Nafasi ya vijana
- Watetezi wa haki za wanyonge Madhubiti anaungana na Amani kuwatetea wanyonge wanaoangusha uongozi dhalimu wa Nasaba Bora.
- Wenye bidii- Madhubuti anaweka bidii masomoni/ Imani na Amani wanafanya kazi kwa bidii.
- Wanapenda amani katika jamii- Amani hataki kuwe na mapinduzi ya umwangikaji wa damu; Amani anamwokoa Nasaba Bora kutoka kwa majambazi.
- Wenye utu na huruma- Amani anaonyesha utu na huruma kwa watoto walemavu wa mwalimu Majisifu.
- Wanaowajali wengine katika jamii- Amani anawagawia vipande vya ardhi.
- Wenye Imani- Imani ana imani kwa watoto walemavu wa Majisifu. Anamwonea Imani Amani ambaye amelazwa hospitalini.
- Wasiobagua kazi- Amani na Imani hawabagui kazi; wanaajiriwa kazi duni kwa Bwana Mtemi na Bwana Majisifu
- Walezi bora- Imani na Amani wanamlea mtoto Uhuru vyema.
- Wachungaji- Bob DJ nawenzake wanachunga ng‘ombe na kuwapeleka kunywa maji katika mto Kiberenge.
- Wanaodhulumiwa na viongozi bila sababu yoyote- Amani na Imani wanatiwa nguvuni na askari wa Bwana Mtemi kwa tuhuma za kumwoa mtoto Uhuru.
- Baadhi ya vijana ni majambazi. Gaddaffi (Oscar Kambona) ni jambazi. Akiwa na wengine alitaka kumwua Mtemi Nasaba Bora kwa risasi.
- Baadhi ya vijana ni washerati- Lowela anafanya mapenzi na Bwana Nasaba Bora.
- Baadhi wanashindwa na kuendelea na masomo, Lowela , Mashaka, Imani , Chwechwe Makweche.
- Wanamapinduzi- Imani na Amani wabadilisha imani ya jadi kuhusu unywaji wa maji ya mto Kiberenge.
- Wanaondoa utabaka- Madhubuti anahamia kibandani mwa Amani.
- Wafunza usamehevu-Amani anamsamehe Nasaba Bora na Majisifu. Anamwonya Oscar Kambona dhidi ya kulipiza kisasi.
- Wanatoa mwongozo kuhusu mfumo ufaao wa kuendesha nchi – Amani anawaonya raia kwamba, kufuata mitindo ya kisiasa na kiuchumi kama vile vyama vingi na ubepari bila kuwazia hali yao kutaangamiza nchi.
- Wanaonya dhidi ya kubagua wanawake- Imani anamwabia Amani asiweke wanawake pembeni katika kitabu atakachoandika.
- Wanahusika katika ujenzi wa jamii mpya yenye maadili- Madhubuti anakataa kazi aliyotafutiwa na babake jeshi kwa njia ya kifisadi.
sharon kalunda answered the question on October 4, 2019 at 06:46
- Kuna mfanano mkubwa kati ya ulumbi na hotuba. Thibitisha.(Solved)
Kuna mfanano mkubwa kati ya ulumbi na hotuba. Thibitisha.
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- "Wema wako umeniua kabisa………Nina jishtaki mwenyewe kila siku kwa miaka na miaka".(Solved)
KIDAGAA KIMEMWOZEA: Ken Walibora.
"Wema wako umeniua kabisa………Nina jishtaki mwenyewe kila siku kwa miaka na miaka".
(a) Eleza muktadha wa maneno haya.
(b) Onyesha kwa kutoa mifano kuwa anayeambiwa maneno haya alikuwa na wema.
(c) Eleza umuhimu wa mhusika mashaka katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- "Dhiki mbalimbali zimekuwapo lakini heri nusu shari kuliko shari kamili".(Solved)
Mstahiki Meya.
"Dhiki mbalimbali zimekuwapo lakini heri nusu shari kuliko shari kamili".
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Taja tamathali ya usemi iliyotumika katika dondoo hili.
(c) Eleza sifa zozote tatu za mzungumzaji.
(d) Fafanua aina zozote nne za migogoro inayojitokeza katika tamthilia ya Mstahiki Meya.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Taja kitamkwa chenye sifa ifuatazo.
Vokali ya nyuma, kati(Solved)
Taja kitamkwa chenye sifa ifuatazo.
Vokali ya nyuma, kati.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Kuna sababu kadha za kuwako na kushamiri kwa ajira ya watoto.(Solved)
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
Kuna sababu kadha za kuwako na kushamiri kwa ajira ya watoto. Moja ya sababu hizo ni umaskini unaozikumba jamaa nyingi pamoja na welewa mdogo wa thamani ya elimu wa baadhi ya watu katika jamii. Wapo watoto ambao hushurutika kubeba jukumu la kujizumbulia riziki wenyewe kutokana na hali duni ya familia zao.
Hali hii huweza kutokana na baadhi ya wazazi kutelekeza majukumu yao ya kimsingi ya kuikimu jamaa yao. Aidha kuna sehemu nyingine ambapo hali hii imetokana na janga sugu la ukimwi. Yapo maeneo ambako kuenea kwa ugonjwa huu kumewafanya viongozi wa jamaa kupukutika kama majani ya mti na kuwalazimisha watoto kuyakatiza masomo yao ili wawakidhie haja wadogo zao. Kuhusiana na kutelekeza majukumu, kuna wazazi ambao wanakosea kwa kutowaelekeza watoto wao kujua maadili mema ni yepi. Kwa njia hii watoto hao wanaishia kutumbukia kwenye matatizo makubwa.
Baadhi ya ajira zina athari kubwa sana kwa watoto. Ukahaba, kwa mfano, ni mojawapo ya ajira ambazo watoto wa kike hulazimika kujiingiza. Hii ni ajira ambayo inaweza kuwatumbukiza watoto hao katika hatari kubwa kutokana na uwezekano mkubwa wa kuambukizwa maradhi ya ukimwi. Asillimia kubwa ya watoto wanaotumbukia katika ajira hii, inapatikana katika maeneo ya mijini na sehemu ambako utalii umeshamiri sana. Umaskini pamoja na dhiki za mijini huwalazimisha watoto hao wa kike kuishia kwenye biashara za aina hiyo. Wengine hufanyiwa hila na wafanyabiashara ambao wametovukwa na utu kutokana na tamaa yao kubwa ya kujitajirisha. Katika maeneo ambako utalii umeshamiri, ukahaba wa watoto unatokana na umaskini pamoja na kusambaa na kuenea kwa maadili ajinabi, ya ulimwengu usio wetu.
Ikiwa umaskini ni chocheo kubwa la kuwapo kwa ajira ya watoto, basi inahalisi serikali zetu zifanye kila juhudi kuhakikisha kuwa umaskini umepigwa vita. Pana umuhimu wa kuhakikisha kuwa wanajamii wote wamepewa nafasi sawa za kujikwamua kutoka lindi la umaskini. Isitoshe, pana umuhimu wa juhudi nyingi kufanywa kuhakikisha kuwa nafasi za shule zimepanuliwa ili kuikidhi idadi kubwa ya watoto ambao wana kiu ya elimu. Serikali haina budi pia kuhakikisha kuwa zimepitishwa sheria zinazomlinda motto dhidi ya ukatili unaotokana na watu waliokosa hisia za utu na ubinadamu. Upo pia umuhimu wa kuvisaidia vikundi vinavyojitahidi kuwasaidia watoto ili kuzifanikisha juhudi zao kwa kuwa chanda kimoja hakivunji chawa kama tujuavyo.
Hatua nyingine ambazo zinaweza kuchukuliwa ili kupunguza ajira ya watoto ni kuwahamasisha wanajamii kuhusu haki za mtoto. mtoto yeyote yule ana haki ya kupata elimu ya msingi. Mtoto pia ana haki ya kuishi na kupata mahitaji ya kimsingi na ya lazima kama chakula, malazi au makazi na matunzo ya kiafya. Aidha mtoto ana haki ya ukuaji, yaani kukua kikamilifu pasi na kizuizi na katika mazingira yasiyombana kwa njia yoyote ile. Isitoshe, mtoto ana haki ya kupata ulinzi dhidi ya unyanyaswaji au udhalilishwaji wa aina yoyote ile au hata maonevu kwenye misingi yoyote iwayo. Mtoto pia ana haki ya kuwa huru kushiriki katika jumuiya yake, kutoa maoni na kujieleza, kushirikiana na kujiunga na vikundi. Mwisho, na muhimu zaidi, mtoto ana haki ya kulindwa dhidi ya ajira au aina yoyote ya kazi ambayo inaihatarisha afya na siha yake au inamzuia asipate elimu.
(a) Fupisha aya mbili za mwanzo bila kubadilisha maana. (maneno 60-70)
(b) Eleza hoja muhimu zinazojitokeza katika aya mbili za mwisho. (Maneno 50-60)
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Tamaa mbele mauti nyuma. Thibitisha ukweli ya methali hii ukirejelea hadithi ya Tazamana na mauti.(Solved)
Tazamana na Mauti” (S.A. Mohammed)
Tamaa mbele mauti nyuma. Thibitisha ukweli ya methali hii ukirejelea hadithi ya Tazamana na mauti.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- "Uniulie nini na ndoa yetu na wewe inamhusu pia yeye?"(Solved)
Mwana wa Darubini (K. Mwende Mbai)
"Uniulie nini na ndoa yetu na wewe inamhusu pia yeye?"
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Eleza sifa zozote nne za msemewa.
c) Jadili madhila yanayomkumba mwanamke katika hadithi hii.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- "Lazima kwanza mnihakikishie kuwa huyo sumu hapati hata fununu ya jambo hili."(Solved)
Mstahiki Meya
"Lazima kwanza mnihakikishie kuwa huyo sumu hapati hata fununu ya jambo hili."
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Taja sifa zozote nne za msemaji.
c) Andika umuhimu wa huyo sumu.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- "Tayari nimemkabidhi barua ya kujiuzulu ninapohusika."(Solved)
Mstahiki Meya
Tayari nimemkabidhi barua ya kujiuzulu ninapohusika."
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Mbali na changamoto inayofanya msemaji kujiuzulu, jadili changamoto nyinginezo zinazowakumba wanacheneo.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Eleza namna mbinu ya Taharuki ilivyotumiwa na mwandishi wa riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.(Solved)
Eleza namna mbinu ya Taharuki ilivyotumiwa na mwandishi wa riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Kwa kufafanua hoja saba thibitisha kwamba kuna haja ya kuwa na Revolution.(Solved)
Kidagaa kimemwozea
Kwa kufafanua hoja saba thibitisha kwamba kuna haja ya kuwa na Revolution.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- "Lakini bila matumaini hatuwezi kwenda mbele na Revolution."(Solved)
Kidagaa kimemwozea
"Lakini bila matumaini hatuwezi kwenda mbele na Revolution."
i) Eleza muktadha wa dondoo hili.
ii) Bainisha tamathali moja ya usemi inayojitokeza katika dondoo hili.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Naingia ukumbini, nyote kuwakariria,(Solved)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Naingia ukumbini, nyote kuwakariria,
Ushairi niwapeni, hoja nitawaachia,
Mnipe masikioni, shike nachoelezea,
Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.
Naanza kwa uzalendo, nchi yetu tuipende,
Yadhihirishe matendo, nchi yetu tuilinde,
Wa kila mtu mwendo, usije kawa mpinde,
Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili
Wote tuwe na umoja, tuuache ukabila
Kabila lisiwe hoja, mwenza kumnyima hela,
Taifa letu ni moja, Mkenya ndilo kabila,
Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.
Linda demokrasia, uongozi tushiriki,
Haki kujielezea, wachotaka na hutaki.
Changu naweza tetea, demokrasia haki,
Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.
Tena adili usawa, mgao raslimali,
Bajeti inapogawa, isawazishe ratili.
Idara zilizoundwa, ‗faidi kila mahali,
Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.
Tuwe na uadilifu, twache tamaa ya hongo,
Tusiwe na udhaifu, wa kuwa watu waongo,
Tukomeshe uhalifu, kisha tuache maringo,
Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.
Ubinafsi si adili, ila ni kusaidia,
Ukiwa nayo mali, asiyenacho patia,
Kama mtu mswahili, ubinafsi achia,
Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.
Na inavyoelezea, katiba ni kielezi,
Tutii kwa mazoea, hadi kijacho kizazi,
Kwa hayo nitamwachia. hiyo ya ziada kazi,
Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili
a) Eleza mambo yoyote manne ambayo mshairi anashauri taifa lifanye ili kuwa na aadili.
b) Taja tamathali yoyote moja inayojitokeza katika shairi hili.
c) Ainisha shairi hili kwa kuzingatia kigezo kifuatacho :
Mpangilio wa vina
d) Bainisha nafsineni (mzungumzaji) katika shairi hili.
e) Eleza toni ya shairi hili
f) Eleza umuhimu wa aina mbili za uhuru wa kishairi zilizotumiwa katika ubeti wa nne
g) Andika ubeti wa pili kw lugha nathari
h) Eleza maana ya neon lifuatalo kama ilivyotumiwa katika shairi:
i) hongo
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Vijana wana kumbwa na changamoto kadhaa katika jamii.Jadili baadhi ya changamoto hizi kwa kurejelea hadithi zozote tano kutoka diwani ya Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine.(Solved)
Vijana wana kumbwa na changamoto kadhaa katika jamii.Jadili baadhi ya changamoto hizi kwa kurejelea hadithi zozote tano kutoka diwani ya Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- "Mungu akikupa kilema, hukupa na mwendowe"
Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kurejelea hadithi Mzizi na Matawi.(Solved)
"Mungu akikupa kilema, hukupa na mwendowe"
Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kurejelea hadithi Mzizi na Matawi.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- "Hivi vitu lazima viwepo,au kama havipo ni lazima viwe ni vipengee mahususi vya uhalisia wamaisha yetu:(Solved)
Damu Nyeusi Na Hadithi Nyingine-Ken Wal'ibora Na S.Ahmed
"Hivi vitu lazima viwepo,au kama havipo ni lazima viwe ni vipengee mahususi vya uhalisia wa maisha yetu:
(a) Liweke dondoo katika muktadha wake faafu.
(b) Fafanua sifa zozote nne za msemaji wa maneno haya.
(c) Eleza kwa tafsili matatizo yoyote mawili yanayoikumba jamii ya hadithi mlimotolewa nukuu hii.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Wewe,Utazame mlolongo wa(Solved)
SHAIRI A
Wewe,
Utazame mlolongo wa
Waja unaoshika njia likiwapo;
Unaofuata pembe za barabara zisokuwapo,
Kwenda kuisaka auni,
Kuitafuta kazi inayowachenga.
Itazame migongo ya wachapa kazi,
Watokwao na jasho kapakapana,
Wanaotafunwa uhai na jua liso huruma:
Wakiinua vyuma na magunia,
Wakiinua makontena,
Wakichubuka mashambani,
Wakiumia viwandani,
Wakiteseka makazini,
Halafu
Uangalie ule ujira wa kijungu meko,
Mshahara uso kifu haja,
Nguo zisizositiri miili dhaifu,
Kilio chao kisichokuwa na machozi,
Na
Ujiangalie
Mwili wako unaomereta ujana wa ufanisi,
Gari lako la kifahari lililozibwa vioo,
Jumba lako la kujishasha kama uwanja mdogo,
Malaki yapesa unayomiliki,
Ujiitapo mwajiri kwa raha, hunusi usaha wa hali yao?
SHAIRI B
Dunia kitendawili, hakuna ateguaye;
Dunia kama tapeli, hadaa nyingi ujuye;
Dunia mwenye akili, inampiku na yeye;
Dunia ina mizungu, tena yapika majungu.
Dunia na yake hali, hupumbaza hatimaye;
Dunia ina akili, binadamu sichezeye;
Dunia uwe na mali, huiwezi dhorubaye;
Dunia ina mizungu, tena yapika majungu.
Dunia wenye muali, ambao waichezeye;
Dunia kipigo kali, huwakumba hatimaye;
Dunia wakaja kuli, ?menipata nini miye?
Dunia ina mizungu, tena yapika majungu
Maswali
(a) Je, mashairi haya mawili ni ya aina gani? Toa sababu.
(b) Taja dhamira kuu katika kila shairi.
(c) Kwa kutoa hoja zozote tatu linganua mashairi haya kiumbo.
(d) Taja na uelezee nafsi-pokezi katika mashairi haya mawili.
(e) Kwa kutolea mfano mmoja mmoja eleza matumizi ya mbinu hizi
(i) Kweli –kinzani
(ii) Mishata
(f) Tambua idhini ya kishairi iliyo tumika katika neno ?Waichezeye"
Na uelezee dhima yake katika utoshelezi wa kian ldhi.
(g) Dondoa mfano mmoja mmoja wa mbinu ya tashihisi kutoka kwenye Mashairi yote mawili.
(h) Andika ubeti wa tatu katika shairi la A kwa lugha nathari.
(i) Eleza maana ya msamiati huu kama ulivyotu? nika katika vifungu hivi.
(i) Inampiku.
(ii) Makontena.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Eleza namna mwandishi wa kidagaa Kimemwozea alivyofaulu kutumia fani ya barua kwa kutolea mifano mitano.(Solved)
Eleza namna mwandishi wa kidagaa Kimemwozea alivyofaulu kutumia fani ya barua kwa kutolea mifano mitano.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- "Tembo itakuua ndugu yangu. Punguza ulevi bwana.Siku hizi naona aibu kukuita ndugu yangu."(Solved)
Kidagaa kimemwozea
"Tembo itakuua ndugu yangu. Punguza ulevi bwana.Siku hizi naona aibu kukuita ndugu yangu."
(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
(b) Wahusika hawa wawili ni kama shilingi kwa ya pili.Thibitisha.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- "...Sote ni wafanyikazi wa baraza. Kile linachochuma Baraza tunagawana sote."(Solved)
Timothy Arege, Mstahiki Meya
"...Sote ni wafanyikazi wa baraza. Kile linachochuma Baraza tunagawana sote."
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Fafanua sifa tano za msemaji
(c) Tunagawana sote ni kinyume ejia hali halisi. Thibitisha.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)