Tabaini ni mbinu yakusisitiza ukweli Fulani kwa kutumia maneno yanayopingana.
1. Majisifu hakusomea dini kwani aliona kama kasumba iliyolewesha umma mpaka ukalewa chakari si hekalu, si kanisa, si msikiti, si mimbari, si miharabu vyote akaviona ombwe tupu.
2. Katika jiko la mwalimu Majisifu kulikuwa na jokofu lililojazwa chupa za vileo anuwai. Si Tusker, si vodka, si pilsner, si Kilimanjaro, si castle, Heineken na Guiness.
3. Wakati wa sikukuu ya wazalendo wimbo wa taifa ukiimbwa kila mtu alivua kofia si kofia za bulibui, si za kitunga, si za za mdongea, si tarbushi.
4. Amani alipompelekea Dj chapatti zikiwa pakachani na kupata kitanda chake kitupu hakuna aliyetaka kumweleza kilichojiri si wagonjwa, si wauguzi, si daktari
5. Amani alipowaza na kuwazua aligundua ardhi ndicho kichocheo kikubwa cha unyama wa binadamu na ukosefu wa utu. Maadamu si koo, si makabila, si mataifa.
6. Uwanja wa Nanasaba bora watu walifika kwa wingi ili kumlaki dikteta mpya. Si watoto, si wakubwa, si utiriri huo wa watu uliofurika uwanjani.
7. Imani alimwabia Amani alipowasili nyumbani kwamba hali ya uhuru ilikuwa taabani. Si wa maji, si wa chakula.
8. Maelezo kuhusu jinsi zahanati ya Nasaba bora ilikuwa na watu sampuli sampuli. Si wa miguu, si wa mikono.
9. Mtemi na nduguye kutosikilizana hawapikiki chungu kimoja. Wakionana vuta nikuvute, shutumu ni kushutumu, kashifu ni kukashifu …../…….
Wilfykil answered the question on October 5, 2019 at 08:22
- “Hawa ndio watu muhimu katika ulimwengu wa sasa”(Solved)
“Hawa ndio watu muhimu katika ulimwengu wa sasa”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Fafanua mchango wa mrejelewa katika kusambaratisha baraza la Cheneo.
c) Cheneo imekandamizwa kutokana na wakazi wake kutotumia akili. Fafanua kauli hii kwa kurejelea tamthilia nzima.
Date posted: October 5, 2019. Answers (1)
- …unaa…seema mimiiii sipakui?...wataka mimi nipike? Ehee? Ati mimi nalaza damu? Wewe unaiamsha damu?(Solved)
…unaa…seema mimiiii sipakui?...wataka mimi nipike? Ehee? Ati mimi nalaza damu? Wewe unaiamsha damu?
a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
b) Eleza mbinu zozote tatu za lugha zilizotumika katika dondoo hili.
c) Jadili ufaafu wa anwani kwa kurejelea mnenaji.
Date posted: October 5, 2019. Answers (1)
- Vile lelo walalama, kwa yale ulotendewa,
Huyakumbuki ya nyuma, pindi ulipochachawa,
(Solved)
Vile lelo walalama, kwa yale ulotendewa,
Huyakumbuki ya nyuma, pindi ulipochachawa,
Ulipotenda unyama, uliona ndiyo sawa,
Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa!
Ulizusha uhasama, leo wewe wapagawa,
Walia bila kukoma, tungadhani umefiwa,
Sasa huna usalama, huwezi kujiopowa
Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa!
Tenda mambo kwa kupima, usiruke huna mbawa,
Una macho kutazama, na akili umepewa,
Matendo hurudi nyuma, atendaye hurudiwa,
Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa!
Dunia haishi njama, sijione umepewa,
Ukadhani usalama, binadamu kuwagawa,
Ukahisi ni wanyama, waso hali kama ngawa,
Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa!
Unapotenda zahama, siku yako itakuwa,
Ambapo utaungama, useme umechachiwa,
Na uanze kutetema, ulie umeonewa,
Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa.
Maswali
a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka.
b) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu.
c) Eleza muundo wa ubeti wa pili.
d) Ni kaida zipi za utunzi zilizozingatiwa na mshairi?
e) Andika ubeti wa kwanza kwa lugha ya mjazo.
f) Toa mifano miwili ya idhini ya mshairi.
g) Kwa nini msemewa hafai kulalamika ?
h) Eleza maana ya maneno yafuatayo.
i) Uhasama
ii) Umepowa
Date posted: October 5, 2019. Answers (1)
- Tafautisha kati ya;
Ngonjera za ushairi na za maigizo.(Solved)
Tafautisha kati ya;
Ngonjera za ushairi na za maigizo.
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Onyesha kwa kutolea mifano minne, jinsi misimu huzuka.(Solved)
Onyesha kwa kutolea mifano minne, jinsi misimu huzuka.
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Jana ilikuwepo, ikapita(Solved)
Soma shairi ifuatalo kish aujibu maswali.
Jana ilikuwepo, ikapita
Kwenye giza la sahau
Jana ilipiga kuathiri
Athari ijayo leo
Leo tunajua kesho tunaibashiria
Kesho ipapo na hatuijui
Kesho, itapiga au itapuliza?
Au itapita pasi na chochote
Kama moshi usio mashiko?
Kesho hatuioni
Lakini yaja ...
Twaihisi
Twaihisi
Twaimaizi
Ipo,
Yajongea
Hiyo na taathira zake
Inakuja
Yasogea
Yaja mbio
Yafikia upeo unaoitwa leo
Basi kumbuka
Maisha ni ubishi, yakabili!
Maisha ni jasiri, jusurisha!
Maisha ni huzuni, yashinde!
Maisha ni msiba, uweze!
Maisha ni wajibu, tekeleza!
Maisha ni ni fumbo, liague!
Maisha ni tatizo, litatue!
Maisha ni ahadi, itemize!
Maisha mapambano, wana nayo!
Maisha ni zawadi, ipokee!
Maisha ni mchezo, uchezee!
Maisha ni nyimbo, iimbe!
Maisha ni fursa, itumie?
Maisha ni ureda, furahia!
Maisha maumbile, changamkie!
Maisha ni lengo, lifike!
Maisha ni mwendo, yaendee!
Maisha ni uzuri, ustarehee!
Maisha liwazo, yapumzikie!
(a) Lipe kichwa mwafaka shairi hili.
(b) Fafanua maudhui ya shairi hili.
(c) Onyesha muundo wa shairi hili.
(d) Taja na ueleze tamathali tatu za semi alizotumia mwandishi wa shairi hili.
(e) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumia katika shairi.
Twaimaizi
Yajongea
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Angaza, mtazame mlimwengu(Solved)
Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata.
Angaza, mtazame mlimwengu
Bidii, nayo matokeo chungu
Wezesha, kuishi bila uchungu
Teknolojia maendeleo.
Angaza, zitazame barabara
Aenda, kwa kasi pia salama
Bidhaa, sokoni upesi fika
Teknolojia maendeleo.
Angaza, majokofu majumbani
Vyakula, na vinywaji hifadhika
Nafuu, zizima maji ridisha
Teknolojia maendeleo.
Angaza, leo pote madukani
Mikebe, vyakula vinywaji tiwa
Mimea, huwawirishwa haraka
Teknolojia maendeleo.
Angaza, nguo kwa mashine stimu
Upesi, runinga na simu juza
Angani, burudika eropleni
Teknolojia maendeleo.
Angaza, tarakilishi nguzoye
Mauzo, mawasiliano kwayo
tibani, ni mwenzi kwake tabibu
Teknolojia maendeleo.
Angaza, mja hajakoma katu
Shughuli, kila uchao shajara
Apate, tulia kwa ufanisi
Teknolojia maendeleo.
(a) Eleza dhamira ya msanii katika shairi hili.
(b) Onyesha mifano mitano ya maendeleo katika maisha ya binadamu.
(c) Eleza umbo la shairi hii.
(d) Andika ubeti wa nne katika lugha ya nathari.
(e) Eleza kwa kifupi mtazamo wa mshairi kuhusu teknolojia.
(f) Eleza maana ya maneno yafuatayo;
(i) Majokofu
(ii) Hunawirisha
(iii) Shajara
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Thibitisha kauli kuwa, "Mla naye huliwa zamu yake ifukapo". Ukirejelea riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.(Solved)
Thibitisha kauli kuwa, "Mla naye huliwa zamu yake ifukapo". Ukirejelea riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Elimu ya kajielewa sisi nani, na twatoka wapi, twaelekea wapi na utu tutaurejeshaje pahali pake....(Solved)
Kidagaa kimemwozea
Elimu ya kajielewa sisi nani, na twatoka wapi, twaelekea wapi na utu tutaurejeshaje pahali pake....
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Taja mfano mmoja wa tamathali ya usemi kwenye dondoo.
(c) Dhihirisha jinsi utu ulivyotoka pahali pake, ukirejelea riwaya nzima.
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- "Siku moja kabla ya kufika kwa wageni. Meya ana mkutano na wawakilishi wa wafanyikaziambao wameketi mkabala naye".(Solved)
Mtahiki Meya; Timothy Arege
"Siku moja kabla ya kufika kwa wageni. Meya ana mkutano na wawakilishi wa wafanyikazi ambao wameketi mkabala naye".
(a) Fafanua madai yaliyotolewa na wafanyakazi katika mkutano huu.
(b) Eleza jinsi Meya alivyojibu madai ya wawakilishi wa wafanyakazi.
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- "Leo ndio mtanitambua. Mama gani anayemtazama mwana akigeuka afriti?"(Solved)
Damu nyeusi na hadithi zingine
"Leo ndio mtanitambua. Mama gani anayemtazama mwana akigeuka afriti?"
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Tambua "mwana aliyegeuka afriti‘na ueleze hulka zake nne.
(c) Jadili maudhui yoyote matano yanayojitokeza katika hadithi husika.
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Wanawake, wanaoishi katika maeneo ya mashambani katika nchi ambazo zinazoendelea ni baadhi ya watu waliotopea na kubobea katika uchochole mkubwa.(Solved)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yafuatayo.
Wanawake, wanaoishi katika maeneo ya mashambani katika nchi ambazo zinazoendelea ni baadhi ya watu waliotopea na kubobea katika uchochole mkubwa. Jumla ya idadi kubwa ya wanawake hawa wanaoishi chini ya kiwango cha chini, cha umaskini inakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 600. Hii ni idadi kubwa hasa ikikumbukwa kuwa ni asilimia kubwa ya wanawake inayoishi kwa maeneo haya. Ulimwengu umeshuhudia ongezeko kubwa la idadi ya watu pamoja na kuwako kwa matatizo ya kiuchumi duniani.Kadhalika matatizo mengine ni mitarafuku na vita vya kikabila, majanga ya kiasili mathalani mafuriko , ukame na milipuko ya volkano. Usisahau kuwa pia kina uharibifu wa kimazingira, mabadiliko ya desturi na kusambaratika kwa familia na misingi yake. Tatizo lingine ni kuwa kuna kuongezeka kwa hali ya wanawake kuwa wazazi pekee na hivyo kuongeza familia zinazosimamiwa na wanawake ( ambao tumewataja kuwa wanakumbwa na umaskini mkubwa).Wanawake wanaoishi mashambani wanakumbwa na makubwa. Kwanza, kama maskini wanaishi katika mazingiramagumu. Vile vile kama wanawake wanakabiliana na mapendeleo ya kisera na kitamaduni yanayowadharau na kuwapuuza wanawake na mchango wao katika maendeleo. Tatu, kama viongozi wa familia hasa wanaolea na kutunza jamaa na mzazi mmoja, wanapambana na uogonzi wa familia pamoja na uzalishaji. Aghalabu hawapati usaidizi wowote katika majukumu kama haya bali wanalazimika kupambana nayo peke yao. Kutokana na hayo yote wanawake hawapati nafasi nzuri kushiriki katika maamuzi ya maswala yanayowahusu. Maswala mengi yanaamuliwa na wanaume pasipokuwahusisha wanawake. Licha ya dhiki yao kubwa, wanawake hawa wanachangia katika maendeleo ya jammi na kiuchumi kwa njia mbalimbali. Mchango huu unaonekana katika kiwango cha jamii,taifa na familia. Katika kiwango cha kijamii na kitaifa wanawake ndio chazo cha nguvukazi kwani ni wao na watoto wao wanatekeleza kazi nyingi hasa za nyumbani na mashambani. Mara nyingi huwa na uwezo bora wa kutunza chochote walichonacho kuliko wenzao wanaume.
Kifamilia wanawake wa shambani wanashughulika mchana kutwa katika hali ngumu ya hewa aidha jua kali au mvua huku wameeleka wanao migongoni wakilima mashamba ili kupata chakula kwa familia zao. Jukumu la kuandaa chakula nyumbani bado linaachiwa wale wale wanawake wanaokizalisha mashambani.
Jambo lisilopingika ni kwamba wanawake wanatekeleza majuku makubwa na muhimu katika kizazi cha binadamu na ndio hasa miimili ya jamii yoyote staarabu. Kwa hivyo, ni kinaya kitupu kudhalilisha wanawake. Mataifa mengi yaliyoendelea ni yale yaliyoondoa vikwazo vyote mbele ya wanawake na kuwaacha watekeleze wajibu wao. Kadhalika wanaume wa huko wanawaona wanawake kama wenzao katika kujenga jamii wala sio watumwa au watumishi wao wanaoumia na kutumikishwa kama vifaa na bidhaa. Inafaa jamii zinazodinisha wanawake zitambue kuwa ubaya wa tendo hili sio tu kudumaza maendeleo yake bali pia kutoa mfano mbaya kwa vijana ambao wataendeleza Ukandamizaji huu kwa vizazi vijavyo. Kwa hivyo, jamii inawajibika kutenda lililo sawa kwa kuwapa hadhi wanawake wote.
Maswali
a) Ipe taarifa hii anwani mwafaka
b) Nakili maafa matatu ya kimaumbile yaliyotajwa katika kifungu hiki.
c) Eleza sababu tatu zinazowazuia wanawake kushiriki katika maamuzi ya masuala yanayowahusu kulingana na makala haya.
d) Wanawake hutekeleza majukumu gani katika jamii na taifa kutokana na makala haya?
e) Kuna tofauti gani baina ya wanawake wa mataifa yaliyoendelea nay ale ambayo hayajastawi.
f) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa kwenye taarifa:
i) uchochole
ii) kudhalilisha
iii) mitafuruku
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Jadili changamoto za elimu katika hadithi ya Kanda la Usufi.(Solved)
Jadili changamoto za elimu katika hadithi ya Kanda la Usufi.
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Sikufahamu ikiwa hisia zenyewe zilikuwa kwa sababu ya "furaha au huzuni." Potelea pote! Liwalo naliwe!! Nilisikia sauti Fulani ikinadi ndani katika nafsi yangu.(Solved)
Damu Nyeusi na Hadithi nyingine
Ndoa ya samani (Omar Babu)
Sikufahamu ikiwa hisia zenyewe zilikuwa kwa sababu ya "furaha au huzuni." Potelea pote! Liwalo naliwe!! Nilisikia sauti Fulani ikinadi ndani katika nafsi yangu.
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Bainisha tamathali mbiliza usemi katika dondoo hili.
c) Ni yapi yaliyodhihirisha 'furaha au huzuni' katika hisia za anayeelezwa?
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Uongozi mbaya una athari kadhaa. Thibitisha madai haya kwa kurejelea Tamthili ya Mstahiki Meya.(Solved)
Uongozi mbaya una athari kadhaa. Thibitisha madai haya kwa kurejelea Tamthili ya Mstahiki Meya.
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Ndiyo yale ya "ngome in‘tuumiza naswi tu mumo ngomeni.‘(Solved)
Mshtahiki Meya: T. Arege
Ndiyo yale ya "ngome in‘tuumiza naswi tu mumo ngomeni.‘
a) Weka dondoo hili katika muktadha wake.
b) Tambua tamathali mbili za usemi zilizo tumika latika dondoo hili.
c) Kwa kurejelea tamthilia onyesha jinsi ngome inavyowaumiza wanacheneo.
d) Wanacheneo wanatumia mikakati gani kukabiliana na hali ya (c) hapo juu.
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Onyesha jinsi mwandishi wa Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea alivyoshughulikia Nafasi ya mwanamke.(Solved)
Onyesha jinsi mwandishi wa Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea alivyoshughulikia Nafasi ya mwanamke.
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Onyesha jinsi mwandishi wa Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea alivyoshughulikia Nafasi ya vijana.(Solved)
Onyesha jinsi mwandishi wa Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea alivyoshughulikia Nafasi ya vijana.
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- Kuna mfanano mkubwa kati ya ulumbi na hotuba. Thibitisha.(Solved)
Kuna mfanano mkubwa kati ya ulumbi na hotuba. Thibitisha.
Date posted: October 4, 2019. Answers (1)
- "Wema wako umeniua kabisa………Nina jishtaki mwenyewe kila siku kwa miaka na miaka".(Solved)
KIDAGAA KIMEMWOZEA: Ken Walibora.
"Wema wako umeniua kabisa………Nina jishtaki mwenyewe kila siku kwa miaka na miaka".
(a) Eleza muktadha wa maneno haya.
(b) Onyesha kwa kutoa mifano kuwa anayeambiwa maneno haya alikuwa na wema.
(c) Eleza umuhimu wa mhusika mashaka katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)