili katika bahari mbili ukitumia:
    Idadi ya
    (i)Mishororo
    (ii)Vina
    (iii) Onyesha muundo wa shairi hili.
    (iv) Andika ubeti wa pili kwa lugha ya nathari.
    (v) Toa mifano ya idhini ya kishairi iliyotumika katika shairi hili.
    (vi) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi.
    (i)Usonono –
    (ii)Msagurano –

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi moja kubainisha tofauti kati ya: i) Samani ii) Zamani(Solved)

    Tunga sentensi moja kubainisha tofauti kati ya:
    i) Samani
    ii) Zamani

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • RIWAYA Kidagaa kimemwozea Ken Walibora Angewezaje kumwambia kwamba mifugo wake walikuwa katika ukalifu tangu Amani kutiwa mbaroni?” a)Eleza muktadha wa dondoo hili? b)Mzungumziwa hakuwa na utu. Fafanua. c)Toa mifano...(Solved)

    RIWAYA
    Kidagaa kimemwozea
    Ken Walibora

    Angewezaje kumwambia kwamba mifugo wake walikuwa katika ukalifu tangu Amani kutiwa mbaroni?”
    a)Eleza muktadha wa dondoo hili?
    b)Mzungumziwa hakuwa na utu. Fafanua.
    c)Toa mifano ya maudhui ya ukatili katika Riwaya ya kidagaa kimemwezea inayofaa.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Habari kuwa watoto chini ya miaka mitatu ‘huwindwa’ kitandani na kuraushwa na wazazi wao waende shuleni mwendo wa saa kumi na moja asubuhi...(Solved)

    Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.

    Habari kuwa watoto chini ya miaka mitatu ‘huwindwa’ kitandani na kuraushwa na wazazi wao waende shuleni mwendo wa saa kumi na moja asubuhi ni za kusikitisha.
    Kwa mujibu wa ripoti za wataalamu wa elimu ya watoto wachanga (ECD), watoto hao hutakikana kuwa darasani kabla ya saa kumi na mbili asubuhi.
    Wanapowasili wao huanza kufukuza ratiba ya masomo ambayo huwapatia muda mfupi mno wa kula, kucheza, kupumzika na hata kuchunguza afya na usalama wao.
    Badala ya kuondoka mapema kuelekea nyumbani, wengi wao hufika saa za usiku pamoja na wazazi wao wakitoka kazini. Wanapowasili nyumbani wanapaswa kuoga na kupata chakula cha jioni kwa pupa ili wafanye mazoezi waliyopewa na walimu wao.
    Mazoezi hayo huwa ya masomo yote matano huku kila somo likiwa na zaidi ya maswali thelathini. Badala ya kupumzika mwishoni mwa juma, watoto hao huhitjika kuhudhuria shule siku nzima ya Jumamosi. Jumapili wanatakiwa Kanisani na hali hii hujirudia mpaka muhula umalizike. Ikiwa ulidhani watapewa nafasi ya kupumzika wakati wa likizo , umekosea kwa sababu watoto hao huhitajika kuhudhuria shule. Hili limekuwa likiendelea hata baada ya Wizara ya Elimu kupiga marufuku kusomesha wakati wa likizo.
    Wazazi-hasa wale wanaofanya kazi mijini- wamekuwa wakiunga mkono mtindo huu kwa sababu unawaondolea mzigo wa malezi na gharama ya kuwaajiri walezi.
    Wataalamu wanasema matokeo ya hali hii ni watoto wakembe wenye afya na maadili mabaya kutokana na kuchanganyishwa akili na walimu wanaowataka wajue kila kitu wakiwa na umri mdogo.
    Kuwashinikiza watoto wakembe wahudhurie shule na zaidi ya hayo wajue kila kitu kuna madhara mengi. Kwanza kabisa, kuraushwa kwa watoto macheo waende shule kunawanyima fursa ya kulala na kupumzika. Utafiti unaonyesha kuwa watoto wanahitaji kulala na kupumzika kwa zaidi ya saa 12 kwa siku. Hii ina maana kuwa mbali na muda mfupi wanaolala na kupumzika mchana kutwa, watoto wanapaswa kutumia usiku mzima kwa usingizi.
    Hii huwasaidia kukua wakiwa na afya nzuri hasa kiakili. Matokeo ya kuwarausha watoto hao waende shule saa hizo huwafanya wakose furaha mbali na kuwafanya wachanganyikiwe kiakili.
    Pili, kuwalazimisha watoto wakae darasani kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni huwa kunawanyima fursa ya kucheza na kutangamana. Wataalamu wa afya ya watoto wanapendekeza kuwa watoto wachanga wanapaswa kucheza ili viungo vya miili yao kama moyo, akili, mapafu na kadhalika vifanye kazi vizuri.
    Kinyume na watu wazima ambao hufanya kazi nzito nzito na kuwawezesha kufanya mazoezi, watoto huwa hawafanyi kazi hizo. Wazazi na walimu wanapaswa kufahamu kuwa kazi ya watoto ni mchezo na wana kila haki ya kupewa furaha ya kucheza wakiwa shuleni na hata nyumbani.
    Tatu, wazazi wengi ambao hufurahia kuwaachia walimu jukumu la kuwalea watoto wao huku wao wakiwa kazini huwa wanasahau kuwa sio kila mwalimu ana maadili yanayopaswa kuigwa na mwanawe. Ingawa tunawatarajia walimu wawe mifano bora ambayo inaweza kuigwa na kila mtu, ukweli ni kwamba baadhi ya walimu hawajui maana wala hawana maadili. Hatari ni kwamba watoto wakembe husoma kwa kuiga wakubwa wao na ikiwa walimu wanaoshinda nao shule wamepotoka kimaadili, kuna uwezekano mkubwa wa watoto hao kupotoka pia. Hii ndiyo sababu wazazi wengi wamekuwa wakilalamika kuwa wanawao tabia mbaya ambazo hawaelewi zilipotoka.
    Kila mzazi anayejali maisha ya mwanawe anapaswa kutekeleza jukumu lake la kumlea na kumwelekeza jinsi anavyotaka akue. Ni kinaya kuwa wanawatarajia wanawao wawe na tabia na maadili kama yao ilhali hawachukui muda wa kukaa nao na kuwaelekeza.
    Nne, kuwawinda, kuwaamsha, kuwaosha na kuwalazimisha watoto waende shule kila siku hata ingawa hawataki huwa kunawafanya wawe wategemezi wasioweza kujipangia na kutekeleza mambo kivyao.

    (a) Ipe taarifa anwani mwafaka
    (b) Mwandishi anatoa maoni gani kuhusu ratiba ya masomo?
    (c) Eleza athari za mfumo wa elimu unaoangaziwa hapa
    (d) Ni ushauri upi unaotolewa kwa wazazi ?
    (e)Taja mbinu zozote mbili za lugha alizotumia mwandishi
    (f) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika taarifa.
    (i) ‘huwindwa’ kitandani
    (ii) Maadili
    (iii) Kuwashinikiza…
    (iv) Wakembe…

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Weka dagaa kwa ngeli yake.(Solved)

    Weka dagaa kwa ngeli yake.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Tamthilia; Mstahiki Meya Timothy M. Arege Au unafikiri pakawa na fursa nyingine hii leo ya kuchagua viongozi matokeo yatakuwa tofauti sana?...................Ukipanda huwezi kuvuna kunazi. a)Eleza muktadha wa...(Solved)

    Tamthilia; Mstahiki Meya
    Timothy M. Arege

    Au unafikiri pakawa na fursa nyingine hii leo ya kuchagua viongozi matokeo yatakuwa tofauti sana?...................Ukipanda huwezi kuvuna kunazi.
    a)Eleza muktadha wa maneno haya?
    b)Mzungumzaji na mzungumziwa wanafanana. Thibitisha.
    c)Taja mbinu za kifasihi zinazojitokeza katika muktadha huu.
    d)Eleza maovu yoyote manne yanayokumba wanacheneo.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Unda nomino kutokana na kitenzi nena.(Solved)

    Unda nomino kutokana na kitenzi nena.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi ukitumia kauli iliyobanwa ya kitenzi ulichopewa. i) soma (kutendeshwa) ii) –ja (kutendewa)(Solved)

    Tunga sentensi ukitumia kauli iliyobanwa ya kitenzi ulichopewa.
    i) soma (kutendeshwa)
    ii) –ja (kutendewa)

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Eleza matumizi ya "ki" katika sentensi hii. Ukikata kipira kitapotea.(Solved)

    Eleza matumizi ya "ki" katika sentensi hii.
    Ukikata kipira kitapotea.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Andika udogo wa: Ndege huyu ana miguu midogo(Solved)

    Andika udogo wa:
    Ndege huyu ana miguu midogo

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha aina za virai vilivyopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo:(Solved)

    Bainisha aina za virai vilivyopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo:
    Uchochole wa kinjinsia umepigwa marufuku na kiongozi mwenye msimamo thabiti mno.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yafuatayo ................napinga hoja iliyotolewa na waziri wa Finance ya kupiga marufuku matumizi ya plastic bags. Baada ya kumsikiza...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yafuatayo
    ................napinga hoja iliyotolewa na waziri wa Finance ya kupiga marufuku matumizi ya plastic bags. Baada ya kumsikiza kwa makini, napenda kumkosoa kwa kudhihirisha kuwa.................. kulingana na kifungu nambari ...................
    i)Bainisha sajili ya mazungumzo hayo.
    ii)Huku ukitoa mifano mwafaka, eleza sifa nne za sajili hii kwa mujibu wa kifungu hiki.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Geuza katika wingi ukizingatia nafasi ya pili. Nitasafiri kuelekea kwake kesho kutwa(Solved)

    Geuza katika wingi ukizingatia nafasi ya pili.
    Nitasafiri kuelekea kwake kesho kutwa

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Kwa kutumika njia ya jedwali, changanua sentensi ifuatayo: Gofu hushabikiwa na watu wengi sana.(Solved)

    Kwa kutumika njia ya jedwali, changanua sentensi ifuatayo:
    Gofu hushabikiwa na watu wengi sana.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Mtoto anapozaliwa huwa ni malaika wa Mungu. Hutaraji kuongozwa kwa kila njia ili awe mwana mwelekea. Jukumu la kulea mtoto huanzia nyumbani. Wako baadhi ya...(Solved)

    Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.

    Mtoto anapozaliwa huwa ni malaika wa Mungu. Hutaraji kuongozwa kwa kila njia ili awe mwana mwelekea. Jukumu la kulea mtoto huanzia nyumbani. Wako baadhi ya watu ambao wanaamini kuwa jukumu hili muhimu hutekeleezwa bora na mama; wengine husema kuwa ni jukumu la baba. Ni kweli kwamba mtoto huwa na mama yake kwa muda mrefu zaidi ya baba lakini kivuli cha baba hakikosi kumwandama na kumwathiri maisha yake.
    Uongozi wa mama huanzia siku ya mwanawe kuingia ulimwenguni. Kwa hivyo, mama zaidi ya baba huwa ndiye chanzo cha chemichemi ya maisha ya mwanawe. Mtoto kwa kawaida ana tabia ya kuiga kila jambo analoliona na kusikia na mambo ya awali ajifunzayo hutokana na mamaye.

    Je; mtoto huiga kutokana na mama pekee? Kila utamaduni hasa huku kwetu Afrika, una taratibu zake zilizopangwa kuhusu malezi ya watoto. Kwa mfano; akina baba wengine wanaoishi maisha ya kijadi huonelea kwamba ni jukumu lao kuwalea watoto wa kiume. Kwa hivyo mvulana anayekulia katika mazingira haya akishachuchuka kiasi cha kujua lipi zuri lipi baya huanzia kuwa mtoto wa baba zaidi ya kuwa wa mama. Baba humuathiri mtoto wake kwa kumshauri kuhusu maneno ya kiada ya wanaume. Hupenda kukaa naye katika uga wake kwa kumshauri kuhusu maneno ya kiada ya wanaume huku akimkataza kukaa jikoni na kumsisitizia kuwa wanawake ni tofauti naye. Aidha, humfunza sifa kama vile ushujaa na uvumilivu kwa namna ambayo huona kuwa ni ya kiume. Pindi mtoto anapoonyesha tabia za kikekike, baba hujiandaa kuzitadaruki kwa kumkaripia. Baba hutaka kujiona mwenyewe katika hulka ya mwanawe.

    Baba kama huyu humpa nafasi ndogo sana mkewe ya kumwongoza mtoto wake wa kiume kwa jambo lolote hata kama wakati mwingine ni la heri. Kwa upande mwngine baba huyu huwa na machache ya kuzungumza na bintiye kwa kuwa huona kuwa si stahili yake kufanya hivyo. Mtoto wa kike huachiwa mamake. Lakini kutokeapo jambo la kulipima mama huona linampita kimo, humwita baba kuingilia kati na aghalabu baba naye humwagiza dadake aje atoe suluhisho mwafaka.

    Ulezi kama huu una nafasi yake katika jamii, lakini ni lazima tukiri kuwa pia unaendeleza maisha ya fawaishi na kuanzisha taasubi ambayo hatima yake ni mwanamke kukandamizwa na mwanaume. Wazazi walio na mwelekeo huu katika malezi yao hufikiri kuwa wataishi na watoto wao katika mazingira finyu na kwa hivyo waendelee kuwapulizia pumzi za kuhilikisha. Lakini ni sharti wakumbuke kuwa wao sio walezi peke yao na wala mtoto hawezi kuishi peke yake na kuwa na tabia ya kipekee. Leo ataishi kwao lakini kesho itambidi atoke aone ulimwengu. Kila atakapotia mguu ataona mambo mapya yatakayompa tajriba mpya na mawazo mapya ambayo aghalabu yataendelea kuiathiri hulka yake. Iwapo tabia alizozipata kwa wazazi wake hapo awali zilikuwa na misingi isiyokuwa madhubuti na mielekeo finyu, zinaweza kuwa pingamizi katika maingiliano yake na watu wengine. Mambo haya yanatuelekeza katika kufikiri kwamba maisha ya siku hizi hayaruhusu ugawaji wa kazi ya malezi ya namna ya baba na mama wa kijadi. Baba na mama ni walezi wa kwanza ambao kwa pamoja wanapaswa kuwaelekeza watoto wao katika maisha ya ulimwengu uliojaa bughudha na ghururi. Ni lazima wazazi watambue tangu awali kuwa katika malezi hakuna cha ubaguzi. Hakuna, mambo ajifunzayo mtoto wa kiume ambayo hayamhusu mtoto wa kike. Uvumilivu, bidii, utiifu na kadhalika ni sifa zinazomwajibikia kila mtoto kama vile upishi, ukulima na usafi. Mwanamke tangu azali ameumbwa kuwa mama na haipasi kulazimishwa kuchagua baina ya mtoto wa kike na kiume. Mapenzi na wajibu wa wazazi yapaswa yasiwe na mipaka bali yawe maridhawa kwa watoto wote.

    Maswali
    (a) Toa kichwa mwafaka cha makala haya
    (b) Kulingana na kifungu hiki, taja mambo mawili ambayo yanaweza kuwa hatari kwa
    malezi ya watoto
    (c) Kwa nini baba humpa nafasi ndogo sana mkewe ya kumwongoza mtoto wa kiume katika
    jambo lolote hata kama wakati mwingine ni la heri
    (d) Eleza mambo mawili ambayo ni ya manufaa katika ulezi jadi
    (e) Kulingana na makala haya, ushahidi gani unaonyesha kwamba kuna kutegemeana
    katika ulezi jadi?
    (f) Taja sifa mbili ambazo baba humfundisha mwana wa kiume
    (g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika kaktika kifungu hiki:
    (i) Chanzo cha chemichemi...
    (ii) Akishachuchuka...
    (iii) Hulka.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Fafanua aina ya hali iliyotumika katika sentensi hii. Wanasiasa wengi hulalamika kila mara. (Solved)

    Fafanua aina ya hali iliyotumika katika sentensi hii.
    Wanasiasa wengi hulalamika kila mara.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha shamirisho katika sentensi ifutayo: Maimuna alimtumia babake barua ndefu.(Solved)

    Bainisha shamirisho katika sentensi ifutayo:
    Maimuna alimtumia babake barua ndefu.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Sahihisha sentensi ifuatayo: Mwalimu mwenye ako nabidii amepeana mazoezi katika darasa yetu.(Solved)

    Sahihisha sentensi ifuatayo:
    Mwalimu mwenye ako nabidii amepeana mazoezi katika darasa yetu.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)