Soma makala haya kisha ujibu maswali yafuatayo HAKI ZA BINADAMU Binadamu wana mazoea ya kufikiria kuwa jinsi wafanyavyo, waongeavyo na wafikiriavyo kuhusu vitu ndivyo inavyopasa...

      

Soma makala haya kisha ujibu maswali yafuatayo
HAKI ZA BINADAMU
Binadamu wana mazoea ya kufikiria kuwa jinsi wafanyavyo, waongeavyo na wafikiriavyo kuhusu vitu ndivyo inavyopasa kuwa. Kama binandamu tunaamini njia yetu ndiyo sahihi, yenye mantiki na inayopasa kufuatwa na kila mtu. Msingi huu huu unakwenda kinyume na kutambua kila binadamu ana haki ya kufikiri, kusema au kuongea na kutenda mradi asikiuke haki ya mwenzake iliyo sawa na yake. Nguzo mojawapo inayogongomelea hoja hii ni Haki za Binadamu.

Azimio kutangaza Haki Bia za Binadamu liliafikiwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 10 Desemba 1948. Baraza kuu hilo liliyasisitizia mataifa wanachama umuhimu wa kuyasambaza, kuenezea, na kusisitiza kusambazwa kwa azimio hilo katika shule na taasisi za kielimu. Msingi wa uhuru, haki na amani ulimwenguni ni kutambua binadamu wote wana haki sawa. Ingawa kimsingi jamii na mataifa yote ya ulimwengu yanapaswa kuthamini, kusambaza na kuhimiza umuhimu wa Haki za Binadamu zipo jamii ambazo hukiuka haki hizo. Matokeo ya ukiukaji huu yana athari hasi sana kama ilivyotokea nchini Rwanda na Bosnia. Herzegovina kulikotokea mauaji ya halaiki.

Azimio la Haki za Binadamu linajumuisha vipengele kadha ambavyo ni mihimili mikuu ya Azimio lenyewe. Kipengele msingi kabisa kinasisitiza kuwa kila kiumbe anazaliwa huru na ana haki na hadhi sawa na kiumbe mwingine. Ukweli wa kauli hii ulikokotezwa na kauli ya mwanafalsafa maarufu Jean Jacques Rosseau aliyesema kuwa kila kiumbe huzaliwa huru lakini huwa katika pingu ulimwengu mzima. Kauli hii ilitambua ukiukaji huu wa kipengele hiki. Kipengele cha pili kinasisitiza kuwa binadamu wote wana haki za kufurahia uhuru wao pasi na kutengwa au kubezwa kwa misingi yoyote ile si rangi, kabila, jinsia, lugha, dini, asilia, utajiri au chochote kile.

Vipengele vingine vinatukumbusha kuwa kila mtu ana haki ya kuishi na kupata ulinzi. Hamna mtu anayepaswa kuishi maisha ya utumwa au unyonge wa kutumikishwa kwa namna yoyote ile. Suala hili linasisitizwa na kipengele cha sita kinachokataza kudhalilishwa kwa watu au kutunzwa kwa namna yoyote ambayo inamfedhehesha kama kiumbe. Azimio la Haki za Binadamu linasisitiza kuwa binadamu yoyote nyule ana haki ya kupata ulinzi wa kisheria. Binadamu huyo hapaswi kubaguliwa na ana haki ya kupata fidia ya kisheria taraa haki zake za kimsingi zikikiukwa.

Hata hivyo sio watu wote ulimwenguni ambao wanazifurahia haki hizi za kimsingi. Zipo lukuki za jamii ulimwenguni ambako haki za kimsingi zinakiukwa. Katika nchi ambazo zinaongozwa na watawala wa kiimla, si ajabu kuona haki za binadamu zikikiukwa. Viongozi wa aina hiyo huwa wamegeuzwa ng’ombe wa shemere na tamaa, ubinafsi na ukatili usiojua thamani ya utu. Viongozi wa aina hii wanasahau kuwa kila binadamu ana haki ya kuishi maisha huru, asipotumikishwa wala kulanguliwa kama bidhaa.

Nchi za kiimla aghalabu huongozwa na itikadi kuwa kiongozi ndiye pekee ambaye ana uwezo wa kufikiri, kuamua na kutenda. Watu wengine wanapaswa kumfuata kisilka kama yule mbwa wa Pavlov ambaye alitokwa na mate kila kengele ilipopigwa. Viongozi wa ama hii hawachelei kuwatenza nguvu raia zao: Kuwadhalilisha kwa namna nyingi. Viongozi wa aina hiyo huiona sheria ya nchi kama iliyowekwa kwa watu wengine bali sio wao. Msimamo huu unakwenda kinyume na kipengele cha saba cha Haki Bia za Binadamu kisemacho kuwa watu wote ni sawa mbele ya sheria.

Baadhi ya haki zinazokiukwa katika jamii za kimabavu ni haki ya watu kuungana, kuwaza, kushiriki katika maamuzi ya serikali, kuwa mwanachama wa jumuia waitakayo, kumiliki mali, kutembea, kuishi anakotaka kutohukumiwa bila ya kuwako na utaratibu wa kisheria. Ni muhimu hata hivyo kujua ni muhimu kwa raia wenyewe kujielimisha na kuzijua haki zao. Serikali inapaswa kuwa mlinzi wa sheria zenyewe. Lakini muhimu kujua pia kuwa mlinzi naye hulindwa pia.

Maswali
a)Kwa maneno kati ya 90 – 100 fafanua Haki Bia za Binadamu zilizoafikiwa na Baraza kuu la umoja wa Mataifa.
Nakala Chafu
Nakala Safi
b) Kwa nini viongozi wa kiimla hukiuka haki za binadamu. (Maneno 50 – 60).
Nakala Chafu

  

Answers


Kavungya
a)Kwa maneno kati ya 90- 100 fafanua Haki Bia za Binadamu Zilizoafikiwa na Baraza kuu la Umoja wa mataifa
Kila kiumbe anazaliwa humu na ana haki na hadhi sawa na kiumbe mwingine’
•Binadamu wote wana haki za kufurahia uhuru wao pasi na kutengwa au kubezwa kwa misingi yoyote ile si rangi, kabila, jinsia, lugha, dini, asilia au chochote kile.
•Kila mtu ana haki ya kuishi na kupata ulinzi
•Hamna mtu anayepaswa kuishi maisha ya utumwa, kutumikishwa, kudhalilishwa au kutunzwa kwa namna inayomfedhehesha kama kiumbe.
•Haki ya kupata ulinzi wa kisheria
•Kutobaguliwa na ana haki ya kupata fidia ya kisheria taraa haki zake za kimsingi zikikiukwa .

b)Kwa nini viongozi wa kiimla hukiuka haki za binadamu
• Tamaa ya uongozi
• Ubinafsi
• Ukatili, hawajui thamani ya utu
• Kiburi cha kujiona kuwa wao ndio wanaofahamu mambo zaidi
• Husahau kuwa binadamu ana haki ya kuishi maisha huru bila kutumikishwa au kutanguliwa kama bidhaa
• Hudhani wao tu ndio wana uwezo wa kufikiri, kuamua na kutenda na wananchi wanapaswa kufuata tu
• Huona kuwa sheria ya nchi imewekewa wengine na wala sio wao hivyo huwatenza nguvu raia zao
Kavungya answered the question on October 11, 2019 at 07:04


Next: Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali Tokea muundo mpya wa serikali ya ugatuzi uanze kutekelezwa miaka miwili iliyopita, kumeendelea kushuhudiwa matatizo mengi hali iliyopelekea kushuhudiwa kwa...
Previous: Tofautisha sauti zifuatazo. /a/ /u/

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions


  • Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali Tokea muundo mpya wa serikali ya ugatuzi uanze kutekelezwa miaka miwili iliyopita, kumeendelea kushuhudiwa matatizo mengi hali iliyopelekea kushuhudiwa kwa...(Solved)

    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
    Tokea muundo mpya wa serikali ya ugatuzi uanze kutekelezwa miaka miwili iliyopita, kumeendelea kushuhudiwa matatizo mengi hali iliyopelekea kushuhudiwa kwa msururu wa migomo na maandamano ya raia. Fujo za karibuni kabisa ni zile zinazoshuhudiwa katika miji mikubwa za wachuuzi na wafanyibiashara wakipinga hatua za serikali za kaunti kuwatoza ushuru takribani kwa kila huduma na bidhaa ikiwemo wanyama, kuku na ndege. La kuhuzunisha zaidi katika baadhi ya majimbo imeripotiwa kuwa raia wamelazimishwa kulipa ushuru kwa kutaka tu kuona maiti za jamaa zao kwenye vyumba vya kuhifadhi maiti.

    Wanasiasa wameonekana kuwa na wakati mgumu kutetea mfumo huu mpya wa ugatuzi huku baadhi wakisema kwamba matatizo yanayoshuhudiwa kwa sasa yametokana na ugeni wa mfumo huo. Wengine wameinyoshea kidole serikali ya kitaifa kwamba ndiyo inayosambaratisha muundo huu. Wengine wanahoji kuwa bado ni mapema na kwamba kunatajika muda mrefu ili kufaulu.

    Ni wazi kwamba kumekosekana nidhamu bora ya kusimamia maisha ya raia nchini Kenya. Matatizo yanayokumba raia kwa sasa ni dalili kuwa mfumo wa serikali ya ugatuzi umeongezea chumvi kwenye kidonda badala ya kutibu. Swali ni je, hadi lini nidhamu ya kusimamia raia itakuwa ni suala la majaribio na makosa?

    Hatua ya kuwarundikizia raia ushuru mkubwa ni kitendo cha unyonyaji na cha dhuluma kinachofaa kupingwa. La kufahamishiwa hapa ni kwamba ushuru ndio njia kubwa ya kuzalisha mapato ya serikali zinazojifunga na mfumo wa kimagharibi wa kiuchumi wa kibepari ikiwemo Kenya. Asilimia 90 ya mapato ya serikali za kibepari huegemea ushuru. Kwa hivyo hatua ya serikali za kaunti katika kuwanyonya raia kwa kuwalipisha ushuru si ajabu bali ni thibitisho kuwa jamii ya Kenya inaongozwa na nidhamu ya kiuchumi ya ubepari mfumo wa unyonyaji na ukandamizaji. Ukweli unabakia kuwa ndani ya serikali za kibepari raia ndio hubebeshwa mzigo wa ushuru unaoishia matumboni mwa viongozi!

    Miito ya mabadiliko ya katiba na ya miundo mipya ya kiutawala si lolote ila ni moja tu ya hatua za mfumo wa kibepari kujipa muda wa kuishi na kuziba aibu zake za kushindwa kusimamia maisha ya watu. Kufeli huku kwa mfumo huu kunashuhudiwa hadi kwenye nchi kubwa za kibepari kama Marekani na Uingereza hivyo nazo zimekumbwa tele na maandamano na fujo za raia wakilalamikia hali ngumu ya maisha.

    Maswali
    a)Yape makala haya anwani mwafaka.
    b)Eleza mtazamo wa wanasiasa kuhusu utepetevu wa mfumo huu.
    c)“Ugatuzi nchini Kenya ni mfumo wa kibepari” Thibitisha kauli hii kwa kurejelea makala.
    d)Migomo ni zao la matatizo yaliyogatuliwa kutoka kuu. Toa sababu nyingine zinazosababisha migomo katika serikali za ugatuzi
    e)Thibitisha jinsi mfumo wa ugatuzi umeongeza chumvi kwenye kidonda badala ya kutibu
    f)Eleza maana ya maneno yafuatayo
    i) Ugatuzi
    ii) Kibepari

    Date posted: October 11, 2019.  Answers (1)

  • (vigelegele vya harusi vililia alilili ; x3) Kuumeni : (waliimba) Tumeupata mpilipili na maua yake chikicha x2 Kukeni : (wimbo wao kwa sauti tofauti) Tausi waendaa x2 Tausi...(Solved)

    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yafuatayo :

    (vigelegele vya harusi vililia alilili ; x3)
    Kuumeni : (waliimba) Tumeupata mpilipili na maua yake chikicha x2

    Kukeni : (wimbo wao kwa sauti tofauti) Tausi waendaa x2
    Tausi waenda wamuacha mama kwenye banda.

    Kuumeni : (wakijibu wimbo) Mwacheni aendee x2
    Mwacheni aende akaone mambo ya nyumba.

    Kukeni : Mama ataota nini x2.
    Ataota nini, hana mtu wa kumletea kuni.

    Kuumeni : Ataota moto wa magunzi, wa magunzi wa magunzi. Twamchukua, kisura wetu,
    kisura wetu, kisura wetu.
    Tausi ni wetu sasa, ni kito chema, ni kito chema ni kito chema.

    (i) Wimbo huu ni wa aina gani, na unastahili katika hafla gani ?
    (ii) Bainisha wahusika Kuumeni na Kukeni
    (iii) Fafanua ujumbe uliojikita katika utungo huu
    (iv) Wimbo huu una umuhimu gani hafla ulioimbiwa?
    (v) Tambua mtindo uliotumika katika utungo huu

    Date posted: October 11, 2019.  Answers (1)

  • Onyesha tofauti kati ya vikundi hivi: (i) Hekaya Hurafa (ii) Visakale Visasili (iii) Ngano za mtanziko Ngano za mazimwi(Solved)

    Onyesha tofauti kati ya vikundi hivi:
    (i) Hekaya
    Hurafa

    (ii) Visakale
    Visasili

    (iii) Ngano za mtanziko
    Ngano za mazimwi

    Date posted: October 11, 2019.  Answers (1)

  • Elezea mbinu nne za kutongolea hadithi(Solved)

    Elezea mbinu nne za kutongolea hadithi

    Date posted: October 11, 2019.  Answers (1)

  • Ni nini maana ya Tendi?(Solved)

    Ni nini maana ya Tendi?

    Date posted: October 11, 2019.  Answers (1)

  • MUITALIA ANAZWE Saa kumi alfajiri Sote tuliamshwa Safari tuliianza Wengi wanauliza Mwitalia alikuja lini? Na...(Solved)

    Soma wimbo/shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata

    MUITALIA ANAZWE
    Saa kumi alfajiri
    Sote tuliamshwa
    Safari tuliianza
    Lazima tuimalize
    Maji ukiyavulia nguo
    Lazima uyaoge

    Wazee kwa vijana waliimba
    Muitalia lazima anazwe
    Mashamba yao walilia
    Uui! Jikaze wavulana
    Hawataki rangi hii

    Wengi wanauliza
    Mwitalia alikuja lini? Na ataondoka lini?
    Mnaze huyu mlowezi
    Hatuchoki
    Hatuchoki
    Lazima yeye anazwe

    Vifaranga na mbuzi
    Mbavu zao zahesabika
    Meee! Sauti zilihinikiza kote
    Haya yote hakika, ni madhila ya Muitalia
    Nguvu kweli tunayo
    Simama mbele tunayo
    Simama mbele uone !
    Muitalia ondoka !
    Au nikuondoe kwa nguvu

    (a) Taja madhila yaliyosababishwa na Muitalia katika makala haya.
    (b) Thibitisha kuwa utungo huu ni wimbo.
    (c) Eleza maana inayojitokeza katika mistari ifuatayo:-
    (i) Mbavu zao zahesabika.
    (ii) Haya yote hakika, ni madhila ya Muitalia.
    (d) Huu ni wimbo wa aina gani? Eleza ukitoa ushahidi
    (e) Eleza kwa sentensi mbili au tatu shughuli muhimu za kiuchumi za watu wanaimba wimbo huu
    (f) Taja mbinu za lugha zilizotumiwa katika wimbo huu. Toa ushahidi
    (g) Taja mafunzo mawili yanayotokana na wimbo huu

    Date posted: October 11, 2019.  Answers (1)

  • Jadili kwa kina matatizo ambayo huenda yakakabili fasihi simulizi katika jamii ya kesho kisha utoe mapendekezo ya jinsi ya kukabiliana na hali hii(Solved)

    Jadili kwa kina matatizo ambayo huenda yakakabili fasihi simulizi katika jamii ya kesho kisha utoe mapendekezo ya jinsi ya kukabiliana na hali hii

    Date posted: October 11, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha tamathali za usemi zilizotumika katika methali zifuatazo:- (i) Ujana ni moshi ukienda haurudi (ii) Usipoziba ufaa utajenga ukuta(Solved)

    Bainisha tamathali za usemi zilizotumika katika methali zifuatazo:-
    (i) Ujana ni moshi ukienda haurudi
    (ii) Usipoziba ufaa utajenga ukuta

    Date posted: October 11, 2019.  Answers (1)

  • Wawe na kimai ni nini katika fasihi simulizi? Eleza faida zake(Solved)

    Wawe na kimai ni nini katika fasihi simulizi? Eleza faida zake

    Date posted: October 9, 2019.  Answers (1)

  • Hapo zamani za kale, Mungu alituma wajumbe wawili waende duniani. Wajumbe hawa ni Kinyonga na Mjusi. Kwanza...(Solved)

    Hapo zamani za kale, Mungu alituma wajumbe wawili waende duniani. Wajumbe hawa ni Kinyonga na Mjusi. Kwanza alimtuma Kinyonga na kumwagiza akaseme “wanadamu hamtakufa.” Kinyonga alienda kwa mwendo wa kuduwaa, akasimama hapa na pale akila matunda ya miti. Kwa sababu ya hali hii alichelewa sana kufikisha ujumbe kwa binadamu.
    Baada ya muda kupita, Mungu alimtuma Mjusi na ujumbe akaseme, “Mwanadamu sharti kufa.” Mjusi aliunyanyua mkia akafyatuka pu! Mbio akawahi duniani kabla ya kinyonga kuwasili. Kwa haraka alitangaza agizo kuu, “Wanadamu sharti kufa!” Akarejelea haraka kwa Mungu. Baada ya muda kinyonga naye akafika duniana na kutangaza, “Wanadamu hamtakufa!” Wanadamu wakapinga mara na kusema, “La! Tumeshapata ujumbe wa Mjusi, wanadamu sharti kufa! Hatuwezi kupokea tena neno lako! Basi kulingana na neno la mjusi, wanadamu hufa.

    (a) (i) Hadithi hii huitwaje?
    (ii) Toa sababu zako
    (b) Eleza sifa tatu zinazohusishwa na ngano za fasihi simulizi katika hadithi hii
    (c) Kinyonga ni mhusika wa aina gani?
    (d) Hadithi hii ina umuhimu gani?
    (e) Taja njia zozote nne za kukusanya kazi za fasihi simulizi
    (f) Tambulisha vipera hivi:-
    (i) Kula hepi
    (ii) Sema yako ni ya kuazima
    (iii) Baba wa Taifa

    Date posted: October 9, 2019.  Answers (1)

  • Lala mtoto lala x2 Mama atakuja lala Alienda sokoni lala Aje na ndizi lala Ndizi ya mtoto lala Na maziwa ya mtoto lala Andazi lako akirudi Pia nyama ya kifupa Kifupa, kwangu, wewe...(Solved)

    Lala mtoto lala x2
    Mama atakuja lala
    Alienda sokoni lala
    Aje na ndizi lala
    Ndizi ya mtoto lala
    Na maziwa ya mtoto lala
    Andazi lako akirudi
    Pia nyama ya kifupa
    Kifupa, kwangu, wewe kinofu
    Kipenzi mwana lala x2

    Titi laja x2

    Basi kipenzi lala
    Baba atakuja lala
    Aje na mkate lala
    Mkate wa mtoto lala
    Tanona ja ndovu lala


    (a) Huku ukithibitisha jibu lako eleza huu ni wimbo wa aina gani?
    (b) Eleza sifa za wimbo wa aina hii
    (c) Onyesha umuhimu wa wimbo huu
    (d) Eleza amali kuhusu jamii zinazojitokeza katika wimbo huu
    (e) Tambua mbinu zozote mbili za utunzi zilizotumika katika wimbo huu
    (f) Taja vitendo viwili vinavyoambatana na uimbaji wa aina hii ya wimbo
    (g) Wimbo huu una wahusika wangapi? Wataje

    Date posted: October 9, 2019.  Answers (1)

  • 1. Ni sumu, sumu hatari Unahatarisha watoto Kwa ndoto zako zako leweshi Za kupanda ngazi Ndoto motomoto ambazo Zimejenga ukuta Baina ya watoto Na maneno laini Ya ulimi wa wazazi 2. Ni sumu, sumu...(Solved)

    1. Ni sumu, sumu hatari
    Unahatarisha watoto
    Kwa ndoto zako zako leweshi
    Za kupanda ngazi
    Ndoto motomoto ambazo
    Zimejenga ukuta
    Baina ya watoto
    Na maneno laini
    Ya ulimi wa wazazi

    2. Ni sumu, sumu hasiri
    Unahasiri watoto
    Kwa pupa yako hangaishi
    Ya kuwa tajiri mtajika
    Pupa pumbazi ambayo
    Imezaa jangwa bahili
    Badala ya chemichemi
    Ya mazungumzo na maadili
    Baina ya watoto na mzazi

    3. Ni sumu, sumu legezi
    Unalegeza watoto
    Kwa mazoea yako tenganishi
    Ya daima kunywa ‘moja baridi’
    Mazoea mabaya ambayo yanafunga katika klabu
    Hadi saa nane usiku
    Huku yakijenga kutofahamiana
    Baina ya watoto na mzazi

    4. Ni sumu, sumu jeruhi
    Unajeruhi watoto kwa pesa,
    Kwa mapenzi yako hatari
    Ya kuwaliwaza watoto kwa pesa
    Zinawafikisha kwenye sigara na ulevi
    Na kisha kwenye madawa ya giza baridi
    Barabara inayofikisha kwenye giza baridi la kaburi la asubuhi


    (a) Pendekeza kichwa kwa shairi hili
    (b) Fafanua maudhui ya shairi hili
    (c) Ni kwa njia gani kinachozungumziwa kinajenga ukuta?
    (d) Dondoa tamathali mbili za usemi zilizotumika katika shairi na uzitolee mfano
    (e) Eleza umbo la shairi hili
    (f) Uandike ubeti wa nne kwa lugha nathari
    (g) Eleza maana ya vifungu hivi vilivyotumika katika shairi ;
    (i) Giza baridi
    (ii) Yanakufunga katika klabu

    Date posted: October 9, 2019.  Answers (1)

  • CHEMA HAKIDUMU Chema hakidumu, kingapendekeza, Saa ikitimu, kitakuteleza, Ukawa na hamu, kukingojeleza, Huwa ni vigumu,(Solved)

    CHEMA HAKIDUMU
    Chema hakidumu, kingapendekeza,
    Saa ikitimu, kitakuteleza,
    Ukawa na hamu, kukingojeleza,
    Huwa ni vigumu, kamwe hutaweza.

    Chema sikiimbi, kwamba nakitweza,
    Japo mara tumbi, kinshaniliza,
    Na japo siombi, kipate n’ongeza,
    Mtu haniambi, pa kujilimbikiza.

    Chema mara ngapi, kinaniondoka,
    Mwahanga yu wapi? Hakukaa mwaka,
    Kwa muda mfupi, aliwatilika,
    Ningefanya lipi, ela kumzika?

    Chema wangu babu, kibwana Bashee,
    Alojipa tabu, kwamba anilee, Na yakwe sababu, ni nitengenee,
    Ilahi wahhabu, mara amtwee.

    Chema wangu poni, kipenzi nyanyangu,
    Hadi siku hini, Yu moyoni mwangu,
    Yu moyoni ndani, hadi kufa kwangu,
    Ningamtamani, hatarudi kwangu.

    (a) Eleza dhamira ya mwandishi
    (b) Fafanua umbo la shairi hili
    (c) Andika ubeti wa kwanza kwa lugha ya nathari
    (d) Taja na kutoa mfano mmoja wa tamathali yoyote ya lugha inayojitokeza katika shairi
    (e) Taja mbinu nne za uhuru wa mshairi huku ukitolea kila mbinu mfano

    (f) Eleza maana ya maneno yafuatayo kulingana na vile yalivyotumika:-
    (i) Nitengenee
    (ii) Ningamtamani
    (iii) Ikitimu

    Date posted: October 9, 2019.  Answers (1)

  • (1).Twamshukuru Mwenyezi. Kamwe wingi ukarimu Alo na kiti cha enzi, Mola wetu akramu Kutupa kitu azizi , lugha kutakalamu Lugha ni kitu kitamu, ujuwapo kutumia (2) Lugha mkuu mlezi...(Solved)

    (1).Twamshukuru Mwenyezi. Kamwe wingi ukarimu
    Alo na kiti cha enzi, Mola wetu akramu
    Kutupa kitu azizi , lugha kutakalamu
    Lugha ni kitu kitamu, ujuwapo kutumia

    (2) Lugha mkuu mlezi , aleaye binadamu
    Hata wanyama ja mbuzi, wema lugha wafahamu
    Hafuguwa simulizi, izaayo tabasamu
    Lugha huwa ni imamu, ujuwapo kutumia

    (3) Lugha hodari mkwezi, akweaye tata ngumu
    Huzifyeka pingamizi, zizushazo uhasama
    Ikazidisha mapenzi, wapendanao kudumu
    Lugha huyeyusha sumu, ujuwapo kutumia

