Faragha ni muhimu kwa binadamu kwani huwa ndio wakati ambapo mtu atakuwa akitulia pekee mahali na huku akijiuliza ni mema mangapi ameyatenda...

      

Soma taarifa kisha fupisha kwa mujibu wa maswali yafuatayo.

Faragha ni muhimu kwa binadamu kwani huwa ndio wakati ambapo mtu atakuwa akitulia pekee mahali na huku akijiuliza ni mema mangapi ameyatenda siku hiyo, maovu mangapi ameyafanya, na kama siku hiyo ilikuwa ya manufaa au la.
Si binadamu wote ambalo wanapendelea kutumia wakati wao wa faragha kwa kupiga domo, nyumbani, kustawisha mabustani yao ya maua au mimea, au hata kuchukua kitabu au magazeti ya kusoma na kujifunza. Watu kama hawa huwa na fikira na mawazo mbalimbali juu ya umuhimu wa thamani ya wakati wa faragha. Watu kama hao utawakuta wakikusanyika katika makundi kwa matarajio ya kujinufaisha kwa mapato fulani au kujiingiza katika upigaji wa kamari. Wengine hunufaika wakasifu mafanikio yao ya siku ya mkusanyiko na baadhi yao ambapo hufanya mhanga wa michezo hii huibuka huku wakilaani na kuapiza bahati zao mbaya.
Kuna kundi jingine ambao hustahabu vilabu vya usiku kwa kujiliwaza au kujitumbuiza ili wapate kujituliza mawazo yao, wakayatafuta makali na kileo. Mwanzo wa ushirika kama huu huwa mzuri, watu huongea na kutoleana mawaidha yenye muafaka kiungwana kabisa. Lakini mara tu baada ya kuyakata makali haya kwa muda hivi, washiriki wake hupumbazwa na huanza kuyakata matindi mithili ya komba mpaka kiasi cha kubwata maneno ovyo ovyo na hatimaye kupoteza mbali fahamu. Ndipo kuruka kwa akili na kuanza zahama zenye kuonyesha utoto badala ya utu uzima. Kadiri makali hayo yanavyosiliwa kwa kuiva kwake, ndivyo wafuasi na mashabiki wake huyatumia kwa wingi na hata kuyaabudu, huyaabufu; huyabugia bila kujali uzito.
Na iwapo ndio kwanza wapokee mabunda yao, hakuna la kutia kikomo tafrija hizo ila uzito wa matendo ya ubadhirifu hujitokeza baada ya kurudi nyumbani, kulala fofofo na wazindukanapo siku ya pili yake ndipo wagundue walivyo taabani.
Mtindo wa matumizi ya faragha hutokea tangu mwanzo wa mazingira ya mtu; hivyo tangu utoto wake; tabia njema na zipasazo huhitajiwa kufunzwa. Sehemu kubwa ya mafunzo haya muhimu hutokana na malezi ya nyumbani chini ya uongozi wa mama na baba. Kama wasemavyo wahenga, mtoto akuavyo ndivyo alivyolelewa. Na mama mtu awe nyoka, hapana budi kuwa mwanawe naye atainuka kustahabu unyoke” wa mama yake. Hivyo ni wajibu wa wazazi kujenga mazingira yanayofaa kwa vizazi vya kesho kwa kuelekezwa namna yake. Ingewezekana himizo kubwa lingesisitizwa katika marekebisho ya tabia za wazazi kuwezesha manufaa yake. Ingewezekana, himizo kubwa lingesisitizwa katika marekebisho ya tabia za wazazi kuwezesha watoto kuiga mtindo au mitindo ya maisha yanayofaa. Kielezo chema ni kuwa na mzazi mwenye tabia njema kwa mtoto wake, rafiki zake na kwa jamii yake.
(a) Ni nini umuhimu wa faragha kwa binadamu kwa mujibu wa aya ya kwanza?
(b) Eleza jinsi watu wengine wanavyoharibu wakati wao wa faragha kwamambo ya upotovu
kwa kurejelea aya ya pili na ya tatu (maneno 30)
(c) Eleza mchango wa mzazi kwa mwanawe kuhusu matumizi bora ya wakati wa faragha.
Zingatia aya ya mwisho

  

Answers


Maurice
(a) – Ndio wakati mtu anaulia peke yake
-Anajisakaknakijiuliza mema mangapi amyatenda siku hiyo
- Maovu mangapi amayatenda
-Iwapo siku hiyo ilikuwa ya manufaa au la

(b) - Hukusanyika katika makundi na kucheza kamari
- Hukusanyika kwa madhumuni ya kupiga gumzo
- Wengine huenda vilabuni kujiliwaza na kujiburudisha kwa vileso


c) – Wazazi watoe maongozi bora
- Wawe vielelezo bora kwa wana wao
maurice.mutuku answered the question on October 4, 2019 at 12:31


Next: The diagram below represents a mammalian nephron.
Previous: Andika sentensi moja ukitumia kivumishi cha nomino.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions


  • Jadili sababu tano zinazofanya "sheng" isiwe lugha ya taifa.(Solved)

    Jadili sababu tano zinazofanya "sheng" isiwe lugha ya taifa.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana ya; i).Mkembe. ii).mkebe.(Solved)

    Eleza maana ya;
    i).Mkembe.
    ii).mkebe.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Uwezo wa kuyakumbuka mambo ni hazina kuu kutoka kwa mtu yeyote yule aliye hai. Uwezo huu wa kukumbuka ni mojawapo ya...(Solved)

    Soma taarifa kisha fupisha kwa mujibu wa maswali yafuatayo.

    Uwezo wa kuyakumbuka mambo ni hazina kuu kutoka kwa mtu yeyote yule aliye hai. Uwezo huu wa kukumbuka ni mojawapo ya shughuli changamano za ubongo. Ubongo wa mwanadamu hutekeleza shughuli hii kwa namna tatu. Kwanza ubongo hunasa jambo kisha
    huliihifadhi. Baadaye huanzisha mfumo wa kutoa kilicho hifadhiwa. Ubongo ukiathirika kwa
    namna yeyote katika moja wapo ya njia hizi, basi uwezo wa kuyakumbuka mambo huvurugika.
    Ingawa inaaminika kuwa uwezo wa kukumbuka hurithishwa toka kizazi kimoja hadi kingine, wataalamu wa maswala ya kiakili wanabaini kuwa uwezo huu unaweza kuimarishwa.
    Uimarishaji huu huhitajika mikakati madhubuti.
    Njia mojawapo ya kustawisha uwezo wa kukumbuka ni kupitia kwa lishe. Vyakula vilivyosheheni vitamini B vyenye amino asidi husaidia kuimarisha uwezo wa kukumbuka. Vyakula kama hivi ni mboga, nyama (hasa maini), bidhaaa za soya, matunda, maziwa, ,bidhaa za ngano, samaki, pamoja na mayai. Vyakula vingine muhimu katika ustawishaji huu ni vile vyenye madini ya chuma. Madini haya huwezesha usambazaji wa hewa katika ubongo kwa wepesi. Vyakula ambavyo vina madina haya ni mboga za kijani, mawele, ndengu, soya, matunda kama maembe, ufuta (simsim) pamoja na nyama, hasa maini na mayai.
    Ubongo wa mwanadamu aliye hai hufanya kazi kila wakati awe macho au amelala. Utendaji kazi wake huendeshwa na glukosi mwilini. Kwa hivyo, vyakula vyenye sukari hii ni muhimu kuliwa. Hata hivyo, lazima mtu awe mwangalifu na kuhakikisha kuwa mwili una kiwango cha sukari kisicho hatarisha maisha. Haya yanawezekana kwa kula vyakula vyenye nyuzinyuzi kama vile mboga na matunda.
    Njia ya pili ni kupiga marufuku vileo kama pombe na nikotini. Vileo hivi huathiri utaratibu wa kunasa, kuhifadhi na kutoa yaliyo ubongoni.
    Iwapo mtu ana tatizo la kuyakumbuka majina ya watu, ni muhimu kufanya mazoezi ya
    kusikiliza kisha kurudia majina hayo wakati wa mazungumzo. Ni bora kulihusisha jina na sura
    ya mtu. Kwa njia hii ubongo utanasa jina na kile kinacholengwa.
    Woga na kuvurugika kiakili ni mambo mengine tunayopaswa kuepuka kila wakati. Ni kawaida mtu kupata woga wakati anapokabili jambo asilokuwa na uhakika na matokeo yake kama mtihani au mahojiano. Lakini anapaswa kuwa makini. Woga huo usikiuke mpaka na kumvuruga kiakili. Vurugu hizi huathiri kilichohifadhiwa ubongoni na pia namna ya kukitoa.
    Halikadhalika, mwili wenye siha nzuri huhakikisha kuwa ubongo ni timamu. Wataalamu wengi wa siha wanakubali kuwa na mazoezi ya kunyoosha viungo hustawisha ubongo na hivyo kuhakikisha kuweko kwa uwezo wa kukumbuka mambo. Ni muhimu kuwa na taratibu ya kunyoosha viungo kila wakati. Fauka ya hayo, mazoezi ya kiakili, kama vile kusoma makala yanayovutia, kujaza mraba na michezo mingine kama mafumbo, vitenzi ndimi ni muhimu katika kustawisha uwezo wa kukumbuka.
    Jamii ya watu wenye uwezo kuyakumbuka mambo ni ya jamii iliyopiga hatua kimaendeleo. Ni jukumu la kila mmoja wetu kuimarisha uwezo wa kukumbuka kila wakati.

    a) Kwa maneno 60 – 65 fupisha mchango wa chakula katika uimarishaji wa uwezo wa
    kukumbuka.
    b) Fupisha aya tatu za mwisho kwa maneno 80 – 90

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Nyambua vitenzi vifuatavyo katika hali ulizopewa.(Solved)

    Nyambua vitenzi vifuatavyo katika hali ulizopewa.
    pic41020191417.png

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha vishazi huru na vishazi tegemezi katika sentensi ifuatayo. Nitaenda maktabani ingawa ninaumwa na kichwa.(Solved)

    Bainisha vishazi huru na vishazi tegemezi katika sentensi ifuatayo.
    Nitaenda maktabani ingawa ninaumwa na kichwa.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita, tumeshuhudia mabadiliko na maendeleo makubwa kuhusu vyombo vya habari nchini Kenya. Hapo awali, redio ndicho chombo...(Solved)

    Soma taarifa ifuatayo kisha ufupishe taarifa hii kulingana na maswali yanayofuata:-

    Katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita, tumeshuhudia mabadiliko na maendeleo makubwa kuhusu vyombo vya habari nchini Kenya. Hapo awali, redio ndicho chombo cha habari cha kipekee kilichotamalaki kote nchini. Familia nyingi ziliweza kumiliki chombo hiki. Runinga ilikuwa miliki ya wachache, hasa mabwenyenye. Sasa hivi, hata akina yahe nchini na mashambani wanamiliki chombo hiki.
    Runinga kama kifaa kingine chochote cha mawasilianao kina manufaa yake. Kwanza kabisa, ni nyenzo mwafaka ya kufundisha. Vipindi vinavyopeperushwa katika runinga huwa na mafunzo kemkem kwa mtu wa kila rika. Hali kadhalika, runinga huweza kuleta vipindi ambavyo huwafahamisha watu mambo yanayoendelea katika mazingira yao na duniani. Aidha, runinga ikitumika pamoja na michezo ya video huauni katika ukuzaji na ustawishaji ya kufundisha au kujielimisha. Michezo ya video, hasa ya kielimu huwafanya watu kujenga umakini pamoja na kuchua misuli ya ubongo na kuwafanya watu kuwa macho wanapofanya kazi.
    Fauka ya hayo, televisheni ni chemichemi bora ya kutumbuiza na kuchangamsha. Hakuna mtu asiyependa kuchangamshwa. Televisheni ni mojawapo wa vyombo mwafaka vya kutekeleza hayo kutokana na vipindi vyake. Uburudishaji huu hupatikana kwa urahisi majumbani mwetu.
    Vivyo hivyo, runinga hutumika kama nyenzo ya kuendeleza utamaduni, kaida na amali za jamii. Vingi vya vipindi vya runinga ni kioo ambacho huakisi mikakati na amali za jamii.
    Kwa upande mwingine, hakuna kizuri kisichokuwa na dosari. Licha ya manufaa yake, televisheni imedhihirika kuwa na udhaifu wake. Kwanza, baadhi ya vipindi vya runinga na video hujumuisha ujumbe usio na maadili, kama vile matumizi ya nguvu za mabavu, ngono za kiholela, lugha isiyo ya adabu, ubaya kimavazi na maonevu ya rangi, dini, jinsia , kabila na utamaduni. Si ajabu kuwa baadhi ya vijana wetu wanaiga baadhi ya mambo haya. Vijana wetu siku hizi wameingilia ulevi wa pombe na afyuni, ngono za mapema kabla ya ndoa na mavazi yanayowaacha takribani uchi wa mnyama. Wengi wamekopa na kuyaiga haya kutoka katika runinga. Ukiwauliza wafanyacho, watakujibu kuwa ni ustaarabu kwani wameupata katika runinga.
    Matumizi ya runinga na michezo ya video yasiyodhibitiwa huweza kuwa kikwazo cha mawasiliano bora miongoni mwa wanafamilia. Matumizi kama haya huwapa wanafamilia fursa ya kujitenga. Imedhihirika kuwa runinga haichangii kujenga uhusiano bora wa kijamii ukilinganisha na vyombo vingine vya burudani ambavyo hutoa nafasi ya watu kutangamana na kujenga uhusiano bora, televisheni haichangii haya. Badala yake, tajriba ya televisheni huwa na kibinafsi. Hali hii inapotokea katika kiwango cha familia, televisheni inaweza kutenganisha wazazi na watoto wao.
    Halikadhalika, runinga na video aghalabu hueneza maadili yasiyofaa. Mathalan, baadhi ya vipindi vya televisheni huendeleza hulka ya kuhadaa, ngono za kiholela, kuvunjika kwa ndoa, n.k. Hulka hizi zisizoendeleza maadili ya kijamii huchukuliwa kama zinazofaa na zinazofuatwa na waliostaarabika. Huu ni upotovu.
    Isitoshe, baadhi ya matangazo huhimiza matumizi ya madawa ya kulevya kama tembo na sigara. Vitu hivi vinapotangazwa, hupambwa kwa hila na udanganyifu mwingi ambao huwavutia vijana na watoto wengi. Si ajabu mtu anapouliza wanaoutumia vileo hivi walivyoanza, watajibu kutokana na athari za matangazo katika runinga na vyombo vingine.
    Utafiti umeonyesha kuwa vipindi vya runinga na video ni chanzo cha matumizi ya nguvu za mabavu miongoni mwa wanafunzi. Wazazi wengi huchukulia vibonzo katika televisheni kuwa vinalenga kuburudisha tu na havina ubaya wowote. Lakini ukweli ni kuwa vipindi vingi vya vibonzo hushirikisha matumizi ya hila na nguvu za mabavu. Haya huibusha hamu ya vijana na watoto huyaiga.
    Kwa hivyo, ni muhimu wazazi na jamii kutambua madhara ya televisheni. Utambuzi huu utawafanya waelekeze vijana na watoto jinsi ya kutumia televisheni na video ili kuepukana na madhara yake.
    Maswali
    (a) Ukitumia maneno 50-60, fupisha manufaa ya runinga
    (b) Fupisha hasara za runinga ukitumia maneno 70-80

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Toa maneno yenye maana sawa na haya. i. Izara ii. Anisi(Solved)

    Toa maneno yenye maana sawa na haya.
    i. Izara
    ii. Anisi

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha shamirisho na chagizo katika sentensi hii. Mbuga za wanyama zitapata wageni wengi mwaka ujao.(Solved)

    Bainisha shamirisho na chagizo katika sentensi hii.
    Mbuga za wanyama zitapata wageni wengi mwaka ujao.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi. Atanishughulikia vizuri.(Solved)

    Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi.
    Atanishughulikia vizuri.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Usawa wa wanadamu upo kimaumbile – maumbile ya mtu kamwe hayatakosewa na yale ya mnyama wa mwituni. Lakini fikira, tabia,...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali:

    Usawa wa wanadamu upo kimaumbile – maumbile ya mtu kamwe hayatakosewa na yale ya mnyama wa mwituni. Lakini fikira, tabia, kimo, uwezo na mahitaji huwa tofauti kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Kwa mintarafu hii yapasa wakufunzi na wazazi kuwapa watoto wao widhaa mapema ili wachague kwa wakati unaofaa kazi watakayoifanya maishani.
    Watoto wanapopelekwa chuoni, wazazi wao huukilia kuwasomesha hadi kiwango fulani cha masomo kisha wajitafutie kazi ambayo itawapa masurufu na pesa za shughuli zingine maishani.
    Katika nchi yetu tangu tupate uhuru mtindo wa kutoa kazi umekuwa ni ule wa kuchukua watu waliofaulu mitihani ya viwango fulani na kuwapa kazi moja kwa moja. Mwenendo huu wa kuajiri watu kazi umeendelea muda mrefu lakini sasa yamkinika utasitishwa na njia mpya kufuatwa. Sababu ya kufanya hivyo ni kuwa nafasi za kazi zimekuwa finyu sana. Kabla na punde baada ya uhuru nafasi hizo zilipatikana kila mahali. Nyingi ya hizo ziliachwa wazi na wageni walioihama nchi hii tulipojitawala. Siku hizi wanafunzi wanaokomea darasa la saba, kidato cha pili na hata cha nne huwa hawazioni ahadi za kupata kazi za madaraka fauka ya kazi yoyote. Wanaoiona tabasamu ya kazi mbele yao ni wale wanaotasawari masomoni wakifuata taaluma fulani.
    Tatizo la kazi laeleweka vema kwa serikali na ni kwa ajili hii serikali imemtasulia kila mwananchi kuwa wakati wa kuania kazi za utanashati umetimiuka. Wakati uliopo ni wakati wa kujifunga vibwebwe kisaki na kuchapa kazi zile ambazo hadi sasa zafikiriwa kazi chafu na zisizofaa wasomi. Dhana kama hiyo ni ya kibwanyenye, na ubwanyenye hauji ila kwa sulubu. Usemapo kuna kazi nzuri na mbaya huwa unazusha maswali mengi. Utatakiwa ueleze kinaganaga kazi nzuri au mbaya kwa nini? Kazi huwa nzuri kwa upande wa tija au kwa upande wa wepesi wake? Kujibu maswali ya namna hii kutahitaji wekevu mwingi, waima mtesi ataonekana dufu.
    Zipo kazi aina mbili. Ipo kazi ya kuajiriwa na ya kujiajiri. Kazi ya kujiajiri kwa kulinganishwa huonekana ngumu na yenye matatizo mengi mwanzoni. Lakini itakubalika pato lake ni kubwa zaidi ikishapata msingi imara. Msingi imara huwekwa kwa juhudi za mwanzoni zikiambatana na ujasiri. Mtu asiyejasiri kutenda tendo lolote maishani ni sawa na yule asiyejua atokako na kule aendako; yuaishi kungozwa. Ardhi ni thawabu, tena thawabu tunu. Ukiwa na kipande cha ardhi ifaayo kwa kilimo ufakiri ukikutawala ni wewe mwenyewe kupenda: la sivyo ufa umo ubongoni unaohitaji bwana mganga

    (a) Bila kupoteza maana iliyokusudiwa na mwandishi wa taarifa, fupisha aya ya kwanza
    na ya pili. maneno 60-70)

    (b) Kwa kuzingatia aya mbili za mwisho. Eleza mambo muhimu yanayoshughulikiwa na mwandishi. (maneno (50-60)

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi ifuatayo katika msemo halisi. Mama alimwuliza mwanawe alikochelewa na kisha akamtahadharisha kuwa haikuwa tabia njema kwa mtoto wa kike kama yeye kuzoea kutembea usiku.(Solved)

    Andika sentensi ifuatayo katika msemo halisi.
    Mama alimwuliza mwanawe alikochelewa na kisha akamtahadharisha kuwa haikuwa tabia njema kwa mtoto wa kike kama yeye kuzoea kutembea usiku.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Usafiri ni upelekezi wa watu na bidhaa au mizigo kutoka mahali pamoja hadi mahali pengine. Tuseme kutoka kituo A na kuenda...(Solved)

    Soma taarifa inayofuata kisha ujibu maswali yaliyoulizwa

    Usafiri ni upelekezi wa watu na bidhaa au mizigo kutoka mahali pamoja hadi mahali pengine. Tuseme kutoka kituo A na kuenda kituo B.
    Katika ulimwengu wa leo, watu na bidhaa husafirishwa barabarani kwa mabasi au motokaa za kila aina au kwa kutumia magari moshi yanayopita juu ya reli, au meli zinazopita majini, kadhalika, usafiri unaweza kufanyiwa hewani.

    Hivyo, hali haikuwa hivyo zamani. Usafiri uliojulikana sana kale ni usafiri kwa miguu. Watu waliposafiri kutoka eneo moja hadi jingine walilazimika kufanya hivyo kwa miguu. Kadhalika, watu waliposafirisha mizigo mizito kutoka eneo moja hadi nyingine, iliwabidi kuibeba mizigo hiyo wao wenyewe. Mpaka leo usafiri huu upo.
    Wanyama vilevile walitumiwa kama njia moja ya usafirishaji. Huku Afrika ya mashariki kulitumika wanyama wengine kama vile punda. Punda ni mnyama anayependwa sana kwa sababu anaweza kuenda mwendo mrefu pasipo na kunywa maji. Mpaka leo, mnyama huyo hutumika sana na wamaasai, wagala, warendile na wengine.
    Mnyama mwingine aliyetumika sana, na mpaka leo anaendelea kutumika ni ngamia. Ngamia anafaa sana katika usafiri wa jangwani. Kwato za ngamia huweza kusafiri kwa urahisi jangwani ama popote penye mchanga mwingi kwa sababu kwato zake hazizami kwenye mchanga. Isitoshe ngamia wanaweza kwenda mwendo mrefu bila maji au chakula huku wakitegemea mafuta yaliyohifadhiwa kwenye nundu zao.
    Katika ulimwengu wa kisasa, binadamu amepiga hatua kubwa sana katika masuala ya usafiri. Baadhi ya maendeleo hayo ni ya kustaajabisha. Kwa mfano, binandamu anaweza kuruka kwa kutumia vyombo vya angani kwenda kwenye anga za mbali. Katika karne iliyopita binadamu anaweza kuruka kwa kutumia vyombo vya angani kwenda kwenye anga za mbali. Katika karne iliyopita binadamu amefika mwezini kwa kutumia vyombo hivyo. Kuna tetesi kwamba sasa anajaribu kuzizuru sayari zilizoko mbali na ardhi.
    Ama kwa hakika, usafiri bora in kipimo kimojawapo cha maendeleo ya nchi yoyote katika ulimwengu wa sasa. Bila njia ya kisasa za usafiri, baadhi ya mambo yanayofanyika katika nchi zetu hayangefanyika.

    (a) Katika habari hii, punda na ngamia wana sifa gani muhimu zinazowawezesha kutumiwa
    kwa usafirishaji? (maneno 30-40)
    (b) Kwa mujibu wa taarifa, usafiri wa zamani unatofautiana vipi na ule wa siku hizi?
    (maneno 40-50)

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Nchi nyingi za ulimwengu wa tatu huathirika na biashara ya kimataifa.Biashara hiyo inaweza kuwa inafanya kwa uagizaji ama uuzaji...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali

    Nchi nyingi za ulimwengu wa tatu huathirika na biashara ya kimataifa.Biashara hiyo inaweza kuwa inafanya kwa uagizaji ama uuzaji wa bidhaa za nchi nyingine.
    Biashara ya kimataifa ina umuhimu mkubwa. Kwanza, inawezesha nchi kupata bidhaa ambazo haitengenezi mbali na kusaidia kuwepo na uhusiano kati ya nchi mbalimbali. Uhusiano huu huiwezesha nchi kupata bidhaa kwa bei rahisi kuliko ambavyo ingekuwa kama zingetengenezwa kwao, hasa ikiwa nchi inayohusika haina malighafi yanayohusika katika utengenezaji wa bidhaa hizo. Pia husaidia wakati nchi imekumbwa na dharura au majanga kwani itaauniwa na nchi nyingine ingawa hali kama hii haihakikishwi, ushirikiano huu vile vile huchochea upatikanaji wa nafasi za kazi kwa wengi.
    Kwa sababu za kushughulikia utengenezaji wa bidhaa na utoaji huduma nyingine kutokana na uzoefu wa muda na kuwepo raslimali, nchi huwa na uzoefu fulani. Ni kwa sababu hii nchi inawezeshwa kupata pesa za kigeni na kuuza bidhaa za ziada.
    Hata hivyo kuna matatizo yanayozikumba nchi za kiafrika katika biashara hii. Kwanza, biashara ya aina hii hutatiza viwanda vichanga katika nchi zinazoendelea kwa ushindani usio sawa. Ajabu ni kwamba nchi zilizoendelea zimetumia bishara hii ‘kutupa’ bidhaa za hali ya chini ama zenye athari kwa hali za kijamii.Urafiki haukosi. Ikiwa nchi inategemea uagizaji wa bidhaa, haitaweza kuikosea ama kuhitilifiana na nchi ambayo inategemea, hivyo kuathiri uhuru wa nchi kama hiyo.
    Hata hivyo, nchi mbalimbali zimeweka mikakati ya kulinda viwanda kutokana na athari ya biashara kama hii. Baadhi zimeweka ushuru wa juu kwa bidhaa zinazoagizwa utoka nje kwa wasio washirika wa kibiashara. Licha ya hayo, baadhi ya bidhaa zinazonuiwa kwa nje kwa matumizi ya kielimu, utafiti wa kisayansi nabidhaa za maonyesho huagizwa bila ushuru huo. Wakati mwingine ni benki kuu ndiyo hutoa leseni kwa niaba ya serikali kama njia ya kudhibiti bidhaa kutoka nje. Njia nyingine ya kuvisaidia viwanda nchini ni kuuza bidhaa kwa njia ya kuvipunguzia ushuru, usafirishaji nafuu na kuvipa ushuru.
    Serikali nyingine huhakikisha kuwa ni bidhaa kiasi fulani tu ambazo zinaweza kuagizwa kwa kipindi fulani. Kwa mfano, kuna idadi fulani ya magari kutoka nje yanayoweza kuagizwa kuja Kenya kwa mwaka mmoja. Hata hivyo, wakati mwingine, serikali husitisha uagizaji wa bidhaa kama vile dawa, sinema, maandishi ya kisiasa na vitabu kutoka nje; bidhaa ambazo zinachukuliwa kuwa hatari kwa nchi. Licha ya matatizo haya, biashara imekuwepo na inaendelea kujiimarisha.
    Maswali
    (a) Kwa mujibu wa mwandishi wa makala haya, biashara ya kimataifa itaendelea kujiimarisha.
    Eleza (maneno 40-50)
    (b) Dondoa hoja muhimu zinazojitokeza katika aya mbili za mwisho. (maneno 40-50)

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Akifisha sentensi ifuatayo. Karibu mgeni akaitika mwenyeji mbona huingii na mlango u wazi stareheni kwenye viti ahsante wakajibu..(Solved)

    Akifisha sentensi ifuatayo.
    Karibu mgeni akaitika mwenyeji mbona huingii na mlango u wazi stareheni kwenye viti ahsante wakajibu..

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana ya nahau zifuatazo: i) Furaha ghaya ii) Maneo yalimkata maini.(Solved)

    Eleza maana ya nahau zifuatazo:
    i) Furaha ghaya
    ii) Maneo yalimkata maini.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • MENO YA BINADAMU Kila mara tunapokula, meno yetu huuma, kutafuna na kusaga chakula tunachokula. Meno yanatuwezesha kukivunja chakula ili kuwezesha mwili wetu kukitumia. Ili mwili uweze...(Solved)

    MENO YA BINADAMU

    Kila mara tunapokula, meno yetu huuma, kutafuna na kusaga chakula tunachokula. Meno yanatuwezesha kukivunja chakula ili kuwezesha mwili wetu kukitumia. Ili mwili uweze kukitumia chakula hicho, pana vitu fulani vinavyokifanyia chakula hicho kazi mpaka kikaweza kuingia kwenye mwili wenyewe. Hivi hujulikana kama vimeng’enya. Binadamu ana meno ya aina nne kuu. Kwanza, kuna meno ya mbele au makato ambayo kazi yake ni kuuma au kukata chakula. Haya yanasaidiana na mengine yanayojulikana kama michonge; yanakata pia lakini yako sehemu ya nyuma. Michonge hufuatwa na meno mengine yanayosaga chakula na ambayo hujulikana kama masagego. Masagego hufanya kazi na meno mengine yajulikanayo kama magego. Kazi ya aina hizi mbili za meno ni kutafuna na kusaga chakula kabisa kabla ya kukimeza. Idadi ya meno ya mtu mzima ni thelathini na mbili. Bila ya kuwa na meno mazuri, binadamu hukabiliwa na matatizo makubwa wakati wa kula. Meno huweza kuharibika kwa sababu ya kutopigwa mswaki vizuri mara kwa mara. Ili kuhakikisha kuwa meno yetu ni mazuri, pana umuhimu wa kudumisha afya nzuri ya meno. Kila baada ya kulala, lazima tuhakikishe tumeyapiga mswaki vizuri bila ya papara ili kuondoa mabaki ya chakula yanayoweza kuwa chanzo cha viini vinavyoharibu meno. Pili, lazima tuhakikishe kuwa hatuharibu ufizi wa meno,yaani ile nyama inayoshikilia meno hasa kwa vijiti katikati ya meno baada ya kula. Afya ya meno ni muhimu ili kuhakikisha kuwa meno yetu yanadumu na kuendelea kutufaidi katika uhai wetu.

    (a) Kwa nini ni muhimu kudumisha usafi wa meno?
    (Tumia maneno yasiyozidi 25)
    (b) Fupisha taarifa uliyosoma. (Tumia maneno yasiyozidi 80).

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Umaskini ni tatizo sugu katika jamii. Binadamu wengi hujikuta katika hali hii kwa sababu hawakubahatika kusoma. Baadhi yao huenda...(Solved)

    Soma taarifa hii kisha ujibu maswali

    Umaskini ni tatizo sugu katika jamii. Binadamu wengi hujikuta katika hali hii kwa sababu hawakubahatika kusoma. Baadhi yao huenda walijaribu kusoma wakashindwa mapema kujipandisha kielimu. Ukosaji wa elimu huchangia sana katika kukuza ukata. Elimu huweza mtu kupata tonge kwa kujipatia kazi za kumwezesha kuyakidhi mahitaji ya maisha. Hali kadhalika, elimu humsaidia binadamu kupata maarifa mengi ya kutendea shughuli zake za kimaendeleo. Kwa mfano, kama ni wakulima wanaweza kutumia pembejeo zifaazo ili kuboresha uzalishaji wa mazao. Wakulima wenye elimu hawatapendelea njia duni za kuendeleza kilimo kama vile kutumia visagilima na mbinu nyingine za kijadi. Badala yake watatumia njia za kisasa za kuvunia mazao yao.
    Umaskini mwingine huwa mwiba wa kujichoma. Baadhi ya watu ni mikunguni. Kulaza damu kwao kunawafanya kuwa wategemezi katika familia na jamii kwa jumla. Kwa vile hawajazoea kuinamia cha mvunguni, hata wakifunzwa kuchakura hawawezi. Ili kujaribu kuutibu uwele wao na ufukara baadhi yao hutafuta njia za mkato kama vile upwekuzi wa vitu vya wale waliojitahidi. Wakifanikiwa huweza kufurisha vibindo vyao. Hata hivyo mkono mrefu wa walinda usalama ukiwakumbatia wao hubakia kusagika kwa dhiki isiyomithilika ndani ya magereza.
    Majanga ya kimaumbile kama vile mitetemeko ya ardhi, mikurupuko ya maradhi hatari, moto, ukame na mafuriko huchangia na kuzidisha umaskini. Matukio hayo yakiandama kidindia watu wengi huhasirika. Licha ya mali nyingi kupotea, manusura huachwa wakiwa maskini hohehahe. Matumizi yao hupotea kwani wengi huhitajika kuanza maisha upya.
    Vijana ni nguzo muhimu katika maendeleo ya nchi yoyote ile. Endapo watajiingiza katika uraibu wa dawa za kulevya, wataathirika wao wenyewe na jamii kwa jumla. Pamoja na kuwa vijana hawa hufuja pesa nyingi katika ununuzi wa dawa hizi, dawa zenyewe huwadhoofisha na kuwapoka nguvu za kushiriki katika uzalishaji mali. Kutokana na hali hii,umaskini hupaliliwa na kushamiri zaidi.
    Umaskini huzua matatizo mbalimbali katika jamii. Ufukara huchachawiza juhudi za serikali za kuwapa raia wake mahitaji ya kimsingi kama vile huduma za afya. Pia umaskini husababisha maovu mbalimbali ya kijamii kama vile mauaji na ukahaba.
    Baadhi ya wanajamii huona kwamba njia ya kipekee ya kukabiliana na changamoto zinazosababishwa na hali ya ulitima ni kupitia kwa biashara haramu. Hali hii huchochea zaidi kudorora kwa maadili ya kijamii.
    Mataifa mbalimbali ulimwenguni yamezua mikakati mahsusi ya kukabiliana na umaskini. Baadhi ya mataifa yamebuni utaratibu maalum wa kupunguza mwanya mkubwa uliopo kati ya matajiri na maskini. Mojawapo ya mipango hiyo ni kupandisha viwango vya kodi inayotozwa wenye mishahara minono na wafanyibiashara wenye pato kubwa. Aidha huduma za burudani hutozwa kodi ya kiwango cha juu. Kupitia kwa kodi hizo, na njia nyinginezo, serikali za nchi hizo hupata pesa za kuwahudumia maskini.
    Mataifa yanayoendelea yanaweza kuwakwamua wananchi kiuchumi kwa kuwapa wahitaji mitaji ya kuanzisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo. Mifano ya miradi hiyo ni viwanda vya ‘Jua kali’, ususi wa vikapu na uchongaji wa vinyago. Hali kadhalika, serikali inaweza kuwatafutia masoko ya nje wafanyi biashara wadogo wadogo. Aidha, serikali inaweza kupunguza ushuru kwa bidhaa zinazoagizwa na masoko ya nje wafanyibiashara wa aina hiyo. Mathalan, ushuru unaotozwa nguo kuukuu zinazoingizwa nchini ukipunguzwa, wauzaji wa nguo hizi watafaidika zaidi na hali ya umaskini itaendelea kupungua.
    Sehemu za mashambani ni mhimili mkubwa wa uchumi. Ingawa kumekuwa na juhudi za kuzistawisha sehemu hizi kwa kusambaza huduma za umeme na maji kwa gharama nafuu, bado hali haijawa ya kuridhirisha. Ili kuimarisha sehemu hizi na kukabiliana vilivyo na tatizo la umaskini, hatuna budi kusambaza huduma hizi hasa katika sehemu kame. Sehemu hizi zikipata maji, kilimo chenye natija kitaendelezwa na umaskini utakuwa karibu kuzikwa katika kaburi la sahau. Ikiwa tutazitekeleza sehemu hizi, vijana wanaoweza kusistawisha watahamia mjini kutafuta maisha ‘bora’. Hali hii itazidisha msongomano wa watu mjini.
    Umaskini ni nduli ambaye lazima aangamizwe ima fa ima. Vijana hawana budi kubadili mtazamo wao hasa kuhusu kazi za mashambani na kujitahidi kuimarisha kilimo. Fauka ya hayo, mifumo mwafaka ya elimu ibuniwe ili kukidhi mahitaji ya kiuchumi ya taifa. Badala ya kuhimiza elimu ya kinadharia, elimu tekelezi isisitizwe zaidi ili wale wanaokosa kazi za kiafisi waweze kujiajiri katika kazi za kiufundi. Ukusanyaji wa ushuru uimarishwe zaidi. Hali ya usalama iendelee kustawishwa ili kuzidi kuwavutia wawekezaji, na hivyo kubuni nafasi zaidi za kazi.


    (a)Kulingana na kifungu ‘umasikini ni hali inayoletwa na udhaifu wa mtu binafsi’. Jadili
    (maneno 30-40)
    (b)Jamii ina uwezo wa kukabiliana na hali ya umaskini inayowakumba raia wake. Thibitisha
    kwa mujibu wa kifungu (maneno 40-50)

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Badilisha sentensi ifuatayo iwe mazoea kwa kutumia "O" rejeshi. Malipo ambayo anapewa ni yale ambayo yanaridhisha.(Solved)

    Badilisha sentensi ifuatayo iwe mazoea kwa kutumia "O" rejeshi.
    Malipo ambayo anapewa ni yale ambayo yanaridhisha.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Andika wingi wa sentensi zifuatazo; i) Sokwe aliukwea mti huo kwa kasi.ii) Mshale mkali ulitumiwa kumwua samba.(Solved)

    Andika wingi wa sentensi zifuatazo;
    i) Sokwe aliukwea mti huo kwa kasi.
    ii) Mshale mkali ulitumiwa kumwua samba.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Tumia neno "vile" kama. i) Kivumishi … ii) Kiwakilishi iii) Kielezi(Solved)

    Tumia neno "vile" kama.
    i) Kivumishi …
    ii) Kiwakilishi
    iii) Kielezi

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)