Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Niaje wasee! Ma-holiday ndizo hizo tena. Najua ma-mission ni mingi! Lakini jo, mambo imebadilika ! Ni kubaya maze. Usifikirie kila kitu unaona ni reality, ukadhani ni...

      

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata:-

Niaje wasee! Ma-holiday ndizo hizo tena. Najua ma-mission ni mingi! Lakini jo,
mambo imebadilika ! Ni kubaya maze. Usifikirie kila kitu unaona ni reality, ukadhani ni gold !
Hiyo siyo real life maze ! Round hii maze ni ‘‘Ku-chill!’’ Usipige ma-stunts zingine zitakuacha uki-regret later! NI POA KU- CHILL au aje maze?


a) Bainisha rejista ya mazungumzo haya
b) Kwa kurejelea kifungu andika sifa za rejista hii.
c) Kwa nini watu hutumia lugha zaidi ya moja.
d) Orodhesha hatua tatu zinazoweza kuchukuliwa kusuluhisha matatizo yanayokumba Kiswahili nchini.

  

Answers


Maurice
(a)Lugha ya vijana

(b) -Kubadilisha msimbo –usifikirie kila kitu unaona ni reality.
-Si lugha sanifu-Najua ma-mission ni nyingi lakini jo, mambo imebadilika
-Matumizi ya sheng- Ma-mission
Ku-chill
Uki-regret

-Matumizi ya sentensi fupi- Ni kibuya maze
Ni poa kuchill

-Kuchanganya msimo-Kuchill ;Ukiregret ;Ma-mission.

(c)
-Ukosefu wa msamiati.
-Kukubalika katika kikundi fulani.
-Kujitambulisha na lugha fulani au kuonyesha umahiri katika lugha zote mbili


(d)-Kutilia mkazo ufundishaji ufaao wa Kiswahili.

-Kupitishwa kwa sera nzuri inayoweka wazi malengo ya serikali kuhusu lugha hii.

-Kuhimiza kuwepo kwa idara za Kiswahili katika taasisi za juu ili kuendeleza utafiti.

-Raia kukumbushwa kuionea fahari lugha hii.

-Wachapishaji kuhimizwa kuchapisha machapisho ya Kiswahili.

-Vipindi vya redio na runinga viwepo vya kuhimiza matumizi fasaha ya Kiswahili.

-Kiswahili kuwa msingi muhimu katika taasisi za elimu. kama Daktari asiweze kuwa
daktari bila kuonyesha uwezo mzuri wa lugha ya Kiswahili.
maurice.mutuku answered the question on October 8, 2019 at 10:26


Next: Fafanua changamoto tano zinazozuia maenezi ya haraka ya lugha ya Kiswahili
Previous: A : Ohh, dada NaomiB : Dada Ruth (anamsogea kwa bashasha wanakumbatiana). Ahh Mungu asifiwe!A: Asifiwe sanaB: Ehh dadangu, miezi ...mingi...sijakuonaA: dada wee...Nilitumwa huko kusini...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions