Soma kifungu kifuatacho kasha ujibu maswali. Ndimi Kisoi, dume laukoo mtukufu.

      

Soma kifungu kifuatacho kasha ujibu maswali

Ndimi Kisoi, dume laukoo mtukufu.
Ulojipambanua kwa mabingwa
Wachezaji hodari wa ngoma
Ndimi dume liloingia nyanjani
Makoo yakatetemeka
Yakangangania gozi kusakata ngoma.

a) Tambulisha kipera kinachojitokeza katika kifungu hiki.
b) Eleza sifa tano bainifu za kipera hiki katika fasihi simulizi.
c) Fafanua umuhimu wa kipera hiki.

  

Answers


Kavungya
(a) Majigambo au Vivugo.

(b) (i) Hutungwa na kughaniwa na mhusika mwenyewe.
(ii) Hutungwa kwa usanii mkubwa sana. Kwa mfano matumizi ya sitiari.
(iii) Anayejigamba hutunga kivugo kuguatia tukio mahususi katika maisha yake michezoni, vitani, kesi, jando na kadhalika.
(iv) Huwa na matumizi ya chuku. Mtunzi hujisifu kupita kiasi kwa kutaja mafanikio na mchango wake.
(v) Majigambo hutungwa papo hapo. Lakini mengine huandikwa na kughaniwa baadaye.
(vi) maudhui makuu ya maj igambo huwa ushuj aa.
(vii) Kwa kawaida hutungwa na kughaniwa na wanaume.
(viii) Anajigamba huweza kuvaa maleba yanayoaana na kazi yake. Pia anaweza kubeba baadhi ya vifaa vya kazi.
(ix) Anayejigamba huweza kutaja na kusifu ukoo/nasaba yake.
(x) Mara nyingi wanaojigamba huwa Walumbi au washairi.

(c) (i) Hukuza ubunifu. Mtunzi huirnarisha uwezo wake wa kubuni mitindo mipya ya utunzi na uwasilishaji anapoendelea kubuni majigambo.
(ii) Ni nyenzo ya burudani. Waliohudhuria sherehe huongolewa na majigambo.
(iii) Kukuza ufasaha wa lugha. Watunzi wengi wa majigambo huwa Walumbi ambao ni Weledi wa lugha.
(iv) Hudumisha utu na hutambulisha mwanamme katika jamii. Wanaume walipaswa kuwa Jasiri katika jamii kwa sababu ya uchokozi uliokuwepo.
(v) Ni nyezo ya kufanya watu waheshimiwe. Hufanya wanaume kuwa na an ya kuwa mashujaa.
Kavungya answered the question on October 4, 2019 at 13:49


Next: Unda vitenzi kutokana na :- (i) Mkufunzi (ii) Maeneo
Previous: Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia vishale Mwalimu huyu mzuri anafundisha darasani.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions