“Tazamana na mauti” S. A. Mohamed. Basi, minyororo ya kufungika kwa hamu ya Uingereza, ilizidi kufunga moyo wake. Lini angepata na ya kupenya kwenye chungio ...“ a)...

      

“Tazamana na mauti” S. A. Mohamed.
Basi, minyororo ya kufungika kwa hamu ya Uingereza, ilizidi kufunga moyo wake. Lini angepata na ya kupenya kwenye chungio ...“
a) Eleza njia ambazo zingetumiwa kutimiza hamu ya Uingereza.
b) Tamaa mbele mauti nyuma. Fafanua ukirejelea hadithi ya Tazamana na Mauti.

  

Answers


Kavungya
(a) (i) Lucy alitamani ajifanye mahututi na maradhi yake hayatibiki hapa pao. Lakini alifahamu kufika ubalozi wa Uingereza ulijua ujanja huu na lazima daktari wao atoe ithibati kwanza.
(ii) Ajifanya anaenda kusoma. Ilibidi apate shule ambayo ingemkubali na awe na mtaji mkubwa
wa fedha. Hakupita vizuri kidato cha sita na hakuwa na pesa.
(iii) Asema yeye ni mtalii tu, lakini angekuwaje mtalii na mifuko yake iwe mitupu? Hangekubaliwa Uingereza.
(iv) Rai ya kuolewa na mwanamume kutoka Uingereza. Kwa vile alikuwa na sura ya kuvutia lakini huyo mwanamme angetoka wapi?

(b) (i) Kuwa na hamu kuu ya kupata kitu kasha matatizo yanakuandama.
(ii) Lucy alikuwa na tama kubwa ya kuwa tajiri haraka. Alitamani kwenda London iii atomize ndoto yake.
(iii) Alitamani kupata mwanamme wa kumuoa iii aweze kufika Uingereza.
(iv) Alikuwa na tama ya kupata raha huko London baada ya kurithishwa.
(v) Alitamani kuwa kama Yule niwanamke aliyekuwa katika Sinema.
(vi) Alidhani angekwenda London kama mkimbizi apewe pesa na ajifiche kutafuta pesa zaidi.
(vii) Aliolewa na (mzee na kwenda Uingereza na akamtunza lakini kabla ya kuhalalisha urithi wa mali ya Crusoe, Lucy kwa furaha alienda kujitembeza mjini na akapata ajali na kufa.
Kavungya answered the question on October 4, 2019 at 13:45


Next: Eleza maana ya misemo ifuatayo :- (i) Giza la ukata… (ii) Meza mate machungu
Previous: Taja aina za vitenzi vilivyopigiwa mstari katika sentensi iuatayo Mama amewahi kupika jikoni

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions