Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

“Damu Nyeusi.” (K Walibora) “Tangu hapo ameendelea kuwa mwanafunzi mzuri ... Amejifunza kuwa hakuna mahali kama nyumbani.” (i) Eleza muktadha wa dondoo hili. (ii) Bainisha mifano mitatu ya...

      

“Damu Nyeusi.” (K Walibora)
“Tangu hapo ameendelea kuwa mwanafunzi mzuri ... Amejifunza kuwa hakuna mahali kama nyumbani.”
(i) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(ii) Bainisha mifano mitatu ya mbinu rejeshi na kiini cha mifano hiyo katika hadithi.

  

Answers


Kavungya
i) (i) Ni maelezo ya mwandishi.
(ii) Akimrejelea Fikirini. Alikuwa Marekani kwa masomo.
Baada ya kuachwa na basi lililoendeshwa na mweupe (kubaguliwa) alianza kuona umuhimu wa nyumbani.

ii) (i) Baada ya kuachwa na basi, alipotembea kando kando ya barabara kwenye kijia cha wapita njia akipepesuka kama mievi alikumbuka siku za hfahari alipotafuta Waragi Kibuye Kampala gongo Ubungo Tanzania na Changaa Mathare — Nairobi.
(ii) Alipotembea akipepesuka kwa baridi kali na theluji nyeupe aliona kila kiu cheupe na mweusi hana sauti na kudhalilishwa kwa mweusi na mweupe, alikumbuka maneno ya rais mstaafu moi, “msifikiri kwamba Mzungu anatupenda sisi watu weusi.”
(iii) Alipokutana na kukaribiana na Fiona Mmarekani mweusi alikumbuka dada zake Wahaya aliokutana nao akiwa chuo cha walimu Mwanza, dada Waganda alipozuru Uganda Magharibi, dada Wakamba alipozuru Kitui..
(iv) Alipokuwa mkahawani alipewa chakula cha marekani ambacho hakukipenda alitamani chakula cha kwao ugali kwa mienda, wall na pilau, matoke na muhogo.
Kavungya answered the question on October 4, 2019 at 13:40


Next: Kanusha. Wanafunzi wale wala wakiongea.
Previous: KIKAZA. ‘Wenzangu wote mwafahamu hadithi ya kobe?’ Mzee babu aliuliza. Wote walijibu, “ndio Eleza umuhimu wa hadithi ya kobe ukirejelea hadithi ya Kikaza.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions