WAFULA KABILIANA NA KISU Ee mpwa wangu, Kwetu hakuna muoga, Uoga ukikufikia, huenda ni wa akina mamayo, Fahali tulichinja ili uwe mwanamme, Eewe mpwa wangu, kisu kikali ajabu ! Iwapo utatingiza...

      

WAFULA KABILIANA NA KISU
Ee mpwa wangu,
Kwetu hakuna muoga,
Uoga ukikufikia, huenda ni wa akina mamayo,
Fahali tulichinja ili uwe mwanamme,
Eewe mpwa wangu, kisu kikali ajabu !
Iwapo utatingiza kichwa,
Uhamie kwa wasiotahiri.

Wanaume wa mbari yetu,
Si waoga wa kisu,
Wao hukatwa kuanzia macheo hadi machweo,
Wewe ndiye wa kwanza,
Iwapo utashindwa,
Wasichana wote,
Watakucheka,
Ubaki msununu,
Simama jiwe liwe juu,
Ndege zote ziangamie.

Simu nimeipokea,
Ngariba alilala jikoni,

Visu ametia makali,
Wewe ndiye wangojewa,
Hadharani utasimama,
Macho yote yawe kwako,
Iwapo haustahimili kisu,
Jiuzulu sasa mpwa wangu,
Hakika sasa mpwa wangu,
Hakika tutakusamehe, mwaka kesho unakuja.


Asubuhi ndio hii,
Mama mtoto aamushwe,
Upweke ni uvundo,
Iwapo utatikisa kichwa,
Iwapo wewe ni mme,
Kabiliana na kisu kikali,
Hakika ni kikali!

Kweli ni kikali!
Wengi wasema ni kikali!
Fika huko uone ukali!
Mbuzi utapata,
Na hata shamba la mahindi,
Simama imara,
Usiende kwa wasiotahiri


(a) Hili ni shairi la aina gani ? Thibitisha
(b) Ni nani anayeimba shairi hili na analiimba kwa nani ?
(c) Toa ithibati kwenye shairi hili kuthibitisha kuwa msimulizi ana taasubi za kiume
(d) Taja kwa kutolea mifano mbinu zozote nne za uandishi katika shairi hili
(e) Taja shughuli zozote mbili za kiuchumi za jamii inayorejelewa katika shairi hili
(f) Eleza kwa mifano, uhuru wa kishairi katika shairi hili
(g) Msamiati ufuatao umetumika kwa maana gani katika shairi hili ?
(i) Mbari
(ii) Msununu
(iii) Ngariba
(iv) Uvundo

  

Answers


Maurice
(a) - Shairi huru
- Halijazingatia kanunu za utunzi wa mashairi wa kuzingatia arudhi

(b) - Anayeimba ni mjomba
- Anayeimbiwa ni mpwa wake

(c) – Anaambiwa uoga ukimtikia huenda ni wa akina mamaye
- Alichinjiwa fahali ili awe mwanaume

(d) – Chuku – wao hukatwa kuanzia macheo hadi machweo
- Takriri – kikali
- Asitiari – upweke ni uvundo
- Tashhisi – uoga ukifikia

(e) - Wakulima – Atapewa shamba la mahindi
- Wafugaji – Atapewa mbuzi

(f) – Tabdila – aamushwe – aamshwe
- Inkisari – Mme – mwanamme
- Kuboronga sarufi – Fahali tulichinja tulichinja fahali

(g) - Mbari Ukoo ; kikundi fulani
- Msununu – Anayenuna
- Ngariba – Mtahirishaji
- Uvundo – Harufu mbaya
maurice.mutuku answered the question on October 9, 2019 at 06:15


Next: Explain five ways of making face-to-face communication effective.
Previous: Underline the odd one out according to the pronunciation of letters ‘S’

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions