Bainisha aina za virai vilivyopigiwa mistari. Uchochole wa kijinsia umepigwa marufuku na kiongozi mwenye msimamo dhabiti mno.

      

Bainisha aina za virai vilivyopigiwa mistari.
Uchochole wa kijinsia umepigwa marufuku na kiongozi mwenye msimamo dhabiti mno.

  

Answers


Kavungya
Wa kijinsia – RH ( Kirai kihusishi)
Kavungya answered the question on October 4, 2019 at 12:51


Next: Tunga sentensi yenye muundo ufuatao KN(N+S)+KT(T+E+E)
Previous: Kanusha sentensi ifuatayo; Angalimpata babu yangu angalimpeleka hospitalini.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions


  • Tunga sentensi yenye muundo ufuatao KN(N+S)+KT(T+E+E)(Solved)

    Tunga sentensi yenye muundo ufuatao
    KN(N+S)+KT(T+E+E)

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Iandike sentensi ifuatayo upya katika hali yakinishi. Hapo napo sipo nitakapo. (Solved)

    Iandike sentensi ifuatayo upya katika hali yakinishi.
    Hapo napo sipo nitakapo.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Imesemwa na kurudiwa tena kwamba, iwapo tuna maono ya kujiondoa katika umaskini wa kupindukia, ni lazima tukipe kilimo umuhimu. Zaidi...(Solved)

    Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali kulingana na maagizo

    Imesemwa na kurudiwa tena kwamba, iwapo tuna maono ya kujiondoa katika umaskini wa kupindukia, ni lazima tukipe kilimo umuhimu. Zaidi ya wakenya milioni kumi wamo katika hatari ya kufa njaa katika maeneo mbali mbali kwa sasa kufuatia uhaba wa chakula nchini.
    Kiini kikubwa cha njaa hiyo ni mapuuza ya muda mrefu katika sekta ya kilimo. Imesahaulika kuwa karibu asilimia sabini na tano ya wakenya wanategemea kilimo kwa chakula na mapato ya kifedha kila siku. Kilimo hutoa karibu robo tatu ya nafasi za kazi kwa wananchi na pia huletea serikali karibu robo ya mapato yake kutokana na mauzo ya mazao katika mataifa ya nje.
    Wataalamu wa maswala ya zaraa wanaeleza kuwa pato la nchi linalotokana na kilimo huangamiza njaa mara nne zaidi ya mapato yanayotokana na shughuli nyinginezo za kiuchumi. Hiyo ni kwa sababu shughuli za kilimo hulenga kuzalisha vyakula moja kwa moja.
    Imebainika kuwa, katika mataifa mengi yanayostawi, asilimia sabini na tano ya wananchi huishi katika maeneo ya mashambani na idadi hii hutegemea kilimo kujimudu kimaisha ilhali hapa Kenya ni asilimia nne pekee ya bajeti inayowekezwa katika kilimo. Kwa wakati huo, ushuru unaotozwa bidhaa za kilimo katika maeneo haya umebainika kuwa mkubwa. Hii imepelekea uwekezaji katika kilimo kupungua na hivyo kuchangia kukithiri kwa baa la njaa.
    Wakati umewadia kwa serikali za Afrika na wapangaji wa masuala ya uchumi kuweka juhudi maradufu katika kushabikia kilimo ili kumaliza njaa na umaskini. Kuna haja ya kuwajulisha, kuwahimiza na kuwaelimisha wakulima wa mashamba madogo madogo kuhusu mihimili ya zaraa kama vile uzalishaji wa matunda na mboga, ufugaji wa ndege, samaki na ng’ombe mbali na kuweka mikakati ya kuanzisha nafasi za kazi katika sekta ya kilimo.
    Serikali itafikia lengo hili iwapo itaanza kufadhili kilimo, kupunguza gharama za pembejeo za kilimo, kuweka sera zinazodhibiti uuzaji na ununuzi wa vyakula hasa baina ya mataifa na kuongeza sehemu ya bajeti inayotengewa kilimo. Bila hilo hatutakuwa na lingine bali kukimbilia mataifa yaliyostawi kuomba misaada ili kuwanusuru raia wetu kutokana na ghadhabu ya njaa.
    (a) Fupisha aya mbili za mwanzo (maneno 50 -55)

    (b) Bila kubadili maana, fupisha aya mbili za mwisho (Maneno 55-60)

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Mafuta yanayopatikana kwenye fukwe za bahari, moshi wa magari, takataka na bidhaa nyinginezo zinazotupwa hapa na hapa ni vichafuzi vya mazingira.(Solved)

    Mafuta yanayopatikana kwenye fukwe za bahari, moshi wa magari, takataka na bidhaa nyinginezo zinazotupwa hapa na hapa ni vichafuzi vya mazingira. Vichafuzihuadhiri afya zetu na kuathiri wanyama na mimea. Wanadamu wanayachafua mazingira yao kwa kila aina ya bidhaa mbaya za kikemikali zinazotoka viwandani mwa kawi / nguvu. Bidhaa hizo ni matokeo ya maisha ya siku hizi anayoishi binadamu. Licha ya ukweli huu, ni muhimu kujua kuwa uchafuzi wa mazingira haukuanza leo. Miaka na miaka iliyopita, viwanda vimekuwa vikitoa mawingu makubwa ya moshi yenye sumu. Hata hivyo, uchafuzi wa mazingira umeongeza mara dufu kutokana na kuongezeka kwa viwanda. Uchafuzi umesambaa ardhini, kwenye anga na majini. Msambao huu unapatikana katika pembe zote za ulimwengu wetu. Je, kuna aina zipi za uchafu? Kwanza, kuna uchafu wa hali ya anga. Huko juu angani kuna tabaka linalojulikana kama ozoni. Tabaka hili ni aina ya gesi ya oksijeni na linaunda kinga fulani dhidi ya miale ya jua. Miale hiyo ya jua huweza kusababisha saratani ya ngoziinapomfikia binadamu. Hata hivyo, uchafu wa mazingira unaelekea kuliathiri tabaka hili vilevile baadhi ya kemikali zinazotumiwa katikajokofu au kwenye mikebe ya marashi ya kupulizia na upakiaji bidhaa, huuharibifu ukanda huo.Uchafu mwingine ni uchafuzi wa kiajali. Uchafuzi huu hutokea bila binadamu kukusudia. Mfano mzuri ni meli inayovuja mafuta baharini. Mafuta haya huwaathiri na kuwaua wanyama wanaoishi baharini kama samaki na ndege na hata kuyaharibu mazingira yenyewe. Miji mikubwa hukumbwa na uchafuzi mwingine unaohusiana na kuwako kwa idadi kubwa ya magari. Magari haya hutoa moshiunaochanganya gesi ambazo huungana na nyingine zinazoletwa na viwanda vikubwa. Mchanganyiko huu unapoungana na maji , husababisha mvua ya asidi. Mvua hii huweza kuiua mimea , kuathiri majengo na hata kuwaua wanyama wa pori ambao huenda wakayatumia maji hayo. Magari hayo hutoa moshi uliochanganyika na madini aina ya risasi ambayo huweza kuathiri siyo tu mazingira bali pia mfumo wa akili wa binadamu. Uchafuzi mkubwa ni utupwaji ovyo wa takataka. Fauka ya hayo, watu hufukia ardhini takataka ambazo huweza kuwa na matokeo mabaya kwa sababu ya kupenyeza kwenye udongo na maji yanayotumiwa na watu na mimea. Kila siku tunatupa takataka bila kujali wala kukubali. Takataka hizi ni kama makopo, mifuko ya plastiki, mabaki ya sigara au maganda ya matunda. Baadhi ya takataka ni hatari kwa wanyama na nyingine huweza pia kusababisha majanga kama moto. Aidha, hufanya mazingira yaonekane machafu.Sote tunajukumu kubwa la kuchangia kupunguza uchafu wamazingira. Kwanza, kuelimisha na kutambua umuhimu wa usafi wa mazingira yetu . Tunapaswa kutia takataka zetu kwenye vijalala maalum au mahali tunapoweza kuzichoma na kuziteketeza. Tuhakikishe tunatunza vitu kama mifuko, chupa na kadhalika ambavyo huweza kuundwa upya na kutumika tena. Hali kadhalika, katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwepo na juhudi za kuwahimiza wenye magari kutumia mafuta ya gari ambayo hayana madini ya risasi. Kwa njia hii, tutasaidia kuyaboresha mazingira yetu. Vilevile pana umuhimu wa kutilia mkazo utumiaji wa bidhaa ambazo zinaweza kuoza na kuvunjikavunjika au kusagika na kuwa sehemu ya udongo. Hatua ya kwanza ya kupambana na uchafuzi wa mazingira ni kujielimisha na kuwajibika. Kila mmoja akitoa mchango wake, tutafanikiwa. Kumbuka: kinga na kinga ndipo moto uwakapo.
    a) Ongezeko la viwanda limechangiaje uchafuzi wa mazingira ?
    b) Tabaka la ozoni huathiriwaje na uchafuzi?
    c) Eleza athari zozote tatu za kutotunza mazingira.
    d) Kwa nini miji mikubwa hukumbwa na uchafuzi kuliko sehemu nyingine?
    e) Eleza nui mbili za uchafuzi wa mazingira zilizotajwa katika kufungu hiki.
    f) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika kifungu.
    i) Msambao -
    ii) Makopo -
    iii) Kinga –

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Tumia maneno yafuatayo katika sentensi moja ili kubainisha tofauti zao kimaana; i) Chuuza ii) Chuza(Solved)

    Tumia maneno yafuatayo katika sentensi moja ili kubainisha tofauti zao kimaana;
    i) Chuuza
    ii) Chuza

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Eleza tofauti kati ya ama za vielezi vifuatavyo; i) Vielezi vya namna mfanano na; Vielezi vya namna hali. ii) Tunga sentensi mbili tofauti ukitumia vielezi vya hapo...(Solved)

    Eleza tofauti kati ya ama za vielezi vifuatavyo;
    i) Vielezi vya namna mfanano na;
    Vielezi vya namna hali.
    ii) Tunga sentensi mbili tofauti ukitumia vielezi vya hapo juu.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi moja ukitumia kivumishi cha nomino.(Solved)

    Andika sentensi moja ukitumia kivumishi cha nomino.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Faragha ni muhimu kwa binadamu kwani huwa ndio wakati ambapo mtu atakuwa akitulia pekee mahali na huku akijiuliza ni mema mangapi ameyatenda...(Solved)

    Soma taarifa kisha fupisha kwa mujibu wa maswali yafuatayo.

    Faragha ni muhimu kwa binadamu kwani huwa ndio wakati ambapo mtu atakuwa akitulia pekee mahali na huku akijiuliza ni mema mangapi ameyatenda siku hiyo, maovu mangapi ameyafanya, na kama siku hiyo ilikuwa ya manufaa au la.
    Si binadamu wote ambalo wanapendelea kutumia wakati wao wa faragha kwa kupiga domo, nyumbani, kustawisha mabustani yao ya maua au mimea, au hata kuchukua kitabu au magazeti ya kusoma na kujifunza. Watu kama hawa huwa na fikira na mawazo mbalimbali juu ya umuhimu wa thamani ya wakati wa faragha. Watu kama hao utawakuta wakikusanyika katika makundi kwa matarajio ya kujinufaisha kwa mapato fulani au kujiingiza katika upigaji wa kamari. Wengine hunufaika wakasifu mafanikio yao ya siku ya mkusanyiko na baadhi yao ambapo hufanya mhanga wa michezo hii huibuka huku wakilaani na kuapiza bahati zao mbaya.
    Kuna kundi jingine ambao hustahabu vilabu vya usiku kwa kujiliwaza au kujitumbuiza ili wapate kujituliza mawazo yao, wakayatafuta makali na kileo. Mwanzo wa ushirika kama huu huwa mzuri, watu huongea na kutoleana mawaidha yenye muafaka kiungwana kabisa. Lakini mara tu baada ya kuyakata makali haya kwa muda hivi, washiriki wake hupumbazwa na huanza kuyakata matindi mithili ya komba mpaka kiasi cha kubwata maneno ovyo ovyo na hatimaye kupoteza mbali fahamu. Ndipo kuruka kwa akili na kuanza zahama zenye kuonyesha utoto badala ya utu uzima. Kadiri makali hayo yanavyosiliwa kwa kuiva kwake, ndivyo wafuasi na mashabiki wake huyatumia kwa wingi na hata kuyaabudu, huyaabufu; huyabugia bila kujali uzito.
    Na iwapo ndio kwanza wapokee mabunda yao, hakuna la kutia kikomo tafrija hizo ila uzito wa matendo ya ubadhirifu hujitokeza baada ya kurudi nyumbani, kulala fofofo na wazindukanapo siku ya pili yake ndipo wagundue walivyo taabani.
    Mtindo wa matumizi ya faragha hutokea tangu mwanzo wa mazingira ya mtu; hivyo tangu utoto wake; tabia njema na zipasazo huhitajiwa kufunzwa. Sehemu kubwa ya mafunzo haya muhimu hutokana na malezi ya nyumbani chini ya uongozi wa mama na baba. Kama wasemavyo wahenga, mtoto akuavyo ndivyo alivyolelewa. Na mama mtu awe nyoka, hapana budi kuwa mwanawe naye atainuka kustahabu unyoke” wa mama yake. Hivyo ni wajibu wa wazazi kujenga mazingira yanayofaa kwa vizazi vya kesho kwa kuelekezwa namna yake. Ingewezekana himizo kubwa lingesisitizwa katika marekebisho ya tabia za wazazi kuwezesha manufaa yake. Ingewezekana, himizo kubwa lingesisitizwa katika marekebisho ya tabia za wazazi kuwezesha watoto kuiga mtindo au mitindo ya maisha yanayofaa. Kielezo chema ni kuwa na mzazi mwenye tabia njema kwa mtoto wake, rafiki zake na kwa jamii yake.
    (a) Ni nini umuhimu wa faragha kwa binadamu kwa mujibu wa aya ya kwanza?
    (b) Eleza jinsi watu wengine wanavyoharibu wakati wao wa faragha kwamambo ya upotovu
    kwa kurejelea aya ya pili na ya tatu (maneno 30)
    (c) Eleza mchango wa mzazi kwa mwanawe kuhusu matumizi bora ya wakati wa faragha.
    Zingatia aya ya mwisho

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Jadili sababu tano zinazofanya "sheng" isiwe lugha ya taifa.(Solved)

    Jadili sababu tano zinazofanya "sheng" isiwe lugha ya taifa.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana ya; i).Mkembe. ii).mkebe.(Solved)

    Eleza maana ya;
    i).Mkembe.
    ii).mkebe.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Uwezo wa kuyakumbuka mambo ni hazina kuu kutoka kwa mtu yeyote yule aliye hai. Uwezo huu wa kukumbuka ni mojawapo ya...(Solved)

    Soma taarifa kisha fupisha kwa mujibu wa maswali yafuatayo.

    Uwezo wa kuyakumbuka mambo ni hazina kuu kutoka kwa mtu yeyote yule aliye hai. Uwezo huu wa kukumbuka ni mojawapo ya shughuli changamano za ubongo. Ubongo wa mwanadamu hutekeleza shughuli hii kwa namna tatu. Kwanza ubongo hunasa jambo kisha
    huliihifadhi. Baadaye huanzisha mfumo wa kutoa kilicho hifadhiwa. Ubongo ukiathirika kwa
    namna yeyote katika moja wapo ya njia hizi, basi uwezo wa kuyakumbuka mambo huvurugika.
    Ingawa inaaminika kuwa uwezo wa kukumbuka hurithishwa toka kizazi kimoja hadi kingine, wataalamu wa maswala ya kiakili wanabaini kuwa uwezo huu unaweza kuimarishwa.
    Uimarishaji huu huhitajika mikakati madhubuti.
    Njia mojawapo ya kustawisha uwezo wa kukumbuka ni kupitia kwa lishe. Vyakula vilivyosheheni vitamini B vyenye amino asidi husaidia kuimarisha uwezo wa kukumbuka. Vyakula kama hivi ni mboga, nyama (hasa maini), bidhaaa za soya, matunda, maziwa, ,bidhaa za ngano, samaki, pamoja na mayai. Vyakula vingine muhimu katika ustawishaji huu ni vile vyenye madini ya chuma. Madini haya huwezesha usambazaji wa hewa katika ubongo kwa wepesi. Vyakula ambavyo vina madina haya ni mboga za kijani, mawele, ndengu, soya, matunda kama maembe, ufuta (simsim) pamoja na nyama, hasa maini na mayai.
    Ubongo wa mwanadamu aliye hai hufanya kazi kila wakati awe macho au amelala. Utendaji kazi wake huendeshwa na glukosi mwilini. Kwa hivyo, vyakula vyenye sukari hii ni muhimu kuliwa. Hata hivyo, lazima mtu awe mwangalifu na kuhakikisha kuwa mwili una kiwango cha sukari kisicho hatarisha maisha. Haya yanawezekana kwa kula vyakula vyenye nyuzinyuzi kama vile mboga na matunda.
    Njia ya pili ni kupiga marufuku vileo kama pombe na nikotini. Vileo hivi huathiri utaratibu wa kunasa, kuhifadhi na kutoa yaliyo ubongoni.
    Iwapo mtu ana tatizo la kuyakumbuka majina ya watu, ni muhimu kufanya mazoezi ya
    kusikiliza kisha kurudia majina hayo wakati wa mazungumzo. Ni bora kulihusisha jina na sura
    ya mtu. Kwa njia hii ubongo utanasa jina na kile kinacholengwa.
    Woga na kuvurugika kiakili ni mambo mengine tunayopaswa kuepuka kila wakati. Ni kawaida mtu kupata woga wakati anapokabili jambo asilokuwa na uhakika na matokeo yake kama mtihani au mahojiano. Lakini anapaswa kuwa makini. Woga huo usikiuke mpaka na kumvuruga kiakili. Vurugu hizi huathiri kilichohifadhiwa ubongoni na pia namna ya kukitoa.
    Halikadhalika, mwili wenye siha nzuri huhakikisha kuwa ubongo ni timamu. Wataalamu wengi wa siha wanakubali kuwa na mazoezi ya kunyoosha viungo hustawisha ubongo na hivyo kuhakikisha kuweko kwa uwezo wa kukumbuka mambo. Ni muhimu kuwa na taratibu ya kunyoosha viungo kila wakati. Fauka ya hayo, mazoezi ya kiakili, kama vile kusoma makala yanayovutia, kujaza mraba na michezo mingine kama mafumbo, vitenzi ndimi ni muhimu katika kustawisha uwezo wa kukumbuka.
    Jamii ya watu wenye uwezo kuyakumbuka mambo ni ya jamii iliyopiga hatua kimaendeleo. Ni jukumu la kila mmoja wetu kuimarisha uwezo wa kukumbuka kila wakati.

    a) Kwa maneno 60 – 65 fupisha mchango wa chakula katika uimarishaji wa uwezo wa
    kukumbuka.
    b) Fupisha aya tatu za mwisho kwa maneno 80 – 90

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Nyambua vitenzi vifuatavyo katika hali ulizopewa.(Solved)

    Nyambua vitenzi vifuatavyo katika hali ulizopewa.
    pic41020191417.png

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha vishazi huru na vishazi tegemezi katika sentensi ifuatayo. Nitaenda maktabani ingawa ninaumwa na kichwa.(Solved)

    Bainisha vishazi huru na vishazi tegemezi katika sentensi ifuatayo.
    Nitaenda maktabani ingawa ninaumwa na kichwa.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita, tumeshuhudia mabadiliko na maendeleo makubwa kuhusu vyombo vya habari nchini Kenya. Hapo awali, redio ndicho chombo...(Solved)

    Soma taarifa ifuatayo kisha ufupishe taarifa hii kulingana na maswali yanayofuata:-

    Katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita, tumeshuhudia mabadiliko na maendeleo makubwa kuhusu vyombo vya habari nchini Kenya. Hapo awali, redio ndicho chombo cha habari cha kipekee kilichotamalaki kote nchini. Familia nyingi ziliweza kumiliki chombo hiki. Runinga ilikuwa miliki ya wachache, hasa mabwenyenye. Sasa hivi, hata akina yahe nchini na mashambani wanamiliki chombo hiki.
    Runinga kama kifaa kingine chochote cha mawasilianao kina manufaa yake. Kwanza kabisa, ni nyenzo mwafaka ya kufundisha. Vipindi vinavyopeperushwa katika runinga huwa na mafunzo kemkem kwa mtu wa kila rika. Hali kadhalika, runinga huweza kuleta vipindi ambavyo huwafahamisha watu mambo yanayoendelea katika mazingira yao na duniani. Aidha, runinga ikitumika pamoja na michezo ya video huauni katika ukuzaji na ustawishaji ya kufundisha au kujielimisha. Michezo ya video, hasa ya kielimu huwafanya watu kujenga umakini pamoja na kuchua misuli ya ubongo na kuwafanya watu kuwa macho wanapofanya kazi.
    Fauka ya hayo, televisheni ni chemichemi bora ya kutumbuiza na kuchangamsha. Hakuna mtu asiyependa kuchangamshwa. Televisheni ni mojawapo wa vyombo mwafaka vya kutekeleza hayo kutokana na vipindi vyake. Uburudishaji huu hupatikana kwa urahisi majumbani mwetu.
    Vivyo hivyo, runinga hutumika kama nyenzo ya kuendeleza utamaduni, kaida na amali za jamii. Vingi vya vipindi vya runinga ni kioo ambacho huakisi mikakati na amali za jamii.
    Kwa upande mwingine, hakuna kizuri kisichokuwa na dosari. Licha ya manufaa yake, televisheni imedhihirika kuwa na udhaifu wake. Kwanza, baadhi ya vipindi vya runinga na video hujumuisha ujumbe usio na maadili, kama vile matumizi ya nguvu za mabavu, ngono za kiholela, lugha isiyo ya adabu, ubaya kimavazi na maonevu ya rangi, dini, jinsia , kabila na utamaduni. Si ajabu kuwa baadhi ya vijana wetu wanaiga baadhi ya mambo haya. Vijana wetu siku hizi wameingilia ulevi wa pombe na afyuni, ngono za mapema kabla ya ndoa na mavazi yanayowaacha takribani uchi wa mnyama. Wengi wamekopa na kuyaiga haya kutoka katika runinga. Ukiwauliza wafanyacho, watakujibu kuwa ni ustaarabu kwani wameupata katika runinga.
    Matumizi ya runinga na michezo ya video yasiyodhibitiwa huweza kuwa kikwazo cha mawasiliano bora miongoni mwa wanafamilia. Matumizi kama haya huwapa wanafamilia fursa ya kujitenga. Imedhihirika kuwa runinga haichangii kujenga uhusiano bora wa kijamii ukilinganisha na vyombo vingine vya burudani ambavyo hutoa nafasi ya watu kutangamana na kujenga uhusiano bora, televisheni haichangii haya. Badala yake, tajriba ya televisheni huwa na kibinafsi. Hali hii inapotokea katika kiwango cha familia, televisheni inaweza kutenganisha wazazi na watoto wao.
    Halikadhalika, runinga na video aghalabu hueneza maadili yasiyofaa. Mathalan, baadhi ya vipindi vya televisheni huendeleza hulka ya kuhadaa, ngono za kiholela, kuvunjika kwa ndoa, n.k. Hulka hizi zisizoendeleza maadili ya kijamii huchukuliwa kama zinazofaa na zinazofuatwa na waliostaarabika. Huu ni upotovu.
    Isitoshe, baadhi ya matangazo huhimiza matumizi ya madawa ya kulevya kama tembo na sigara. Vitu hivi vinapotangazwa, hupambwa kwa hila na udanganyifu mwingi ambao huwavutia vijana na watoto wengi. Si ajabu mtu anapouliza wanaoutumia vileo hivi walivyoanza, watajibu kutokana na athari za matangazo katika runinga na vyombo vingine.
    Utafiti umeonyesha kuwa vipindi vya runinga na video ni chanzo cha matumizi ya nguvu za mabavu miongoni mwa wanafunzi. Wazazi wengi huchukulia vibonzo katika televisheni kuwa vinalenga kuburudisha tu na havina ubaya wowote. Lakini ukweli ni kuwa vipindi vingi vya vibonzo hushirikisha matumizi ya hila na nguvu za mabavu. Haya huibusha hamu ya vijana na watoto huyaiga.
    Kwa hivyo, ni muhimu wazazi na jamii kutambua madhara ya televisheni. Utambuzi huu utawafanya waelekeze vijana na watoto jinsi ya kutumia televisheni na video ili kuepukana na madhara yake.
    Maswali
    (a) Ukitumia maneno 50-60, fupisha manufaa ya runinga
    (b) Fupisha hasara za runinga ukitumia maneno 70-80

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Toa maneno yenye maana sawa na haya. i. Izara ii. Anisi(Solved)

    Toa maneno yenye maana sawa na haya.
    i. Izara
    ii. Anisi

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha shamirisho na chagizo katika sentensi hii. Mbuga za wanyama zitapata wageni wengi mwaka ujao.(Solved)

    Bainisha shamirisho na chagizo katika sentensi hii.
    Mbuga za wanyama zitapata wageni wengi mwaka ujao.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi. Atanishughulikia vizuri.(Solved)

    Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi.
    Atanishughulikia vizuri.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Usawa wa wanadamu upo kimaumbile – maumbile ya mtu kamwe hayatakosewa na yale ya mnyama wa mwituni. Lakini fikira, tabia,...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali:

    Usawa wa wanadamu upo kimaumbile – maumbile ya mtu kamwe hayatakosewa na yale ya mnyama wa mwituni. Lakini fikira, tabia, kimo, uwezo na mahitaji huwa tofauti kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Kwa mintarafu hii yapasa wakufunzi na wazazi kuwapa watoto wao widhaa mapema ili wachague kwa wakati unaofaa kazi watakayoifanya maishani.
    Watoto wanapopelekwa chuoni, wazazi wao huukilia kuwasomesha hadi kiwango fulani cha masomo kisha wajitafutie kazi ambayo itawapa masurufu na pesa za shughuli zingine maishani.
    Katika nchi yetu tangu tupate uhuru mtindo wa kutoa kazi umekuwa ni ule wa kuchukua watu waliofaulu mitihani ya viwango fulani na kuwapa kazi moja kwa moja. Mwenendo huu wa kuajiri watu kazi umeendelea muda mrefu lakini sasa yamkinika utasitishwa na njia mpya kufuatwa. Sababu ya kufanya hivyo ni kuwa nafasi za kazi zimekuwa finyu sana. Kabla na punde baada ya uhuru nafasi hizo zilipatikana kila mahali. Nyingi ya hizo ziliachwa wazi na wageni walioihama nchi hii tulipojitawala. Siku hizi wanafunzi wanaokomea darasa la saba, kidato cha pili na hata cha nne huwa hawazioni ahadi za kupata kazi za madaraka fauka ya kazi yoyote. Wanaoiona tabasamu ya kazi mbele yao ni wale wanaotasawari masomoni wakifuata taaluma fulani.
    Tatizo la kazi laeleweka vema kwa serikali na ni kwa ajili hii serikali imemtasulia kila mwananchi kuwa wakati wa kuania kazi za utanashati umetimiuka. Wakati uliopo ni wakati wa kujifunga vibwebwe kisaki na kuchapa kazi zile ambazo hadi sasa zafikiriwa kazi chafu na zisizofaa wasomi. Dhana kama hiyo ni ya kibwanyenye, na ubwanyenye hauji ila kwa sulubu. Usemapo kuna kazi nzuri na mbaya huwa unazusha maswali mengi. Utatakiwa ueleze kinaganaga kazi nzuri au mbaya kwa nini? Kazi huwa nzuri kwa upande wa tija au kwa upande wa wepesi wake? Kujibu maswali ya namna hii kutahitaji wekevu mwingi, waima mtesi ataonekana dufu.
    Zipo kazi aina mbili. Ipo kazi ya kuajiriwa na ya kujiajiri. Kazi ya kujiajiri kwa kulinganishwa huonekana ngumu na yenye matatizo mengi mwanzoni. Lakini itakubalika pato lake ni kubwa zaidi ikishapata msingi imara. Msingi imara huwekwa kwa juhudi za mwanzoni zikiambatana na ujasiri. Mtu asiyejasiri kutenda tendo lolote maishani ni sawa na yule asiyejua atokako na kule aendako; yuaishi kungozwa. Ardhi ni thawabu, tena thawabu tunu. Ukiwa na kipande cha ardhi ifaayo kwa kilimo ufakiri ukikutawala ni wewe mwenyewe kupenda: la sivyo ufa umo ubongoni unaohitaji bwana mganga

    (a) Bila kupoteza maana iliyokusudiwa na mwandishi wa taarifa, fupisha aya ya kwanza
    na ya pili. maneno 60-70)

    (b) Kwa kuzingatia aya mbili za mwisho. Eleza mambo muhimu yanayoshughulikiwa na mwandishi. (maneno (50-60)

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi ifuatayo katika msemo halisi. Mama alimwuliza mwanawe alikochelewa na kisha akamtahadharisha kuwa haikuwa tabia njema kwa mtoto wa kike kama yeye kuzoea kutembea usiku.(Solved)

    Andika sentensi ifuatayo katika msemo halisi.
    Mama alimwuliza mwanawe alikochelewa na kisha akamtahadharisha kuwa haikuwa tabia njema kwa mtoto wa kike kama yeye kuzoea kutembea usiku.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Usafiri ni upelekezi wa watu na bidhaa au mizigo kutoka mahali pamoja hadi mahali pengine. Tuseme kutoka kituo A na kuenda...(Solved)

    Soma taarifa inayofuata kisha ujibu maswali yaliyoulizwa

    Usafiri ni upelekezi wa watu na bidhaa au mizigo kutoka mahali pamoja hadi mahali pengine. Tuseme kutoka kituo A na kuenda kituo B.
    Katika ulimwengu wa leo, watu na bidhaa husafirishwa barabarani kwa mabasi au motokaa za kila aina au kwa kutumia magari moshi yanayopita juu ya reli, au meli zinazopita majini, kadhalika, usafiri unaweza kufanyiwa hewani.

    Hivyo, hali haikuwa hivyo zamani. Usafiri uliojulikana sana kale ni usafiri kwa miguu. Watu waliposafiri kutoka eneo moja hadi jingine walilazimika kufanya hivyo kwa miguu. Kadhalika, watu waliposafirisha mizigo mizito kutoka eneo moja hadi nyingine, iliwabidi kuibeba mizigo hiyo wao wenyewe. Mpaka leo usafiri huu upo.
    Wanyama vilevile walitumiwa kama njia moja ya usafirishaji. Huku Afrika ya mashariki kulitumika wanyama wengine kama vile punda. Punda ni mnyama anayependwa sana kwa sababu anaweza kuenda mwendo mrefu pasipo na kunywa maji. Mpaka leo, mnyama huyo hutumika sana na wamaasai, wagala, warendile na wengine.
    Mnyama mwingine aliyetumika sana, na mpaka leo anaendelea kutumika ni ngamia. Ngamia anafaa sana katika usafiri wa jangwani. Kwato za ngamia huweza kusafiri kwa urahisi jangwani ama popote penye mchanga mwingi kwa sababu kwato zake hazizami kwenye mchanga. Isitoshe ngamia wanaweza kwenda mwendo mrefu bila maji au chakula huku wakitegemea mafuta yaliyohifadhiwa kwenye nundu zao.
    Katika ulimwengu wa kisasa, binadamu amepiga hatua kubwa sana katika masuala ya usafiri. Baadhi ya maendeleo hayo ni ya kustaajabisha. Kwa mfano, binandamu anaweza kuruka kwa kutumia vyombo vya angani kwenda kwenye anga za mbali. Katika karne iliyopita binadamu anaweza kuruka kwa kutumia vyombo vya angani kwenda kwenye anga za mbali. Katika karne iliyopita binadamu amefika mwezini kwa kutumia vyombo hivyo. Kuna tetesi kwamba sasa anajaribu kuzizuru sayari zilizoko mbali na ardhi.
    Ama kwa hakika, usafiri bora in kipimo kimojawapo cha maendeleo ya nchi yoyote katika ulimwengu wa sasa. Bila njia ya kisasa za usafiri, baadhi ya mambo yanayofanyika katika nchi zetu hayangefanyika.

    (a) Katika habari hii, punda na ngamia wana sifa gani muhimu zinazowawezesha kutumiwa
    kwa usafirishaji? (maneno 30-40)
    (b) Kwa mujibu wa taarifa, usafiri wa zamani unatofautiana vipi na ule wa siku hizi?
    (maneno 40-50)

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)