Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

1. Nitampa nani, sauti yangu ya dhati Kwa kipimo gani, ingawa kiwakatiti Amefanya nini, la kutetea umati Kipimo ni kipi? 2. Yupi wa maani, asosita katikati Alo na maoni, yasojua...

      

1. Nitampa nani, sauti yangu ya dhati
Kwa kipimo gani, ingawa kiwakatiti
Amefanya nini, la kutetea umati
Kipimo ni kipi?

2. Yupi wa maani, asosita katikati
Alo na maoni, yasojua gatigati
Atazame chini, kwa kile ule wakati
Kipimo ni kipi?

3. Alo mzalendo, atambuaye shuruti
Asiye mafundo, asojua mangiriti
Anoshika pendo, hata katika mauti
Kipimo ni kipi?

4. Kipimo ni kipi, changu mimi kudhibiti
Utu uko wapi, ni wapi unapoketi
Nje kwa mkwapi, au ndani kwa buheti
Kipimo ni kipi?

a) Eleza umbo la shairi hili
b) Taja na ueleze jinsi mwandishi alivyotumia uhuru wa ushairi
c) Eleza ujumbe unaowasilishwa na mshairi
d) Andika ubeti wa tatu katika lugha ya nathari
e) Taja bahari tatu zinazojitokeza katika shairi na utoe sababu
f) Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika shairi hili
i) Katiti
ii) Gatigati
iii) Mangiriti

  

Answers


Maurice
a) - Beti nne
- Mishororo mine katika kila ubet (tarbia)
- Mshororo wa nne mfupi (msuko)
- Mizani 6:8 mshororo wa 1-3 kikai
6 mshororo wa mwisho

b) Inkisari – Anoshika
- Alo
- Asosita
Lafudhi – Katiti
- mangiriti


c) - Anataka asikike (mawazo yake yasikika)
- Anatafuta atakayoeleza ujumbe wake
- anashindwa atatumia kipimo kipi
- Mtu huyo lazima awe mzalendo aliye jasiri
- Lazima awe anayetambua utu

d) Lugha ya nadharia
Aliye mzalendo na alambuaye haya mtu asiye mwoga, aliyejawa na upendo hata wakati wa
hatari, Ni kipimo kipi cha kumtambua mtu kama huyu

e) tarbia – Mishororo mine kila ubeti
Kikai – Mizani isiyozidi 15
Msuko – Kibwagizo kifupi

f) i) katili – Kidogo
Gati gati – Ubaguzi
Mangiriti - mambo ya upipi
maurice.mutuku answered the question on October 9, 2019 at 06:36


Next: Fill in each blank space in the passage below with the most appropriate word.
Previous: Read the poem below and answer the questions that follow.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • 1. Mke wangu wameshanipoka Ndugu zangu, wamedai ububu Wazazi kuzoea kunigombeza(Solved)

    HATIMA YANGU
    1. Mke wangu wameshanipoka
    Ndugu zangu, wamedai ububu
    Wazazi kuzoea kunigombeza

    2. Juzi mali lilimbikiza
    Furaha lilitanda
    Makanwa yalijaziwa
    Hoi hoi ikawa desturi

    3. Kilabu tulikwenda
    Nyama tulichoma
    Mahali tulizuru
    Tuliteremsha!

    4. Leo mambo yamenigeuka
    Wao masahibu siwaoni
    Matumbo yakaninguruma
    Kama radi ya mvua

    5. Nyumbani nimebaki pweke
    Mke amenitoroka
    Watoto wameparara
    Skuli kugharamia
    Imegeuka balaa belua

    6. Ndipo nimeamua
    Afadhali kitanzi badala ya balaa
    Kumbe kupanga ndiyo maana
    Maisha na waasia


    (a) Eleza mambo muhimu yanayoelezwa katika shairi hili
    (b) Fafanua sifa mbili za anayezungumza katika shairi
    (c) Dondoa na ufafanue mbinu zozote mbili za lugha katika shairi hili
    (d) Eleza maana ya:-
    (i) Ndugu zangu wamedai ububu
    (ii) Kumbe kupanga ndiyo maana

    Date posted: October 9, 2019.  Answers (1)

  • WAFULA KABILIANA NA KISU Ee mpwa wangu, Kwetu hakuna muoga, Uoga ukikufikia, huenda ni wa akina mamayo, Fahali tulichinja ili uwe mwanamme, Eewe mpwa wangu, kisu kikali ajabu ! Iwapo utatingiza...(Solved)

    WAFULA KABILIANA NA KISU
    Ee mpwa wangu,
    Kwetu hakuna muoga,
    Uoga ukikufikia, huenda ni wa akina mamayo,
    Fahali tulichinja ili uwe mwanamme,
    Eewe mpwa wangu, kisu kikali ajabu !
    Iwapo utatingiza kichwa,
    Uhamie kwa wasiotahiri.

    Wanaume wa mbari yetu,
    Si waoga wa kisu,
    Wao hukatwa kuanzia macheo hadi machweo,
    Wewe ndiye wa kwanza,
    Iwapo utashindwa,
    Wasichana wote,
    Watakucheka,
    Ubaki msununu,
    Simama jiwe liwe juu,
    Ndege zote ziangamie.

    Simu nimeipokea,
    Ngariba alilala jikoni,

    Visu ametia makali,
    Wewe ndiye wangojewa,
    Hadharani utasimama,
    Macho yote yawe kwako,
    Iwapo haustahimili kisu,
    Jiuzulu sasa mpwa wangu,
    Hakika sasa mpwa wangu,
    Hakika tutakusamehe, mwaka kesho unakuja.


    Asubuhi ndio hii,
    Mama mtoto aamushwe,
    Upweke ni uvundo,
    Iwapo utatikisa kichwa,
    Iwapo wewe ni mme,
    Kabiliana na kisu kikali,
    Hakika ni kikali!

    Kweli ni kikali!
    Wengi wasema ni kikali!
    Fika huko uone ukali!
    Mbuzi utapata,
    Na hata shamba la mahindi,
    Simama imara,
    Usiende kwa wasiotahiri


    (a) Hili ni shairi la aina gani ? Thibitisha
    (b) Ni nani anayeimba shairi hili na analiimba kwa nani ?
    (c) Toa ithibati kwenye shairi hili kuthibitisha kuwa msimulizi ana taasubi za kiume
    (d) Taja kwa kutolea mifano mbinu zozote nne za uandishi katika shairi hili
    (e) Taja shughuli zozote mbili za kiuchumi za jamii inayorejelewa katika shairi hili
    (f) Eleza kwa mifano, uhuru wa kishairi katika shairi hili
    (g) Msamiati ufuatao umetumika kwa maana gani katika shairi hili ?
    (i) Mbari
    (ii) Msununu
    (iii) Ngariba
    (iv) Uvundo

    Date posted: October 9, 2019.  Answers (1)

  • Sinisumbuwe akili, nakusihi e mwandani.Afya yangu dhahili, mno nataka amaniNawe umenikabili, nenende sipitaliniSisi tokea azali, twende zetu mizumuniNifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?Mababu hawakujali, wajihisipo...(Solved)

    Sinisumbuwe akili, nakusihi e mwandani.
    Afya yangu dhahili, mno nataka amani
    Nawe umenikabili, nenende sipitalini
    Sisi tokea azali, twende zetu mizumuni
    Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?

    Mababu hawakujali, wajihisipo tabani
    Tuna dawa za asili, hupati sipitalini
    Kwa nguvu za kirijali, Mkuyati uamini
    Kaafuri pia kali, dawa ya ndwele fulani
    Nifuateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?

    Mtu akiwa hali, tumbo lina walakini,
    Dawa yake ni subili, au zongo huanoni
    Zabadili pia sahali, kwa maradhi yalo ndani
    Au kwenda wasaili, wenyewe walo pangani
    Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?

    Mtu kwenda sipitali, ni kutojuwa yakini
    Daktari k’ona mwili, tanena kensa tumboni
    Visu visitiwe makali, tayari kwa pirisheni
    Ukatwe kama fagili, tumbo nyangwe na maini
    Nifuateni sipitalini, na dawa ziko nyumbani?

    Japo maradhi dhalili, kutenguliwa tegoni
    Yakifika sipitali, huwa hayana kifani
    Wambiwa damu kaliti, ndugu msaidieni
    Watu wakitaamali, kumbe ndiyo bunani
    Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?

    Mizimu wakupa kweli, Wakueleze undani.
    Maradhiyo ni ajali, yataka vitu thamani
    Utete huku wawili, wa manjano na kijani
    Matunda pia asali, vitu vyae shamoni
    Nifuateni sipati, na dawa zi langoni?


    (a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka
    (b) Mtunzi alikuwa na lengo gani alipotunga shairi hili
    (c) Mbona mshairi hataki kwenda hospitalini
    (d) Eleza umbo la shairi hili
    (e) Kwa nini mshairi alitumia ritifaa katika ushairi ?
    (f) Andika maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa kwenye shairi :-
    (i) Dhalili –
    (ii) Azali-
    (iii)Sahali-

    Date posted: October 9, 2019.  Answers (1)

  • Umekata mti mtima Umeangukia nyumba yako Umeziba mto hasira ...................(Solved)

    SHAIRI ‘A’.
    Umekata mti mtima
    Umeangukia nyumba yako
    Umeziba mto hasira
    Nyumba yako sasa mafurikoni
    Na utahama
    Watoto Wakukimbia
    Mbuzi kumkaribia chui
    Alijigeuza Panya
    Akalia kulikuwa na pala
    Kichwani
    Mchawi kutaka sana kutisha
    Alijigeuza Simba
    Akalia na risasi kichwani
    Jongoo kutaka sana kukimbia
    Aliomba miguu elfu
    Akaachwa na nyoka
    Hadija wapi sasa yatakwenda
    Bwanako kumpa sumu ?
    Hadija umeshika nyoka kwa mkia
    Hadija umepitia nyuma ya punda


    SHAIRI ‘B’
    Piteni jamani, Piteni haraka
    Nendeni, nendeni huko mwendako
    Mimi haraka, haraka sina
    Mzigo wangu, mzigo mzito mno
    Na chini sitaki kuweka
    Vijana kwa nini hampiti ?
    Kwa nini mwanicheka kisogo ?
    Mzigo niliobeba haupo.
    Lakini umenipinda ngongo na
    Nendako
    Haya piteni ! Piteni haraka ! Heei !
    Mwafikiri mwaniacha nyuma !
    Njia ya maisha ni moja tu.
    Huko mwendako ndiko nilikotoka
    Na nilipofikia wengi wenu
    Hawatafika.
    Kula nimekula na sasa mwasema
    Niko nyuma ya wakati
    Lakini kama mungepita mbele
    Na uso wangu kutazama
    Ningewambia siri miaka
    Mingi.

    (a) Haya ni mashairi ya aina gani ? Toa saabu
    (b) Washairi hawa wawili wanalalamika. Yafafanue malalamishi yao
    (c) Onyesha jinsi kinaya kinavyojitokeza katika tungo hizi mbili
    (d) Ni vipi Hadija :-
    (i) Amekata mti mtima ?
    (ii) Amepita nyuma ya Punda
    (e) Toa mifano 2 ya uhuru wa mashairi kwa kurejelea mashairi haya
    (f) Kwa kurejelea shairi ‘B’ eleza maana ya:-
    (i) Mzigo
    (ii) Siri
    (iii) Kula nimekula
    (iv) Niko nyuma ya wakati

    Date posted: October 9, 2019.  Answers (1)

  • Mzee Oluoch :....................................................................ni kweli hayo! Mzee Mwenda : Ndio. Huyu mtoto wangu nimemsomesha mpaka akahitimu chuo kikuu na anafanya kazi ya uhasibu. Mzee Oluoch : Na wangu...(Solved)

    Mzee Oluoch :....................................................................ni kweli hayo!

    Mzee Mwenda : Ndio. Huyu mtoto wangu nimemsomesha mpaka akahitimu chuo kikuu na anafanya kazi ya uhasibu.

    Mzee Oluoch : Na wangu amehitimu na sasa ana shahada ya uzamili. Yeye ni mhandisi
    mkuu. Chukua tu mbuzi hamsini na utukubalie kujenga uhusiano wa ukwe.

    Mzee Mwenda : Je, mbuzi hao ni wa ‘mfuko’ au ni .......?

    (a) Mazungumzo ya aina hii hutokea katika muktadha wa aina gani?
    (b) Eleza sifa nane za lugha inayotumika katika wa aina hii

    Mzee Oluoch : Kuna wa mfuko ......thelathini na hao wengine ishirini.

    Mzee Mwenda : Basi lete hao ulio nao. Wengine hamsini watabaki deni. Utakuwa
    ukinilipa polepole. Idhini yangu nimetoa ili mipango iendelee.

    Date posted: October 9, 2019.  Answers (1)

  • AZIZ : Ingia 46! Adams mbao Kenyatta, railways beba! 46 Adams mbao kenyatta, railways! SHIKU : Namba nane ngapi? AZIZ : Mbao ingia, blue. SHIKU : Nina hashuu. AZIZ...(Solved)

    AZIZ : Ingia 46! Adams mbao Kenyatta, railways beba! 46 Adams mbao kenyatta, railways!

    SHIKU : Namba nane ngapi?

    AZIZ : Mbao ingia, blue.

    SHIKU : Nina hashuu.

    AZIZ : Blue Auntie.

    SHIKU : Sina.

    AZIZ : Ingia. 46 Adams mbao, kenyatta railways gari bebabeba.

    AHENDERA : Mimi sinako shirini. Chukuako tu kumi.

    AZIZ : Dinga inakunywanga petrol mzee.

    AHENDERA: Kumi mingi.

    AZIZ : Haaya ingia twende. Driver imeshon twende.


    (i) Eleza muktadha wa mazungumzo haya
    (ii) Taja sifa sita za lugha iliyotumika katika mazungumzo haya

    Date posted: October 9, 2019.  Answers (1)

  • Eleza juhudi tano zinazotumika kukiendeleza Kiswahili(Solved)

    Eleza juhudi tano zinazotumika kukiendeleza Kiswahili

    Date posted: October 8, 2019.  Answers (1)

  • Bw. Mosuka : Mheshimiwa spika, naichukua fursa hii kuipinga hoja iliyowasilishwa na mbunge wa Mahira, mheshimiwa Kochaberi kuhusu suala la kuavya.... (a) Hii ni sajili gani? (b) Eleza...(Solved)

    Bw. Mosuka : Mheshimiwa spika, naichukua fursa hii kuipinga hoja iliyowasilishwa na
    mbunge wa Mahira, mheshimiwa Kochaberi kuhusu suala la kuavya....
    (a) Hii ni sajili gani?
    (b) Eleza sifa za mazungumzo ya sajili hii

    Date posted: October 8, 2019.  Answers (1)

  • A : Ohh, dada NaomiB : Dada Ruth (anamsogea kwa bashasha wanakumbatiana). Ahh Mungu asifiwe!A: Asifiwe sanaB: Ehh dadangu, miezi ...mingi...sijakuonaA: dada wee...Nilitumwa huko kusini...(Solved)

    Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali :

    A : Ohh, dada Naomi
    B : Dada Ruth (anamsogea kwa bashasha wanakumbatiana). Ahh Mungu asifiwe!
    A: Asifiwe sana
    B: Ehh dadangu, miezi ...mingi...sijakuona
    A: dada wee...Nilitumwa huko kusini ...Kuwahubiria watu injili (mtuo mdogo)singeweza kukata...
    B: Ehh, usiwe kama Yona
    A: Habari ya siku nyingi?
    B; Nzuri Mungu bado ameendelea kunibariki
    A: Amen!
    B: Nimeendelea kuiona neema yake
    A: Amen! Asifiwe Bwana
    B: Halleluya
    A: Ni Mungu wa miujiza!
    B : Amen. Hata nami nimeona neema yake
    Bado niko imara katika wokovu katika siku hizi za mwisho
    A : Amen !
    B : Ni Mungu wa ajabu kweli !
    A : Nilikumbana na matatizo lakini nikategemea sala
    Kama Paulo na sila… Na nikashinda (anatua). Sikuweza kumpa shetani nafasi…maana
    ameshindwa
    B : Ameshindwa kabisa


    (i) Hii ni sajili ya wapi ? Fafanua
    (ii) Taja na ueleze sifa za sajili hii
    (iii) Taja na ueleze mambo mawili muhimu yaliyosaidia katika maenezi ya Kiswahili
    Afrika mashariki na kati

    Date posted: October 8, 2019.  Answers (1)

  • Niaje wasee! Ma-holiday ndizo hizo tena. Najua ma-mission ni mingi! Lakini jo, mambo imebadilika ! Ni kubaya maze. Usifikirie kila kitu unaona ni reality, ukadhani ni...(Solved)

    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata:-

    Niaje wasee! Ma-holiday ndizo hizo tena. Najua ma-mission ni mingi! Lakini jo,
    mambo imebadilika ! Ni kubaya maze. Usifikirie kila kitu unaona ni reality, ukadhani ni gold !
    Hiyo siyo real life maze ! Round hii maze ni ‘‘Ku-chill!’’ Usipige ma-stunts zingine zitakuacha uki-regret later! NI POA KU- CHILL au aje maze?


    a) Bainisha rejista ya mazungumzo haya
    b) Kwa kurejelea kifungu andika sifa za rejista hii.
    c) Kwa nini watu hutumia lugha zaidi ya moja.
    d) Orodhesha hatua tatu zinazoweza kuchukuliwa kusuluhisha matatizo yanayokumba Kiswahili nchini.

    Date posted: October 8, 2019.  Answers (1)

  • Fafanua changamoto tano zinazozuia maenezi ya haraka ya lugha ya Kiswahili(Solved)

    Fafanua changamoto tano zinazozuia maenezi ya haraka ya lugha ya Kiswahili

    Date posted: October 8, 2019.  Answers (1)

  • Fafanua mikakati mitano inayoweza kuchapuza kukua na kuenea kwa kiswahili nchini Kenya(Solved)

    Fafanua mikakati mitano inayoweza kuchapuza kukua na kuenea kwa kiswahili nchini Kenya

    Date posted: October 8, 2019.  Answers (1)

  • Uchunguzi uliofanywa umeonyesha kuwa anasumbuliwa na uto mwingi mwilini. Uto unaweza kudondoshwa kwa kufanya mazoezi, kupunguza ulaji wa vyakula vya wanga na hata protini. Protini...(Solved)

    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata

    Uchunguzi uliofanywa umeonyesha kuwa anasumbuliwa na uto mwingi mwilini. Uto unaweza kudondoshwa kwa kufanya mazoezi, kupunguza ulaji wa vyakula vya wanga na hata protini. Protini iwapo nyingi mwilini hugeuzwa kuwa glukosi ambayo huhifadhiwa mwilini. Hii huwa msingi wa unene pia ambao unahatarisha afya. Jamaa yake aliyeaga dunia alikuwa mgonjwa wa bolisukari ambayo inaweza kurithishwa. Kimsingi, lazima awe na welewa bora kabisa wa lishe. Mwenzake naye aliathiriwa na aflatoxins zilikuwa kwenye chakula alichokula.
    (a) Sajili hii inapatikana wapi? Kwa nini?
    (b) Taja sifa zinazohusishwa na sajili yenyewe

    Date posted: October 8, 2019.  Answers (1)

  • Lugha ya kiswahili inakabiliwa na matatizo mengi sana. Yataje na kuyaeleza.(Solved)

    Lugha ya kiswahili inakabiliwa na matatizo mengi sana. Yataje na kuyaeleza.

    Date posted: October 8, 2019.  Answers (1)

  • Saidi : Hallo............Hallo....Huyo ni Bw. Mohamed?Mohamed : Ndio...uko wapi...Saidi : Shuleni...sasa...ulinifikishia ujumbe?Mohamed : La. Parade ilikuwa imehitimishwaSaidi : Sina credit. Nipigie tafadhali.Mohamed : Sina...(Solved)

    Isimu Jamii

    Saidi : Hallo............Hallo....Huyo ni Bw. Mohamed?
    Mohamed : Ndio...uko wapi...
    Saidi : Shuleni...sasa...ulinifikishia ujumbe?
    Mohamed : La. Parade ilikuwa imehitimishwa
    Saidi : Sina credit. Nipigie tafadhali.
    Mohamed : Sina pia, nitatuma sms
    Saidi : Iwe saa hii eh?
    Mohamed : Baada ya dakika tano
    Saidi : Good day
    Mohamed : Welcome

    (a) Taja na uthibitishe sifa zinazojitokeza katika mazungumzo haya
    (b) Eleza sababu za wazungumzaji kutumia mbinu zifuatazo katika mazungumzo yao
    (i) Mdokezo
    (ii) Lugha mseto

    Date posted: October 8, 2019.  Answers (1)

  • Nomino zifuatazo ni za ngeli gani? i) Nzi ii) Soksi(Solved)

    Nomino zifuatazo ni za ngeli gani?
    i) Nzi

    ii) Soksi

    Date posted: October 8, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha aina za shamirisho katika sentensi ifuatayo Soroveya atapimia wanunuzi viwanja.(Solved)

    Bainisha aina za shamirisho katika sentensi ifuatayo
    Soroveya atapimia wanunuzi viwanja.

    Date posted: October 8, 2019.  Answers (1)

  • Changanua sentensi ifuaatayo kwa kielelezo visandu. Mwanafunzi aliyeleta kitabu chake amepongezwa(Solved)

    Changanua sentensi ifuaatayo kwa kielelezo visandu.
    Mwanafunzi aliyeleta kitabu chake amepongezwa

    Date posted: October 8, 2019.  Answers (1)

  • Eleza na udhibitishe kwa mfano, matumizi mawili ya tu.(Solved)

    Eleza na udhibitishe kwa mfano, matumizi mawili ya tu.

    Date posted: October 8, 2019.  Answers (1)

  • Kanusha sentensi hii;- Ukionana naye mwambie aje anione.(Solved)

    Kanusha sentensi hii;-
    Ukionana naye mwambie aje anione.

    Date posted: October 8, 2019.  Answers (1)