    (4) Lugha ndiye mpagazi, mazito kuyahudumu
    Pia hupanga vizazi, pasi mbari kudhulumu
    Aidha hufanya kazi, ikawa mustakumu
    Lugha kwayo ni timamu, ujuwapo kutumia

    (5) Lugha ni mpelelezi, maovu kuwakasimu
    Huwatowa palo wazi, kashuhudia kaumu
    Yasifiwa na wajuzi, kuwa ni kitu adhimu
    Lugha mkuu hakimu, ujuwapo kutumia

    (6) Lugha huizuwa kazi, kutatiza mahakimu
    Huwaacha kanwa wazi, wakili kitakalamu
    Muhalifu na jambazi, wakaishinda hukumu
    Urongo huwa timamu, ujuwapo kutumia

    (7) Lugha iwe ni kiongozi, Kizungu au Kiamu
    Iwekapo waziwazi, silabi na tarakimu
    Huyakimu maongezi,yakasikizwa kwa hamu
    Lugha huwa ni muhimu, ujuwapo kutumia.

    (8) Lugha ni mapinduzi, wanyonge na wajukumu
    Kadhalika ni jahazi, ya nahodha muhitimu
    Kufa maji haiwezi, si vina si miizamu
    Lugha maji zam-zamu, ujuwapo kutumia

    (a) Eleza maudhui ya shairi hili
    (b) Eleza muundo wa shairi hili
    (c) Andika ubeti wa nne katika lugha ya nadhari/ nadharia
    (d) Taja huku ukitoa mifano, mbinu tatu za lugha alizotumia mshairi kuwasilisha ujumbe
    (e) Eleza maana ya msamiati kama ulivyotumika
    (i) Azizi
    (ii) Uhasimu
    (iii) Adimu.

    Date posted: October 9, 2019.  Answers (1)

  • Msituni nikakuta, nyuki wamo mzingani, Kwa juhudi wanakita, mara nje mara ndani, Husuda wameikata, hata hawasengenyani, Nyuki ni wadudu duni, wanashinda kwa umoja Mchwa nao nikaona, wamejenga masikani, Wafanya bidii...(Solved)

    Msituni nikakuta, nyuki wamo mzingani,
    Kwa juhudi wanakita, mara nje mara ndani,
    Husuda wameikata, hata hawasengenyani,
    Nyuki ni wadudu duni, wanashinda kwa umoja

    Mchwa nao nikaona, wamejenga masikani,
    Wafanya bidii sana, uvivu hawatamani,
    Wao husaidiana, tena hawadanganyani,
    Mchwa wadudu wa chini, wanaishi kwa umoja

    Nalo jeshi la siafu, hutandawaa njiani,
    Laenda bila ya hofu, maana ajiamini,
    Silaha zao dhaifu, meno, tena hawaoni
    Wa kuwatadia nini ? Kwani wanao umoja.

    Nao chungu wachukuzi, nyama warima njiani,
    Masikini wapagazi, mizigo yao kichwani,
    Ingawa si wachokozi, wakali ukiwahini,
    Katu hawafarakani, wanadamu kwa umoja.

    Sisi ni wana Adamu, mbona hatusikizani,
    Tusitietie hamu, ukubwa kuutamani,
    Wachache wataalamu, tuwasadi kwa imani,
    Hii “Huyu awezani,” yatuvunjia umoja


    (a) Lipe shairi hili anwani mwafaka.
    (b) Ni sifa zipi nne zinazopewa wanaozungumza.
    (c) Onyesha jinsi mwandishi alivyotumia uhuru wake katika shairi hili.
    (d) Eleza muundo wa shairi hili.
    (e) Andika ubeti wa mwisho kwa lugha nathari.
    (f) Taja mafunzo mawili unayopata kutokana na wahusika wanaozungumziwa.
    (g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi hilo.
    (i) Chungu
    (ii) Tuwasadi

    Date posted: October 9, 2019.  Answers (1)

  • Alipokwenda kwao, mamaye alimwambia, Nipa fedha au nguo, nataka kwenda tumia! Nikosapo hivi leo, nipa kisu tajitia ! Huzunguka akilia kwa maana ya uketo Ndipo mamaye kawaza, pamwe na...(Solved)

    Alipokwenda kwao, mamaye alimwambia,
    Nipa fedha au nguo, nataka kwenda tumia!
    Nikosapo hivi leo, nipa kisu tajitia !
    Huzunguka akilia kwa maana ya uketo

    Ndipo mamaye kawaza, pamwe na kuzingatia,
    Fedha zako umesoza, na leo zimekwisha,
    Kisu sikukukataza, twaa upate jitia!
    Mbele zangu n’ondokea! Wende na ukiwa wako!


    Ulipogeuka nondo, nguo ukazingilia,
    Kakaka kwa vishindo, usisaze hata moya,
    Leo wanuka uvundo, wambeja wakukimbia!
    Mbele zangu n’ondokea ! Wende na ukiwa wako!
    Ukijigeuza nyama, kama Simba ukilia,
    Watumwa ukawaegema, ukawla wote pia,
    Pasi kuona huruma, kutoa wahurumia,
    Mbona hukuzingatia? Wende na ukiwa wako!


