Mwezi jana, Serikali ya kitaifa na zile za kaunti ziliwasilisha makadirio yao ya bajeti, miezi miwili kabla ya mwaka wa kifedha kuisha kama zinavyohitajika na...

      

Mwezi jana, Serikali ya kitaifa na zile za kaunti ziliwasilisha makadirio yao ya bajeti, miezi miwili kabla ya mwaka wa kifedha kuisha kama zinavyohitajika na katiba. Serikali hizo zilieleza jinsi zinavyonuia kutumia mabilioni ya pesa kufadhili shughuli zao mwaka ujao wa kifedha wa 2013/2014.
Serikali ya Rais Uhuru Kenyatta ilisema itatumia shilingi 1.6 Trilioni kufadhili maendeleo na shughuli za sekta na idara zake tofauti. Makadirio haya ambayo yaliwasilishwa na kiongozi wa walio wengi bungeni, Bw Aden Duale. Hata hivyo yalikosa kueleza jambo moja muhimu – jinsi kitita hicho kitakavyopatikana. Nasema hivi kwa sababu kuna habari ambazo zimenipa tumbojoto na wasiwasi mkubwa. Imebainika kuwa kufikia mwishoni mwa Machi mwaka huu, Kenya ilikuwa inadaiwa Shilingi 1.8 Trilioni na wafadhili wa humu nchini na kigeni.
Kama habari hizi hazijakushtua sitakulaumu kwa sababu huenda ukawa hujui ukubwa wa kiasi hiki cha fedha. Ili uweze kuelewa, nitazigawanya fedha hizi miongoni mwa wakenya milioni 40 ili tujue kila mkenya anadaiwa kiasi gani. Kila mkenya nchini, wakiwemo watoto na wazee wakongwe, anadaiwa Shilingi 45,000 ! Hivyo basi ili deni hili liweze kulipwa, kila mkenya atalazimika kutoa kiasi hicho cha fedha.
Ni deni ambalo Rais Uhuru Kenyatta alirithi kutoka kwa mtangulizi wake, Rais Mwai Kibaki ambayo utawala wake ulivunja rekodi ya kukopa. Wahenga hawakukosea waliposema dawa ya deni ni kulipa. Deni hili linapaswa kumkosesha usingizi Rais Kenyatta ambaye anapaswa kutafuta njia za kulilipa bila kuathiri uchumi, maendeleo na utekelezaji wa ahadi nyingi alizowapatia wakenya wakati wa kampeni.
Hili halitafanyika kama serikali itatenga fedha nyingi kuwalipa maafisa wake mishahara na marupurupu minono pamoja na kuwapa mabilioni ya pesa kununulia magari ya kifahari. Pengine Rais hajafahamishwa kuwa mwaka ujao wa kifedha serikali itajipata pabaya kwani Halmashauri ya ukusanyaji ushuru nchini (KRA), haitaweza kukusanya kiwango kilichowekewa na serikali baada ya shughuli ya ushuru kutatizwa na hofu iliyotanda wakati wa uchaguzi
KRA imekusanya shilingi 560 bilioni kufikia mwishoni mwa Machi ilhali ilikuwa imeagizwa kukusanya shilingi 881 bilioni.
Serikali za kaunti, ambazo zingali changa, zimependekeza kutumia mabilioni ya fedha ambazo hazitaweza kukusanya. Badala yake zimeomba serikali kuu ijaze pengo hilo au zipewe idhini ya kukopa.
Rais Kenyatta hana budi kuchukua hatua za dharura kuhakikisha kuwa wakenya hawataendelea kuandamwa na madeni maishani mwao.

Maswali
a) Kwa maneno yasiyozidi 70, fupisha aya za kwanza nne
b) Kwa nini serikali haitaweza kulipa madeni yake? (maneno 40 -50)

  

Answers


Wilfred
A.
- Serikali kuwasilisha ajeti.
- Kueleza jinsi mabilioni yaliyotumiwa.
- Serikali kusema itatumia shilingi 1.6 trilioni kwa maendeleo.
- Makadirio kuwasilishwa na kiongozi wa walio wengi bungeni.
- Kukosa kueleza jinsi ya kupata kitita hicho.
- Habari hizi kunipa wasiwasi.
- Kenya kudaiwa shilingi 1.8 trilioni na wafadhili.
- Kutolaumu wale wasioelewa ukubwa wa deni hili.
- Kugawanya deni hili kwa wakenya wote.
- Kila mkenya kudaiwa shilingi 45,000
- Deni kumkosesha usingizi Rais.
- Kutafuta njia ya kulipa bila kuathiri uchumi.


B.
i) Serikali kutenga fedha nyingi kuwalipa wafanyikazi.
ii) KRA kutokusanya kiwango kinachohitajika.
iii) Ukusanyaji wa ushuru kukatizwa na hofu wakati wa uchaguzi.
iv) Serikali za kaunti kupendekeza kutumia mabilioni ambayo hawana
Wilfykil answered the question on October 5, 2019 at 07:20


Next: Onyesha viwakilishi katika sentensi zifuatazo kisha ueleze ni vya aina gani:- i) Unamjua vyema kweli? (ii) Hicho wanachokitaka hakipo
Previous: Bainisha sifa zinazotofautisha sauti zifuatazo: /e/ na /u/

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions