AZIZ : Ingia 46! Adams mbao Kenyatta, railways beba! 46 Adams mbao kenyatta, railways! SHIKU : Namba nane ngapi? AZIZ : Mbao ingia, blue. SHIKU : Nina hashuu. AZIZ...

      

AZIZ : Ingia 46! Adams mbao Kenyatta, railways beba! 46 Adams mbao kenyatta, railways!

SHIKU : Namba nane ngapi?

AZIZ : Mbao ingia, blue.

SHIKU : Nina hashuu.

AZIZ : Blue Auntie.

SHIKU : Sina.

AZIZ : Ingia. 46 Adams mbao, kenyatta railways gari bebabeba.

AHENDERA : Mimi sinako shirini. Chukuako tu kumi.

AZIZ : Dinga inakunywanga petrol mzee.

AHENDERA: Kumi mingi.

AZIZ : Haaya ingia twende. Driver imeshon twende.


(i) Eleza muktadha wa mazungumzo haya
(ii) Taja sifa sita za lugha iliyotumika katika mazungumzo haya

  

Answers


Maurice
i) - Hii ni sajili ya magari ya uchukuzi
- Inatokea katika kituo cha matatu au barabarani gari linaposimama kubeba abiria
- Kuna utingo anayetangaza kiasi cah nauli kwa wasafiri wanaotaka kulipa malipo nafuu


ii) - Kuna matumizi ya lugha maalum kama 46, ingia twende shona
- Kuna kutaja vituo mbalimbali ambako gari litapitia
- Ni lugha ya kuchanganya ndimi kama vile “driver”
- Inatumia misimu au simi k.m hashuu, dinga n.k
- Haizingatii sarufi sanifu k.m inakunywanga, sinako
- Sentensi ni fupi fupi
- Ina ucheshi mwingi
maurice.mutuku answered the question on October 9, 2019 at 05:10


Next: State the criticism of learner-centered curriculum design approach ?
Previous: Mzee Oluoch :....................................................................ni kweli hayo! Mzee Mwenda : Ndio. Huyu mtoto wangu nimemsomesha mpaka akahitimu chuo kikuu na anafanya kazi ya uhasibu. Mzee Oluoch : Na wangu...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions