Trusted since 2008
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Kwa kipindi cha miezi kadha iliyopita tumeshuhudia vyombo vya dola vikitia makali yake kwenye upekuzi na hata kupiga...

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.

Kwa kipindi cha miezi kadha iliyopita tumeshuhudia vyombo vya dola vikitia makali yake kwenye upekuzi na hata kupiga doria usiku na mchana katika jitihada za kulinda nchi.
Mpango huu ni kweli umeonekana kufanya kazi hivi kwamba hata magaidi wenyewe wameshindwa kupenya katika miji na sasa kuhiari kijinga kushambulia magari ya abiria, kitendo ambacho ni cha kuonyesha uwoga. Kwa hatua hiyo, navipa vyombo vya dola kongole. Jambo ambalo lafaa kujulikana ni kwamba mikakati ya kulinda nchi haifai kuwa ni ya wakati mmoja tu, mbali inafaa kuwa ni zoezi la kila siku.
Magaidi nao huwa macho huku yakijua bayana kwamba wakati wa kulala kwa walinzi unapokuwepo, basi wanapata nafasi ya kututupia ‘viazi’ ukipenda grunedi.
Kama ilivyo kawaida katika mataifa mengi barani Afrika, ni bayana kwamba bado kungali na mianya mingi ambayo magaidi wa kimataifa huendelea kutumia. Dosari bado zipo. Kwa mfano, mipaka mingi ya nchi hizi huwa kama lango kuu la ugaidi wa kimataifa, kwani kuenea kwa saratani ya ufisadi halimo tu maofisini mbali pia kwenye mipaka yetu.
Kama kupata kitambulisho, pasipoti na stakabadhi zingine za kusafiri nchini Kenya ashakum si matusi ziligeuzwa ‘maandazi’ ya Kariakoo basi niambie ni nani hawezi kuingia na kutoka nchini bila usumbufu wowote ule bora tu anayehitaji ana hela mkononi? Kwa kuikubali hongo kuwa ufunguo wa kila kitu, Wakenya wenzangu hapo naona ni kama tumejiweka kwenye kikaango kilicho juu ya moto mkali. Hapa hakuna aliye na bahati, tajiri kwa masikini wamo kwenye mtego huu hatari.
Kwa mtindo ambao tunafuata wa kutoa ajira katika idara mbalimbali za ulinzi, inabidi serikali iwe na uangalifu sana hasa kwenye suala nzima la kuhakikisha stakabadhi wanazohitaji si ghushi.
Pasina kufanya hivyo hapo tena tunaweza kuwapata maadui wanaopenya na kujifanya walinzi wetu kumbe ni majasusi wa magaidi. Kila Mkenya anafaa kujihisi kulindwa. Miji, vijiji na hata vitongoji vinafaa kuwa na usalama wa kutosha, kwani kila Mkenya ni mlipa ushuru na hatufai kuona labda tabaka la juu likipendelewa huku mitaa ya mabanda ikiachiwa mbwa koko kama walinzi wao.
Suala lingine muhimu ni kuangaziwa upya usalama kwenye magari ya usafiri.
Juzi tulishuhudia mabasi mawili yakilipuliwa kwenye barabara ya Thika huku tukijua fika kwamba, mpango wa walinda nchi ungalipo.
La kusikitisha ni kuona kwamba, madereva na utingo wao walikamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa kutozuia shambulizo hilo. Je, hii ni sheria gani? Dereva ataendesha gari au atachukua jukumu la walinda usalama?
Waswahili walinena kwamba ukubwa ni jaa na kwa hivyo Rais wa taifa ndiye anayefaa kubeba mzigo mzima wa usalama wetu bila kubananga wasaa. Wengine ambao wanafaa kuwajibika ni wakuu wote wa idara mbalimbali za usalama.
Usalama wako na wangu ni muhimu, elewa bayana kwamba bila usalama watalii hawawezi kuja kututembelea. Bila ya usalama maendeleo ya taifa kamwe hayawezi kupatikana, ndiposa kila jitihada sharti zifanywe ili wote waweze kuendelea kuyafurahia matunda ya uhuru wetu.
Ada ya mja kunena muungwana ni vitendo, hatufai tu kuimba wimbo wa ‘linda nchi’ ilhali mabasi barabarani hayana usalama. Hebu na tuuone ulinzi endelevu na hapo tutawakomoa magaidi kwa yakini.

Maswali
1.Ipe taarifa hii anwani mwafaka.
2.Kwa nini magaidi wanashambulia magari ya abiria?
3.Kulingana na taarifa pamoja na maoni yako, eleza njia tatu ambazo zinatumiwa na magaidi ili kufanikisha utekelezaji wa unyama wao.
4.Ni njia gani ambazo magaidi hutumia kuingia katika nchi wanapoazimia kutekeleza uhalifu?
5.Kwa nini suala la usalama kwenye magari ya usafiri muhimu?
6.Ni njia zipi zinazoweza kutumiwa kupunguza mashambulizi ya kigaidi kulingana na mwandishi?
7.Eleza athari za utovu wa usalama.
8.Eleza neno au mafungu ya maneno kama yalivyotumiwa katika kifungu.
a)Vyombo vya dola
b)Jaa

Answers


Kavungya
1. Ugaidi / usalama n.k.
2. Wameshindwa kupenya katika miji na wana uwoga
3. -Kutupa guruneti
-Kuteka nyara na kuua watu (westgate)
-Kulipua ndege (Mariakani, Sept 11)
-Walipuaji wa kujitolea
4. - Kutumia hongo mipakani
-Kutumia mipaka ya nchi isiyolindwa
-Kughushi stakabadhi za kuingia katika idara za ulinzi
-Kupata ajira katika idara za ulinzi wakitumia stakabathi ghushi.
5. -Ni raia muhimu kama wengine
-Ni njia inayotumiwa ya usafiri na raia wengi
-Ni wanyonge wasio na ujuzi au silaha zozote za kujikinga
6. - Kuhakikisha ufisadi umekomeshwa mipakani
-Kuhakikisha stakabadhi za wanaotafuta ajira katika idara za ulinzi.
7. - Watalii kukosa kututembelea
-Maendeleo ya taifa kutopatikana
8. - Vyombo vya utawala k.v. bunge, mahakama n.k.
-Mahali pa kutia taka
Kavungya answered the question on October 12, 2019 at 09:39

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions