Trusted since 2008
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

(vigelegele vya harusi vililia alilili ; x3) Kuumeni : (waliimba) Tumeupata mpilipili na maua yake chikicha x2 Kukeni : (wimbo wao kwa sauti tofauti) Tausi waendaa x2 Tausi...

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yafuatayo :

(vigelegele vya harusi vililia alilili ; x3)
Kuumeni : (waliimba) Tumeupata mpilipili na maua yake chikicha x2

Kukeni : (wimbo wao kwa sauti tofauti) Tausi waendaa x2
Tausi waenda wamuacha mama kwenye banda.

Kuumeni : (wakijibu wimbo) Mwacheni aendee x2
Mwacheni aende akaone mambo ya nyumba.

Kukeni : Mama ataota nini x2.
Ataota nini, hana mtu wa kumletea kuni.

Kuumeni : Ataota moto wa magunzi, wa magunzi wa magunzi. Twamchukua, kisura wetu,
kisura wetu, kisura wetu.
Tausi ni wetu sasa, ni kito chema, ni kito chema ni kito chema.

(i) Wimbo huu ni wa aina gani, na unastahili katika hafla gani ?
(ii) Bainisha wahusika Kuumeni na Kukeni
(iii) Fafanua ujumbe uliojikita katika utungo huu
(iv) Wimbo huu una umuhimu gani hafla ulioimbiwa?
(v) Tambua mtindo uliotumika katika utungo huu

Answers


Maurice
i)
Tumbuizo – wimbo wa kuburudisha katika hafla ya arusi
Wimbo wa kitamaduni

ii) Kuumeni – wanaume
Kukeni – wanawake
Wanaume wanawakilisha wakwe na Tausi (anayeolewa) na wanawake wanawakilisha wazazi wa Tausi

iii) - Watu wa kukeni wana moyo wa kisebusebu na roho kipapo. Walipenda mtoto
wao aolewe lakini awaondokeapo na kwenda kwa mumewe waliona
uchungu, kwani walijua huduma alizokuwa akiwapa tausi, zingekoma mara moja
- Upande wa kuumeni walifurahi kwani walijua Tausi angeongezea huduma upande wao

iv) – Unaburudisha waliofika kwenye sherehe ya arusi
- Unaleta ushirikiano baina ya pande mbili
- Unatoa ujumbe kuwa kuondoka kwa mtu mliyezoena huwa ni wakati mgumu sana

v) takriri – Kurudia maneno kwa madhumuni ya kusisistiza mfano kisura wetu,
maurice.mutuku answered the question on October 11, 2019 at 06:17

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions

  • Onyesha tofauti kati ya vikundi hivi: (i) Hekaya Hurafa (ii) Visakale Visasili (iii) Ngano za mtanziko Ngano za mazimwi (Solved)

    Onyesha tofauti kati ya vikundi hivi:
    (i) Hekaya
    Hurafa

    (ii) Visakale
    Visasili

    (iii) Ngano za mtanziko
    Ngano za mazimwi

    Date posted: October 11, 2019 .    Answers (1)

  • Elezea mbinu nne za kutongolea hadithi (Solved)

    Elezea mbinu nne za kutongolea hadithi

    Date posted: October 11, 2019 .    Answers (1)

  • Ni nini maana ya Tendi? (Solved)

    Ni nini maana ya Tendi?

    Date posted: October 11, 2019 .    Answers (1)

  • MUITALIA ANAZWE Saa kumi alfajiri Sote tuliamshwa Safari tuliianza Wengi wanauliza Mwitalia alikuja lini? Na... (Solved)

    Soma wimbo/shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata

    MUITALIA ANAZWE
    Saa kumi alfajiri
    Sote tuliamshwa
    Safari tuliianza
    Lazima tuimalize
    Maji ukiyavulia nguo
    Lazima uyaoge

    Wazee kwa vijana waliimba
    Muitalia lazima anazwe
    Mashamba yao walilia
    Uui! Jikaze wavulana
    Hawataki rangi hii

    Wengi wanauliza
    Mwitalia alikuja lini? Na ataondoka lini?
    Mnaze huyu mlowezi
    Hatuchoki
    Hatuchoki
    Lazima yeye anazwe

    Vifaranga na mbuzi
    Mbavu zao zahesabika
    Meee! Sauti zilihinikiza kote
    Haya yote hakika, ni madhila ya Muitalia
    Nguvu kweli tunayo
    Simama mbele tunayo
    Simama mbele uone !
    Muitalia ondoka !
    Au nikuondoe kwa nguvu

    (a) Taja madhila yaliyosababishwa na Muitalia katika makala haya.
    (b) Thibitisha kuwa utungo huu ni wimbo.
    (c) Eleza maana inayojitokeza katika mistari ifuatayo:-
    (i) Mbavu zao zahesabika.
    (ii) Haya yote hakika, ni madhila ya Muitalia.
    (d) Huu ni wimbo wa aina gani? Eleza ukitoa ushahidi
    (e) Eleza kwa sentensi mbili au tatu shughuli muhimu za kiuchumi za watu wanaimba wimbo huu
    (f) Taja mbinu za lugha zilizotumiwa katika wimbo huu. Toa ushahidi
    (g) Taja mafunzo mawili yanayotokana na wimbo huu

    Date posted: October 11, 2019 .    Answers (1)

  • Jadili kwa kina matatizo ambayo huenda yakakabili fasihi simulizi katika jamii ya kesho kisha utoe mapendekezo ya jinsi ya kukabiliana na hali hii (Solved)

    Jadili kwa kina matatizo ambayo huenda yakakabili fasihi simulizi katika jamii ya kesho kisha utoe mapendekezo ya jinsi ya kukabiliana na hali hii

    Date posted: October 11, 2019 .    Answers (1)

  • Bainisha tamathali za usemi zilizotumika katika methali zifuatazo:- (i) Ujana ni moshi ukienda haurudi (ii) Usipoziba ufaa utajenga ukuta (Solved)

    Bainisha tamathali za usemi zilizotumika katika methali zifuatazo:-
    (i) Ujana ni moshi ukienda haurudi
    (ii) Usipoziba ufaa utajenga ukuta

    Date posted: October 11, 2019 .    Answers (1)

  • Wawe na kimai ni nini katika fasihi simulizi? Eleza faida zake (Solved)

    Wawe na kimai ni nini katika fasihi simulizi? Eleza faida zake

    Date posted: October 9, 2019 .    Answers (1)

  • Hapo zamani za kale, Mungu alituma wajumbe wawili waende duniani. Wajumbe hawa ni Kinyonga na Mjusi. Kwanza... (Solved)

    Hapo zamani za kale, Mungu alituma wajumbe wawili waende duniani. Wajumbe hawa ni Kinyonga na Mjusi. Kwanza alimtuma Kinyonga na kumwagiza akaseme “wanadamu hamtakufa.” Kinyonga alienda kwa mwendo wa kuduwaa, akasimama hapa na pale akila matunda ya miti. Kwa sababu ya hali hii alichelewa sana kufikisha ujumbe kwa binadamu.
    Baada ya muda kupita, Mungu alimtuma Mjusi na ujumbe akaseme, “Mwanadamu sharti kufa.” Mjusi aliunyanyua mkia akafyatuka pu! Mbio akawahi duniani kabla ya kinyonga kuwasili. Kwa haraka alitangaza agizo kuu, “Wanadamu sharti kufa!” Akarejelea haraka kwa Mungu. Baada ya muda kinyonga naye akafika duniana na kutangaza, “Wanadamu hamtakufa!” Wanadamu wakapinga mara na kusema, “La! Tumeshapata ujumbe wa Mjusi, wanadamu sharti kufa! Hatuwezi kupokea tena neno lako! Basi kulingana na neno la mjusi, wanadamu hufa.

    (a) (i) Hadithi hii huitwaje?
    (ii) Toa sababu zako
    (b) Eleza sifa tatu zinazohusishwa na ngano za fasihi simulizi katika hadithi hii
    (c) Kinyonga ni mhusika wa aina gani?
    (d) Hadithi hii ina umuhimu gani?
    (e) Taja njia zozote nne za kukusanya kazi za fasihi simulizi
    (f) Tambulisha vipera hivi:-
    (i) Kula hepi
    (ii) Sema yako ni ya kuazima
    (iii) Baba wa Taifa

    Date posted: October 9, 2019 .    Answers (1)

  • Lala mtoto lala x2 Mama atakuja lala Alienda sokoni lala Aje na ndizi lala Ndizi ya mtoto lala Na maziwa ya mtoto lala Andazi lako akirudi Pia nyama ya kifupa Kifupa, kwangu, wewe... (Solved)

    Lala mtoto lala x2
    Mama atakuja lala
    Alienda sokoni lala
    Aje na ndizi lala
    Ndizi ya mtoto lala
    Na maziwa ya mtoto lala
    Andazi lako akirudi
    Pia nyama ya kifupa
    Kifupa, kwangu, wewe kinofu
    Kipenzi mwana lala x2

    Titi laja x2

    Basi kipenzi lala
    Baba atakuja lala
    Aje na mkate lala
    Mkate wa mtoto lala
    Tanona ja ndovu lala


    (a) Huku ukithibitisha jibu lako eleza huu ni wimbo wa aina gani?
    (b) Eleza sifa za wimbo wa aina hii
    (c) Onyesha umuhimu wa wimbo huu
    (d) Eleza amali kuhusu jamii zinazojitokeza katika wimbo huu
    (e) Tambua mbinu zozote mbili za utunzi zilizotumika katika wimbo huu
    (f) Taja vitendo viwili vinavyoambatana na uimbaji wa aina hii ya wimbo
    (g) Wimbo huu una wahusika wangapi? Wataje

    Date posted: October 9, 2019 .    Answers (1)

  • 1. Ni sumu, sumu hatari Unahatarisha watoto Kwa ndoto zako zako leweshi Za kupanda ngazi Ndoto motomoto ambazo Zimejenga ukuta Baina ya watoto Na maneno laini Ya ulimi wa wazazi 2. Ni sumu, sumu... (Solved)

    1. Ni sumu, sumu hatari
    Unahatarisha watoto
    Kwa ndoto zako zako leweshi
    Za kupanda ngazi
    Ndoto motomoto ambazo
    Zimejenga ukuta
    Baina ya watoto
    Na maneno laini
    Ya ulimi wa wazazi

    2. Ni sumu, sumu hasiri
    Unahasiri watoto
    Kwa pupa yako hangaishi
    Ya kuwa tajiri mtajika
    Pupa pumbazi ambayo
    Imezaa jangwa bahili
    Badala ya chemichemi
    Ya mazungumzo na maadili
    Baina ya watoto na mzazi

    3. Ni sumu, sumu legezi
    Unalegeza watoto
    Kwa mazoea yako tenganishi
    Ya daima kunywa ‘moja baridi’
    Mazoea mabaya ambayo yanafunga katika klabu
    Hadi saa nane usiku
    Huku yakijenga kutofahamiana
    Baina ya watoto na mzazi

    4. Ni sumu, sumu jeruhi
    Unajeruhi watoto kwa pesa,
    Kwa mapenzi yako hatari
    Ya kuwaliwaza watoto kwa pesa
    Zinawafikisha kwenye sigara na ulevi
    Na kisha kwenye madawa ya giza baridi
    Barabara inayofikisha kwenye giza baridi la kaburi la asubuhi


    (a) Pendekeza kichwa kwa shairi hili
    (b) Fafanua maudhui ya shairi hili
    (c) Ni kwa njia gani kinachozungumziwa kinajenga ukuta?
    (d) Dondoa tamathali mbili za usemi zilizotumika katika shairi na uzitolee mfano
    (e) Eleza umbo la shairi hili
    (f) Uandike ubeti wa nne kwa lugha nathari
    (g) Eleza maana ya vifungu hivi vilivyotumika katika shairi ;
    (i) Giza baridi
    (ii) Yanakufunga katika klabu

    Date posted: October 9, 2019 .    Answers (1)

  • CHEMA HAKIDUMU Chema hakidumu, kingapendekeza, Saa ikitimu, kitakuteleza, Ukawa na hamu, kukingojeleza, Huwa ni vigumu, (Solved)

    CHEMA HAKIDUMU
    Chema hakidumu, kingapendekeza,
    Saa ikitimu, kitakuteleza,
    Ukawa na hamu, kukingojeleza,
    Huwa ni vigumu, kamwe hutaweza.

    Chema sikiimbi, kwamba nakitweza,
    Japo mara tumbi, kinshaniliza,
    Na japo siombi, kipate n’ongeza,
    Mtu haniambi, pa kujilimbikiza.

    Chema mara ngapi, kinaniondoka,
    Mwahanga yu wapi? Hakukaa mwaka,
    Kwa muda mfupi, aliwatilika,
    Ningefanya lipi, ela kumzika?

    Chema wangu babu, kibwana Bashee,
    Alojipa tabu, kwamba anilee, Na yakwe sababu, ni nitengenee,
    Ilahi wahhabu, mara amtwee.

    Chema wangu poni, kipenzi nyanyangu,
    Hadi siku hini, Yu moyoni mwangu,
    Yu moyoni ndani, hadi kufa kwangu,
    Ningamtamani, hatarudi kwangu.

    (a) Eleza dhamira ya mwandishi
    (b) Fafanua umbo la shairi hili
    (c) Andika ubeti wa kwanza kwa lugha ya nathari
    (d) Taja na kutoa mfano mmoja wa tamathali yoyote ya lugha inayojitokeza katika shairi
    (e) Taja mbinu nne za uhuru wa mshairi huku ukitolea kila mbinu mfano

    (f) Eleza maana ya maneno yafuatayo kulingana na vile yalivyotumika:-
    (i) Nitengenee
    (ii) Ningamtamani
    (iii) Ikitimu

    Date posted: October 9, 2019 .    Answers (1)

  • Msituni nikakuta, nyuki wamo mzingani, Kwa juhudi wanakita, mara nje mara ndani, Husuda wameikata, hata hawasengenyani, Nyuki ni wadudu duni, wanashinda kwa umoja Mchwa nao nikaona, wamejenga masikani, Wafanya bidii... (Solved)

    Msituni nikakuta, nyuki wamo mzingani,
    Kwa juhudi wanakita, mara nje mara ndani,
    Husuda wameikata, hata hawasengenyani,
    Nyuki ni wadudu duni, wanashinda kwa umoja

    Mchwa nao nikaona, wamejenga masikani,
    Wafanya bidii sana, uvivu hawatamani,
    Wao husaidiana, tena hawadanganyani,
    Mchwa wadudu wa chini, wanaishi kwa umoja

    Nalo jeshi la siafu, hutandawaa njiani,
    Laenda bila ya hofu, maana ajiamini,
    Silaha zao dhaifu, meno, tena hawaoni
    Wa kuwatadia nini ? Kwani wanao umoja.

    Nao chungu wachukuzi, nyama warima njiani,
    Masikini wapagazi, mizigo yao kichwani,
    Ingawa si wachokozi, wakali ukiwahini,
    Katu hawafarakani, wanadamu kwa umoja.

    Sisi ni wana Adamu, mbona hatusikizani,
    Tusitietie hamu, ukubwa kuutamani,
    Wachache wataalamu, tuwasadi kwa imani,
    Hii “Huyu awezani,” yatuvunjia umoja


    (a) Lipe shairi hili anwani mwafaka.
    (b) Ni sifa zipi nne zinazopewa wanaozungumza.
    (c) Onyesha jinsi mwandishi alivyotumia uhuru wake katika shairi hili.
    (d) Eleza muundo wa shairi hili.
    (e) Andika ubeti wa mwisho kwa lugha nathari.
    (f) Taja mafunzo mawili unayopata kutokana na wahusika wanaozungumziwa.
    (g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi hilo.
    (i) Chungu
    (ii) Tuwasadi

    Date posted: October 9, 2019 .    Answers (1)

  • Alipokwenda kwao, mamaye alimwambia, Nipa fedha au nguo, nataka kwenda tumia! Nikosapo hivi leo, nipa kisu tajitia ! Huzunguka akilia kwa maana ya uketo Ndipo mamaye kawaza, pamwe na... (Solved)

    Alipokwenda kwao, mamaye alimwambia,
    Nipa fedha au nguo, nataka kwenda tumia!
    Nikosapo hivi leo, nipa kisu tajitia !
    Huzunguka akilia kwa maana ya uketo

    Ndipo mamaye kawaza, pamwe na kuzingatia,
    Fedha zako umesoza, na leo zimekwisha,
    Kisu sikukukataza, twaa upate jitia!
    Mbele zangu n’ondokea! Wende na ukiwa wako!


    Ulipogeuka nondo, nguo ukazingilia,
    Kakaka kwa vishindo, usisaze hata moya,
    Leo wanuka uvundo, wambeja wakukimbia!
    Mbele zangu n’ondokea ! Wende na ukiwa wako!
    Ukijigeuza nyama, kama Simba ukilia,
    Watumwa ukawaegema, ukawla wote pia,
    Pasi kuona huruma, kutoa wahurumia,
    Mbona hukuzingatia? Wende na ukiwa wako!


    Si mimi naliokupa, ukata huo, sikia!
    Kwamba utakuja hapa, nipate kuondolea,
    Naapa thama, naapa, sina la kukutendea!
    Mbele zangu n’ondokea! Wende na ukiwa wako!

    Tamati, nalikomile, ni hayo nalokwambia,
    Hapahitaji kelele na kujirisha mabaya,
    Na kwamba yakutukie, sema yapate n’elea!
    Zidi radhi kuniwea ! Wende na ukiwa wako!


    (a) Lipe shairi hili anwani mwafaka
    (b) Ni maudhui gani yanayojitokeza katika shairi hili
    (c) Taja na ueleze tabia za mnenewa katika shairi hili
    (d) Mshairi ametumia uhuru wa utunzi. Taja sehemu mbili alikotumia uhuru huo
    (e) Eleza umbo la shairi hili
    (f) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi :-
    (i) Uketo
    (ii) Ukata

    Date posted: October 9, 2019 .    Answers (1)

  • 1. Namwona yu shambani, Na jembe mkononi, Analima, Mwanamama, (Solved)

    MWANAMKE
    1. Namwona yu shambani,
    Na jembe mkononi,
    Analima,
    Mwanamama,
    Mavuno si yake,
    Ni ya mume wake.

    2. Namwona viwandani,
    Pia maofisini,
    Yu kazini,
    Hamkani,
    Anabaguliwa,
    Na anaonewa.

    3. Namwona yu nyumbnai,
    Mpishi wa jikoni,
    Yaya yeye,
    Dobi yeye,
    Hakuna malipo,
    Likizo haipo.

    4. Namwona kitandani,
    Yu uchi maungoni.
    Ni mrembo
    Kama chombo,
    Chenye ushawishi,
    Mzima utashi.

    5. Namwona mkekani,
    Yuwamo uzazini,
    Apumua,
    Augua,
    Kilio cha kite,
    Cha mpiga pute.

    6. Kwa nini mwanamke,
    Ni yeye peke yake,
    Heshimaye,
    Haki anakosa,
    Kwa kweli ni kosa
    (Muhammed Seif Khatib)


    (a) “Shairi hili ni la kukatisha tamaa”. Fafanua dai hili kwa kutoa mifano minne
    (b) Eleza umbo la shairi hili
    (c) Andika ubeti wa tatu katika lugha ya nathari
    (d) Taja tamathali ya usemi iliyotawala katika shairi zima utoe mifano miwili ya jinsi
    ilivyotumika
    (e) Onyesha mifano miwili ya ubabedume inayojitokeza katika shairi hili
    (f) Eleza maana ya maneno yafuatayo jinsi yalivyotumiwa katika shairi:
    (i) mzima utashi
    (ii) maungoni

    Date posted: October 9, 2019 .    Answers (1)

  • KIPI NIKITENDE? Tayari ni sarakani, niambie yote johara,Mosi nimpe shukrani, kanizaa bira zira,Wapo haiko hisani, ningefaa kwa uparara,Kipi takachokitenda, ni nene heko kwa mama?Miezi tisa... (Solved)

    KIPI NIKITENDE?
    Tayari ni sarakani, niambie yote johara,
    Mosi nimpe shukrani, kanizaa bira zira,
    Wapo haiko hisani, ningefaa kwa uparara,
    Kipi takachokitenda, ni nene heko kwa mama?


    Miezi tisa tumboni, yote nina kajinyima,
    Kanikopa uchunguni, safari ndefu kazima’
    Kama kinda kiotani, kiniasa huyu mama’
    Kipi takachokitenda, ninene heko mama ?

    Baba siku jana madadi, kawa vingaito mambo,
    Kaolewa na asadi, kachalazwa kwa wimbombo,
    Kaona – bali jadili, kuchao puani bombo,
    Kipi takachokitenda, ninene heko mama?


    Kila kuchao zarani, kupalilia kondeni,
    Kachanika mpinini, chungu povuka motoni,
    Kaviyariya fingani, kinijali jikoni,
    Kipi tukachokitenda , ninene heko mama?


    Wa siku hizi vijana, wakahujuru nyumbani,
    Wengine wao jagina, kawa lofa mutaani,
    Hali ukashiba nina, afikapo tu, “kongoni!”
    Kipi takachokitenda, ninene heko mama?


    Nawe bwana siwe maya, vita hasha kiwa kombo,
    Tena simfanye yaya, ya kikoa ndio mambo,
    Simtende ya hizaya, siwe mwao kila jambo,
    Kipi takachokitenda, ninene heko mama?


    Sasa jamvi nakuja, kisa nimesakarika,
    Naomba niliyotaja, tatia manani kaka,
    Nenayo yasiwe ngoja, ili nipokee baraka,
    Mema nitamtendea, apate futahi pia.



    (a) Eleza umbo la shairi hili
    (b) Kwa nini msanii amshukuru mamaye ?
    (c) Ni kina nani wanaokashifiwa na msanii ? Kwa nini ?
    (d) Onyesha tofauti katika ujumbe iliyoko katika beti nne za kwanza na mbili zinazofuata
    (e) Toa majina mengine yenye maana sawa na haya yaliyotumiwa katika shairi hili :
    (i) Mama
    (ii) Dawati
    (iii) Imara/thabiti
    (f) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika kaika shairi:
    (i) Kawa vangaito mambo
    (ii) Wimbombo
    (iii) Kongoni

    Date posted: October 9, 2019 .    Answers (1)

  • 1. Nitampa nani, sauti yangu ya dhati Kwa kipimo gani, ingawa kiwakatiti Amefanya nini, la kutetea umati Kipimo ni kipi? 2. Yupi wa maani, asosita katikati Alo na maoni, yasojua... (Solved)

    1. Nitampa nani, sauti yangu ya dhati
    Kwa kipimo gani, ingawa kiwakatiti
    Amefanya nini, la kutetea umati
    Kipimo ni kipi?

    2. Yupi wa maani, asosita katikati
    Alo na maoni, yasojua gatigati
    Atazame chini, kwa kile ule wakati
    Kipimo ni kipi?

    3. Alo mzalendo, atambuaye shuruti
    Asiye mafundo, asojua mangiriti
    Anoshika pendo, hata katika mauti
    Kipimo ni kipi?

    4. Kipimo ni kipi, changu mimi kudhibiti
    Utu uko wapi, ni wapi unapoketi
    Nje kwa mkwapi, au ndani kwa buheti
    Kipimo ni kipi?

    a) Eleza umbo la shairi hili
    b) Taja na ueleze jinsi mwandishi alivyotumia uhuru wa ushairi
    c) Eleza ujumbe unaowasilishwa na mshairi
    d) Andika ubeti wa tatu katika lugha ya nathari
    e) Taja bahari tatu zinazojitokeza katika shairi na utoe sababu
    f) Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika shairi hili
    i) Katiti
    ii) Gatigati
    iii) Mangiriti

    Date posted: October 9, 2019 .    Answers (1)

  • WAFULA KABILIANA NA KISU Ee mpwa wangu, Kwetu hakuna muoga, Uoga ukikufikia, huenda ni wa akina mamayo, Fahali tulichinja ili uwe mwanamme, Eewe mpwa wangu, kisu kikali ajabu ! Iwapo utatingiza... (Solved)

    WAFULA KABILIANA NA KISU
    Ee mpwa wangu,
    Kwetu hakuna muoga,
    Uoga ukikufikia, huenda ni wa akina mamayo,
    Fahali tulichinja ili uwe mwanamme,
    Eewe mpwa wangu, kisu kikali ajabu !
    Iwapo utatingiza kichwa,
    Uhamie kwa wasiotahiri.

    Wanaume wa mbari yetu,
    Si waoga wa kisu,
    Wao hukatwa kuanzia macheo hadi machweo,
    Wewe ndiye wa kwanza,
    Iwapo utashindwa,
    Wasichana wote,
    Watakucheka,
    Ubaki msununu,
    Simama jiwe liwe juu,
    Ndege zote ziangamie.

    Simu nimeipokea,
    Ngariba alilala jikoni,

    Visu ametia makali,
    Wewe ndiye wangojewa,
    Hadharani utasimama,
    Macho yote yawe kwako,
    Iwapo haustahimili kisu,
    Jiuzulu sasa mpwa wangu,
    Hakika sasa mpwa wangu,
    Hakika tutakusamehe, mwaka kesho unakuja.


    Asubuhi ndio hii,
    Mama mtoto aamushwe,
    Upweke ni uvundo,
    Iwapo utatikisa kichwa,
    Iwapo wewe ni mme,
    Kabiliana na kisu kikali,
    Hakika ni kikali!

    Kweli ni kikali!
    Wengi wasema ni kikali!
    Fika huko uone ukali!
    Mbuzi utapata,
    Na hata shamba la mahindi,
    Simama imara,
    Usiende kwa wasiotahiri


    (a) Hili ni shairi la aina gani ? Thibitisha
    (b) Ni nani anayeimba shairi hili na analiimba kwa nani ?
    (c) Toa ithibati kwenye shairi hili kuthibitisha kuwa msimulizi ana taasubi za kiume
    (d) Taja kwa kutolea mifano mbinu zozote nne za uandishi katika shairi hili
    (e) Taja shughuli zozote mbili za kiuchumi za jamii inayorejelewa katika shairi hili
    (f) Eleza kwa mifano, uhuru wa kishairi katika shairi hili
    (g) Msamiati ufuatao umetumika kwa maana gani katika shairi hili ?
    (i) Mbari
    (ii) Msununu
    (iii) Ngariba
    (iv) Uvundo

    Date posted: October 9, 2019 .    Answers (1)

  • Sinisumbuwe akili, nakusihi e mwandani.Afya yangu dhahili, mno nataka amaniNawe umenikabili, nenende sipitaliniSisi tokea azali, twende zetu mizumuniNifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?Mababu hawakujali, wajihisipo... (Solved)

    Sinisumbuwe akili, nakusihi e mwandani.
    Afya yangu dhahili, mno nataka amani
    Nawe umenikabili, nenende sipitalini
    Sisi tokea azali, twende zetu mizumuni
    Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?

