Trusted since 2008
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

KIPI NIKITENDE? Tayari ni sarakani, niambie yote johara,Mosi nimpe shukrani, kanizaa bira zira,Wapo haiko hisani, ningefaa kwa uparara,Kipi takachokitenda, ni nene heko kwa mama?Miezi tisa...

KIPI NIKITENDE?
Tayari ni sarakani, niambie yote johara,
Mosi nimpe shukrani, kanizaa bira zira,
Wapo haiko hisani, ningefaa kwa uparara,
Kipi takachokitenda, ni nene heko kwa mama?


Miezi tisa tumboni, yote nina kajinyima,
Kanikopa uchunguni, safari ndefu kazima’
Kama kinda kiotani, kiniasa huyu mama’
Kipi takachokitenda, ninene heko mama ?

Baba siku jana madadi, kawa vingaito mambo,
Kaolewa na asadi, kachalazwa kwa wimbombo,
Kaona – bali jadili, kuchao puani bombo,
Kipi takachokitenda, ninene heko mama?


Kila kuchao zarani, kupalilia kondeni,
Kachanika mpinini, chungu povuka motoni,
Kaviyariya fingani, kinijali jikoni,
Kipi tukachokitenda , ninene heko mama?


Wa siku hizi vijana, wakahujuru nyumbani,
Wengine wao jagina, kawa lofa mutaani,
Hali ukashiba nina, afikapo tu, “kongoni!”
Kipi takachokitenda, ninene heko mama?


Nawe bwana siwe maya, vita hasha kiwa kombo,
Tena simfanye yaya, ya kikoa ndio mambo,
Simtende ya hizaya, siwe mwao kila jambo,
Kipi takachokitenda, ninene heko mama?


Sasa jamvi nakuja, kisa nimesakarika,
Naomba niliyotaja, tatia manani kaka,
Nenayo yasiwe ngoja, ili nipokee baraka,
Mema nitamtendea, apate futahi pia.



(a) Eleza umbo la shairi hili
(b) Kwa nini msanii amshukuru mamaye ?
(c) Ni kina nani wanaokashifiwa na msanii ? Kwa nini ?
(d) Onyesha tofauti katika ujumbe iliyoko katika beti nne za kwanza na mbili zinazofuata
(e) Toa majina mengine yenye maana sawa na haya yaliyotumiwa katika shairi hili :
(i) Mama
(ii) Dawati
(iii) Imara/thabiti
(f) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika kaika shairi:
(i) Kawa vangaito mambo
(ii) Wimbombo
(iii) Kongoni

Answers


Maurice
a)
-Beti saba
-Tarbia – mishororo mine
-Vina vya ndani na vya nje hubadilika badilika
-Pande mbili – ukwapi na utao
-Mizani 8, 8 jumla 16 katika kila mshororo
-Kibwagizo kipo – kipi titakachotenda, ninene huko mama

b)
-Kwa kumzaa bila zira (chuki)
-Kumpenda na kutomuua
-Kujinyima yote mazuri kwa niaba yake
-Kumtunza mfano wa ndege na makinda wake
-Kumtafutia riziki – kufanya kazi (kulima) ili asitaabike
Kumjali
-Kutojali visiki katika ulezi wake kama vile baba yake mkali Zozote
c)
-Vijana ambao baada ya kulelewa na kunenepa hawajali wazazi wao (mama zao)
-Akina baba wanaowapiga wake wao kwa makosa madogo madogo
-Pia akina baba wanaowatesa wake wao. Huwafanya yay nyumabni mwao Zozote

d) katika beti nne za kwanza mshairi anaangazia mema aliyotendewa na mama yake ilhali
katika beti mbili zinazofuata anawakashifu wanaowatendea akina mama wao mabaya

e) Mama – nina (Ubeti wa 2)
Dawati – saraka (Ubeti wa 1)
Imara/ thabiti – jahidi (ubeti wa 3)

f) i) Mambo yakavurugika
ii) Wimbombo – Kipande cha miti cha kupekecha moto. Chuma cha kupulizia moto
iii) Kongoni – Jina la kumkaribisha mtu
maurice.mutuku answered the question on October 9, 2019 at 06:56

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions