Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.
Mwalimu alimwambia mwanafunzi Yule kuwa michezo yao ya mpriaingeng’oa nanga siku ambayo ingefuata
Kavungya answered the question on October 4, 2019 at 12:55
- Eleza maana mbili zinazopatikana katika sentensi ifuatayo;
Tafadhali niletee pia nichezee. (Solved)
Eleza maana mbili zinazopatikana katika sentensi ifuatayo;
Tafadhali niletee pia nichezee.
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Biashara ya kimataifa ni muhimu sana katika ukuaji wa uchumi wa nchi yoyote ile.Nchi mbalimbali zimekuwa
zikitegemeana kwa namna moja na nyingine(Solved)
Biashara ya kimataifa ni muhimu sana katika ukuaji wa uchumi wa nchi yoyote ile.Nchi mbalimbali zimekuwa
zikitegemeana kwa namna moja na nyingine. Kwa mfano, nchi ya Kenya imekuwa ikiuza maua na mboga katika nchi za ng‘ambo na kupata fedha za kigeni ambazo hutumiwa humu nchini kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo Biashara ya kimataifa huziwezesha nchi ambazo hazizalishi bidhaa na hata huduma mbalimbali kupata bidhaa hizo kutoka nchi nyingine zinazohusiana nayo kibiashara. Mathalan, Kenya ni nchi ambayo imekuwa ikitegemea kilimo lakini haijaendelea katika sekta ya viwanda. Kenya huagiza bidhaa kama vile vipuri vya magari na hata magari yenyewe kutoka nchi kama vile Japan. Nayo Kenya huuza mazao ya shambani kama vile pareto, chai na kahawa ng‘ambo. Kupitia kwa biashara ya kimataifa, nchi hupata masoko kwa bidhaa zake. Kwa vile biashara ya kimataifa huziwezesha nchi husika kuzalisha bidhaa mahususi ambazo hazitahigharimu pesa nyingi kuzalisha, nchi hizo aghalabu huzalisha kiwango kikubwa cha bidhaa kuliko mahitaji yake ya nyumbani. Nchi basi hulazimika kutafuta masoko nje ya mipaka yake. Kwa njia hii, uchumi wa nchi huendelea kuimarika. Aidha, biashara ya kimataifa huwezesha nchi kupata huduma za kitaaluma ambazo hazipatikani katika nchi husika. Kuna nyanja za kiuchumi ambazo huhitaji wataalamu mahususi. Kwa mfano, katika sekta ya matibabu nchini humu tumepata kwamba kuna baadhi ya magonjwa ambayo yanahitaji matibabu maalumu. Wanaougua magonjwa haya huagiziwa madaktari kutoka ng‘ambo au hata kupelekwa ng‘ambo kwa uchunguzi na matibabu zaidi.Biashara ya kimataifa hukuza ushirikiano wa kimataifa . Nyakati za majanga ya kimaumbile na hata mengine yanayosababishwa na kutowajibika kwa binadamu, nchi hupata husaidiza kutoka nchi za ng‘ambo. Kwa mfano, wakati wa mkasa wa bomu wa 1998, Kenya ilipata msaada wa kukabiliana na janga hili kutoka Israeli, Marekani, na hata Ujerumani ambako baadhi ya waathiriwa wa mkasa huo walipelekwa kwa matibabu zaidi. Ushirikiano huo wa kimataifa huwezesha wananchi kutoka nchi fulani kuenda kusomea na hata kufanya kazi katika nchi nyingine. Katika miaka ya hivi karibuni, Wakenya wengi wamekuwa wakienda kusomea vyuo vikuu vya ng‘ambo. Wengine wamediriki kupata kazi katika mashirika ya kimataifa katika nchi mbalimbali kama vile Afrika Kusini , Rwanda , Msumbiji na kadhalika. Biashara ya kimataifa husaidia kukuza ushindani kati ya nchi husika. Ushindani huu ni hakikisho la uzalishaji wa bidhaa za thamani bora . Kila nchi itafanya juu chini kuzalisha bidhaa ambazo zinaweza kukubalika katika soko la kimataifa. Pia,wananchi wa nchi husika hupata aina tofauti za bidhaa badala ya kutegemea ainamoja tu ya bidhaa zinazozalishwa nchini mwao.Biashara ya kimataifa huleta ushirikiano wa kisiasa na uelewano zaidi kati ya madola mbalimbali. Mathalan muungano wa nchi za Afrika Mashariki – Kenya, Uganda na Tanzania, hauchangii tu kuleta manufaa ya kiuchumi bali huleta ushirikiano zaidi wa kisiasa.Ingawa biashara ya kimataifa inahitajika, biashara hii huandamana na hasara mbalimbali. Biashara hii imesababisha kuwapo kwa masoko huru ambayo yameleta ushindani mkubwa kwa wafanyibiashara wadogo wa humu nchini. Baadhi ya wafanyibiashara wamelazimika kufunga biashara baada ya kufilisika. Ushuru mkubwa unaotozwa baadhi ya bidhaa zinazoingia huwafanya wananchi wengi kutofaidika kwa bidhaa na huduma kutoka nje. Aidha, kuna ucheleweshaji wa bidhaa zilizoagizwa. Bidhaa hizi mara nyingi huchukua muda kabla ya kutoka nchini. Kwa hivyo, wafanyibiashara wengi hulazimikakungojea kupata bidhaa hizi na kuwauzia wateja wao. Vilevile, kutokana na biashara ya kimataifa, bidhaa duni huweza kupenyezwa katika mataifa yanayoendelea. Pia, baadhi ya wafanyibiashara wa kimataifa huchukua fursa hii kulangua dawa mbalimbali za kulevya ambazo huwaathiri vijana wa nchi husika. Wengine huhusika katika vitendo vya kigaidi kama vile ulipuaji wa majengo mbalimbali kwa bomu na mauaji ya wananchi wasio na hatia. Ni kweli kuwa biashara ya kimataifa ina hasara zake. Hata hivyo, ni mhimili mkubwa wa uchumi wa mataifa machanga.
a) Kwa maneno yasiyozidi themanini , eleza umuhimu wa biashara ya kimataifa.
b) Kwa maneno maneno yasiyozidi 40 , eleza ujumbe wa aya tatu za mwisho.
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Kwa hali nyingine , tunaweza kusema kuwa uchafuzi wa mazingira ni uharibifu wa vile
vitu vinavyowazunguka binadamu na wanyama maishani mwao....(Solved)
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Kwa hali nyingine , tunaweza kusema kuwa uchafuzi wa mazingira ni uharibifu wa vile
vitu vinavyowazunguka binadamu na wanyama maishani mwao. Kuna uchafuzi wa aina mbalimbali na kila uchafuzi humhusu binadamu kwa njia fulani.
Maendeleo ya viwanda duniani ni sababu mojawapo ya uchafuzi wa hewa. Mitambo katika karakana huwa inatoa moshi mwingi wakati bidhaa zinapotengenezwa. Moshi husambaa eneo kubwa na kuchanganyika na hewa inayovutwa na binadamu. Uchafu hutupwa ovyo ovyo na kuwa hatari kwa afya ya binadamu. Maji machafu huweza kutiririkia mtoni, maziwani na hata baharini. Yale yanayotiririka mitoni na maziwani huchafua maji ambayo hutumiwa na watu wa eneo hilo kwa kunywa, kupika na kunywesha mifugo wao. Yale yanayotiririka baharini huwa ni hatari kwa samaki wanaotegemewa na binadamu kuwa kitoweo muruwa.
Ongezeko la watu pia ni hali nyingine ya uchafuzi wa mazingira. Halaiki ya watu hufanya
uharibifu wa misitu ya asili. Hii ni kwa sababu ya kutaka kuongeza ekari za mashamba. Hili husababisha mmomonyoko wa udongo ; hivyo basi kuiacha ardhi bila rutuba yoyote. Katika hali hii, kilimo ambacho ni uti wa mgongo wa nchi nyingi duniani huzoroteshwa. ‘‘Maisha ya binadamu hutegemea kilimo kwa kila hali kwa hivyo kilimo kinapozoroteka hata uchumi nao huathirika. Kila uchao tunasikia kwamba nchi fulani imekabiliwa na njaa.
Ufugaji wa wanyama wengi bila mpango maalum pia huharibu mazingira ya asili kama nyasi na vichaka. Watu wengi hufuga ng’ombe, mbuzi na kondoo. Kwa kuwa hawana mahali maalum pa kuwalisha, huzunguka nao huku na huko kutafuta nyasi na majani ya kuwalisha. Wanyama wanaotangishwatangishwa namna hiyo humaliza majani na nyasi zote na kuacha ardhi tupu ambayo hatimaye huyabisika kwa jua. Ardhi ya namna hii haishiki maji mvua inyeshapo. Nchi iliyoneemeka huweza kuwa jangwa lililo na chungu ya mchanga.
Watu wanapoongezeka huko mashambani huwabidi wakate misitu ili waanzishe maskani mapyapamoja na mashamba yao. Miti hukatwa bila hadhari na mabiwi ya matawi pamoja na majani huchomwa moto. Jambo la kusikitisha ni kwamba miti hiyo inapokatwa hakuna mingine inayopandwa kuchukua mahali pake.
Mahitaji ya binadamu ya kuendeleza njia za mawasiliano pia huzusha balaa nyingine. Barabara zinazidi kuongezeka na pia watu wanaozidi kuongezeka pamoja na mazao yao. Kwanza, barabara zinapotengenezwa misitu hukatwa mahali zinapopitia. Pili, wingi wa magari huzidi na baadhi ya hayo hutoa moshi unaoharibu hewa.
Njia kadha wa kadha za kuzuia uharibifu wa mazingira zimependekezwa. Ingawa suluhisho timamuhalijafikiwa, Serikali nyingi duniani zimo katika harakati za kutafuta suluhisho la uchafuzi huo.
Njia mojawapo ni kukomesha ujenzi wa viwanda katika miji mikuu na mahali palipo na watu wengi.Wenye viwanda pia wanahimizwa kufikiria jinsi ya kutupa takataka na maji machafu bila kudhuru afya ya binadamu.
Watu wakizingatia suala la upangaji wa uzazi na kuwa na familia ndogo ndogo, idadi ya watu haitaongezeka kwa kasi kwa hivyo itakuwa hakuna haja ya kuanzisha makao mapya mara kwa mara.
Serikali nyingi zimechukua jukumu la kuwaelimisha raia juu ya madhara yanayotokana na uharibifuwa mazingira. Raia wanahimizwa kupanda miti kwa wingi.
Jitihada zinazofanywa kuzuia uchafuzi wa mazingira hukumbana na matatizo. Tatizo kubwa ni fedha za kuendeleza miradi inayopendekezwa. Shida nyingine ni kwamba juhudi zingine huwa zinamwingilia binadamu na mali yake.
Maswali.
(a) Fupisha aya za kwanza sita za taarifa uliyosoma (maneno 50-60)
(b) Fupisha aya za mwisho tano kwa maneno 40-45
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Kanusha sentensi ifuatayo;
Angalimpata babu yangu angalimpeleka hospitalini.
(Solved)
Kanusha sentensi ifuatayo;
Angalimpata babu yangu angalimpeleka hospitalini.
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Bainisha aina za virai vilivyopigiwa mistari.
Uchochole wa kijinsia umepigwa marufuku na kiongozi mwenye msimamo dhabiti mno.
(Solved)
Bainisha aina za virai vilivyopigiwa mistari.
Uchochole wa kijinsia umepigwa marufuku na kiongozi mwenye msimamo dhabiti mno.
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Tunga sentensi yenye muundo ufuatao
KN(N+S)+KT(T+E+E)(Solved)
Tunga sentensi yenye muundo ufuatao
KN(N+S)+KT(T+E+E)
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Iandike sentensi ifuatayo upya katika hali yakinishi.
Hapo napo sipo nitakapo.
(Solved)
Iandike sentensi ifuatayo upya katika hali yakinishi.
Hapo napo sipo nitakapo.
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Imesemwa na kurudiwa tena kwamba, iwapo tuna maono ya kujiondoa katika umaskini wa kupindukia, ni lazima tukipe kilimo umuhimu. Zaidi...(Solved)
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali kulingana na maagizo
Imesemwa na kurudiwa tena kwamba, iwapo tuna maono ya kujiondoa katika umaskini wa kupindukia, ni lazima tukipe kilimo umuhimu. Zaidi ya wakenya milioni kumi wamo katika hatari ya kufa njaa katika maeneo mbali mbali kwa sasa kufuatia uhaba wa chakula nchini.
Kiini kikubwa cha njaa hiyo ni mapuuza ya muda mrefu katika sekta ya kilimo. Imesahaulika kuwa karibu asilimia sabini na tano ya wakenya wanategemea kilimo kwa chakula na mapato ya kifedha kila siku. Kilimo hutoa karibu robo tatu ya nafasi za kazi kwa wananchi na pia huletea serikali karibu robo ya mapato yake kutokana na mauzo ya mazao katika mataifa ya nje.
Wataalamu wa maswala ya zaraa wanaeleza kuwa pato la nchi linalotokana na kilimo huangamiza njaa mara nne zaidi ya mapato yanayotokana na shughuli nyinginezo za kiuchumi. Hiyo ni kwa sababu shughuli za kilimo hulenga kuzalisha vyakula moja kwa moja.
Imebainika kuwa, katika mataifa mengi yanayostawi, asilimia sabini na tano ya wananchi huishi katika maeneo ya mashambani na idadi hii hutegemea kilimo kujimudu kimaisha ilhali hapa Kenya ni asilimia nne pekee ya bajeti inayowekezwa katika kilimo. Kwa wakati huo, ushuru unaotozwa bidhaa za kilimo katika maeneo haya umebainika kuwa mkubwa. Hii imepelekea uwekezaji katika kilimo kupungua na hivyo kuchangia kukithiri kwa baa la njaa.
Wakati umewadia kwa serikali za Afrika na wapangaji wa masuala ya uchumi kuweka juhudi maradufu katika kushabikia kilimo ili kumaliza njaa na umaskini. Kuna haja ya kuwajulisha, kuwahimiza na kuwaelimisha wakulima wa mashamba madogo madogo kuhusu mihimili ya zaraa kama vile uzalishaji wa matunda na mboga, ufugaji wa ndege, samaki na ng’ombe mbali na kuweka mikakati ya kuanzisha nafasi za kazi katika sekta ya kilimo.
Serikali itafikia lengo hili iwapo itaanza kufadhili kilimo, kupunguza gharama za pembejeo za kilimo, kuweka sera zinazodhibiti uuzaji na ununuzi wa vyakula hasa baina ya mataifa na kuongeza sehemu ya bajeti inayotengewa kilimo. Bila hilo hatutakuwa na lingine bali kukimbilia mataifa yaliyostawi kuomba misaada ili kuwanusuru raia wetu kutokana na ghadhabu ya njaa.
(a) Fupisha aya mbili za mwanzo (maneno 50 -55)
(b) Bila kubadili maana, fupisha aya mbili za mwisho (Maneno 55-60)
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Mafuta yanayopatikana kwenye fukwe za bahari, moshi wa magari, takataka na bidhaa nyinginezo zinazotupwa hapa na hapa ni vichafuzi vya mazingira.(Solved)
Mafuta yanayopatikana kwenye fukwe za bahari, moshi wa magari, takataka na bidhaa nyinginezo zinazotupwa hapa na hapa ni vichafuzi vya mazingira. Vichafuzihuadhiri afya zetu na kuathiri wanyama na mimea. Wanadamu wanayachafua mazingira yao kwa kila aina ya bidhaa mbaya za kikemikali zinazotoka viwandani mwa kawi / nguvu. Bidhaa hizo ni matokeo ya maisha ya siku hizi anayoishi binadamu. Licha ya ukweli huu, ni muhimu kujua kuwa uchafuzi wa mazingira haukuanza leo. Miaka na miaka iliyopita, viwanda vimekuwa vikitoa mawingu makubwa ya moshi yenye sumu. Hata hivyo, uchafuzi wa mazingira umeongeza mara dufu kutokana na kuongezeka kwa viwanda. Uchafuzi umesambaa ardhini, kwenye anga na majini. Msambao huu unapatikana katika pembe zote za ulimwengu wetu. Je, kuna aina zipi za uchafu? Kwanza, kuna uchafu wa hali ya anga. Huko juu angani kuna tabaka linalojulikana kama ozoni. Tabaka hili ni aina ya gesi ya oksijeni na linaunda kinga fulani dhidi ya miale ya jua. Miale hiyo ya jua huweza kusababisha saratani ya ngoziinapomfikia binadamu. Hata hivyo, uchafu wa mazingira unaelekea kuliathiri tabaka hili vilevile baadhi ya kemikali zinazotumiwa katikajokofu au kwenye mikebe ya marashi ya kupulizia na upakiaji bidhaa, huuharibifu ukanda huo.Uchafu mwingine ni uchafuzi wa kiajali. Uchafuzi huu hutokea bila binadamu kukusudia. Mfano mzuri ni meli inayovuja mafuta baharini. Mafuta haya huwaathiri na kuwaua wanyama wanaoishi baharini kama samaki na ndege na hata kuyaharibu mazingira yenyewe. Miji mikubwa hukumbwa na uchafuzi mwingine unaohusiana na kuwako kwa idadi kubwa ya magari. Magari haya hutoa moshiunaochanganya gesi ambazo huungana na nyingine zinazoletwa na viwanda vikubwa. Mchanganyiko huu unapoungana na maji , husababisha mvua ya asidi. Mvua hii huweza kuiua mimea , kuathiri majengo na hata kuwaua wanyama wa pori ambao huenda wakayatumia maji hayo. Magari hayo hutoa moshi uliochanganyika na madini aina ya risasi ambayo huweza kuathiri siyo tu mazingira bali pia mfumo wa akili wa binadamu. Uchafuzi mkubwa ni utupwaji ovyo wa takataka. Fauka ya hayo, watu hufukia ardhini takataka ambazo huweza kuwa na matokeo mabaya kwa sababu ya kupenyeza kwenye udongo na maji yanayotumiwa na watu na mimea. Kila siku tunatupa takataka bila kujali wala kukubali. Takataka hizi ni kama makopo, mifuko ya plastiki, mabaki ya sigara au maganda ya matunda. Baadhi ya takataka ni hatari kwa wanyama na nyingine huweza pia kusababisha majanga kama moto. Aidha, hufanya mazingira yaonekane machafu.Sote tunajukumu kubwa la kuchangia kupunguza uchafu wamazingira. Kwanza, kuelimisha na kutambua umuhimu wa usafi wa mazingira yetu . Tunapaswa kutia takataka zetu kwenye vijalala maalum au mahali tunapoweza kuzichoma na kuziteketeza. Tuhakikishe tunatunza vitu kama mifuko, chupa na kadhalika ambavyo huweza kuundwa upya na kutumika tena. Hali kadhalika, katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwepo na juhudi za kuwahimiza wenye magari kutumia mafuta ya gari ambayo hayana madini ya risasi. Kwa njia hii, tutasaidia kuyaboresha mazingira yetu. Vilevile pana umuhimu wa kutilia mkazo utumiaji wa bidhaa ambazo zinaweza kuoza na kuvunjikavunjika au kusagika na kuwa sehemu ya udongo. Hatua ya kwanza ya kupambana na uchafuzi wa mazingira ni kujielimisha na kuwajibika. Kila mmoja akitoa mchango wake, tutafanikiwa. Kumbuka: kinga na kinga ndipo moto uwakapo.
a) Ongezeko la viwanda limechangiaje uchafuzi wa mazingira ?
b) Tabaka la ozoni huathiriwaje na uchafuzi?
c) Eleza athari zozote tatu za kutotunza mazingira.
d) Kwa nini miji mikubwa hukumbwa na uchafuzi kuliko sehemu nyingine?
e) Eleza nui mbili za uchafuzi wa mazingira zilizotajwa katika kufungu hiki.
f) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika kifungu.
i) Msambao -
ii) Makopo -
iii) Kinga –
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Tumia maneno yafuatayo katika sentensi moja ili kubainisha tofauti zao kimaana;
i) Chuuza
ii) Chuza(Solved)
Tumia maneno yafuatayo katika sentensi moja ili kubainisha tofauti zao kimaana;
i) Chuuza
ii) Chuza
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Eleza tofauti kati ya ama za vielezi vifuatavyo;
i) Vielezi vya namna mfanano na;
Vielezi vya namna hali.
ii) Tunga sentensi mbili tofauti ukitumia vielezi vya hapo...(Solved)
Eleza tofauti kati ya ama za vielezi vifuatavyo;
i) Vielezi vya namna mfanano na;
Vielezi vya namna hali.
ii) Tunga sentensi mbili tofauti ukitumia vielezi vya hapo juu.
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Andika sentensi moja ukitumia kivumishi cha nomino.(Solved)
Andika sentensi moja ukitumia kivumishi cha nomino.
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Faragha ni muhimu kwa binadamu kwani huwa ndio wakati ambapo mtu atakuwa akitulia pekee mahali na huku akijiuliza ni mema mangapi ameyatenda...(Solved)
Soma taarifa kisha fupisha kwa mujibu wa maswali yafuatayo.
Faragha ni muhimu kwa binadamu kwani huwa ndio wakati ambapo mtu atakuwa akitulia pekee mahali na huku akijiuliza ni mema mangapi ameyatenda siku hiyo, maovu mangapi ameyafanya, na kama siku hiyo ilikuwa ya manufaa au la.
Si binadamu wote ambalo wanapendelea kutumia wakati wao wa faragha kwa kupiga domo, nyumbani, kustawisha mabustani yao ya maua au mimea, au hata kuchukua kitabu au magazeti ya kusoma na kujifunza. Watu kama hawa huwa na fikira na mawazo mbalimbali juu ya umuhimu wa thamani ya wakati wa faragha. Watu kama hao utawakuta wakikusanyika katika makundi kwa matarajio ya kujinufaisha kwa mapato fulani au kujiingiza katika upigaji wa kamari. Wengine hunufaika wakasifu mafanikio yao ya siku ya mkusanyiko na baadhi yao ambapo hufanya mhanga wa michezo hii huibuka huku wakilaani na kuapiza bahati zao mbaya.
Kuna kundi jingine ambao hustahabu vilabu vya usiku kwa kujiliwaza au kujitumbuiza ili wapate kujituliza mawazo yao, wakayatafuta makali na kileo. Mwanzo wa ushirika kama huu huwa mzuri, watu huongea na kutoleana mawaidha yenye muafaka kiungwana kabisa. Lakini mara tu baada ya kuyakata makali haya kwa muda hivi, washiriki wake hupumbazwa na huanza kuyakata matindi mithili ya komba mpaka kiasi cha kubwata maneno ovyo ovyo na hatimaye kupoteza mbali fahamu. Ndipo kuruka kwa akili na kuanza zahama zenye kuonyesha utoto badala ya utu uzima. Kadiri makali hayo yanavyosiliwa kwa kuiva kwake, ndivyo wafuasi na mashabiki wake huyatumia kwa wingi na hata kuyaabudu, huyaabufu; huyabugia bila kujali uzito.
Na iwapo ndio kwanza wapokee mabunda yao, hakuna la kutia kikomo tafrija hizo ila uzito wa matendo ya ubadhirifu hujitokeza baada ya kurudi nyumbani, kulala fofofo na wazindukanapo siku ya pili yake ndipo wagundue walivyo taabani.
Mtindo wa matumizi ya faragha hutokea tangu mwanzo wa mazingira ya mtu; hivyo tangu utoto wake; tabia njema na zipasazo huhitajiwa kufunzwa. Sehemu kubwa ya mafunzo haya muhimu hutokana na malezi ya nyumbani chini ya uongozi wa mama na baba. Kama wasemavyo wahenga, mtoto akuavyo ndivyo alivyolelewa. Na mama mtu awe nyoka, hapana budi kuwa mwanawe naye atainuka kustahabu unyoke” wa mama yake. Hivyo ni wajibu wa wazazi kujenga mazingira yanayofaa kwa vizazi vya kesho kwa kuelekezwa namna yake. Ingewezekana himizo kubwa lingesisitizwa katika marekebisho ya tabia za wazazi kuwezesha manufaa yake. Ingewezekana, himizo kubwa lingesisitizwa katika marekebisho ya tabia za wazazi kuwezesha watoto kuiga mtindo au mitindo ya maisha yanayofaa. Kielezo chema ni kuwa na mzazi mwenye tabia njema kwa mtoto wake, rafiki zake na kwa jamii yake.
(a) Ni nini umuhimu wa faragha kwa binadamu kwa mujibu wa aya ya kwanza?
(b) Eleza jinsi watu wengine wanavyoharibu wakati wao wa faragha kwamambo ya upotovu
kwa kurejelea aya ya pili na ya tatu (maneno 30)
(c) Eleza mchango wa mzazi kwa mwanawe kuhusu matumizi bora ya wakati wa faragha.
Zingatia aya ya mwisho
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Jadili sababu tano zinazofanya "sheng" isiwe lugha ya taifa.(Solved)
Jadili sababu tano zinazofanya "sheng" isiwe lugha ya taifa.
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Eleza maana ya;
i).Mkembe.
ii).mkebe.(Solved)
Eleza maana ya;
i).Mkembe.
ii).mkebe.
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Uwezo wa kuyakumbuka mambo ni hazina kuu kutoka kwa mtu yeyote yule aliye hai. Uwezo huu wa kukumbuka ni mojawapo ya...(Solved)
Soma taarifa kisha fupisha kwa mujibu wa maswali yafuatayo.
Uwezo wa kuyakumbuka mambo ni hazina kuu kutoka kwa mtu yeyote yule aliye hai. Uwezo huu wa kukumbuka ni mojawapo ya shughuli changamano za ubongo. Ubongo wa mwanadamu hutekeleza shughuli hii kwa namna tatu. Kwanza ubongo hunasa jambo kisha
huliihifadhi. Baadaye huanzisha mfumo wa kutoa kilicho hifadhiwa. Ubongo ukiathirika kwa
namna yeyote katika moja wapo ya njia hizi, basi uwezo wa kuyakumbuka mambo huvurugika.
Ingawa inaaminika kuwa uwezo wa kukumbuka hurithishwa toka kizazi kimoja hadi kingine, wataalamu wa maswala ya kiakili wanabaini kuwa uwezo huu unaweza kuimarishwa.
Uimarishaji huu huhitajika mikakati madhubuti.
Njia mojawapo ya kustawisha uwezo wa kukumbuka ni kupitia kwa lishe. Vyakula vilivyosheheni vitamini B vyenye amino asidi husaidia kuimarisha uwezo wa kukumbuka. Vyakula kama hivi ni mboga, nyama (hasa maini), bidhaaa za soya, matunda, maziwa, ,bidhaa za ngano, samaki, pamoja na mayai. Vyakula vingine muhimu katika ustawishaji huu ni vile vyenye madini ya chuma. Madini haya huwezesha usambazaji wa hewa katika ubongo kwa wepesi. Vyakula ambavyo vina madina haya ni mboga za kijani, mawele, ndengu, soya, matunda kama maembe, ufuta (simsim) pamoja na nyama, hasa maini na mayai.
Ubongo wa mwanadamu aliye hai hufanya kazi kila wakati awe macho au amelala. Utendaji kazi wake huendeshwa na glukosi mwilini. Kwa hivyo, vyakula vyenye sukari hii ni muhimu kuliwa. Hata hivyo, lazima mtu awe mwangalifu na kuhakikisha kuwa mwili una kiwango cha sukari kisicho hatarisha maisha. Haya yanawezekana kwa kula vyakula vyenye nyuzinyuzi kama vile mboga na matunda.
Njia ya pili ni kupiga marufuku vileo kama pombe na nikotini. Vileo hivi huathiri utaratibu wa kunasa, kuhifadhi na kutoa yaliyo ubongoni.
Iwapo mtu ana tatizo la kuyakumbuka majina ya watu, ni muhimu kufanya mazoezi ya
kusikiliza kisha kurudia majina hayo wakati wa mazungumzo. Ni bora kulihusisha jina na sura
ya mtu. Kwa njia hii ubongo utanasa jina na kile kinacholengwa.
Woga na kuvurugika kiakili ni mambo mengine tunayopaswa kuepuka kila wakati. Ni kawaida mtu kupata woga wakati anapokabili jambo asilokuwa na uhakika na matokeo yake kama mtihani au mahojiano. Lakini anapaswa kuwa makini. Woga huo usikiuke mpaka na kumvuruga kiakili. Vurugu hizi huathiri kilichohifadhiwa ubongoni na pia namna ya kukitoa.
Halikadhalika, mwili wenye siha nzuri huhakikisha kuwa ubongo ni timamu. Wataalamu wengi wa siha wanakubali kuwa na mazoezi ya kunyoosha viungo hustawisha ubongo na hivyo kuhakikisha kuweko kwa uwezo wa kukumbuka mambo. Ni muhimu kuwa na taratibu ya kunyoosha viungo kila wakati. Fauka ya hayo, mazoezi ya kiakili, kama vile kusoma makala yanayovutia, kujaza mraba na michezo mingine kama mafumbo, vitenzi ndimi ni muhimu katika kustawisha uwezo wa kukumbuka.
Jamii ya watu wenye uwezo kuyakumbuka mambo ni ya jamii iliyopiga hatua kimaendeleo. Ni jukumu la kila mmoja wetu kuimarisha uwezo wa kukumbuka kila wakati.
a) Kwa maneno 60 – 65 fupisha mchango wa chakula katika uimarishaji wa uwezo wa
kukumbuka.
b) Fupisha aya tatu za mwisho kwa maneno 80 – 90
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Nyambua vitenzi vifuatavyo katika hali ulizopewa.(Solved)
Nyambua vitenzi vifuatavyo katika hali ulizopewa.
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Bainisha vishazi huru na vishazi tegemezi katika sentensi ifuatayo.
Nitaenda maktabani ingawa ninaumwa na kichwa.(Solved)
Bainisha vishazi huru na vishazi tegemezi katika sentensi ifuatayo.
Nitaenda maktabani ingawa ninaumwa na kichwa.
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita, tumeshuhudia mabadiliko na maendeleo makubwa kuhusu vyombo vya habari nchini Kenya. Hapo awali, redio ndicho chombo...(Solved)
Soma taarifa ifuatayo kisha ufupishe taarifa hii kulingana na maswali yanayofuata:-
Katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita, tumeshuhudia mabadiliko na maendeleo makubwa kuhusu vyombo vya habari nchini Kenya. Hapo awali, redio ndicho chombo cha habari cha kipekee kilichotamalaki kote nchini. Familia nyingi ziliweza kumiliki chombo hiki. Runinga ilikuwa miliki ya wachache, hasa mabwenyenye. Sasa hivi, hata akina yahe nchini na mashambani wanamiliki chombo hiki.
Runinga kama kifaa kingine chochote cha mawasilianao kina manufaa yake. Kwanza kabisa, ni nyenzo mwafaka ya kufundisha. Vipindi vinavyopeperushwa katika runinga huwa na mafunzo kemkem kwa mtu wa kila rika. Hali kadhalika, runinga huweza kuleta vipindi ambavyo huwafahamisha watu mambo yanayoendelea katika mazingira yao na duniani. Aidha, runinga ikitumika pamoja na michezo ya video huauni katika ukuzaji na ustawishaji ya kufundisha au kujielimisha. Michezo ya video, hasa ya kielimu huwafanya watu kujenga umakini pamoja na kuchua misuli ya ubongo na kuwafanya watu kuwa macho wanapofanya kazi.
Fauka ya hayo, televisheni ni chemichemi bora ya kutumbuiza na kuchangamsha. Hakuna mtu asiyependa kuchangamshwa. Televisheni ni mojawapo wa vyombo mwafaka vya kutekeleza hayo kutokana na vipindi vyake. Uburudishaji huu hupatikana kwa urahisi majumbani mwetu.
Vivyo hivyo, runinga hutumika kama nyenzo ya kuendeleza utamaduni, kaida na amali za jamii. Vingi vya vipindi vya runinga ni kioo ambacho huakisi mikakati na amali za jamii.
Kwa upande mwingine, hakuna kizuri kisichokuwa na dosari. Licha ya manufaa yake, televisheni imedhihirika kuwa na udhaifu wake. Kwanza, baadhi ya vipindi vya runinga na video hujumuisha ujumbe usio na maadili, kama vile matumizi ya nguvu za mabavu, ngono za kiholela, lugha isiyo ya adabu, ubaya kimavazi na maonevu ya rangi, dini, jinsia , kabila na utamaduni. Si ajabu kuwa baadhi ya vijana wetu wanaiga baadhi ya mambo haya. Vijana wetu siku hizi wameingilia ulevi wa pombe na afyuni, ngono za mapema kabla ya ndoa na mavazi yanayowaacha takribani uchi wa mnyama. Wengi wamekopa na kuyaiga haya kutoka katika runinga. Ukiwauliza wafanyacho, watakujibu kuwa ni ustaarabu kwani wameupata katika runinga.
Matumizi ya runinga na michezo ya video yasiyodhibitiwa huweza kuwa kikwazo cha mawasiliano bora miongoni mwa wanafamilia. Matumizi kama haya huwapa wanafamilia fursa ya kujitenga. Imedhihirika kuwa runinga haichangii kujenga uhusiano bora wa kijamii ukilinganisha na vyombo vingine vya burudani ambavyo hutoa nafasi ya watu kutangamana na kujenga uhusiano bora, televisheni haichangii haya. Badala yake, tajriba ya televisheni huwa na kibinafsi. Hali hii inapotokea katika kiwango cha familia, televisheni inaweza kutenganisha wazazi na watoto wao.
Halikadhalika, runinga na video aghalabu hueneza maadili yasiyofaa. Mathalan, baadhi ya vipindi vya televisheni huendeleza hulka ya kuhadaa, ngono za kiholela, kuvunjika kwa ndoa, n.k. Hulka hizi zisizoendeleza maadili ya kijamii huchukuliwa kama zinazofaa na zinazofuatwa na waliostaarabika. Huu ni upotovu.
Isitoshe, baadhi ya matangazo huhimiza matumizi ya madawa ya kulevya kama tembo na sigara. Vitu hivi vinapotangazwa, hupambwa kwa hila na udanganyifu mwingi ambao huwavutia vijana na watoto wengi. Si ajabu mtu anapouliza wanaoutumia vileo hivi walivyoanza, watajibu kutokana na athari za matangazo katika runinga na vyombo vingine.
Utafiti umeonyesha kuwa vipindi vya runinga na video ni chanzo cha matumizi ya nguvu za mabavu miongoni mwa wanafunzi. Wazazi wengi huchukulia vibonzo katika televisheni kuwa vinalenga kuburudisha tu na havina ubaya wowote. Lakini ukweli ni kuwa vipindi vingi vya vibonzo hushirikisha matumizi ya hila na nguvu za mabavu. Haya huibusha hamu ya vijana na watoto huyaiga.
Kwa hivyo, ni muhimu wazazi na jamii kutambua madhara ya televisheni. Utambuzi huu utawafanya waelekeze vijana na watoto jinsi ya kutumia televisheni na video ili kuepukana na madhara yake.
Maswali
(a) Ukitumia maneno 50-60, fupisha manufaa ya runinga
(b) Fupisha hasara za runinga ukitumia maneno 70-80
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Toa maneno yenye maana sawa na haya.
i. Izara
ii. Anisi(Solved)
Toa maneno yenye maana sawa na haya.
i. Izara
ii. Anisi
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)