RIWAYA. K Walibora: Kidagaa Kimemwozea. “Kama ilivyo ada yake usiku uliotangulia alikuwa kenda kwa shughuli fulani alizoziita kusuluhisha mgogoro wa ardhi.” Eleza migogoro inayojidhihirisha katika riwaya ya Kidagaa...

      

RIWAYA.
K Walibora: Kidagaa Kimemwozea.

“Kama ilivyo ada yake usiku uliotangulia alikuwa kenda kwa shughuli fulani alizoziita kusuluhisha mgogoro wa ardhi.”
Eleza migogoro inayojidhihirisha katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.

  

Answers


Kavungya
Mvutano katikajamii ya Sokomoko.
(i) Mtemi na Madhubuti.
Madhubuti anakataa ufisadi, matendo maovu ya mtemi.
(ii) Mtemi na Amani.
Mtemi alishuku uhusiano kati ya Amani na Zuhura mkewa akamwadhibu vibaya. Amani alitaka kufahamu ukweli wa kifo cha babu Chichir. Hamadi na kufungwa kwa amu Yusuf Hamadi.
(iii) Mtemi na Zuhura.
Zuhura alikashifu ukatili wa Mtemi, kutowajibikia ndoa. Mtemi kumtaliki Zuhura kwa kumshuku kuwa mzinzi.
(iv) Dora na majisifti.
Dora hakufurahia ulevi na kutosaidiwa ulezi wa watoto walemavu. Majisifu anamlaumu Dora kwa kuzaa watoto walemavu.
(v) Mtemi na Lowela.
Lowela anamlaumu Mtemi kwa kuwafungia Imani na Amani kwa tuhuma ya kuua kitoto.
(vi) Majisifu na Mtemi.
Mtemi anakashifu aibu inayotokana na Majisifu kuwa mievi. Majisifu hafurahii ukatili wa mtemi k.m kumtesa Amani.
(vii) Mashaka na Ben bella.
Ben Bella anavunja uhusiano na Mashaka kwa sababu Mtemi Nasaba Bora alikuwa na uhusiano na dadake Lowela.
(viii) Imani, Amani na Wauguzi.
Wauguzi walikosa kuwajibikia kazi yao (mapuuza kitoto).
(ix) Mamake Imani na Askari.
Askari walimlazimisha ahame kutoka shambani licha ya kuwa na hati miliki.
(x) Majinuni na Michelle.
Tamaa ya michelle kutaka nyumba kubwa inapojengwa haimvutii (vyumba kumi na tatu). (xi) Amani na Majisifu.
Wizi na mswada wa Amani na kuchapishwa
(xii) Chwechwe makweche najamii.
Jamii kujivunia matokeo mazuri ya Songoa FC na kutomshughulikia alipovunjika fupaja. (xiii) Oscar Kambora na Mtemi.
Kunyakuliwa kwa shamba lao na askari kusababisha kifo cha mamake Imani na kuchomewa nyumba.
(xiv) Amani na wanafunzi chuoni Songoni. Walimwonea ghere kwa ufanifu wake masomoni kusababisha afungwe.
(xv) Matuko weye na Serikali (Uingereza na Sokomoko)
Baada ya kupigana katika vita vikuu vya dunia hakuzawadiwa alibaki kuwa kichaa.
(xvi) Mtemi aria mvutano nafsini mwake kuhusu maovu aliyoyatenda (uk 152).
Kavungya answered the question on October 4, 2019 at 13:31


Next: Ainisha nomino zilizopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo; Kikosi cha askari kiliwanasa wezi waliohusika katika wizi wa ng‘ombe katika tarafa ya kindondoni.
Previous: Andika sentensi tatu ambazo zaweza kuwa sahihisho la sentensi hii:- Kule ndimo alipoingia

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions