Vile lelo walalama, kwa yale ulotendewa, Huyakumbuki ya nyuma, pindi ulipochachawa,

      

Vile lelo walalama, kwa yale ulotendewa,
Huyakumbuki ya nyuma, pindi ulipochachawa,
Ulipotenda unyama, uliona ndiyo sawa,
Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa!

Ulizusha uhasama, leo wewe wapagawa,
Walia bila kukoma, tungadhani umefiwa,
Sasa huna usalama, huwezi kujiopowa
Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa!

Tenda mambo kwa kupima, usiruke huna mbawa,
Una macho kutazama, na akili umepewa,
Matendo hurudi nyuma, atendaye hurudiwa,
Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa!

Dunia haishi njama, sijione umepewa,
Ukadhani usalama, binadamu kuwagawa,
Ukahisi ni wanyama, waso hali kama ngawa,
Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa!

Unapotenda zahama, siku yako itakuwa,
Ambapo utaungama, useme umechachiwa,
Na uanze kutetema, ulie umeonewa,
Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa.


Maswali
a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka.
b) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu.
c) Eleza muundo wa ubeti wa pili.
d) Ni kaida zipi za utunzi zilizozingatiwa na mshairi?
e) Andika ubeti wa kwanza kwa lugha ya mjazo.
f) Toa mifano miwili ya idhini ya mshairi.
g) Kwa nini msemewa hafai kulalamika ?
h) Eleza maana ya maneno yafuatayo.
i) Uhasama
ii) Umepowa

  

Answers


Wilfred
a) Kichwa – Mtenda akitendewa.

b) Tarbia – Mishororo minne kila ubeti

c) Muundo
- Vipande viwili
- Mishororo minne katika ubeti
- Mizani 8, 8 - 16
- Vina – ma- wa
Wa – ma

d) Kaida za utunzi
- Urari wa mizani
- Lina mishororo
- Lina beti
- Lina muwala
- Lina vipande
- Lina kibwagizo

e) Ni vipi unakasirika kwa yale uliyotendewa.
Hukumbuki yaliyopita baada ya kukasirika wewe ulipotenda mabaya hukujali. Mtu anayefanya mabaya hulalamika.

f) Idhini ya mshairi.
- Inkisari - ulotendewa
- Kuboronga sarufi - na akili umepewa.

g) Kwa vile naye hutendea wengine mabaya.

h) Uhasama - chuki
Umepowa – umetulia / umenyamaza.
Wilfykil answered the question on October 5, 2019 at 08:09


Next: Bainisha aina za nomino zilizopigiwa mistari katika sentensi hii:- Uhodari wa wanariadha wa Kenya unahitajika kote duniani
Previous: Tunga sentensi ukitumia mzizi – choyo kama :- (i) nomino (ii) Kivumishi (iii) Kiwakilishi

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions


  • Tafautisha kati ya; Ngonjera za ushairi na za maigizo.(Solved)

    Tafautisha kati ya;
    Ngonjera za ushairi na za maigizo.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Onyesha kwa kutolea mifano minne, jinsi misimu huzuka.(Solved)

    Onyesha kwa kutolea mifano minne, jinsi misimu huzuka.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Jana ilikuwepo, ikapita(Solved)

    Soma shairi ifuatalo kish aujibu maswali.
    Jana ilikuwepo, ikapita
    Kwenye giza la sahau
    Jana ilipiga kuathiri
    Athari ijayo leo
    Leo tunajua kesho tunaibashiria
    Kesho ipapo na hatuijui
    Kesho, itapiga au itapuliza?
    Au itapita pasi na chochote
    Kama moshi usio mashiko?
    Kesho hatuioni
    Lakini yaja ...
    Twaihisi
    Twaihisi
    Twaimaizi
    Ipo,

    Yajongea
    Hiyo na taathira zake
    Inakuja
    Yasogea
    Yaja mbio
    Yafikia upeo unaoitwa leo
    Basi kumbuka
    Maisha ni ubishi, yakabili!
    Maisha ni jasiri, jusurisha!
    Maisha ni huzuni, yashinde!
    Maisha ni msiba, uweze!

    Maisha ni wajibu, tekeleza!
    Maisha ni ni fumbo, liague!
    Maisha ni tatizo, litatue!
    Maisha ni ahadi, itemize!
    Maisha mapambano, wana nayo!
    Maisha ni zawadi, ipokee!
    Maisha ni mchezo, uchezee!
    Maisha ni nyimbo, iimbe!
    Maisha ni fursa, itumie?
    Maisha ni ureda, furahia!
    Maisha maumbile, changamkie!
    Maisha ni lengo, lifike!
    Maisha ni mwendo, yaendee!
    Maisha ni uzuri, ustarehee!
    Maisha liwazo, yapumzikie!
    (a) Lipe kichwa mwafaka shairi hili.
    (b) Fafanua maudhui ya shairi hili.
    (c) Onyesha muundo wa shairi hili.
    (d) Taja na ueleze tamathali tatu za semi alizotumia mwandishi wa shairi hili.
    (e) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumia katika shairi.
    Twaimaizi
    Yajongea

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Angaza, mtazame mlimwengu(Solved)

    Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata.
    Angaza, mtazame mlimwengu
    Bidii, nayo matokeo chungu
    Wezesha, kuishi bila uchungu
    Teknolojia maendeleo.

    Angaza, zitazame barabara
    Aenda, kwa kasi pia salama
    Bidhaa, sokoni upesi fika
    Teknolojia maendeleo.

    Angaza, majokofu majumbani
    Vyakula, na vinywaji hifadhika
    Nafuu, zizima maji ridisha
    Teknolojia maendeleo.

    Angaza, leo pote madukani
    Mikebe, vyakula vinywaji tiwa
    Mimea, huwawirishwa haraka
    Teknolojia maendeleo.

    Angaza, nguo kwa mashine stimu
    Upesi, runinga na simu juza
    Angani, burudika eropleni
    Teknolojia maendeleo.

    Angaza, tarakilishi nguzoye
    Mauzo, mawasiliano kwayo
    tibani, ni mwenzi kwake tabibu
    Teknolojia maendeleo.

    Angaza, mja hajakoma katu
    Shughuli, kila uchao shajara
    Apate, tulia kwa ufanisi
    Teknolojia maendeleo.

    (a) Eleza dhamira ya msanii katika shairi hili.
    (b) Onyesha mifano mitano ya maendeleo katika maisha ya binadamu.
    (c) Eleza umbo la shairi hii.
    (d) Andika ubeti wa nne katika lugha ya nathari.
    (e) Eleza kwa kifupi mtazamo wa mshairi kuhusu teknolojia.
    (f) Eleza maana ya maneno yafuatayo;
    (i) Majokofu
    (ii) Hunawirisha
    (iii) Shajara

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Thibitisha kauli kuwa, "Mla naye huliwa zamu yake ifukapo". Ukirejelea riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.(Solved)

    Thibitisha kauli kuwa, "Mla naye huliwa zamu yake ifukapo". Ukirejelea riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Elimu ya kajielewa sisi nani, na twatoka wapi, twaelekea wapi na utu tutaurejeshaje pahali pake....(Solved)

    Kidagaa kimemwozea
    Elimu ya kajielewa sisi nani, na twatoka wapi, twaelekea wapi na utu tutaurejeshaje pahali pake....
    (a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    (b) Taja mfano mmoja wa tamathali ya usemi kwenye dondoo.
    (c) Dhihirisha jinsi utu ulivyotoka pahali pake, ukirejelea riwaya nzima.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • "Siku moja kabla ya kufika kwa wageni. Meya ana mkutano na wawakilishi wa wafanyikaziambao wameketi mkabala naye".(Solved)

    Mtahiki Meya; Timothy Arege
    "Siku moja kabla ya kufika kwa wageni. Meya ana mkutano na wawakilishi wa wafanyikazi ambao wameketi mkabala naye".
    (a) Fafanua madai yaliyotolewa na wafanyakazi katika mkutano huu.
    (b) Eleza jinsi Meya alivyojibu madai ya wawakilishi wa wafanyakazi.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • "Leo ndio mtanitambua. Mama gani anayemtazama mwana akigeuka afriti?"(Solved)

    Damu nyeusi na hadithi zingine
    "Leo ndio mtanitambua. Mama gani anayemtazama mwana akigeuka afriti?"
    (a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    (b) Tambua "mwana aliyegeuka afriti‘na ueleze hulka zake nne.
    (c) Jadili maudhui yoyote matano yanayojitokeza katika hadithi husika.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Wanawake, wanaoishi katika maeneo ya mashambani katika nchi ambazo zinazoendelea ni baadhi ya watu waliotopea na kubobea katika uchochole mkubwa.(Solved)

    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yafuatayo.
    Wanawake, wanaoishi katika maeneo ya mashambani katika nchi ambazo zinazoendelea ni baadhi ya watu waliotopea na kubobea katika uchochole mkubwa. Jumla ya idadi kubwa ya wanawake hawa wanaoishi chini ya kiwango cha chini, cha umaskini inakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 600. Hii ni idadi kubwa hasa ikikumbukwa kuwa ni asilimia kubwa ya wanawake inayoishi kwa maeneo haya. Ulimwengu umeshuhudia ongezeko kubwa la idadi ya watu pamoja na kuwako kwa matatizo ya kiuchumi duniani.Kadhalika matatizo mengine ni mitarafuku na vita vya kikabila, majanga ya kiasili mathalani mafuriko , ukame na milipuko ya volkano. Usisahau kuwa pia kina uharibifu wa kimazingira, mabadiliko ya desturi na kusambaratika kwa familia na misingi yake. Tatizo lingine ni kuwa kuna kuongezeka kwa hali ya wanawake kuwa wazazi pekee na hivyo kuongeza familia zinazosimamiwa na wanawake ( ambao tumewataja kuwa wanakumbwa na umaskini mkubwa).Wanawake wanaoishi mashambani wanakumbwa na makubwa. Kwanza, kama maskini wanaishi katika mazingiramagumu. Vile vile kama wanawake wanakabiliana na mapendeleo ya kisera na kitamaduni yanayowadharau na kuwapuuza wanawake na mchango wao katika maendeleo. Tatu, kama viongozi wa familia hasa wanaolea na kutunza jamaa na mzazi mmoja, wanapambana na uogonzi wa familia pamoja na uzalishaji. Aghalabu hawapati usaidizi wowote katika majukumu kama haya bali wanalazimika kupambana nayo peke yao. Kutokana na hayo yote wanawake hawapati nafasi nzuri kushiriki katika maamuzi ya maswala yanayowahusu. Maswala mengi yanaamuliwa na wanaume pasipokuwahusisha wanawake. Licha ya dhiki yao kubwa, wanawake hawa wanachangia katika maendeleo ya jammi na kiuchumi kwa njia mbalimbali. Mchango huu unaonekana katika kiwango cha jamii,taifa na familia. Katika kiwango cha kijamii na kitaifa wanawake ndio chazo cha nguvukazi kwani ni wao na watoto wao wanatekeleza kazi nyingi hasa za nyumbani na mashambani. Mara nyingi huwa na uwezo bora wa kutunza chochote walichonacho kuliko wenzao wanaume.
    Kifamilia wanawake wa shambani wanashughulika mchana kutwa katika hali ngumu ya hewa aidha jua kali au mvua huku wameeleka wanao migongoni wakilima mashamba ili kupata chakula kwa familia zao. Jukumu la kuandaa chakula nyumbani bado linaachiwa wale wale wanawake wanaokizalisha mashambani.
    Jambo lisilopingika ni kwamba wanawake wanatekeleza majuku makubwa na muhimu katika kizazi cha binadamu na ndio hasa miimili ya jamii yoyote staarabu. Kwa hivyo, ni kinaya kitupu kudhalilisha wanawake. Mataifa mengi yaliyoendelea ni yale yaliyoondoa vikwazo vyote mbele ya wanawake na kuwaacha watekeleze wajibu wao. Kadhalika wanaume wa huko wanawaona wanawake kama wenzao katika kujenga jamii wala sio watumwa au watumishi wao wanaoumia na kutumikishwa kama vifaa na bidhaa. Inafaa jamii zinazodinisha wanawake zitambue kuwa ubaya wa tendo hili sio tu kudumaza maendeleo yake bali pia kutoa mfano mbaya kwa vijana ambao wataendeleza Ukandamizaji huu kwa vizazi vijavyo. Kwa hivyo, jamii inawajibika kutenda lililo sawa kwa kuwapa hadhi wanawake wote.

    Maswali
    a) Ipe taarifa hii anwani mwafaka
    b) Nakili maafa matatu ya kimaumbile yaliyotajwa katika kifungu hiki.
    c) Eleza sababu tatu zinazowazuia wanawake kushiriki katika maamuzi ya masuala yanayowahusu kulingana na makala haya.
    d) Wanawake hutekeleza majukumu gani katika jamii na taifa kutokana na makala haya?
    e) Kuna tofauti gani baina ya wanawake wa mataifa yaliyoendelea nay ale ambayo hayajastawi.
    f) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa kwenye taarifa:
    i) uchochole
    ii) kudhalilisha
    iii) mitafuruku

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Jadili changamoto za elimu katika hadithi ya Kanda la Usufi.(Solved)

    Jadili changamoto za elimu katika hadithi ya Kanda la Usufi.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Sikufahamu ikiwa hisia zenyewe zilikuwa kwa sababu ya "furaha au huzuni." Potelea pote! Liwalo naliwe!! Nilisikia sauti Fulani ikinadi ndani katika nafsi yangu.(Solved)

    Damu Nyeusi na Hadithi nyingine
    Ndoa ya samani (Omar Babu)
    Sikufahamu ikiwa hisia zenyewe zilikuwa kwa sababu ya "furaha au huzuni." Potelea pote! Liwalo naliwe!! Nilisikia sauti Fulani ikinadi ndani katika nafsi yangu.
    a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    b) Bainisha tamathali mbiliza usemi katika dondoo hili.
    c) Ni yapi yaliyodhihirisha 'furaha au huzuni' katika hisia za anayeelezwa?

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Uongozi mbaya una athari kadhaa. Thibitisha madai haya kwa kurejelea Tamthili ya Mstahiki Meya.(Solved)

    Uongozi mbaya una athari kadhaa. Thibitisha madai haya kwa kurejelea Tamthili ya Mstahiki Meya.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Ndiyo yale ya "ngome in‘tuumiza naswi tu mumo ngomeni.‘(Solved)

    Mshtahiki Meya: T. Arege
    Ndiyo yale ya "ngome in‘tuumiza naswi tu mumo ngomeni.‘
    a) Weka dondoo hili katika muktadha wake.
    b) Tambua tamathali mbili za usemi zilizo tumika latika dondoo hili.
    c) Kwa kurejelea tamthilia onyesha jinsi ngome inavyowaumiza wanacheneo.
    d) Wanacheneo wanatumia mikakati gani kukabiliana na hali ya (c) hapo juu.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Onyesha jinsi mwandishi wa Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea alivyoshughulikia Nafasi ya mwanamke.(Solved)

    Onyesha jinsi mwandishi wa Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea alivyoshughulikia Nafasi ya mwanamke.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Onyesha jinsi mwandishi wa Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea alivyoshughulikia Nafasi ya vijana.(Solved)

    Onyesha jinsi mwandishi wa Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea alivyoshughulikia Nafasi ya vijana.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Kuna mfanano mkubwa kati ya ulumbi na hotuba. Thibitisha.(Solved)

    Kuna mfanano mkubwa kati ya ulumbi na hotuba. Thibitisha.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • "Wema wako umeniua kabisa………Nina jishtaki mwenyewe kila siku kwa miaka na miaka".(Solved)

    KIDAGAA KIMEMWOZEA: Ken Walibora.
    "Wema wako umeniua kabisa………Nina jishtaki mwenyewe kila siku kwa miaka na miaka".
    (a) Eleza muktadha wa maneno haya.
    (b) Onyesha kwa kutoa mifano kuwa anayeambiwa maneno haya alikuwa na wema.
    (c) Eleza umuhimu wa mhusika mashaka katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • "Dhiki mbalimbali zimekuwapo lakini heri nusu shari kuliko shari kamili".(Solved)

    Mstahiki Meya.
    "Dhiki mbalimbali zimekuwapo lakini heri nusu shari kuliko shari kamili".
    (a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    (b) Taja tamathali ya usemi iliyotumika katika dondoo hili.
    (c) Eleza sifa zozote tatu za mzungumzaji.
    (d) Fafanua aina zozote nne za migogoro inayojitokeza katika tamthilia ya Mstahiki Meya.

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Taja kitamkwa chenye sifa ifuatazo. Vokali ya nyuma, kati(Solved)

    Taja kitamkwa chenye sifa ifuatazo.
    Vokali ya nyuma, kati.

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Kuna sababu kadha za kuwako na kushamiri kwa ajira ya watoto.(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
    Kuna sababu kadha za kuwako na kushamiri kwa ajira ya watoto. Moja ya sababu hizo ni umaskini unaozikumba jamaa nyingi pamoja na welewa mdogo wa thamani ya elimu wa baadhi ya watu katika jamii. Wapo watoto ambao hushurutika kubeba jukumu la kujizumbulia riziki wenyewe kutokana na hali duni ya familia zao.
    Hali hii huweza kutokana na baadhi ya wazazi kutelekeza majukumu yao ya kimsingi ya kuikimu jamaa yao. Aidha kuna sehemu nyingine ambapo hali hii imetokana na janga sugu la ukimwi. Yapo maeneo ambako kuenea kwa ugonjwa huu kumewafanya viongozi wa jamaa kupukutika kama majani ya mti na kuwalazimisha watoto kuyakatiza masomo yao ili wawakidhie haja wadogo zao. Kuhusiana na kutelekeza majukumu, kuna wazazi ambao wanakosea kwa kutowaelekeza watoto wao kujua maadili mema ni yepi. Kwa njia hii watoto hao wanaishia kutumbukia kwenye matatizo makubwa.
    Baadhi ya ajira zina athari kubwa sana kwa watoto. Ukahaba, kwa mfano, ni mojawapo ya ajira ambazo watoto wa kike hulazimika kujiingiza. Hii ni ajira ambayo inaweza kuwatumbukiza watoto hao katika hatari kubwa kutokana na uwezekano mkubwa wa kuambukizwa maradhi ya ukimwi. Asillimia kubwa ya watoto wanaotumbukia katika ajira hii, inapatikana katika maeneo ya mijini na sehemu ambako utalii umeshamiri sana. Umaskini pamoja na dhiki za mijini huwalazimisha watoto hao wa kike kuishia kwenye biashara za aina hiyo. Wengine hufanyiwa hila na wafanyabiashara ambao wametovukwa na utu kutokana na tamaa yao kubwa ya kujitajirisha. Katika maeneo ambako utalii umeshamiri, ukahaba wa watoto unatokana na umaskini pamoja na kusambaa na kuenea kwa maadili ajinabi, ya ulimwengu usio wetu.
    Ikiwa umaskini ni chocheo kubwa la kuwapo kwa ajira ya watoto, basi inahalisi serikali zetu zifanye kila juhudi kuhakikisha kuwa umaskini umepigwa vita. Pana umuhimu wa kuhakikisha kuwa wanajamii wote wamepewa nafasi sawa za kujikwamua kutoka lindi la umaskini. Isitoshe, pana umuhimu wa juhudi nyingi kufanywa kuhakikisha kuwa nafasi za shule zimepanuliwa ili kuikidhi idadi kubwa ya watoto ambao wana kiu ya elimu. Serikali haina budi pia kuhakikisha kuwa zimepitishwa sheria zinazomlinda motto dhidi ya ukatili unaotokana na watu waliokosa hisia za utu na ubinadamu. Upo pia umuhimu wa kuvisaidia vikundi vinavyojitahidi kuwasaidia watoto ili kuzifanikisha juhudi zao kwa kuwa chanda kimoja hakivunji chawa kama tujuavyo.
    Hatua nyingine ambazo zinaweza kuchukuliwa ili kupunguza ajira ya watoto ni kuwahamasisha wanajamii kuhusu haki za mtoto. mtoto yeyote yule ana haki ya kupata elimu ya msingi. Mtoto pia ana haki ya kuishi na kupata mahitaji ya kimsingi na ya lazima kama chakula, malazi au makazi na matunzo ya kiafya. Aidha mtoto ana haki ya ukuaji, yaani kukua kikamilifu pasi na kizuizi na katika mazingira yasiyombana kwa njia yoyote ile. Isitoshe, mtoto ana haki ya kupata ulinzi dhidi ya unyanyaswaji au udhalilishwaji wa aina yoyote ile au hata maonevu kwenye misingi yoyote iwayo. Mtoto pia ana haki ya kuwa huru kushiriki katika jumuiya yake, kutoa maoni na kujieleza, kushirikiana na kujiunga na vikundi. Mwisho, na muhimu zaidi, mtoto ana haki ya kulindwa dhidi ya ajira au aina yoyote ya kazi ambayo inaihatarisha afya na siha yake au inamzuia asipate elimu.
    (a) Fupisha aya mbili za mwanzo bila kubadilisha maana. (maneno 60-70)
    (b) Eleza hoja muhimu zinazojitokeza katika aya mbili za mwisho. (Maneno 50-60)

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)