Umekata mti mtima Umeangukia nyumba yako Umeziba mto hasira ...................

      

SHAIRI ‘A’.
Umekata mti mtima
Umeangukia nyumba yako
Umeziba mto hasira
Nyumba yako sasa mafurikoni
Na utahama
Watoto Wakukimbia
Mbuzi kumkaribia chui
Alijigeuza Panya
Akalia kulikuwa na pala
Kichwani
Mchawi kutaka sana kutisha
Alijigeuza Simba
Akalia na risasi kichwani
Jongoo kutaka sana kukimbia
Aliomba miguu elfu
Akaachwa na nyoka
Hadija wapi sasa yatakwenda
Bwanako kumpa sumu ?
Hadija umeshika nyoka kwa mkia
Hadija umepitia nyuma ya punda


SHAIRI ‘B’
Piteni jamani, Piteni haraka
Nendeni, nendeni huko mwendako
Mimi haraka, haraka sina
Mzigo wangu, mzigo mzito mno
Na chini sitaki kuweka
Vijana kwa nini hampiti ?
Kwa nini mwanicheka kisogo ?
Mzigo niliobeba haupo.
Lakini umenipinda ngongo na
Nendako
Haya piteni ! Piteni haraka ! Heei !
Mwafikiri mwaniacha nyuma !
Njia ya maisha ni moja tu.
Huko mwendako ndiko nilikotoka
Na nilipofikia wengi wenu
Hawatafika.
Kula nimekula na sasa mwasema
Niko nyuma ya wakati
Lakini kama mungepita mbele
Na uso wangu kutazama
Ningewambia siri miaka
Mingi.

(a) Haya ni mashairi ya aina gani ? Toa saabu
(b) Washairi hawa wawili wanalalamika. Yafafanue malalamishi yao
(c) Onyesha jinsi kinaya kinavyojitokeza katika tungo hizi mbili
(d) Ni vipi Hadija :-
(i) Amekata mti mtima ?
(ii) Amepita nyuma ya Punda
(e) Toa mifano 2 ya uhuru wa mashairi kwa kurejelea mashairi haya
(f) Kwa kurejelea shairi ‘B’ eleza maana ya:-
(i) Mzigo
(ii) Siri
(iii) Kula nimekula
(iv) Niko nyuma ya wakati

  

Answers


Maurice
a) (i) Mashairi huru
ii) Hayazingatii arudhi za betu,vina, mishororo, mizani na kibwagizo

b) i) SHAIRI A – Anamlalamikia Hadija kwa kumuuwa mumewe kwa kumpa sumu.
ii) SHAIRI B – Anawalalamikia vijana ambao wanamcheka eti amezeeka na kupitwa
na wakati Wanamramba Kisogo

c) i) Katika SHAIRI ‘A’ - Hadija alidhani kumuua mmewe angepata suluhisho lakini badala
yake amejiletea matatizo zaidi. Watu sasa wamemsuta kwa kitendo chake na watoto
wanamsumbua.
ii) Katika SHAIRI ‘B’ – Mshairi anawakejeli vijana ambao wnamramba mzee kisogo
bila kujua kwamba hawataki kupita.

d)i) Amemuua mumewe – Mti mkuu au kichwa cha nyumba.
ii) Anapata shida za Kujitakia – matatizo yamefurika ngyumbani kama mto (ukupita nyuma ya
punda atakutega au kukupiga teke)

e) Inkisari – Nendako – Niendako
- Mwendako – Mnakoenda
- Bwanako – Bwana yako

f) -Mzigo – uzee/umri.
-Siri – Tajriba /Waarifa / Elimu ya maisha.
-Kula nimekula - Ameishi miaka mingi
Niko nyuma ya wakati - Amebaki nyuma na usasa
maurice.mutuku answered the question on October 9, 2019 at 05:51


Next: Rearrange the adjectives in the following sentences in the correct order to describe the italicized nouns.
Previous: Rewrite the following sentences changing them into the passive form.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions