Sinisumbuwe akili, nakusihi e mwandani.Afya yangu dhahili, mno nataka amaniNawe umenikabili, nenende sipitaliniSisi tokea azali, twende zetu mizumuniNifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?Mababu hawakujali, wajihisipo...

      

Sinisumbuwe akili, nakusihi e mwandani.
Afya yangu dhahili, mno nataka amani
Nawe umenikabili, nenende sipitalini
Sisi tokea azali, twende zetu mizumuni
Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?

Mababu hawakujali, wajihisipo tabani
Tuna dawa za asili, hupati sipitalini
Kwa nguvu za kirijali, Mkuyati uamini
Kaafuri pia kali, dawa ya ndwele fulani
Nifuateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?

Mtu akiwa hali, tumbo lina walakini,
Dawa yake ni subili, au zongo huanoni
Zabadili pia sahali, kwa maradhi yalo ndani
Au kwenda wasaili, wenyewe walo pangani
Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?

Mtu kwenda sipitali, ni kutojuwa yakini
Daktari k’ona mwili, tanena kensa tumboni
Visu visitiwe makali, tayari kwa pirisheni
Ukatwe kama fagili, tumbo nyangwe na maini
Nifuateni sipitalini, na dawa ziko nyumbani?

Japo maradhi dhalili, kutenguliwa tegoni
Yakifika sipitali, huwa hayana kifani
Wambiwa damu kaliti, ndugu msaidieni
Watu wakitaamali, kumbe ndiyo bunani
Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?

Mizimu wakupa kweli, Wakueleze undani.
Maradhiyo ni ajali, yataka vitu thamani
Utete huku wawili, wa manjano na kijani
Matunda pia asali, vitu vyae shamoni
Nifuateni sipati, na dawa zi langoni?


(a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka
(b) Mtunzi alikuwa na lengo gani alipotunga shairi hili
(c) Mbona mshairi hataki kwenda hospitalini
(d) Eleza umbo la shairi hili
(e) Kwa nini mshairi alitumia ritifaa katika ushairi ?
(f) Andika maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa kwenye shairi :-
(i) Dhalili –
(ii) Azali-
(iii)Sahali-

  

Answers


Maurice
a) – Matibabu ya kiasili | Dawa za asili| dawa za Kisasa.

b) kuonyesha kuwa dawa asili zinafaa kwa matibabu kuliko za Kisasa. Watu wazirejele.

c) Ana matibabu ya kiasili
Hospitali kuna operasheni ya visu.
Kuna dawa za asili zisizopatikana hospitali.

d) Beti Sita.
-Takhmisa| mishoro mitano.
-Mtiririko – vina bvya ukwapi na utao vinafanana katika beti zote.
-Mathnawi – vipande viwili.
-Mizani ni 8,8
-Lina kiisho – mshoro wa mwisho unarudiwa beti hadi beti katika beti zote.

e) kupata idai ya mizani inayotakikana

f) i) Dhalili – Kudharauliwa,nyonge, maskini,dhaifu.
ii)Azali – zamani.
iii)Sahali – Urahisi/ wepesi.
maurice.mutuku answered the question on October 9, 2019 at 06:05


Next: Fill in the blank spaces with the most appropriate words.
Previous: Read the poem below and answer the questions. A freedom song

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions