Licha ya kuwa na historia ya kiasi, maisha ya binadamu ni kioja kikubwa. Hebu jiulize jinsi uhai wako wewe mwenyewe ulivyoanza sembuse...

      

Soma taarifa hii kisha ujibu maswali

Licha ya kuwa na historia ya kiasi, maisha ya binadamu ni kioja kikubwa. Hebu jiulize jinsi uhai wako wewe mwenyewe ulivyoanza sembuse unavyoweza kupumua na kuishi siku nenda siku rudi.
Dini zimefahamisha kuwa sisi binadamu tumeumbwa na Mwenyezi Muumba. Hata hivyo muumba hutumia mume na mke kutuanzishia maisha yetu humu humu duniani. Uhai wa hapa duniani huanzia katika tumbo la mwanamke muda mfupi tu baada ya mume na mke kushirikiana katika tendo la kujamiana. Katika ngono hii yenye ufanisi, mbegu moja ya manii kutoka kwa mwanamume, hudunga na kujiingiza katika yai la mwanamke huku ikilirutubisha. Tangu hapo mtu huwa na mama akawa mjamzito. Hatua ya kwanza ya uhai!
Wanasayansi wametuthibitishia kuwa mbegu katika shahawa kutoka kwa mwanamume ina kromosomu ishirini na tatu (23) nalo yai la mwanamke lina idadi iyo hiyo ya kromosomu. Basi katika hatua ya kwanza ya uhai wake, binadamu ana kromosomu arubaini na sita (46).
Kromosomu hizo zote ndizo humfanya mtu kuwa mkamilifu kwa kukadiria mambo mbalimbali adhimu. Kwa mfano, kukadiria kama kiumbe kitakuwa cha kike au cha kiume, mtu mweupe au mtu mweusi, mwerevu au wa wakia chache, mwenye nywele za singa au za kipilipili, atakuwa na damu ya namna gani, michoro ya vidole vyake itakuwa vipi na hata utu wake utakuwa wa namna gani katika siku za usoni.
Elimu yote anayopata mtu kutoka kwa jamii na mazingira huweza tu kujenga juu ya yaliyokwisha kuanzilishwa na kromosomu katika yai lililorutubishwa tumboni.
Haihalisi kabisa kufikiria kwamba huwa katika hali ya ukupe. La hasha! Yeye hujitegemea kwa vyovyote na ana upekee wake. Hatangamani na mama yake. Roho yake humdunda mwenyewe na damu yake ambayo huenda ikawa tofauti kabisa na ya mama yake, humtembea na kumpiga mishipani mwake. Isitoshe, yeye si mojawapo katika viungo vya mwili wa mama yake vinavyomdhibiti katika himaya yake ndogo.
Amini usiamini, hapana binadamu hata mmoja ambaye amewahi kuwa sawa kimaumbile na mwingine na wala hatakuweko. Hata watoto pacha kutoka yai moja la mama hawawi sawa, lazima watofautiane. Si nadra kusikia mtu amepata ajali akahitaji msaada wa damu, na pakakosekana kabisa mtu hata mmoja kutoka jamaa yake wa kimwauni. Basi ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni.

1. Ipe taarifa uliosoma anwani mwafaka
2. Mwandishi ana maana gani anaposema ‘ngono yenye ufanisi’?
3. Uchunguzi wa sayansi umekita mizizi imani gani ya kidini?
4. Taja majukumu yoyote matano yanayotekelezwa na kromosomu
5. Katika makala, elimu kutoka kwa jamii na mazingira yaelekea kuwa bure ghali. Kwa nini?
6. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika makala:-
(i) huwa katika hali ya ukupe…
(ii) himaya
(iii) hatangamani na mama yake

  

Answers


Maurice
1.i. Uhai unavyoanza
ii. Hatua ya kwanza katika uhai wa binadamu
iii. Kioja cha mwanzo wa uhai n.k.

2. Ana maana ya kujamiana ambapo mamba hutungwa

3. Imani inayokita mizizi ni kwamba mungu huwatumia mume na mke kumwanzishia
binadamu maisha ya duniani

4. Kromosomu humkadiria inadamu
i. Rangi ya ngozi yake
ii. Aina ya nywele
iii. Jinsia- kama atakuwa mume au mke
iv. Kiasi cha werevu
v. Aina ya damu
vi. Utu wake katika maisha ya usoni

5. Kwa sababu elimu kutoka kwa jamii na mazingara, pekee haifai kitu, lazima ijenge juu ya msingi wa kromosomu

6.- Kunyonya au kutegemea
-Mamlaka
Hana uhusiano na mama yake
maurice.mutuku answered the question on October 4, 2019 at 08:56


Next: a)List three forces that facilitate the transport of water and mineral salts up the stem. b)Name the tissue that is removed when the bark of a...
Previous: Elimu ya kajielewa sisi nani, na twatoka wapi, twaelekea wapi na utu tutaurejeshaje pahali pake....

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions


  • Chamkosi alipiga goti huku machozi yakimdondoka njia nne nne. Mbele yake, palikuwa na makaburi mawili. Waliokuwa wamelala mle hawakuwa na habari juu ya...(Solved)

    Soma taarifa hii kisha ujibu maswali

    Chamkosi alipiga goti huku machozi yakimdondoka njia nne nne. Mbele yake, palikuwa na makaburi mawili. Waliokuwa wamelala mle hawakuwa na habari juu ya kihoro na simanzi ya aliyepiga magoti pale. La kwanza, lilikuwa kongwe kiasi na lilikuwa limemea vichaka na magugu. La pili lilionyesha upya kwani shada za maua zilizowekwa na waombolezaji zilikuwa bado kukauka. La kwanza, ndimo babake mzazi alipolala. Nalo la pili, ndimo mamake alimolazwa kiasi cha siku mbili zilizopita.
    Kwa Chamkosi, maisha hayakuwa na maana tena. Alikuwa mwanafunzi wa miaka kumi na miwili. Hakuwa amehitimu kujitegemea na kukimu mahitaji yake. Aliokuwa akiwategemea sasa wamemwacha akiwa yatima. Hakuna yeyote ambaye angejaza pengo la wazazi wake wawili kwa kipindi cha mwaka mmoja. Haya yalikuwa kama donda sugu lisilopona.
    Kwa sasa, Chamkosi anayakumbuka mengi. Anakumbuka maisha ya babake. Alikuwa jibaba nene, zito lenye sura jamala na sifa nzuri. Baba mtu alikuwa na chake na alijiweza kiuchumi. Wengi pale mjini walimheshimu na kumstahi kutokana na uwezo wake wa kiuchumi.
    Alitunza familia yake vizuri. Chamkosi hakumbuki siku moja aliyokosa chochote alichohitaji kutoka kwa babake. Alikuwa na bidii kazini mwake pia.
    Walakini, kama mja asiyekamilika, baba mtu alikuwa na dosari moja. Aliyapenda maisha ya anasa na kufukuzia wasichana wadogo pale mtaani. Mamake Chamkosi aliyajua haya. Alijaribu kuzozana na mumewe ili aachane na tiabia hizi lakini kila akitaka ushauri, mama mtu alikemewa na kufokewa kuwa aache upuzi wa wanawake. Akafikia kufyata ulimi na kumwachia Mungu aongoze maisha ya bwanake.
    Hata hivyo hakuna marefu yasiyo na kikomo. Baada ya kuponda raha na vimada si haba, baba mtu alianza kuugua. Maradhi yake yakawa ni msururu. Mara, alipata mafua yasiyopona, mara kuendesha, mara maradhi ya ngozi. Haya yalimtia wasiwasi. Baada ya kukaguliwa na daktari, alipatikana kuwa ameumwa na mbuzi. Hakuamini haya. Baba aliyekuwa bashasha na mcheshi aliingiwa na upweke na kutotaka kutangamana na yeyote hata jamaa zake.
    Waliosema kuwa hakuna msiba usiokuwa na mwenzake, hawakukosea. Maradhi ya baba mtu yaliifilisi jamaa huku waking’ang’ania kumtafutia tiba. Wakaenda kwa waganga si haba. Waganga nao wakafaidi tamu.
    Muda si mrefu, mama mtu naye akaanza kuugua. Baada ya uchunguzi, alipatikana kuwa na maradhi yayo hayo ya bwanake. Ikawa ni kama mji umelogwa. Baada ya muda mfupi baba mtu aliaga dunia, mama naye hakukawia. Naye akasalimu amri na kumfuata bwanake kaburini. Familia ikawa kama inaangamia. Chamkosi kijana mdogo akaachwa pweke.
    Kama kawaida, mja hakosi neno. Wengi walisikika wakisema hili na lile kuhusu vifo hivi. Wengi walieneza uvumi. Lakini, Chamkosi alijua ukweli wa vifo vya wazazi wake.
    Sasa hapa alipo aliyatambulia macho makaburi ya wazazi wake, anasononeka. Anaomboleza zaidi kifo cha mamake ambaye alimwona hana hatia na hakupaswa kufa kwa maradhi yale. Anaukumbuka vizuri wema wa mamake usio na kifani. anakumbuka alivyojitunza kama mke na mzazi.
    Anakumbuka jinsi mamake alivyomshughulikia babake katika siku zake za mwisho licha ya baba mtu kuungama maisha yake maovu. Chamkosi alishindwa kujua kwa nini mamake akawa msamehevu kiasi hicho. Hakukosa kukumbuka wasia wa mama yake. Haya yalimfariji. Faraja hizi zilimpa nguvu mpya za kuyakabili maisha.
    Chamkosi aliwaza juu ya maisha yake. Akaona kuwa, kama yatima atawategemea wafadhili miongoni mwa jamaa na marafiki wenye huruma iwapo wapo. Aliwaza jinsi anasa za babake zilivyowaathiri watu wengi.Alitambua kuwa Ukimwi haumwathiri aliyeupata tu, bali na wengine wengi. Kweli, mtego wa Panya huingia waliokuwemo na wasiokuwemo. Lakini akiwatazama watu, hakuelewa kwa nini walidhamiria kuishi ujingani. Aliwaona baadhi ya vimada wa babake wakishikana viuno na vijana wadogo. Akawasikitikia. Akabaki na swali kwa nini watu wengine wanafikiria kuwa virusi hivi haviwezi kuwapata. Kwani wanafikiria kuwa vinabagua na kuwa wao hawahatarishi maisha yao? Alishindwa kufahamu watu watabadili vipi mienendo yao miovu na waweze kukabili janga hili lini?
    Kwa wakati huu, Chamkosi alikata shauri kusomea Taaluma ya Uelekezi na Ushauri kutokana na vifo vya wazazi wake. Alitaka kupata ujuzi utakaomwezesha kuwashauri na kuwaelekeza vijana wenzake ambao wanahatarisha maisha yao. Kama mshauri, alinuia kuhamasisha na kuzindua jamii juu ya hatari za Ukimwi.
    Alitaka kuhakikisha kuwa hatua zimechukuliwa na kila mtu katika jamii kukabili janga hili n kuliangamiza
    Chamkosi aliomba dua fupi. Akainuka na kuondoka huku akiwa na faraja na matumaini moyoni kutokana na azimio lake lile.


    (a) Toa kichwa mwafaka kwa makala haya
    (b) Eleza madhara mawili ya ugonjwa sugu uliotajwa katika makala haya
    (c) Taja mifano ya tabia zinazoweza kumfanya mtu aathiriwe na ugonjwa wa Ukimwi
    (d) Tofautisha tabia za baba na mama wa Chamkosi
    (e) Chamkosi baada ya kufikwa na madhila hayo yote aliamua kufanya nini? Toa maoni
    (f) Eleza maana ya:

    (i) Tumbulia macho
    (ii) Ameumwa na mbuzi

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Eleza sifa tano za sajili ya magazeti.(Solved)

    Eleza sifa tano za sajili ya magazeti.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Andika maana ya msemo. Kuwa na mihayara.(Solved)

    Andika maana ya msemo.
    Kuwa na mihayara.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Andika upya sentensi hii kwa kutumia visuwe vya maneno yaliyopigwa mstri. Lupita ndiye alitakadamu upelelezi wa shamba hili.(Solved)

    Andika upya sentensi hii kwa kutumia visuwe vya maneno yaliyopigwa mstri.
    Lupita ndiye alitakadamu upelelezi wa shamba hili.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Andika kinyume. Ukipitia kwao utalaaniwa.(Solved)

    Andika kinyume.
    Ukipitia kwao utalaaniwa.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Mwanafunzi aliadhibiwa kwa uongo wake. (Anza kwa .......Uongo)(Solved)

    Mwanafunzi aliadhibiwa kwa uongo wake.
    (Anza kwa .......Uongo)

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Tambua kinai kilichopigwa mstari katika senensi hii; Watu wenye woga mwingi hukimbia ovyo.(Solved)

    Tambua kinai kilichopigwa mstari katika senensi hii;
    Watu wenye woga mwingi hukimbia ovyo.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Andika maana mbili za neno "mlango".(Solved)

    Andika maana mbili za neno "mlango".

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Jibu kulingana na maagizo. (i) Ufisadi (unda kitenzi) (ii) - pya (unda nomino)(Solved)

    Jibu kulingana na maagizo.
    (i) Ufisadi (unda kitenzi)
    (ii) - pya (unda nomino)

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Kanusha sentensi hii katika hali ya "a" Kibofu hupaa angani.(Solved)

    Kanusha sentensi hii katika hali ya "a"
    Kibofu hupaa angani.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • CHIMBUKO LA USHAIRI Ushairi ni fani kongwe kama mwanadamu mwenyewe alivyo mkongwe duniani. Na mashairi yamekuwepo kitambo sana hata kabla ya lugha...(Solved)

    CHIMBUKO LA USHAIRI
    Ushairi ni fani kongwe kama mwanadamu mwenyewe alivyo mkongwe duniani. Na mashairi yamekuwepo kitambo sana hata kabla ya lugha ya Kiswahili bado haijanawiri na kushamiri kama ilivyo hivi leo. Ndipo tunasikia kuna mashiri ya kipemba, mashairi ya kimvita, mashairi ya kivumba, mashairi ya kipate, mashairi ya kiyunani, ya kirumi na kadhalika,. Almradi kila jamii na kila kabila lilikuwa na mashairi yake.
    Katika utafiti na kongomano zao, wataalam wa arudhi za Kiswahili asili wamechambua na kufafanua kwamba mashairi ya Kiswahili asili yake ni nyimbo za jadi zilizokuwa zikiimbwa na manju, wangoi au waimbaji stadi wa tangu na tangu walipojumuika katika matukio na hafla mbalimbali kama za jando, arusi, matanga, ngoma na shangwe zao za maishani.
    Nyimbo hizi zilitumiwa na watangulizi wetu, kidhamira hazikuhitalafiana hata kidogo na mashairi ya Kiswahili tunayohimiza wakati huu. Farka iko katika lugha na umbo kwani kila jamii ilitumia lugha yake na lahaja ya mazingira yake. Na kwa upande wa umbo, tungo hizo za awali kabisa hazikuwa na sanaa kwa maana ya ushauri tunauona leo. Bali tungo hizo zilijengeka katika nguzo mbili kuu. Kwanza ni uzito wa mawazo maadilifu ambayo yalitaamaniwa sana. Na pili ni mizani ya sauti ya manju kulingana na lahani, pumzi zake pamoja na madoido katika uimbaji ambao ulikuwa burudani naathari katika noyo za wasikilizaji wake.
    Kwa kifupi ni kwamba, nyimbo hizo ziliuhifaid umma kwa njia mbili, mawaidha kwa mapana na taathira au jadhba kutokana na sauti tamu ya manju.
    Kama utakubalika, basi huo ndio ushairi wa awali kabisa ullioambatana na nyimbo zetu za kienyeji. Kila kabila katika nchi zetu lilikuwa na ushauri wake au nyimbo zake zenye undani uliolenga sababu maalum na tukio maalum katika jamii.
    Nyimbo kama hizo kwa jina la sasa tunaweza kuita mashairi ndizo zile zilizoitwa ‘mwali’ na wakamba; gichandi kwa ‘wakikuyu’; ‘gigia gi sigele’ kwa waluo na ‘wagashe’ kwa wasukuma zilikuwa na undani wa kipekee tena uliodidimia ambao si bure kutolewa hadharani.
    Aina za mashairi ya watu wa mwambao ni kama lelemama, misemele, gungu, nyiso, kongozi n.k.
    (Walla Bin Walla – Malenga wa Ziwa Kuu , E.A.E.P)



    1. Ni nini haswa chimbuko la ushairi?
    2. Kulingana na kifungu hiki, ni nini umuhimu wa ushairi ?
    3. Ni maswala gani yaliyowapendeza wasikilizaji wa tungo hizo za zama ?
    4. Tofauti kati ya nyimbo za zama na ushairi wa leo upo kwenye vipengele gani viwili ?
    5. Kifungu : ‘haijanawiri na kushamiri’ ina maana gani katika lugha nyepesi ?
    6. Eleza maana ya :
    (a) Kongamano …
    (b) Jadhiba
    (c) Farka
    (d) Awali..

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Andika katika msemo halisi. Mwalimu alishangaa ni kwa nini Juma hakuwa amebeba mkoba wake siku hiyo.(Solved)

    Andika katika msemo halisi.
    Mwalimu alishangaa ni kwa nini Juma hakuwa amebeba mkoba wake siku hiyo.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi ifuatayo kwa udogo wingi. Mtu yule haachi kuandamana na mbwa wake aliyedhoofika kiafya.(Solved)

    Andika sentensi ifuatayo kwa udogo wingi.
    Mtu yule haachi kuandamana na mbwa wake aliyedhoofika kiafya.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi moja yenye kishazi huru na kishazi kitegemezi ukitumia "O" rejeshi tamati.(Solved)

    Tunga sentensi moja yenye kishazi huru na kishazi kitegemezi ukitumia "O" rejeshi tamati.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Changanua sentensi hii kwa kutumia jedwali. Mama alilima kwa bidii ingawa hakupata faida.(Solved)

    Changanua sentensi hii kwa kutumia jedwali.
    Mama alilima kwa bidii ingawa hakupata faida.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi ukitumia kitenzi cha katika hali ya kutendwa.(Solved)

    Tunga sentensi ukitumia kitenzi cha katika hali ya kutendwa.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha shamirisho na chagizo katika sentensi ifuatayo. Kimathi alimwandikia babake barua kwa kalamu jana jioni.(Solved)

    Bainisha shamirisho na chagizo katika sentensi ifuatayo.
    Kimathi alimwandikia babake barua kwa kalamu jana jioni.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Asifuye mvua imemnyea. Huu ni msemo wenye hakika isiopingika, na kutilia shaka ni sawa na kudai jua linaweza kubadilika na kuchomozea upande...(Solved)

    Soma taarifa hii kisha ujibu maswali

    Asifuye mvua imemnyea. Huu ni msemo wenye hakika isiopingika, na kutilia shaka ni sawa na kudai jua linaweza kubadilika na kuchomozea upande wa magharibi badala ya mashariki. Huu ndio ukweli uliodhihirika juzi katika vyombo vyetu vya magazeti.
    Lisemwalo lipo, na kama halipo li njiani. Waama, pafukapo moshi pana moto. Mwanafunzi mmoja wa kike kwa jina P.N. katika chuo kikuu kimojawapo nchini alishangaza umma wa Kenya na ulimwengu kwa jumla alipodai kuwaambukiza wanafunzi wenzake wa kiume mia moja na ishirini na wanne virusi vya Ukimwi.
    Kisa na maana? Aliambukizwa Ukimwi na mwanafunzi mwenzake aliyekuwa akifanya majaribio ya ualimu katika shule yao ya upili. Baada ya kushawishika sana alijuana naye kimwili, na matokeo yakawa kifo ambacho sasa alikuwa anawagawia wenzake.
    Kisa kama hiki kinachangia kueleza kina kirefu cha kutamauka na upweke ambao maisha ya waja wengi yameingia kiasi cha kuwaacha wanyama ijapo wanaenda kwa miguu miwili bado. Katika mojawapo ya mafunzo ya kidini ambayo Padre alinifunza mimi na wanafunzi wenzangu, tuliambiwa kisasi ni chake Mola, sisi waja wetu ni kushukuru tu. Mbona basi mwanafunzi kama huyu kutaka kulipiza?
    Ima fa ima, na waswahili husema, “mlaumu nunda na kuku pia”. Huyu mwanafunzi hawezi kuachiwa atende alivyotenda. Aliyekula naye raha alikuwa mtu aliyefahamika vizuri sana kwake. Isitoshe, huenda wakati huo alikosana na mama na baba kulala nje. Huenda alikosana na ndugu zake kwa kuepa nyumbani usiku wa manane kwenda kumwona huyu kalameni. Huenda alikosana na mwalimu wake kwa sababu kiburi kilianza kuingia. Kwa vyovyote vile, alikula raha na hastahili kuwaadhibu watu wasio na hatia kufidia makosa yake. Je, kama yeye na huyo jamaa wasingekuwa na Ukimwi, raha kiasi gani wangezila hadi leo?
    Jamii na watu wote kwa jumla hawana budi basi kulaani vitendo vya P.N. vya kuambukiza wanafunzi wenzake virusi huku akijua. Hili ni kosa ambalo linastahili adhabu ya kifo. Dawa ya moto ni moto ni adhabu inastahili kuchukuliwa haraka ili P.N. ambaye tayari amekiri hatia, atiwe nguvuni na adhabu itolewe.
    Barua ya P.N. inafafanua jambo jingine sugu. Kwamba kiwango cha maadili katika vyuo vyetu kimezorota kiasi cha kufanyiana unyama usiosemeka. Vijana wengi siku hizi wanashiriki tendo la ndoa bila haya. Huu upotofu wa maadili katika jamii wapaswa kushutumiwa na wote. P.N. hana sababu yoyote ya kibinadamu, kidini au kitu chochote kile kudai haki kwa uovu huo wake.


    1.Taja kichwa kwa makala haya
    2. Katika aya mbili za kwanza, mwandishi anamlaumu mwanafunzi kwa kosa gani? Eleza chanzo cha tabia za P.N
    4. Mwandishi wa taarifa hii anataka P.N achukuliwe hatua gani? Kwa nini?
    5. Barua ya P.N. bila shaka imeonyesha uvumbuzi mpya. Utaje
    6. Eleza maana ya vifungu hivi kama vilivyotumiwa katika taarifa:
    (a) Kina kirefu cha kutamauka
    (b) Ima fa ima
    (c) Kufidia makosa yake

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi kwa kutumia. (i) Kivumishi cha "ki" ya mfanano. (ii) Kielezi cha kiasi cha jumla.(Solved)

    Tunga sentensi kwa kutumia.
    (i) Kivumishi cha "ki" ya mfanano.
    (ii) Kielezi cha kiasi cha jumla.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Onyesha matumizi ya "kwa" katika sentensi hii. Kwa kuwa alikuwa amechelewa kwenda kwa nyanyake alisafiri kwa baiskeli.(Solved)

    Onyesha matumizi ya "kwa" katika sentensi hii.
    Kwa kuwa alikuwa amechelewa kwenda kwa nyanyake alisafiri kwa baiskeli.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)