Katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita, tumeshuhudia mabadiliko na maendeleo makubwa kuhusu vyombo vya habari nchini Kenya. Hapo awali, redio ndicho chombo...

      

Soma taarifa ifuatayo kisha ufupishe taarifa hii kulingana na maswali yanayofuata:-

Katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita, tumeshuhudia mabadiliko na maendeleo makubwa kuhusu vyombo vya habari nchini Kenya. Hapo awali, redio ndicho chombo cha habari cha kipekee kilichotamalaki kote nchini. Familia nyingi ziliweza kumiliki chombo hiki. Runinga ilikuwa miliki ya wachache, hasa mabwenyenye. Sasa hivi, hata akina yahe nchini na mashambani wanamiliki chombo hiki.
Runinga kama kifaa kingine chochote cha mawasilianao kina manufaa yake. Kwanza kabisa, ni nyenzo mwafaka ya kufundisha. Vipindi vinavyopeperushwa katika runinga huwa na mafunzo kemkem kwa mtu wa kila rika. Hali kadhalika, runinga huweza kuleta vipindi ambavyo huwafahamisha watu mambo yanayoendelea katika mazingira yao na duniani. Aidha, runinga ikitumika pamoja na michezo ya video huauni katika ukuzaji na ustawishaji ya kufundisha au kujielimisha. Michezo ya video, hasa ya kielimu huwafanya watu kujenga umakini pamoja na kuchua misuli ya ubongo na kuwafanya watu kuwa macho wanapofanya kazi.
Fauka ya hayo, televisheni ni chemichemi bora ya kutumbuiza na kuchangamsha. Hakuna mtu asiyependa kuchangamshwa. Televisheni ni mojawapo wa vyombo mwafaka vya kutekeleza hayo kutokana na vipindi vyake. Uburudishaji huu hupatikana kwa urahisi majumbani mwetu.
Vivyo hivyo, runinga hutumika kama nyenzo ya kuendeleza utamaduni, kaida na amali za jamii. Vingi vya vipindi vya runinga ni kioo ambacho huakisi mikakati na amali za jamii.
Kwa upande mwingine, hakuna kizuri kisichokuwa na dosari. Licha ya manufaa yake, televisheni imedhihirika kuwa na udhaifu wake. Kwanza, baadhi ya vipindi vya runinga na video hujumuisha ujumbe usio na maadili, kama vile matumizi ya nguvu za mabavu, ngono za kiholela, lugha isiyo ya adabu, ubaya kimavazi na maonevu ya rangi, dini, jinsia , kabila na utamaduni. Si ajabu kuwa baadhi ya vijana wetu wanaiga baadhi ya mambo haya. Vijana wetu siku hizi wameingilia ulevi wa pombe na afyuni, ngono za mapema kabla ya ndoa na mavazi yanayowaacha takribani uchi wa mnyama. Wengi wamekopa na kuyaiga haya kutoka katika runinga. Ukiwauliza wafanyacho, watakujibu kuwa ni ustaarabu kwani wameupata katika runinga.
Matumizi ya runinga na michezo ya video yasiyodhibitiwa huweza kuwa kikwazo cha mawasiliano bora miongoni mwa wanafamilia. Matumizi kama haya huwapa wanafamilia fursa ya kujitenga. Imedhihirika kuwa runinga haichangii kujenga uhusiano bora wa kijamii ukilinganisha na vyombo vingine vya burudani ambavyo hutoa nafasi ya watu kutangamana na kujenga uhusiano bora, televisheni haichangii haya. Badala yake, tajriba ya televisheni huwa na kibinafsi. Hali hii inapotokea katika kiwango cha familia, televisheni inaweza kutenganisha wazazi na watoto wao.
Halikadhalika, runinga na video aghalabu hueneza maadili yasiyofaa. Mathalan, baadhi ya vipindi vya televisheni huendeleza hulka ya kuhadaa, ngono za kiholela, kuvunjika kwa ndoa, n.k. Hulka hizi zisizoendeleza maadili ya kijamii huchukuliwa kama zinazofaa na zinazofuatwa na waliostaarabika. Huu ni upotovu.
Isitoshe, baadhi ya matangazo huhimiza matumizi ya madawa ya kulevya kama tembo na sigara. Vitu hivi vinapotangazwa, hupambwa kwa hila na udanganyifu mwingi ambao huwavutia vijana na watoto wengi. Si ajabu mtu anapouliza wanaoutumia vileo hivi walivyoanza, watajibu kutokana na athari za matangazo katika runinga na vyombo vingine.
Utafiti umeonyesha kuwa vipindi vya runinga na video ni chanzo cha matumizi ya nguvu za mabavu miongoni mwa wanafunzi. Wazazi wengi huchukulia vibonzo katika televisheni kuwa vinalenga kuburudisha tu na havina ubaya wowote. Lakini ukweli ni kuwa vipindi vingi vya vibonzo hushirikisha matumizi ya hila na nguvu za mabavu. Haya huibusha hamu ya vijana na watoto huyaiga.
Kwa hivyo, ni muhimu wazazi na jamii kutambua madhara ya televisheni. Utambuzi huu utawafanya waelekeze vijana na watoto jinsi ya kutumia televisheni na video ili kuepukana na madhara yake.
Maswali
(a) Ukitumia maneno 50-60, fupisha manufaa ya runinga
(b) Fupisha hasara za runinga ukitumia maneno 70-80

  

Answers


Maurice
(a) – Ni nyenzo mwafaka ya kufundishia.
- Huwafahamisha watu mambo yanayoendelea katika mazingira yao na duniani kote
- Huauni katika kukuza stadi ya kujifundisha au kujielimisha
- Hutumbuiza na kuchangamsha
- Hutumika kama nyenzo ya kuendeleza utamaduni, kaida na amali za jamii

(b) – Hujumuisha ujumbe usio na maadili kama matumizi ya mabavu, ngono za kiholela, lugha chafu .
-Kuwafanya vijana kuingilia ulevi na afyuni na kuvaa vibaya
-Matumizi ya runinga na michezo ya video yasiyodhibitiwa huweza kuwa kikwazo cha mawasiliano
bora miongoni mwa familia.
-Mawasiliano yakikosa, familia hutengana.
-Haichangii uhusiano bora
-Hukuza ubinafsi
-Huendeleza hulka ya kuhadaa na mengine mabaya
maurice.mutuku answered the question on October 4, 2019 at 11:12


Next: With a reason, state a phase in respiration that yields more energy.
Previous: Bainisha vishazi huru na vishazi tegemezi katika sentensi ifuatayo. Nitaenda maktabani ingawa ninaumwa na kichwa.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions


  • Toa maneno yenye maana sawa na haya. i. Izara ii. Anisi(Solved)

    Toa maneno yenye maana sawa na haya.
    i. Izara
    ii. Anisi

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha shamirisho na chagizo katika sentensi hii. Mbuga za wanyama zitapata wageni wengi mwaka ujao.(Solved)

    Bainisha shamirisho na chagizo katika sentensi hii.
    Mbuga za wanyama zitapata wageni wengi mwaka ujao.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi. Atanishughulikia vizuri.(Solved)

    Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi.
    Atanishughulikia vizuri.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Usawa wa wanadamu upo kimaumbile – maumbile ya mtu kamwe hayatakosewa na yale ya mnyama wa mwituni. Lakini fikira, tabia,...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali:

    Usawa wa wanadamu upo kimaumbile – maumbile ya mtu kamwe hayatakosewa na yale ya mnyama wa mwituni. Lakini fikira, tabia, kimo, uwezo na mahitaji huwa tofauti kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Kwa mintarafu hii yapasa wakufunzi na wazazi kuwapa watoto wao widhaa mapema ili wachague kwa wakati unaofaa kazi watakayoifanya maishani.
    Watoto wanapopelekwa chuoni, wazazi wao huukilia kuwasomesha hadi kiwango fulani cha masomo kisha wajitafutie kazi ambayo itawapa masurufu na pesa za shughuli zingine maishani.
    Katika nchi yetu tangu tupate uhuru mtindo wa kutoa kazi umekuwa ni ule wa kuchukua watu waliofaulu mitihani ya viwango fulani na kuwapa kazi moja kwa moja. Mwenendo huu wa kuajiri watu kazi umeendelea muda mrefu lakini sasa yamkinika utasitishwa na njia mpya kufuatwa. Sababu ya kufanya hivyo ni kuwa nafasi za kazi zimekuwa finyu sana. Kabla na punde baada ya uhuru nafasi hizo zilipatikana kila mahali. Nyingi ya hizo ziliachwa wazi na wageni walioihama nchi hii tulipojitawala. Siku hizi wanafunzi wanaokomea darasa la saba, kidato cha pili na hata cha nne huwa hawazioni ahadi za kupata kazi za madaraka fauka ya kazi yoyote. Wanaoiona tabasamu ya kazi mbele yao ni wale wanaotasawari masomoni wakifuata taaluma fulani.
    Tatizo la kazi laeleweka vema kwa serikali na ni kwa ajili hii serikali imemtasulia kila mwananchi kuwa wakati wa kuania kazi za utanashati umetimiuka. Wakati uliopo ni wakati wa kujifunga vibwebwe kisaki na kuchapa kazi zile ambazo hadi sasa zafikiriwa kazi chafu na zisizofaa wasomi. Dhana kama hiyo ni ya kibwanyenye, na ubwanyenye hauji ila kwa sulubu. Usemapo kuna kazi nzuri na mbaya huwa unazusha maswali mengi. Utatakiwa ueleze kinaganaga kazi nzuri au mbaya kwa nini? Kazi huwa nzuri kwa upande wa tija au kwa upande wa wepesi wake? Kujibu maswali ya namna hii kutahitaji wekevu mwingi, waima mtesi ataonekana dufu.
    Zipo kazi aina mbili. Ipo kazi ya kuajiriwa na ya kujiajiri. Kazi ya kujiajiri kwa kulinganishwa huonekana ngumu na yenye matatizo mengi mwanzoni. Lakini itakubalika pato lake ni kubwa zaidi ikishapata msingi imara. Msingi imara huwekwa kwa juhudi za mwanzoni zikiambatana na ujasiri. Mtu asiyejasiri kutenda tendo lolote maishani ni sawa na yule asiyejua atokako na kule aendako; yuaishi kungozwa. Ardhi ni thawabu, tena thawabu tunu. Ukiwa na kipande cha ardhi ifaayo kwa kilimo ufakiri ukikutawala ni wewe mwenyewe kupenda: la sivyo ufa umo ubongoni unaohitaji bwana mganga

    (a) Bila kupoteza maana iliyokusudiwa na mwandishi wa taarifa, fupisha aya ya kwanza
    na ya pili. maneno 60-70)

    (b) Kwa kuzingatia aya mbili za mwisho. Eleza mambo muhimu yanayoshughulikiwa na mwandishi. (maneno (50-60)

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi ifuatayo katika msemo halisi. Mama alimwuliza mwanawe alikochelewa na kisha akamtahadharisha kuwa haikuwa tabia njema kwa mtoto wa kike kama yeye kuzoea kutembea usiku.(Solved)

    Andika sentensi ifuatayo katika msemo halisi.
    Mama alimwuliza mwanawe alikochelewa na kisha akamtahadharisha kuwa haikuwa tabia njema kwa mtoto wa kike kama yeye kuzoea kutembea usiku.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Usafiri ni upelekezi wa watu na bidhaa au mizigo kutoka mahali pamoja hadi mahali pengine. Tuseme kutoka kituo A na kuenda...(Solved)

    Soma taarifa inayofuata kisha ujibu maswali yaliyoulizwa

    Usafiri ni upelekezi wa watu na bidhaa au mizigo kutoka mahali pamoja hadi mahali pengine. Tuseme kutoka kituo A na kuenda kituo B.
    Katika ulimwengu wa leo, watu na bidhaa husafirishwa barabarani kwa mabasi au motokaa za kila aina au kwa kutumia magari moshi yanayopita juu ya reli, au meli zinazopita majini, kadhalika, usafiri unaweza kufanyiwa hewani.

    Hivyo, hali haikuwa hivyo zamani. Usafiri uliojulikana sana kale ni usafiri kwa miguu. Watu waliposafiri kutoka eneo moja hadi jingine walilazimika kufanya hivyo kwa miguu. Kadhalika, watu waliposafirisha mizigo mizito kutoka eneo moja hadi nyingine, iliwabidi kuibeba mizigo hiyo wao wenyewe. Mpaka leo usafiri huu upo.
    Wanyama vilevile walitumiwa kama njia moja ya usafirishaji. Huku Afrika ya mashariki kulitumika wanyama wengine kama vile punda. Punda ni mnyama anayependwa sana kwa sababu anaweza kuenda mwendo mrefu pasipo na kunywa maji. Mpaka leo, mnyama huyo hutumika sana na wamaasai, wagala, warendile na wengine.
    Mnyama mwingine aliyetumika sana, na mpaka leo anaendelea kutumika ni ngamia. Ngamia anafaa sana katika usafiri wa jangwani. Kwato za ngamia huweza kusafiri kwa urahisi jangwani ama popote penye mchanga mwingi kwa sababu kwato zake hazizami kwenye mchanga. Isitoshe ngamia wanaweza kwenda mwendo mrefu bila maji au chakula huku wakitegemea mafuta yaliyohifadhiwa kwenye nundu zao.
    Katika ulimwengu wa kisasa, binadamu amepiga hatua kubwa sana katika masuala ya usafiri. Baadhi ya maendeleo hayo ni ya kustaajabisha. Kwa mfano, binandamu anaweza kuruka kwa kutumia vyombo vya angani kwenda kwenye anga za mbali. Katika karne iliyopita binadamu anaweza kuruka kwa kutumia vyombo vya angani kwenda kwenye anga za mbali. Katika karne iliyopita binadamu amefika mwezini kwa kutumia vyombo hivyo. Kuna tetesi kwamba sasa anajaribu kuzizuru sayari zilizoko mbali na ardhi.
    Ama kwa hakika, usafiri bora in kipimo kimojawapo cha maendeleo ya nchi yoyote katika ulimwengu wa sasa. Bila njia ya kisasa za usafiri, baadhi ya mambo yanayofanyika katika nchi zetu hayangefanyika.

    (a) Katika habari hii, punda na ngamia wana sifa gani muhimu zinazowawezesha kutumiwa
    kwa usafirishaji? (maneno 30-40)
    (b) Kwa mujibu wa taarifa, usafiri wa zamani unatofautiana vipi na ule wa siku hizi?
    (maneno 40-50)

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Nchi nyingi za ulimwengu wa tatu huathirika na biashara ya kimataifa.Biashara hiyo inaweza kuwa inafanya kwa uagizaji ama uuzaji...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali

    Nchi nyingi za ulimwengu wa tatu huathirika na biashara ya kimataifa.Biashara hiyo inaweza kuwa inafanya kwa uagizaji ama uuzaji wa bidhaa za nchi nyingine.
    Biashara ya kimataifa ina umuhimu mkubwa. Kwanza, inawezesha nchi kupata bidhaa ambazo haitengenezi mbali na kusaidia kuwepo na uhusiano kati ya nchi mbalimbali. Uhusiano huu huiwezesha nchi kupata bidhaa kwa bei rahisi kuliko ambavyo ingekuwa kama zingetengenezwa kwao, hasa ikiwa nchi inayohusika haina malighafi yanayohusika katika utengenezaji wa bidhaa hizo. Pia husaidia wakati nchi imekumbwa na dharura au majanga kwani itaauniwa na nchi nyingine ingawa hali kama hii haihakikishwi, ushirikiano huu vile vile huchochea upatikanaji wa nafasi za kazi kwa wengi.
    Kwa sababu za kushughulikia utengenezaji wa bidhaa na utoaji huduma nyingine kutokana na uzoefu wa muda na kuwepo raslimali, nchi huwa na uzoefu fulani. Ni kwa sababu hii nchi inawezeshwa kupata pesa za kigeni na kuuza bidhaa za ziada.
    Hata hivyo kuna matatizo yanayozikumba nchi za kiafrika katika biashara hii. Kwanza, biashara ya aina hii hutatiza viwanda vichanga katika nchi zinazoendelea kwa ushindani usio sawa. Ajabu ni kwamba nchi zilizoendelea zimetumia bishara hii ‘kutupa’ bidhaa za hali ya chini ama zenye athari kwa hali za kijamii.Urafiki haukosi. Ikiwa nchi inategemea uagizaji wa bidhaa, haitaweza kuikosea ama kuhitilifiana na nchi ambayo inategemea, hivyo kuathiri uhuru wa nchi kama hiyo.
    Hata hivyo, nchi mbalimbali zimeweka mikakati ya kulinda viwanda kutokana na athari ya biashara kama hii. Baadhi zimeweka ushuru wa juu kwa bidhaa zinazoagizwa utoka nje kwa wasio washirika wa kibiashara. Licha ya hayo, baadhi ya bidhaa zinazonuiwa kwa nje kwa matumizi ya kielimu, utafiti wa kisayansi nabidhaa za maonyesho huagizwa bila ushuru huo. Wakati mwingine ni benki kuu ndiyo hutoa leseni kwa niaba ya serikali kama njia ya kudhibiti bidhaa kutoka nje. Njia nyingine ya kuvisaidia viwanda nchini ni kuuza bidhaa kwa njia ya kuvipunguzia ushuru, usafirishaji nafuu na kuvipa ushuru.
    Serikali nyingine huhakikisha kuwa ni bidhaa kiasi fulani tu ambazo zinaweza kuagizwa kwa kipindi fulani. Kwa mfano, kuna idadi fulani ya magari kutoka nje yanayoweza kuagizwa kuja Kenya kwa mwaka mmoja. Hata hivyo, wakati mwingine, serikali husitisha uagizaji wa bidhaa kama vile dawa, sinema, maandishi ya kisiasa na vitabu kutoka nje; bidhaa ambazo zinachukuliwa kuwa hatari kwa nchi. Licha ya matatizo haya, biashara imekuwepo na inaendelea kujiimarisha.
    Maswali
    (a) Kwa mujibu wa mwandishi wa makala haya, biashara ya kimataifa itaendelea kujiimarisha.
    Eleza (maneno 40-50)
    (b) Dondoa hoja muhimu zinazojitokeza katika aya mbili za mwisho. (maneno 40-50)

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Akifisha sentensi ifuatayo. Karibu mgeni akaitika mwenyeji mbona huingii na mlango u wazi stareheni kwenye viti ahsante wakajibu..(Solved)

    Akifisha sentensi ifuatayo.
    Karibu mgeni akaitika mwenyeji mbona huingii na mlango u wazi stareheni kwenye viti ahsante wakajibu..

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana ya nahau zifuatazo: i) Furaha ghaya ii) Maneo yalimkata maini.(Solved)

    Eleza maana ya nahau zifuatazo:
    i) Furaha ghaya
    ii) Maneo yalimkata maini.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • MENO YA BINADAMU Kila mara tunapokula, meno yetu huuma, kutafuna na kusaga chakula tunachokula. Meno yanatuwezesha kukivunja chakula ili kuwezesha mwili wetu kukitumia. Ili mwili uweze...(Solved)

    MENO YA BINADAMU

    Kila mara tunapokula, meno yetu huuma, kutafuna na kusaga chakula tunachokula. Meno yanatuwezesha kukivunja chakula ili kuwezesha mwili wetu kukitumia. Ili mwili uweze kukitumia chakula hicho, pana vitu fulani vinavyokifanyia chakula hicho kazi mpaka kikaweza kuingia kwenye mwili wenyewe. Hivi hujulikana kama vimeng’enya. Binadamu ana meno ya aina nne kuu. Kwanza, kuna meno ya mbele au makato ambayo kazi yake ni kuuma au kukata chakula. Haya yanasaidiana na mengine yanayojulikana kama michonge; yanakata pia lakini yako sehemu ya nyuma. Michonge hufuatwa na meno mengine yanayosaga chakula na ambayo hujulikana kama masagego. Masagego hufanya kazi na meno mengine yajulikanayo kama magego. Kazi ya aina hizi mbili za meno ni kutafuna na kusaga chakula kabisa kabla ya kukimeza. Idadi ya meno ya mtu mzima ni thelathini na mbili. Bila ya kuwa na meno mazuri, binadamu hukabiliwa na matatizo makubwa wakati wa kula. Meno huweza kuharibika kwa sababu ya kutopigwa mswaki vizuri mara kwa mara. Ili kuhakikisha kuwa meno yetu ni mazuri, pana umuhimu wa kudumisha afya nzuri ya meno. Kila baada ya kulala, lazima tuhakikishe tumeyapiga mswaki vizuri bila ya papara ili kuondoa mabaki ya chakula yanayoweza kuwa chanzo cha viini vinavyoharibu meno. Pili, lazima tuhakikishe kuwa hatuharibu ufizi wa meno,yaani ile nyama inayoshikilia meno hasa kwa vijiti katikati ya meno baada ya kula. Afya ya meno ni muhimu ili kuhakikisha kuwa meno yetu yanadumu na kuendelea kutufaidi katika uhai wetu.

    (a) Kwa nini ni muhimu kudumisha usafi wa meno?
    (Tumia maneno yasiyozidi 25)
    (b) Fupisha taarifa uliyosoma. (Tumia maneno yasiyozidi 80).

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Umaskini ni tatizo sugu katika jamii. Binadamu wengi hujikuta katika hali hii kwa sababu hawakubahatika kusoma. Baadhi yao huenda...(Solved)

    Soma taarifa hii kisha ujibu maswali

    Umaskini ni tatizo sugu katika jamii. Binadamu wengi hujikuta katika hali hii kwa sababu hawakubahatika kusoma. Baadhi yao huenda walijaribu kusoma wakashindwa mapema kujipandisha kielimu. Ukosaji wa elimu huchangia sana katika kukuza ukata. Elimu huweza mtu kupata tonge kwa kujipatia kazi za kumwezesha kuyakidhi mahitaji ya maisha. Hali kadhalika, elimu humsaidia binadamu kupata maarifa mengi ya kutendea shughuli zake za kimaendeleo. Kwa mfano, kama ni wakulima wanaweza kutumia pembejeo zifaazo ili kuboresha uzalishaji wa mazao. Wakulima wenye elimu hawatapendelea njia duni za kuendeleza kilimo kama vile kutumia visagilima na mbinu nyingine za kijadi. Badala yake watatumia njia za kisasa za kuvunia mazao yao.
    Umaskini mwingine huwa mwiba wa kujichoma. Baadhi ya watu ni mikunguni. Kulaza damu kwao kunawafanya kuwa wategemezi katika familia na jamii kwa jumla. Kwa vile hawajazoea kuinamia cha mvunguni, hata wakifunzwa kuchakura hawawezi. Ili kujaribu kuutibu uwele wao na ufukara baadhi yao hutafuta njia za mkato kama vile upwekuzi wa vitu vya wale waliojitahidi. Wakifanikiwa huweza kufurisha vibindo vyao. Hata hivyo mkono mrefu wa walinda usalama ukiwakumbatia wao hubakia kusagika kwa dhiki isiyomithilika ndani ya magereza.
    Majanga ya kimaumbile kama vile mitetemeko ya ardhi, mikurupuko ya maradhi hatari, moto, ukame na mafuriko huchangia na kuzidisha umaskini. Matukio hayo yakiandama kidindia watu wengi huhasirika. Licha ya mali nyingi kupotea, manusura huachwa wakiwa maskini hohehahe. Matumizi yao hupotea kwani wengi huhitajika kuanza maisha upya.
    Vijana ni nguzo muhimu katika maendeleo ya nchi yoyote ile. Endapo watajiingiza katika uraibu wa dawa za kulevya, wataathirika wao wenyewe na jamii kwa jumla. Pamoja na kuwa vijana hawa hufuja pesa nyingi katika ununuzi wa dawa hizi, dawa zenyewe huwadhoofisha na kuwapoka nguvu za kushiriki katika uzalishaji mali. Kutokana na hali hii,umaskini hupaliliwa na kushamiri zaidi.
    Umaskini huzua matatizo mbalimbali katika jamii. Ufukara huchachawiza juhudi za serikali za kuwapa raia wake mahitaji ya kimsingi kama vile huduma za afya. Pia umaskini husababisha maovu mbalimbali ya kijamii kama vile mauaji na ukahaba.
    Baadhi ya wanajamii huona kwamba njia ya kipekee ya kukabiliana na changamoto zinazosababishwa na hali ya ulitima ni kupitia kwa biashara haramu. Hali hii huchochea zaidi kudorora kwa maadili ya kijamii.
    Mataifa mbalimbali ulimwenguni yamezua mikakati mahsusi ya kukabiliana na umaskini. Baadhi ya mataifa yamebuni utaratibu maalum wa kupunguza mwanya mkubwa uliopo kati ya matajiri na maskini. Mojawapo ya mipango hiyo ni kupandisha viwango vya kodi inayotozwa wenye mishahara minono na wafanyibiashara wenye pato kubwa. Aidha huduma za burudani hutozwa kodi ya kiwango cha juu. Kupitia kwa kodi hizo, na njia nyinginezo, serikali za nchi hizo hupata pesa za kuwahudumia maskini.
    Mataifa yanayoendelea yanaweza kuwakwamua wananchi kiuchumi kwa kuwapa wahitaji mitaji ya kuanzisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo. Mifano ya miradi hiyo ni viwanda vya ‘Jua kali’, ususi wa vikapu na uchongaji wa vinyago. Hali kadhalika, serikali inaweza kuwatafutia masoko ya nje wafanyi biashara wadogo wadogo. Aidha, serikali inaweza kupunguza ushuru kwa bidhaa zinazoagizwa na masoko ya nje wafanyibiashara wa aina hiyo. Mathalan, ushuru unaotozwa nguo kuukuu zinazoingizwa nchini ukipunguzwa, wauzaji wa nguo hizi watafaidika zaidi na hali ya umaskini itaendelea kupungua.
    Sehemu za mashambani ni mhimili mkubwa wa uchumi. Ingawa kumekuwa na juhudi za kuzistawisha sehemu hizi kwa kusambaza huduma za umeme na maji kwa gharama nafuu, bado hali haijawa ya kuridhirisha. Ili kuimarisha sehemu hizi na kukabiliana vilivyo na tatizo la umaskini, hatuna budi kusambaza huduma hizi hasa katika sehemu kame. Sehemu hizi zikipata maji, kilimo chenye natija kitaendelezwa na umaskini utakuwa karibu kuzikwa katika kaburi la sahau. Ikiwa tutazitekeleza sehemu hizi, vijana wanaoweza kusistawisha watahamia mjini kutafuta maisha ‘bora’. Hali hii itazidisha msongomano wa watu mjini.
    Umaskini ni nduli ambaye lazima aangamizwe ima fa ima. Vijana hawana budi kubadili mtazamo wao hasa kuhusu kazi za mashambani na kujitahidi kuimarisha kilimo. Fauka ya hayo, mifumo mwafaka ya elimu ibuniwe ili kukidhi mahitaji ya kiuchumi ya taifa. Badala ya kuhimiza elimu ya kinadharia, elimu tekelezi isisitizwe zaidi ili wale wanaokosa kazi za kiafisi waweze kujiajiri katika kazi za kiufundi. Ukusanyaji wa ushuru uimarishwe zaidi. Hali ya usalama iendelee kustawishwa ili kuzidi kuwavutia wawekezaji, na hivyo kubuni nafasi zaidi za kazi.


    (a)Kulingana na kifungu ‘umasikini ni hali inayoletwa na udhaifu wa mtu binafsi’. Jadili
    (maneno 30-40)
    (b)Jamii ina uwezo wa kukabiliana na hali ya umaskini inayowakumba raia wake. Thibitisha
    kwa mujibu wa kifungu (maneno 40-50)

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Badilisha sentensi ifuatayo iwe mazoea kwa kutumia "O" rejeshi. Malipo ambayo anapewa ni yale ambayo yanaridhisha.(Solved)

    Badilisha sentensi ifuatayo iwe mazoea kwa kutumia "O" rejeshi.
    Malipo ambayo anapewa ni yale ambayo yanaridhisha.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Andika wingi wa sentensi zifuatazo; i) Sokwe aliukwea mti huo kwa kasi.ii) Mshale mkali ulitumiwa kumwua samba.(Solved)

    Andika wingi wa sentensi zifuatazo;
    i) Sokwe aliukwea mti huo kwa kasi.
    ii) Mshale mkali ulitumiwa kumwua samba.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Tumia neno "vile" kama. i) Kivumishi … ii) Kiwakilishi iii) Kielezi(Solved)

    Tumia neno "vile" kama.
    i) Kivumishi …
    ii) Kiwakilishi
    iii) Kielezi

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana mbili za sentensi ifuatayo(Solved)

    Eleza maana mbili za sentensi ifuatayo.
    Nitakuja kukagua kazi hiyo baada ya saa mbili.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Kiwango cha ufanisi wa taifa lolote lile hugezwa kutokana na hali ya miundomsingi. Mataifa sampuli hii hutenga fulusi si akali ya makadirio ya bajeti yake...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
    Kiwango cha ufanisi wa taifa lolote lile hugezwa kutokana na hali ya miundomsingi. Mataifa sampuli hii hutenga fulusi si akali ya makadirio ya bajeti yake kwa miradi ya maendeleo. Nchi nyingi zinazoendelea hujikuta katika njia panda kwa mujibu wa utekelezaji wa sera amilifu za kukwamua chumi zao. Utawala wa Kenya umekuwa ukijikuna kichwa katika harakati za ujenzi wa nguzo hii ya ufanisi. Mbali na asasi za utabibu kuwa chache. Zile zilizopo ziko katika hali mahututi. Udufu huu umesambaratishwa zaidi na idadi kubwa ya madaktari na wauguzi wanaoendelea kugura tangu usimamizi wa huduma zao kuhamishiwa serikali za gatuzi, sikwambii changamoto zinazonyemelea sekta za elimu, utumishi wa umma na zaraa. Katika harakati za kupata suluhu, serikali imetoa rai ya kupunguza tija kwa watumishi wake. Rais, naibu wake na makatibu wa wizara wamekuwa vielelezo kwa kujitolea kunyoa 20% ya mishahara yao. Katika mdahalo wa kitaifa kuhusu matumizi ya mfuko wa umma ulioandaliwa na tume ya Mishahara nchini, rais alizirai bunge, mahakama, seneti, mashirika ya umma na magatuzi kudurusu mishahara kwa watumishi wake. Hii ni kwa sababu serikali inatumia 55% ya mapato ya ushuru ambayo inafasirika kama 13% ya mfuko wa umma kulipia mishahara. Kiasi hiki kimekuwa kikiongezeka kutoka shilingi bilioni 240 hadi bilioni 500 kwa muda wa miaka minne iliyopita. Wabobezi wa maswala ya iktisadi wamefichua kuwa hiki ni zaidi ya kiwango cha kimataifa cha 35% kinachotekelezwa na nchi zilizoendelea. Mbona tussige nchi za Malasya na Uswizi ambazo zimepunguza janguo kwa viongozi wao kwa 50%? Wataalam hawa wanashauri kuwa harakati hizi ni kama tone la suluhu kwenye bahari ya sintofahamu ikizingatiwa kuwa kupunguza mishahara ya wafanyakazi hasa wa ngazi za chini. Kutawanyonga katika uchumi ambao mfumuko wa bei umefikia kiwango cha kuvunda. Uhunifu unahitajika kupanua mfuko wa umma. Makadirio yanayotengewa wizara na shughuli nyingine za serikali zisizo za kimsingi yapunguzwe. Serikali pia inahitajika kuziba mianya ambayo kwayo darahimu lukuki hunywelea kutokana na ubadhirifu. Inatarnausha kutanabahi kuwa wizara ya usalama wa ndani haiwezi kuwajibikia matumizi ya shilingi milioni 548.7!
    Wakenya walitoteza mamilioni kutokana na Benk Kuu ya Kenya kukaidi ushauri wa kisheria na kanuni za zabuni za kandarasi zinazohusu mitambo ya usalam na utengenezaji wa pesa. Si ajabu gavana wake Profesa Njuguna Ndung‘u alifunguliwa mashtaka ya utepetevu na matumizi mabaya ya mamlaka.
    Wanaotolea nchi hii futuko wataweza tu kutua mori iwapo makabiliano haya na vyombo vya sheria yatawasukuma wahitifaki hawa wa chauchau nyuma ya kizimba. Waaidha, ziara za ughaibuni ambazo zilimpokonya mlipa ushuru milioni 348 mwaka wa 2013 pekee hazina budi kupunguzwa maradufu. Maafisa wa serikali lazima waghairi kutumia magari mazito yanayogubia mafuta. Inabainika kuwa gharama ya warsha na makongamano yanayonuiwa kuboresha ujuzi wa watumishi wa umma imeghushiwa licha ya utupu unaoambatana na mada zake.Serikali itaelezaje kauli kwamba imekuwa ikitumia shilingi bilioni 2 kuwakimu wafanyikazi hewa?Isitoshe, kuna wafanyikazi wengi wanaofanya kazi ombwe. Kwa mfano, makamishina wa magatuzi waliotumwa huko na serikali kuu wanatoa huduma zipi zisizoweza kutolewa na magavana? Ni ruya au halisi kuwa makdmishna wa Tume ya Mishahara nchini hulipwa marupurupu ya shilingi 400,000 kila mwezi kando na mishahara yao yenye minofu? Hii ni haramu ambayo lazima ilaaniwe.Ninashuku kuwa wakenya wangepigwa na mshtuko wa moyo iwapo marupurupu yanayohusishwa na taasisi nyingine za umma kama vile urais, mahakama na bunge yangeanikwa.
    a) Dondoa hoja muhimu katika aya mbili za mwanzo. (Maneno 75-80)
    b) Kwa kutumia maneno yasiyopungua 90 wala kuzidi 95, eleza mikakati inayoweza kutumiwa kudhibiti mfuko wa umma.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Waajiri wengi wanazilaumu taasisi za elimu kwa kukosa kutoa wafanya kazi wenye ujuzi tosha, hasa wa kiteknolojia za kisasa kama kutumia...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha kisha ujibu maswali:-

    Waajiri wengi wanazilaumu taasisi za elimu kwa kukosa kutoa wafanya kazi wenye ujuzi tosha, hasa wa kiteknolojia za kisasa kama kutumia kompyuta kutenda kazi mbalimbali. Hali hii imekuwa ya kuhuzunisha sana.
    Ujuzi wa kuweza kutumia Kompyuta unaweza kumfaa mwanafunzi hata anapokosa nafasi ya kujiunga na chuo kikuu kwa vile anaweza kuendelea na elimu yake kupitia kwa elimu mtandao. Pia anaweza kufanya utafiti wa kina kupitia intaneti na kwa njia hii akaimarisha elimu yake.
    Mojawapo ya njia ya kuimarisha elimu kuhusu maswala ya teknolojia ni kuanzishwa kwa mikakati mipya ya kufunza. Somo la Kompyuta laweza kuimarika mashuleni endapo kwanza walimu watahamasishwa juu ya faida za ujuzi huu.
    Kwa kutumia Kompyuta kufunza, walimu wanaweza kufunza madarasa kadhaa katika kipindi kimoja bila kulazimika kuyahudhuria. Hii itapunguza kiwango cha kazi kwa walimu kwa vile watapata muda wa kufanya utafiti mpana. Aidha, watapata habari na ufahamu zaidi wa mambo kwa kutumia mitambo ya Kompyuta kutoka kwenye intaneti, kupitia tovuti.

    Hata hivyo mipango hii inakabiliwa na changamoto kama vile bei za juu za mitambo na vifaa vya Kompyuta, ukosefu wa miundo msingi itakayowezesha utumiaji wa mitambo hii na ukosefu wa walimu waliohitimu somo la Kompyuta.
    Pia, kuna tatizo la ukosefu wa nguvu za umeme hasa maeneo ya mashambani; vile vile, katika maeneo yaya haya, wanafunzi na wazazi wengi huvichukulia somo la Kompyuta kuwa gumu na linalofaa wakaazi na wanafunzi kutoka maeneo ya mijini na linalofaa wakaazi muhimu kwao mashambani.



    Maswali
    (a) Ipe taarifa uliyoisoma anwani inayoifaa
    (b) “Hali hii imekuwa ya kuhuzunisha.” Ni hali gani inayozungumziwa katika aya ya 1?
    (c) Ujuzi wa kutumia Kompyuta unaweza kumfaidi vipi mwanafunzi?
    (d) Mikakati mipya ya kuimarisha elimu kuhusu maswala ya teknolojia inakabiliwa na
    vizingiti vipi?
    (e) Taja manufaa mawili ambayo mwalimu anaweza kupata kutokana na ujuzi wa teknolojia
    ya Kompyuta
    (f) Andika msamiati mwafaka zaidi kwa maneno yafuatayo:
    (i) Kompyuta
    (ii) Intaneti

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Takwimu za hivi punde zinaonyesha kuwa maradhi ya saratani imejifaragua na kuwa miongoni mwa senene kuduku duniani maadam inatishia kuupiku ukimwi.(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
    Takwimu za hivi punde zinaonyesha kuwa maradhi ya saratani imejifaragua na kuwa miongoni mwa senene kuduku duniani maadam inatishia kuupiku ukimwi. Wagonjwa wanoendelea kuyasalimia amri wanaelekea kufikia kiwango cha kutisha.Licha ya tawala nyingi duniani kuwekezea tafiti anuai za kuyapindua, miale ya welewa wa kiini chake bado ni hafifu ajabu. Wataalam wa utabibu wanaeleza chanzo cha saratani kama mgawanyiko usio wa kawaida wa chembechembe za damu katika viungo vya mwili vinavyohusika. Viungo huanza kukua kwa kasi isiyo ya kawaida.Japo uvumbuzi unaonyesha kwamba kuna uwezekano mkubwa kwa watu wa umri wa makamo kuambukizwa ugonjwa huu. Wazee wamo hatarini zaidi.Hata hivyo vimeshuhudiwa visa vingi ambavyo hata watoto wachanga huathiriwa pakubwa.Saratani ya tezi-kibofu. Ya koromeo nay a mapafu ni baadhi ya aina zinazowaathiri wanaume. Saratani ya tezikibofu huwasogelea zaidi mabuda wa umri wa miaka zaidi ya sitini. Kwenda haja ndogo kila mara. Ugumu wa kupitisha mkojo, ugume wa kuanza au kumaliza kukojoa, damu kwenye mkojo na maumivu ya mgongo ni baadhi ya dalili zake. Mwishowe, tezi-kibofu huzidi kuwa kubwa na kufungia mkojo kutoka. Kansa zinazowalenga sana wanawake ni pamoja nay a nyumba ya uzazi, mlango wa uzazi na maziwa. Kansa ya maziwa huwachachawiza zaidi wanawake wenye umri wa miaka thelathini na mitano au zaidi. Dalili ya awali ni uvimbe unaohisika kwa ndani na maziwa kutoa usaha. Inaenea haraka na kuviambukiza viungo vya ujirani mathalani mapafu na ini. Saratani ya mlango wa uzazi inaambukizwa na virusi vinavyoita papolloma. Virusi hivi hupata mwanya iwapo mwanamke aliaza mahusiano ya kimapenzi katika umri mdogo,akiwa na wapenzi wengi, akiwa matumizi wa dawa fulani za kupanga uzazi na apulizapo moshi wa sigara. Inapendekezwa kuwa ukaguzi wa ada ufanywe ili kuugundua kabla haujasambaa kutokana na kauli kwamba mwanzoni hausababishi uchungu wowote. Ukaguzi wa kibinafsi kwenye viungo vilivy na uwezekano mkubwa wa kuambukizwa kisha jambo lolote lisilo la kawaida kama vile uvimbe na ugumu wa kumeza liwasilishwe mara moja kwa daktari. Ushauri zaidi unahusu aina ya vyakula na mitindo ya kisasa ya maisha. Vyakula vilivyosheheniwa na protini zipatikanazo katika nyama na mayai ni miongoni mwa vyakula hatari. Vyakula vya kiasili kama mboga, miwa, matunda, mafuta yanayotokana na mimea na nyama nyeupe hupendekezwa. Uvutaji wa sigara, unywaji pombe, na baadhi ya vipodozi vyenye zebaki huweza kurutubisha uwezekano wa kuambukizwa saratani.
    Ijapokuwa saratani ni kama sikio la kufa lisilosikia dawa, ni muhimu wawele wazibe ufa kabla ya kuangukiwa na ukuta usioweza kujengeka tena. Ikigunduliwa mapema. Maradhi haya huweza kudenguliwa kutumia tibakemikali, tabamiale, chanjo dhidi ya baadhi ya virusi vya saratani, upasuaji wa viungo vilivyoathiriwa na dawa za kupunguza makali yake. Utafiti wa kina uliofanywa na kukamilishwa mwezi wa Machi, mwaka wa 2014 na madktari wa Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta kwa ushirikiano wa wengine kutoka Uingereza umegundua kuwa dawa aina ya Lopinavir inyotumiwa kupunguza makali ya ukimwi ina uwezo wa kukabiliana na maradhi haya. Uchunguzi uliofanyiwa wawele baada ya muda Fulani wa uwekaji wa dawa hii kwenye mlango wa uzazi ulibainisha kuwa chembechembe za saratani huangamizwa na dawa hii. Ni jambo la kutia moyo kuwa harakati za kukabiliana na janga la ukimwi zinaelekea kutoa sulhu kawa maradhi haya ya kansa.Inakuwa shani inaposadifu kuwa nuhusi iliyowahi kutokea katika mapisi ya siha ya insi imekuwa kitivo kinachopaswa kuenziwa. Hakika hizi ni harakati zinazostahili kupongezwa na kuzidishwa iwapo zimwi hili litafukiwa katika lindi la usahaulivu.

    a) Kwa nini maradhi ya saratani yanaelekea kuwa hatari zaidi kuliko ukimwi?
    b) Ni kwa nini ni vigumu kuitambua saratani mwanzoni?
    c) Taja mambo yanayoweza kuchangia maambukizi ya saratani ya mlango wa uzazi.
    d) Eleza njia ambazo mtu anaweza kutumia kugundua kama ana saratani.
    e) Eleza baadhi ya mambo yanayoweza kuchochea maambukizi ya saratani.
    f) Eleza maana ya methali ifuatayo kwa mujibu wa makala haya.
    Dalili za mvua ni mawingu.
    g) Toa maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa kwenye makala.
    i) senene kuduku
    ii) maziwa
    iii) ukaguzi wa ada

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Kwa zaidi ya mwongo mmoja uliopita, ulimwengu mzima uliathiriwa na masaibu ya kifua kikuu kwa kiwango cha kuogofya kiasi kwamba katika mwaka...(Solved)

    Kwa zaidi ya mwongo mmoja uliopita, ulimwengu mzima uliathiriwa na masaibu ya kifua kikuu kwa kiwango cha kuogofya kiasi kwamba katika mwaka wa 1993, shirika la afya duniani (WHO) lilitangaza ugonjwa huu kuwa swala dharura la kimataifa.
    Ongezeko kubwa la visa vya kifua kikuu lililotokana na kuchipuka kwa viini vinavyosababisha maradhi hatari ya Ukimwi na magonjwa yaliyohusiana na punde baadaye ilibainika kuwa bara la Afrika lilikuwa ndilo lililoathiriwa zaidi na Ukimwi pamoja na maradhi ya kifua kikuu. Hii ndiyo hali inayotawala sasa ulimwenguni. Afrika likiwa bara linaloongoza kwa wagonjwa walioambukizwa viini vya Ukimwi lilikuwa likishuhudia visa vya maradhi ya kifua kikuu.

    Viini vya Ukimwi vinapunguza uwezo wa mwili wa mgonjwa kupigana na vijidudu vya maambukizi. Swala linalowafanya wagonjwa hawa kutodhibiti maambukizi ya magonjwa mbalimbali. Katika hali ya kawaida mwili wa mtu kama huyo unaweza kujikinga dhidi ya viini kama hivyo. Maambukizi kama haya kawaida hujitokeza kukiwa na nafasi duni ya kinga mwilini. Katika baadhi ya mataifa kama vile Kenya, maambukizi ya kifua kikuu hufanyika mapema katika umri mchanga maishani.
    Kwa kawaida, viini hivyo huwa havisababishi ugonjwa wenyewe. Badala yake, kinga katika mwili wa aliyeambukizwa unaweza kusitiri maambukizi hayo bila mhusika kuwa mgonjwa kutokana na sababu mbalimbali. Viini hivyo baadaye vinaweza kuwa hai tena na kumfanya mgonjwa kukumbwa na ugonjwa. Swala hili kwa kawaida hujitokeza wakati mgonjwa anapoambukizwa virusi vya Ukimwi. Virusi hivyo pia huongeza hatari ya ugonjwa kujitokeza baada ya maambukizi au pengine kujitokeza tena baada ya mgonjwa kupokea tiba ya kwanza.
    Kulingana na utafiti, inakadiriwa kwamba mmoja kati ya wagonjwa wawili au watu wenye virusi vya Ukimwi watapata kifua kikuu wakati mmoja katika maisha yao. Inakadiriwa kwamba karibu asilimia 50 hadi 60 ya wagonjwa wenye maradhi ya kifua kikuu nchini Kenya pia wameambukizwa viini vya Ukimwi. Kwa upande mwingine, maradhi ya kifua kikuu hujitokeza kama kawaida kwa wagonjwa wenye virusi vya ukimwi. Kwa hivyo, wakati wa kushughulikia wagonjwa ni lazima pia wafanyiwe uchunguzi wa kubaini ikiwa wameambukizwa kifua kikuu.


    (a) Ipe taarifa uliyoisoma kichwa mwafaka
    (b) Ni nini hasa kilichochangia kuongezeka sana kwa maradhi ya kifua kikuu?
    (c) Kwa kifupi, eleza ni kwa nini ugonjwa wa Ukimwi ni hatari mwilini
    (d) Ukimwi na kifua kikuu una uhusiano mkubwa, eleza uhusiano huu kulingnana na
    taarifa uliyoisoma
    (e) Andika urefu wa neno ‘Ukimwi”
    (f) Eleza mambo mawili ambayo yametokana na utafiti
    (g) Ni jambo lipi ambalo ni la kushangaza kuhusiana na kifua kikuu
    (h) Andika maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika kifungu hiki
    (i) Kusitiri
    (ii) Mwongo
    (iii) Swala la dharura.
    (iv)Viini

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Licha ya kuwa na historia ya kiasi, maisha ya binadamu ni kioja kikubwa. Hebu jiulize jinsi uhai wako wewe mwenyewe ulivyoanza sembuse...(Solved)

    Soma taarifa hii kisha ujibu maswali

    Licha ya kuwa na historia ya kiasi, maisha ya binadamu ni kioja kikubwa. Hebu jiulize jinsi uhai wako wewe mwenyewe ulivyoanza sembuse unavyoweza kupumua na kuishi siku nenda siku rudi.
    Dini zimefahamisha kuwa sisi binadamu tumeumbwa na Mwenyezi Muumba. Hata hivyo muumba hutumia mume na mke kutuanzishia maisha yetu humu humu duniani. Uhai wa hapa duniani huanzia katika tumbo la mwanamke muda mfupi tu baada ya mume na mke kushirikiana katika tendo la kujamiana. Katika ngono hii yenye ufanisi, mbegu moja ya manii kutoka kwa mwanamume, hudunga na kujiingiza katika yai la mwanamke huku ikilirutubisha. Tangu hapo mtu huwa na mama akawa mjamzito. Hatua ya kwanza ya uhai!
    Wanasayansi wametuthibitishia kuwa mbegu katika shahawa kutoka kwa mwanamume ina kromosomu ishirini na tatu (23) nalo yai la mwanamke lina idadi iyo hiyo ya kromosomu. Basi katika hatua ya kwanza ya uhai wake, binadamu ana kromosomu arubaini na sita (46).
    Kromosomu hizo zote ndizo humfanya mtu kuwa mkamilifu kwa kukadiria mambo mbalimbali adhimu. Kwa mfano, kukadiria kama kiumbe kitakuwa cha kike au cha kiume, mtu mweupe au mtu mweusi, mwerevu au wa wakia chache, mwenye nywele za singa au za kipilipili, atakuwa na damu ya namna gani, michoro ya vidole vyake itakuwa vipi na hata utu wake utakuwa wa namna gani katika siku za usoni.
    Elimu yote anayopata mtu kutoka kwa jamii na mazingira huweza tu kujenga juu ya yaliyokwisha kuanzilishwa na kromosomu katika yai lililorutubishwa tumboni.
    Haihalisi kabisa kufikiria kwamba huwa katika hali ya ukupe. La hasha! Yeye hujitegemea kwa vyovyote na ana upekee wake. Hatangamani na mama yake. Roho yake humdunda mwenyewe na damu yake ambayo huenda ikawa tofauti kabisa na ya mama yake, humtembea na kumpiga mishipani mwake. Isitoshe, yeye si mojawapo katika viungo vya mwili wa mama yake vinavyomdhibiti katika himaya yake ndogo.
    Amini usiamini, hapana binadamu hata mmoja ambaye amewahi kuwa sawa kimaumbile na mwingine na wala hatakuweko. Hata watoto pacha kutoka yai moja la mama hawawi sawa, lazima watofautiane. Si nadra kusikia mtu amepata ajali akahitaji msaada wa damu, na pakakosekana kabisa mtu hata mmoja kutoka jamaa yake wa kimwauni. Basi ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni.

    1. Ipe taarifa uliosoma anwani mwafaka
    2. Mwandishi ana maana gani anaposema ‘ngono yenye ufanisi’?
    3. Uchunguzi wa sayansi umekita mizizi imani gani ya kidini?
    4. Taja majukumu yoyote matano yanayotekelezwa na kromosomu
    5. Katika makala, elimu kutoka kwa jamii na mazingira yaelekea kuwa bure ghali. Kwa nini?
    6. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika makala:-
    (i) huwa katika hali ya ukupe…
    (ii) himaya
    (iii) hatangamani na mama yake

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)