Mzee Oluoch :....................................................................ni kweli hayo! Mzee Mwenda : Ndio. Huyu mtoto wangu nimemsomesha mpaka akahitimu chuo kikuu na anafanya kazi ya uhasibu. Mzee Oluoch : Na wangu...

      

Mzee Oluoch :....................................................................ni kweli hayo!

Mzee Mwenda : Ndio. Huyu mtoto wangu nimemsomesha mpaka akahitimu chuo kikuu na anafanya kazi ya uhasibu.

Mzee Oluoch : Na wangu amehitimu na sasa ana shahada ya uzamili. Yeye ni mhandisi
mkuu. Chukua tu mbuzi hamsini na utukubalie kujenga uhusiano wa ukwe.

Mzee Mwenda : Je, mbuzi hao ni wa ‘mfuko’ au ni .......?

(a) Mazungumzo ya aina hii hutokea katika muktadha wa aina gani?
(b) Eleza sifa nane za lugha inayotumika katika wa aina hii

Mzee Oluoch : Kuna wa mfuko ......thelathini na hao wengine ishirini.

Mzee Mwenda : Basi lete hao ulio nao. Wengine hamsini watabaki deni. Utakuwa
ukinilipa polepole. Idhini yangu nimetoa ili mipango iendelee.

  

Answers


Maurice
a) Muktadha wa ndoa/ arusi/ kuzungumza juu ya mahari

b)
i. Lugha ya kujibizana
ii. Kukatana kalmia/ kauli
iii. Sentensi fupifupi- lugha ya mkato
iv. Kuna matumizi ya udokezo mfano au ni………………..
v. Lugha ya kupatana/ kuelewana mfano basi lete hao ulio nao…
vi. Lugha ya kujisifu mfano huyu motto wangu nimemsomesha
vii. Lugha ya ahadi
viii. Lugha ya istiara mfano je mbuzi hao ni wa mfuko au……….
ix. Lugha yenye misemo- kujenga ukwe
maurice.mutuku answered the question on October 9, 2019 at 05:20


Next: AZIZ : Ingia 46! Adams mbao Kenyatta, railways beba! 46 Adams mbao kenyatta, railways! SHIKU : Namba nane ngapi? AZIZ : Mbao ingia, blue. SHIKU : Nina hashuu. AZIZ...
Previous: Fill in the blank spaces in the passage below with the most appropriate word.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions