RIWAYA. K Walibora: Kidagaa Kimemwozea. “Naam walisimuliana kumhusu msichana ambaye alipindua mtazamo wa wengi kuelekea watu waitwao walemavu.” a) Eleza jinsi msichana anayerejelewa alivyoleta mabadiliko ya mtazamo. b)...

      

RIWAYA.
K Walibora: Kidagaa Kimemwozea.
“Naam walisimuliana kumhusu msichana ambaye alipindua mtazamo wa wengi kuelekea watu waitwao walemavu.”
a) Eleza jinsi msichana anayerejelewa alivyoleta mabadiliko ya mtazamo.
b) Fafanua kwa kutolea mifano mtazamo wa watu kwa walemavu kabla ya msichana kuleta mapinduzi katika riwaya ya kidagaa.
c) Kwa kutolea mifano mingine, fafanua maudhui ya utengano.

  

Answers


Kavungya
(a) Imani iliajiriwa kazi kwa mwalimu majisifu. Alikuwa mtu wa kwanza kuwaona na kuwatendea utu watoto walemavu wa Majisifu (uk. 30) Majisifu aliwahurumia mkewe na Imani kwa ulezi wa watoto vilema. (uk. 137) Na kitambo aliwachukia na kuwaita masimbi na mashata.

(b) (i) Mtemi Nasaba Bora alimpenda msichana akiwa safarini na alipogundua alikuwa kiguru alimkataa (Uk. 100)
(ii) Dora aliwaficha watoto wake walemavu wageni walipoingia. (uk. 45)
(iii) Mashaka aliwachukia na kuwadharau watoto walemavu wa Amu yake. Aliwaona kuwa wasiokamilika au kama madubwasha.
(iv) Chwechwe Makweche alishabikiwa na watu wengi alipoiletea sifa Songoa F.C. lakini alipovunjika fupaja hawakushughulikia hadi akakatwa mguu.
(v) Matuko Weye alifungiwa Sali na kupigwa (wazimu).

(c) (i) Maakazi ya wakoloni yalij itenga nay a Wafrika.
(ii) Madhubuti baada ya kutoka Urusi alihamia kibanda cha Amani akajitenga na wazazi wake.
(iii) Ben Bella alipogundua lowela dadake ni rafikiye Mtemi Nasaba Bora alijitenga na Mashaka.
(iv) Uhasama wa mtemi ulifanya Majisifu nduguye kujitenga naye (Hakusherehekea na Mtemi kurudi kwa Madhubuti).
(v) Mtemi Nasaba Bora alimtaliki mkewe Zuhura kwa tuhuma za kuwa na uhusiano na Amani. (vi) Amani aliishi katika vibanda vilivyokuwa vimetengana na Kasri la Mtemi Nasaba Bora.
(vii) Mtemi nasaba Bora alitengana na Uhai kwa kujitia kitanzi kwa sababu ya shida zajimbo la Sokomoko.
(viii) Mwalimu Majisifu aliposhindwa kutoa mhadhara Wangwana katika chuo cha mkokoteni alijitenga na wanavyuoni na kurejea nyumbani.

Kavungya answered the question on October 4, 2019 at 13:28


Next: Badilisha sentensi ifuatayo iwe mazoea kwa kutumia kirejeshi “O” Mtoto anayelia huchapwa
Previous: Andika kinyume Wavulana watatu wanaingia darasani kwa haraka.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions


  • Badilisha sentensi ifuatayo iwe mazoea kwa kutumia kirejeshi “O” Mtoto anayelia huchapwa(Solved)

    Badilisha sentensi ifuatayo iwe mazoea kwa kutumia kirejeshi “O”

    Mtoto anayelia huchapwa

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Soma shairi lifuatalo kisha uyajibu maswali.Mungu naomba subira, subira nayo imaniImani iliyo bora, bora hapa dunianiDuniani mwa kombora, kombora nayo hianiHiani pamwe ukora wenye kuhini.Kuhini...(Solved)

    Soma shairi lifuatalo kisha uyajibu maswali.

    Mungu naomba subira, subira nayo imani
    Imani iliyo bora, bora hapa duniani
    Duniani mwa kombora, kombora nayo hiani
    Hiani pamwe ukora wenye kuhini.

    Kuhini kwenye kiburi, kiburi na ufidhulu
    Ufidhuli wa kudhuri, kudhuri wangu muwili
    Muwili hata kiclari, kidari kuwa thakili
    Thakili kisinawiri, kisinawiri misuli.

    Misuli kuwa hafith, hafifu kama muwele
    Muwele wa hitilafu, hitilafi ya nduwele
    Nduwele kutakilifu, kutakilifu milele
    Milele kutoniafu, kutoniafu na vishale.

    Vishale vinitomele, vitomele vikwato
    Vikwato pia maole, maole kufanya mito
    Mito ya matozi tele, tele mithili kitoto
    Kitoto kilo vipele, vipele vyenye fiakuto.

    Fukuto lanipa neno, neno hili kutamka
    Kutamka wazi vino, vino subira kutaka
    Kutaka imani mno, mno n’sipate wahaka
    Wahaka wa matukano, matukano na mashaka.

    Mashaka haya ya leo, leo yawe yamepita
    Yaniepita na vilio, vilia vipishe nyota
    Nyota njema ing’arao, ing’arao kunikita
    Kunikita salamani, salamani nikadata.

    a) Kwa nini nafsi neni inaomba subira na amani?
    b) Shairi hili ni la aina gani kwa kuzingatia
    (i) Mpangilio wa maneno
    (ii) Mpangilio wa vina.
    c) Kwa kutolea mifano eleza mbinu mbili za lugha zilizotumika katika shairi
    d) Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari.
    e) Kwa kutolea mifano, eleza jinsi uhuru wa kishairi ulivyotumiwa kutekeleza arudhi

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Tumia amba – rejeshi na nomino ulizopewa katika sentensi kuonyesha upatanisho wa kisarufi. i) ukwenzi ii) sandukuni.(Solved)

    Tumia amba – rejeshi na nomino ulizopewa katika sentensi kuonyesha upatanisho wa kisarufi.
    i) ukwenzi
    ii) sandukuni.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha mofimu katika neno hili; Alinizindusha(Solved)

    Bainisha mofimu katika neno hili;
    Alinizindusha

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Taja ngeli za nomino zifuatazo; i) Muundo ii) Senti.(Solved)

    Taja ngeli za nomino zifuatazo;
    i) Muundo
    ii) Senti.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Tumia neno kitoto kama; i) kivumishi ii) kielezi(Solved)

    Tumia neno kitoto kama;
    i) kivumishi
    ii) kielezi

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Taja na ueleze pingamizi zozote tano zinazokwamiza juhudi za kukuza Kiswahili (Solved)

    Taja na ueleze pingamizi zozote tano zinazokwamiza juhudi za kukuza Kiswahili

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Andika katika ukubwa wingi. Ukitaka kumla nguruwe chagua aliyenona.(Solved)

    Andika katika ukubwa wingi.
    Ukitaka kumla nguruwe chagua aliyenona.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Changanua sentensi hii kwa kutumia kielelezo cha visanduku. Mzee aliyemdhulumu msichana yule ametiwa mbaroni tena.(Solved)

    Changanua sentensi hii kwa kutumia kielelezo cha visanduku.
    Mzee aliyemdhulumu msichana yule ametiwa mbaroni tena.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Eleza juhudi zozote tano za serikali ya Kenya katika kukuza Kiswahili (Solved)

    Eleza juhudi zozote tano za serikali ya Kenya katika kukuza Kiswahili

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • WAJIBU Sisi vijana ni wa taifa. Hatuna budi kutumikia umma kwa moyo wetu wote.Hakuna haja ya kulaza damu ikiwa taifa linatuhitaji. Ni lazima tuwe shupavu kwa...(Solved)

    WAJIBU

    Sisi vijana ni wa taifa. Hatuna budi kutumikia umma kwa moyo wetu wote.Hakuna haja ya kulaza damu ikiwa taifa linatuhitaji. Ni lazima tuwe shupavu kwa mambo yote. Tuwe wenye busara, adabu njema na ari ya kutenda kazi kwa moyo wa utu. Ni muhimu kabisa kulinda, kutumikia na kuendeleza taifa hili changa katika mbinu zake na mipango yake yote kuhusu zaraa, elimu, uchumi, ulinzi na mipango yote ya maendeleo ya ustawi wa nchi na jamii. Inatupasa tuelewe ujamaa wetu na jinsi ya kupambana na ubepari, ukabila, ukupe, unyonyaji na ukoloni mamboleo. Hii itaondoa kabisa jasho letu. Inatubidi sisi vijana tujifunze jinsi na namna ya kuwa watu bora.
    Elimu tuipatayo kutoka nyumbani, shuleni na katika jamii, lazima igeuze fikira zetu. Elimu hiyo lazima tuitumie ili itupatie uwezo wa kuelewa mema na mabaya maishani mwetu. Ni bora tujue wajibu wetu katika kufikiri, kusema na hata kutenda kufuatana na wajibu huo kwa mioyo na dhamiri safi. Tuwe vielezo kwa wengine. Hasa tujitayarishe kuwa wazazi na viongozi bora wa kesho. Mno mno tuwe wazalendo na raia wema wa taifa hili changa. Tuhimize na kuendeleza utamaduni wetu wa lugha yetu ya taifa. Hatimaye tutambue usawa wa kila binadamu, popote alipo bila kujali taifa, kabila, rangi na hata dhehebu yake.
    Tujifunze kujishutumu. Pia tukubali kusahihishwa makosa yetu na watu wengine. Hasa tuwe nguzo, kinga na ngao ya nchi yetu inapopigwa adharusi.
    Acha nirudie kusema tena kuwa ni shabaha yetu sisi vijana kuwa na nidhamu njema. Nidhamu njema ni chanzo cha asili cha siha ya ujamaa na kujitegemea. Kwa hivyo, uongozi bora na bidii, ushirikiano mzuri na kujishughulisha. Uchaguzi bora wa viongozi na mifano mizuri ni kurunzi ya maendeleo ya ustawi wetu.

    (i) Ni nguzo zipi ambazo kifungu hiki kimezipa kipaombele kwamba zitasimamisha ustawi
    na maendeleo ya nchi kutokana na vijana? Jadili kwa maneno thelathini
    (ii) Vijana wameshauriwa wafanye mambo mengi mema. Jadili kinyume cha ushauri huu
    ukitumia maneno yako mwenyewe

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Eleza matumizi ya "ku" katika sentensi hii. Kucheza kwake kulifurahisha wengi(Solved)

    Eleza matumizi ya "ku" katika sentensi hii.
    Kucheza kwake kulifurahisha wengi

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi sahihi ukitumia kitenzi — nywa katika kauli ya kutendesha (Solved)

    Tunga sentensi sahihi ukitumia kitenzi — nywa katika kauli ya kutendesha

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Geuza sentensi hizi katika kauli ulizopewa kwenye mabano; i) Mwalimu aliyakataa maoni ya wanafunzi. (kutendwa) ii) Msamaria mwena alimuokoa mtoto aliyekuwa ametupwa pipani. (kutendata)(Solved)

    Geuza sentensi hizi katika kauli ulizopewa kwenye mabano;
    i) Mwalimu aliyakataa maoni ya wanafunzi. (kutendwa)
    ii) Msamaria mwena alimuokoa mtoto aliyekuwa ametupwa pipani. (kutendata)

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Yakinisha sentensi hii Mpishi asipokuwa mwangalifu chakula hakitaiva vizuri (Solved)

    Yakinisha sentensi hii
    Mpishi asipokuwa mwangalifu chakula hakitaiva vizuri

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Ainisha viwakilishi katika sentensi hii Usibanduke papa hapa (Solved)

    Ainisha viwakilishi katika sentensi hii
    Usibanduke papa hapa

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Uchumi wa soko huria ni hali ya kiuchumi ambapo itokeapo amali, shughuli na harakati zote za kiuchumi ghairi ya zile...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali

    Uchumi wa soko huria ni hali ya kiuchumi ambapo itokeapo amali, shughuli na harakati zote za kiuchumi ghairi ya zile ambazo ni za lazima kwa serikali au dola kama ulinzi, sheria na
    mpangilio wa jamii huwa huria kwa watu binafsi. Msingi wa soko huria, sifa kuu ya utandawazi, ni kuibua na kudumisha mazingira na hali zinazochochea na kumruhusu mtu yeyote kuongozwa na hawaa, au matamanio ya kibiashara anayoyaona sawa pasi na hofu ya kuingilia na udhibiti wa serikali.
    Mazingira hayo yanawapa watu satua ya kufanya maamuzi kuhusu hatima yao ya kiuchumi, uamuzi kuhusu suala la ajira yao, matumizi ya mtaji kipato na harija zake, na uwekezaji mzima. Suala mojawapo linaloibuka kuhusiana na mfano wa soko huria ni kuweka mipaka bainifu na wazi baina ya amali na shughuli zinazohusishwa na serikali na zile ambazo huachwa huria kwa watu. Kwa mfano, inaaminiwa kuwa haki ya kuishi na kulindwa dhidi ya shambulizi, liwe la kijambazi au la kigaidi, ni ya kimsingi ambayo haiwezi kuhusishwa na uwezo wa kiuchumi wa mtu binafsi. Aidha huduma za kimsingi za afya nazo zinaingia katika kumbo hili. Ikiwa huduma hizi zitaachwa huria pana uwezekano mkubwa kuwa zitaishia kuwa istihaki ya wenye mtaji na kipato cha juu tu.
    Licha ya kuwepo kwa sheria au kanuni huria kutoka nyanja maalum, hutokea hali ambapo adhibiti wa kiserikali ni lazima. Hii hutokea pale ambapo ipo haja ya kuyalinda mazingira hasa kutokana na uchafuzi wa viwanda au tasnia. Aidha udhibiti huo ni lazima pale ambapo haki za watu wengine zinahusika: yaani ikiwa uhuru wa hata mtu mmoja unaadhirika kutokana na sera hizo pana haja ya kuingilia ili kuisawazisha hali yenyewe.
    (a) Andika kwa muhtasari maana ya uchumi wa soko huria kulingana na taarifa hii.
    (maneno 25-30)
    (b) Eleza mawazo makuu yanayojitokeza katika aya ya pili na ya tatu.
    (maneno 70-75)

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Toa maana ya semi Shupaa mwili.(Solved)

    Toa maana ya semi Shupaa mwili.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Taja dhamira ya sentensi ifuatayo Kimbia mbio ulete sahani (Solved)

    Taja dhamira ya sentensi ifuatayo
    Kimbia mbio ulete sahani

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Vijana wa siku hizi hujifikiria kuwa wao ni bora kuliko wazee wao. Wao hujifikiria kuwa wameelimika zaidi, wana busara...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali

    Vijana wa siku hizi hujifikiria kuwa wao ni bora kuliko wazee wao. Wao hujifikiria kuwa wameelimika zaidi, wana busara zaidi, wanauelewa ulimwengu vizuri zaidi na wanaweza kujiamulia hatima yao bila uongozi wa wazazi wao. Wazee kwa upande wao, hawakubali kabisa madai ya aina hiyo. Kwao ni maasi tu. Wanachojua wazee kwa hakika ni kuwa vijana wa siku hizi hawaajibiki kwa lolote, wamedekezwa mno na wanapenda sana nafsi zao. Kwa sababu hiyo, vijana wanahitaji uongozi na ushauri wa wazeee.
    Je, kuishi kwingi ni kuona mengi? Ingawa wazee wanafikiria wanajua mengi kwa sababu ya umri wao, vijana hupenda sana kukosoa fikira za wazee wao. Hawakubali imani na itikadi za wazee wao. Kwa mfano; vijana hupendelea mitindo ya mywele ambayo wazee wao hufikiria kuwa kichaa tu.
    Wazee husifiwa sana enzi zao. Husifia jinsi walivyolelewa kwa kuchapwa na kufanyishwa kazi zinazohitaji uvumilivu mkubwa kama vile kuchanja kuni, kufyeka misitu, kutayarisha mashamba, kuwinda na kadhalika. Kwa sababu ya malezi hayo, wazee husema wao walirithi nidhamu nzuri na ushujaa. Vijabna kwa upande wao hawaoni chochote cha kujivunia katika zama za wazee wao; wao hufikiria kuwa wazee wao walilelewa kwa ukatili kwa sababu zama zao zilikuwa enzi za giza, kabla ya majilio ya uungwana na ustaarabu wa kisasa.
    Wazee husifia kuwakumbusha vijana ule msemo mashuhuri wa wahenga usemao kuwa ‘mwacha mila ni mtumwa.’ Kwa maoni ya wazee, vijana wengi wamekuwa watumwa kwa sababu wao huonyesha kwa vitendo kuwa hawadhamini desturi za wazee wao. Ka mfano; vijana hawafuati miiko ya jadi, hawapendi kuhudhuria sherehe za kienyeji, kwa mfano sherehe za kutoa makafara. Vijana pia hawapendi ngoma za kitamaduni, na isitoshe vijana hawazionei fahari koo zao. Vijana hawakubali kuwa wao ni watumwa wa mtu yeyote. Mila wanazosifia wazeee wao si vitu vyenye umuhimu wowote kwa vijana. Kwa mfano; baadhi ya miiko ni kisayansi. Kuhusu ukoo, si vijana wengi wanaona umuhimu wake. Ukoo na kabila zilikuwa muhimu zamani wakati ambapo kulikuwa hakuna serikali, bima na hata kazi ya mtu binafsi. Mambo haya sasa ni kama masalia ya zamani ambayo yamepitwa na wakati.
    Je, vijana hupenda sana burudani na anasa tu kama wanavyodai wazee! Wazee wengi hufikiria kuwa vijana hupoteza muda wao mwingi kujitafutia anasa na burudani kwa mfano vijana wengi hurandaranda barabarani au mitaani wakisingizia kupunga hewa. Wengine huenda sinema na kuhudhuria dansi na karamu zisizo na manufaa. Vijana kwa upande wao hawaoni kinachowawasha wazee wao; pilipili wasioila yawashia nini?
    (i) Katika makala haya wazee wana malalamiko yapi kuhusu vijana? (maneno 50-60)
    (ii) Msemo unaosema “Mwacha mila ni mtumwa” unathibitishwa vipi katika maoni ya wazee
    katika makala haya? (maneno 15- 25)

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)