    Mababu hawakujali, wajihisipo tabani
    Tuna dawa za asili, hupati sipitalini
    Kwa nguvu za kirijali, Mkuyati uamini
    Kaafuri pia kali, dawa ya ndwele fulani
    Nifuateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?

    Mtu akiwa hali, tumbo lina walakini,
    Dawa yake ni subili, au zongo huanoni
    Zabadili pia sahali, kwa maradhi yalo ndani
    Au kwenda wasaili, wenyewe walo pangani
    Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?

    Mtu kwenda sipitali, ni kutojuwa yakini
    Daktari k’ona mwili, tanena kensa tumboni
    Visu visitiwe makali, tayari kwa pirisheni
    Ukatwe kama fagili, tumbo nyangwe na maini
    Nifuateni sipitalini, na dawa ziko nyumbani?

    Japo maradhi dhalili, kutenguliwa tegoni
    Yakifika sipitali, huwa hayana kifani
    Wambiwa damu kaliti, ndugu msaidieni
    Watu wakitaamali, kumbe ndiyo bunani
    Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?

    Mizimu wakupa kweli, Wakueleze undani.
    Maradhiyo ni ajali, yataka vitu thamani
    Utete huku wawili, wa manjano na kijani
    Matunda pia asali, vitu vyae shamoni
    Nifuateni sipati, na dawa zi langoni?


    (a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka
    (b) Mtunzi alikuwa na lengo gani alipotunga shairi hili
    (c) Mbona mshairi hataki kwenda hospitalini
    (d) Eleza umbo la shairi hili
    (e) Kwa nini mshairi alitumia ritifaa katika ushairi ?
    (f) Andika maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa kwenye shairi :-
    (i) Dhalili –
    (ii) Azali-
    (iii)Sahali-

    Date posted: October 9, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza juhudi tano zinazotumika kukiendeleza Kiswahili (Solved)

    Eleza juhudi tano zinazotumika kukiendeleza Kiswahili

    Date posted: October 8, 2019 .    Answers (1)

  • A : Ohh, dada NaomiB : Dada Ruth (anamsogea kwa bashasha wanakumbatiana). Ahh Mungu asifiwe!A: Asifiwe sanaB: Ehh dadangu, miezi ...mingi...sijakuonaA: dada wee...Nilitumwa huko kusini... (Solved)

    Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali :

    A : Ohh, dada Naomi
    B : Dada Ruth (anamsogea kwa bashasha wanakumbatiana). Ahh Mungu asifiwe!
    A: Asifiwe sana
    B: Ehh dadangu, miezi ...mingi...sijakuona
    A: dada wee...Nilitumwa huko kusini ...Kuwahubiria watu injili (mtuo mdogo)singeweza kukata...
    B: Ehh, usiwe kama Yona
    A: Habari ya siku nyingi?
    B; Nzuri Mungu bado ameendelea kunibariki
    A: Amen!
    B: Nimeendelea kuiona neema yake
    A: Amen! Asifiwe Bwana
    B: Halleluya
    A: Ni Mungu wa miujiza!
    B : Amen. Hata nami nimeona neema yake
    Bado niko imara katika wokovu katika siku hizi za mwisho
    A : Amen !
    B : Ni Mungu wa ajabu kweli !
    A : Nilikumbana na matatizo lakini nikategemea sala
    Kama Paulo na sila… Na nikashinda (anatua). Sikuweza kumpa shetani nafasi…maana
    ameshindwa
    B : Ameshindwa kabisa


    (i) Hii ni sajili ya wapi ? Fafanua
    (ii) Taja na ueleze sifa za sajili hii
    (iii) Taja na ueleze mambo mawili muhimu yaliyosaidia katika maenezi ya Kiswahili
    Afrika mashariki na kati

    Date posted: October 8, 2019 .    Answers (1)