    Si mimi naliokupa, ukata huo, sikia!
    Kwamba utakuja hapa, nipate kuondolea,
    Naapa thama, naapa, sina la kukutendea!
    Mbele zangu n’ondokea! Wende na ukiwa wako!

    Tamati, nalikomile, ni hayo nalokwambia,
    Hapahitaji kelele na kujirisha mabaya,
    Na kwamba yakutukie, sema yapate n’elea!
    Zidi radhi kuniwea ! Wende na ukiwa wako!


    (a) Lipe shairi hili anwani mwafaka
    (b) Ni maudhui gani yanayojitokeza katika shairi hili
    (c) Taja na ueleze tabia za mnenewa katika shairi hili
    (d) Mshairi ametumia uhuru wa utunzi. Taja sehemu mbili alikotumia uhuru huo
    (e) Eleza umbo la shairi hili
    (f) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi :-
    (i) Uketo
    (ii) Ukata

    Date posted: October 9, 2019.  Answers (1)

  • KIACHE KINACHONG’AA Katu siwe na harara, wala moyo kukupapa, Usichukue hasira, na moyo kutapa-tapa, Utaharibu na sura, mwishowe uende kapa, Kiache kinachokwepa, mbeleye kina madhara Mbeleye kina madhara, kile kinachokukukwepa, Mbele...(Solved)

    KIACHE KINACHONG’AA
    Katu siwe na harara, wala moyo kukupapa,
    Usichukue hasira, na moyo kutapa-tapa,
    Utaharibu na sura, mwishowe uende kapa,
    Kiache kinachokwepa, mbeleye kina madhara

    Mbeleye kina madhara, kile kinachokukukwepa,
    Mbele yake ni hasara, si chema kitakutupa,
    Hutaipata ijara, kuchuma ama kukopa,
    Kiache kinachokwepa, mbeleye kina madhara

    Hicho jangwa la Sahara, si mnofu ni mfupa,
    Hakina njema ishara, humtupa mwenye pupa,
    Kibovu kama tambara, hupasuka kama chupa,
    Kiache kinachokwepa, mbeleye kina madhara

    Kitaleta ufukura, si huko wala si hapa,
    Kina mengi mazingira, na mbele kitakuchapa,
    Sijitie usogora, ukavimbisha mishipa,
    Kiache kinachokwepa, mbeleye kina madhara


    Si kazi yenye ujira, mshahara kukulipa,
    Ya cheo chenye kinara, na heshima wakikupa,
    Mbele haina imara, japo leo wajitapa,
    Kiache kinachokwepa, mbeleye kina madhara

    Japo kazi ya biashara, kutwa wauza makopa,
    Uwe mtu na kipara, Mwananchi ama Yuripa,
    Bora uwe na busara, fedha tajaza mapipa,
    Kiache kinachokwepa, mbeleye kina madhara

    Usione kinang’ara, huku chapiga marapa,
    Ukimbilie kupora, moyo wako kukuzipa,
    Kitakugeuza chura, mbele yake utaapa,
    Kiache kinachokwepa, mbeleye kina madhara


    Usitupe sarara, nyuma kisogo kuipa,
    Ukaenda kwa papara, kiumbe mbele kitanepa,
    Kwanza tumia fikira, uchague njema chapa,
    Kiache kinachokwepa, mbeleye kina madhara

    Na sisemi masihara, hakika kweli nawapa
    Mlio pwani na bara, wa Mufindi na wa lupa
    Maneno haya kitara, muarifu na Wachepa,
    Kiache kinachokwepa, mbeleye kina madhara

    Tamati niliyochora, ya shikeni si kuepa
    Kisha muwe na basira, na Mola kumuogopa,
    Kinachokwepa si nyara, ufunge ndani ya kwapa,
    Kiache kinachokwepa, mbeleye kina madhara


    (a) Eleza hii ni bahari gani ya shairi
    (b) Eleza dhamira ya mshairi
    (c) Fafanua hasara nne zinazoletwa na tamaa - vile ving’aavyo
    (d) Taja na ueleze mbinu mbili za kifasihi zilizotumika katika shairi
    (e) Andika ubeti wa tano katika lugha ya nathari
    (f) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika shairi
    (i) Kuchuma
    (ii) Kisogo kuipa

    Date posted: October 9, 2019.  Answers (1)

  • 1. Namwona yu shambani, Na jembe mkononi, Analima, Mwanamama,(Solved)

    MWANAMKE
    1. Namwona yu shambani,
    Na jembe mkononi,
    Analima,
    Mwanamama,
    Mavuno si yake,
    Ni ya mume wake.

    2. Namwona viwandani,
    Pia maofisini,
    Yu kazini,
    Hamkani,
    Anabaguliwa,
    Na anaonewa.

    3. Namwona yu nyumbnai,
    Mpishi wa jikoni,
    Yaya yeye,
    Dobi yeye,
    Hakuna malipo,
    Likizo haipo.

    4. Namwona kitandani,
    Yu uchi maungoni.
    Ni mrembo
    Kama chombo,
    Chenye ushawishi,
    Mzima utashi.

    5. Namwona mkekani,
    Yuwamo uzazini,
    Apumua,
    Augua,
    Kilio cha kite,
    Cha mpiga pute.

    6. Kwa nini mwanamke,
    Ni yeye peke yake,
    Heshimaye,
    Haki anakosa,
    Kwa kweli ni kosa
    (Muhammed Seif Khatib)


    (a) “Shairi hili ni la kukatisha tamaa”. Fafanua dai hili kwa kutoa mifano minne
    (b) Eleza umbo la shairi hili
    (c) Andika ubeti wa tatu katika lugha ya nathari
    (d) Taja tamathali ya usemi iliyotawala katika shairi zima utoe mifano miwili ya jinsi
    ilivyotumika
    (e) Onyesha mifano miwili ya ubabedume inayojitokeza katika shairi hili
    (f) Eleza maana ya maneno yafuatayo jinsi yalivyotumiwa katika shairi:
    (i) mzima utashi
    (ii) maungoni

    Date posted: October 9, 2019.  Answers (1)

  • KIPI NIKITENDE? Tayari ni sarakani, niambie yote johara,Mosi nimpe shukrani, kanizaa bira zira,Wapo haiko hisani, ningefaa kwa uparara,Kipi takachokitenda, ni nene heko kwa mama?Miezi tisa...(Solved)

    KIPI NIKITENDE?
    Tayari ni sarakani, niambie yote johara,
    Mosi nimpe shukrani, kanizaa bira zira,
    Wapo haiko hisani, ningefaa kwa uparara,
    Kipi takachokitenda, ni nene heko kwa mama?


    Miezi tisa tumboni, yote nina kajinyima,
    Kanikopa uchunguni, safari ndefu kazima’
    Kama kinda kiotani, kiniasa huyu mama’
    Kipi takachokitenda, ninene heko mama ?

    Baba siku jana madadi, kawa vingaito mambo,
    Kaolewa na asadi, kachalazwa kwa wimbombo,
    Kaona – bali jadili, kuchao puani bombo,
    Kipi takachokitenda, ninene heko mama?


    Kila kuchao zarani, kupalilia kondeni,
    Kachanika mpinini, chungu povuka motoni,
    Kaviyariya fingani, kinijali jikoni,
    Kipi tukachokitenda , ninene heko mama?


    Wa siku hizi vijana, wakahujuru nyumbani,
    Wengine wao jagina, kawa lofa mutaani,
    Hali ukashiba nina, afikapo tu, “kongoni!”
    Kipi takachokitenda, ninene heko mama?


    Nawe bwana siwe maya, vita hasha kiwa kombo,
    Tena simfanye yaya, ya kikoa ndio mambo,
    Simtende ya hizaya, siwe mwao kila jambo,
    Kipi takachokitenda, ninene heko mama?


    Sasa jamvi nakuja, kisa nimesakarika,
    Naomba niliyotaja, tatia manani kaka,
    Nenayo yasiwe ngoja, ili nipokee baraka,
    Mema nitamtendea, apate futahi pia.



    (a) Eleza umbo la shairi hili
    (b) Kwa nini msanii amshukuru mamaye ?
    (c) Ni kina nani wanaokashifiwa na msanii ? Kwa nini ?
    (d) Onyesha tofauti katika ujumbe iliyoko katika beti nne za kwanza na mbili zinazofuata
    (e) Toa majina mengine yenye maana sawa na haya yaliyotumiwa katika shairi hili :
    (i) Mama
    (ii) Dawati
    (iii) Imara/thabiti
    (f) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika kaika shairi:
    (i) Kawa vangaito mambo
    (ii) Wimbombo
    (iii) Kongoni

    Date posted: October 9, 2019.  Answers (1)

  • 1. Nitampa nani, sauti yangu ya dhati Kwa kipimo gani, ingawa kiwakatiti Amefanya nini, la kutetea umati Kipimo ni kipi? 2. Yupi wa maani, asosita katikati Alo na maoni, yasojua...(Solved)

    1. Nitampa nani, sauti yangu ya dhati
    Kwa kipimo gani, ingawa kiwakatiti
    Amefanya nini, la kutetea umati
    Kipimo ni kipi?

    2. Yupi wa maani, asosita katikati
    Alo na maoni, yasojua gatigati
    Atazame chini, kwa kile ule wakati
    Kipimo ni kipi?

    3. Alo mzalendo, atambuaye shuruti
    Asiye mafundo, asojua mangiriti
    Anoshika pendo, hata katika mauti
    Kipimo ni kipi?

    4. Kipimo ni kipi, changu mimi kudhibiti
    Utu uko wapi, ni wapi unapoketi
    Nje kwa mkwapi, au ndani kwa buheti
    Kipimo ni kipi?

    a) Eleza umbo la shairi hili
    b) Taja na ueleze jinsi mwandishi alivyotumia uhuru wa ushairi
    c) Eleza ujumbe unaowasilishwa na mshairi
    d) Andika ubeti wa tatu katika lugha ya nathari
    e) Taja bahari tatu zinazojitokeza katika shairi na utoe sababu
    f) Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika shairi hili
    i) Katiti
    ii) Gatigati
    iii) Mangiriti

    Date posted: October 9, 2019.  Answers (1)