Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Viongozi wa Cheneo walionekana kutowajibika. Thibitisha kauli hii kwa kurejelea Tamthilia yote.

      

Viongozi wa Cheneo walionekana kutowajibika. Thibitisha kauli hii kwa kurejelea Tamthilia yote.

  

Answers


Kavungya
(i) Meya kukosa kustawisha mji wa Cheneo na kulinganisha ufanisi wake na miji midogo na dhaifu.
(ii) Meya kukataa kuonana na viongozi wa wafanyakazi. Na anapokutana nao anapuuza malalamishi yao.
(iii) Meya anapuuza mpango wa miaka kumi na kusema kuwa ana mipango ya millennia.
(iv) Mikutano ya baraza kufanywa kwa nadra, kama tunavyoelezwa na Diwani I kuwa inafanywa hasa wakati jambo kama mgomo kutokea.
(v) Meya anatoa ahadi za uongo. Alidanganya kuwa shehena ya dawa iko katika bahari kuu.
(vi) Uchafu unaenea kila mahali na uvundo kukoleza hata ndani mwa majumba kwa sababu wafanyakazi wamegoma.
(vii) Meya anakataa kuongea na wanahabari kwa kisingizio kuwa ana wageni.
(viii) Badala ya kutunza fimbo ya Meya, wanakula kiapo kuficha sin za wizi wa fimbo.
(ix) Askari badala ya kutoa ulinzi wanawafursha watu kutoka mjini.
(x) Badala ya kustawisha Cheneo, anaagiza nyimbo za kizalendo zichezwe kabla na baada ya habari miaka hamsini baada ya uhuru.
(xi) Viongozi kujiongeza mishahara kiholela, kujilipa overtime na marupurupu ilhali baraza lina nakisi.
(xii) Meya kujifanya kuwa hajui watu wa Cheneo wanateseka (njaa, umaskini, magonjwa). Amefumbia macho matatizo yao.
(xiii) Meya kutoshughulika kuboresha elimu Cheneo na kuwapeleka wanawe ng’ambo kusomea huko.
(xiv) Diwani I na Diwani II wamekosa kuwajibika kama washauri wa meya wanampotosha badala ya kumkosoa.
(xv) Meya kutegemea ushauri wa mtu asiye na taaluma wala sifa za uongozi kwa mfano kesi ya mwanakandarasi, kuuza fimbo.
Kavungya answered the question on October 4, 2019 at 13:35


Next: Jaza viashiria vya uradidi vya mbali kidogo. i) Mbuzi – ii) Gazeti –
Previous: Tunga sentensi mbili kuonyesha matumizi mawili ya po – ya wakati.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions