Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuatia: Shule yangu ya upili

      

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuatia:

Shule yangu ya upili

Majio yangu katika shule hii ya upili hayakutokea kwa bahati nasibu bali kwa mipango kabambe niliyoianza tangu nikiwa shule ya vichekechea. Nikiwa sitetereki hata kwa wazazi wangu waliponisihi nijiunge na shule nyingine za karibu nikawa sisikii la mwadhini wala la mteka maji msikitini. Nikawa na ragba ya mkanja nikingoja siku ya kujiunga na shule yenyewe. Kweli majuto ni mjukuu na huja kinyume.
Nilizaliwa katika aila yenye nafasi iliyotopea na kubobea katika ukwasi uliodhihirika kutokana na mitaa tulikoselelea kwa muda kabla ya baba kuaamua kununua nyumba yake mwenyewe huko upande wa Karen hivyo tukagura kutoka Runda. Wakati wa likizo tukawa tunaruka hadi pwani ambako mama yangu alikuwa amemiliki jumba lililokuwa katika ufuo wa bahari lililojengwa katika kipande kisichopungua ekari tatu alilotunukiwa wakati wa nikahi yao na wakwe wa baba yangu.
Wavyele wangu wakawa wanaendesha magari meusi ya kifahari ingawa sikuwahi kumwona mama akichangamka kuendesha magari yake ya maana, kila macheo ya siku za kazi gari lililoendeshwa na dereva ambaye alimstahi mama hadi akawa anamfungulia mlango wa gari na kuufunga baada ya mama kujitoma katika tumbo la gari lilimjia na kumrejesha kwa wakati. Nikajiunga na shule ya msingi ya kibinafsi ambako nilishughulikiwa kama kikembe. Wengi wa wale tuliosoma nao walikuwa wa tabaka langu na walikuwa wametoka katika kila sehemu nchini Kenya.
Hayawi hayawi huwa na siku ya kuripoti ikafika. Alfajiri, dereva mmoja akatumwa kwenda hadi Kisumu ili atulaki na kutusafirisha kutoka uwanja wa ndege hadi shule ya upili ambayo ilikuwa yangu ya rohoni. Nasi tukaelekea hadi uwanja wa ndege ili turuke hadi Kisumu. Safari yetu kutoka kitongoji cha kifahari hadi Airport ilikuwa njema, safari yetu tulipoabiri ndege ilikuwa bila bughudha, safari yetu kutoka Kisumu mjini haikuwa na kasoro na tulienda kulingana na mpango. Safari yetu ilikuwa mufti hadi tulipofika katika lango la shule ya kitaifa!
Tulipotia ozi tu!!....jamani......jamani nikafa moyo. Labda mama aliweza kubaini mabadiliko ya hisia zangu, nilitamauka, nikawa mchege na kusema kweli niliyoyaona sikuamini. Mvua iliyokuwa imepasua hapo awali ilikuwa imeacha vitua vya maji kwenye vijia vya kutembea vilivyochakaa na kubomoka bila yeyote kujali kuvikarabati. Majengo yalikuwa makongwe yaliyojengwa miaka mia moja iliyopita na yalistahili kuitwa makafadhi badala ya pahali pa kumkaribishia mwanafunzi aliyepita kwa alama mia nne na thelathini na tano.
Asiye na wake ana Mungu, nikapiga moyo konde lazima nisajiliwe katika shule ya ndoto langu. Ningewezaje kughairi wazo langu baada ya siku hizo zote za maandalizi tena mbele ya wanuna walioniona kama kielelezo chao tangu walipozaliwa. Nikasajiliwa!
Sikujua, hakika sikujua, sikujua shule ya upili ya kitaifa yaweza kuwa hivi. Kweli mwanafunzi aweza kukosa viatu na hata kushindwa kununua rangi ya kupaka viatu hivyo iwapo amenunuliwa na wahisani? Nilimlaumu ninamaana hakunieleza kuwa mtu anaweza kula chakula ambacho mbwa wetu hawezi hata kukiangalia. Nilipoingia katika ukumbi wa chakula nilihisi kitefutefu nusura nichafukwe na moyo, makapi ya mboga na uchafu usioelezeka ulinikumba, kisha nikapewa kisahani cha plastiki na kupakuliwa kipande cha ugali ambacho bado kilikuwa na unga na kuachiwa hiari ya kukila au kukitupa. Wenzangu wakawa wanakirambatia chakula kwa kasi
huku mmoja wao alipoona jinsi nilivyokiangalia changu akanihisi nimpe chote na kukimaliza fyu. Wote walikuwa na furaha kemkem na kuajabia utukufu wa shule iliyotukuka ya kitaifa ila mimi.
Baada ya mlo ‘rojo rojo’, tukaelekea darasani nilikopigwa na mghuma mkubwa. Tulikuwa wanafunzi hamsini na watano katika darasa moja tu! Mwalimu mmoja akaja na kutukaribisha shuleni kisha akatuarifu kuwa atakuwa mwalimu wa darasa letu. Nilipomsikia akinena nusura niishiwe na stahamala, kimombo chake kilinishangaza, hasa matamshi yake yalipungukiwa na kudhirisha athari za lugha ya asili. Nilihisi kana kwamba ningemrekebisha lakini sikudhubutu.
Tukafululiza hadi bweni na nikajilaza kitandani chembamba huku mwingine nisiyemjua lakini asiyejua kuwa kuna nguo maalum za kulala akalala uchi katika ghorofa ya juu ya kitanda chetu. Mgeni njoo mwenyeji apone maana baada ya muda wadudu ambao sikuwahi kuwaona aushini mwangu wakanza kunishambulia. Nikaamka baada ya kumnasa mmoja wa wadudu hawa na kuuliza mmoja wa wenzangu ni wepi wadudu hawa na kwa kutojali hata kidogo, akanieleza kuwa hawana neno bali ni kunguni tu, sikujua na kwa kweli mama hakuniambia kuwa kuna wadudu wanaotafuna mtu na hunuka fye! Sikulala kwa hofu huku wenzangu wakiforota kwa njia ya kunighasi. Sikuwahi kudhani kuwa watu wengi wanaweza kulala chumba kimoja huku changu kikiwa na hamamu na vifaa vyote muhimu kikibaki bila mtu!
Tulisomeshwa na walimu wasiojali kana kwamba tunaelewa au la. Hawakushughulika iwapo tulifanya kazi za ziada au la, ndio, hakujali chochote. Kilichonishangaza ni kuwa wanafunzi waliojiunga nasi kutoka shule za umma wenye alama duni waliwapenda na kuelewa haraka walichosomeshwa na hawakujali matamshi yao, labda hawakuyatambua.
Hatimaye tukafanya mtihani wa mwisho wa muhula wa kwanza. Nilishangaa ghaya iliponibainikia kuwa aliyetuongoza alikuwa ghulamu mmoja mshamba niliyempuuza tu mvulana kutoka kijijini ambacho singetambua katika ramani ya nchi ambaye hata vitu vya kimsingi vilimpiga chenga. Nikafanya uchunguzi nikatambua mwenzangu alikuwa na alama mia mbili hamsini na tatu akitoka katika darasa la nane, nilifanikiwa kuwa nambari mia mbili hamsini na tatu kwa jumla ya wanafunzi mia tatu!
Tulipofunga kwa likizo ya Pasaka nikaamua kuchukua hatua nyingine sitawahi kuhama kutoka shule hii ya upili wala kuwa zaidi ya nambari kumi!

Maswali

a) Thibitisha kauli kuwa msimulizi ana msimamo dhabiti.

b) Tofautisha jinsi mwandishi alivyofunzwa katika shule ya kibinafsi na shule ya upili.

c) Taja mambo matatu yanayotuonyesha kuwa msimulizi alilelewa katika aila ya kikabaila kulingana na aya ya pili.

d) Andika masuala matatu yaliyomshangaza katika shule ya upili.

e) Andika tamathali mbili zilizotumika katika kifungu.

f) Eleza maana ya msamiati huu kama ulivyotumika katika kifungu.

i) alimstahi

ii) kughairi

iii) kunighasi

  

Answers


Martin
A.
- Hatetereki anapoishiwa abadilishe wazo kuhusu shule ya ndoto lake.
- Uamuzi wa kutohama kutoka shule hii hata baada ya kuona yaliyompata.

B:Shule ya binafsi
- Alitunzwa kama kikembe.
- Walimu waliomfunza walitamka kimombo kwa njia bora.

Shule ya upili
- Matamshi ya walimu yaliathiriwa na lugha ya asili. walimu wasiojali uelewa wa wanafunzi.
- Wasioshughulika wasipofanya kazi za ziada. zozote

C:
- Mitaa walikoishi
- Uamuzi wa kununua nyumba Karen.
- Kuruka hadi pwani.
- Mama yake kumiliki jumba katika shamba la ekari. tatu ufuoni. zozote

D:
- Mwanafunzi kukosa viatu.
- Chakula duni katika shule hii.
- Idadi ya wanafunzi katika darasa.
- Kushambuliwa na wadudu.
- Kuongozwa na mvulana wa alama 253. zozote

E:
- Uhuishi - Tumbo la gari.
- Misemo - Ragba ya mkanja.
- Takriri - Sikujua.
- Methali - Mgeni njoo mwenyeji apone.

F:
- Alimstahi - Heshimu.

- Kughairi - badilisha.

- Kunighasi - kunikasirisha
marto answered the question on October 15, 2019 at 05:34


Next: Study the table below and answer the questions that follow.
Previous: Work out the oxidation number of phosphorous in the following compound H3PO3

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions


  • Fafanua sifa za sajili ya matanga. (Solved)

    Fafanua sifa za sajili ya matanga.

    Date posted: October 14, 2019.  Answers (1)

  • Eleza wajibu wa lugha ya Kiswahili kama lugha ya taifa nchini Kenya.(Solved)

    Eleza wajibu wa lugha ya Kiswahili kama lugha ya taifa nchini Kenya.

    Date posted: October 14, 2019.  Answers (1)

  • Tumia kivumishi kionyeshi cha mbali pamoja na nomino katika ngeli ya I - I.(Solved)

    Tumia kivumishi kionyeshi cha mbali pamoja na nomino katika ngeli ya I - I.

    Date posted: October 14, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha yambwa katika sentensi hii. Simu aliyonunuliwa Ali na mjombake imepotea. (Solved)

    Bainisha yambwa katika sentensi hii.
    Simu aliyonunuliwa Ali na mjombake imepotea.

    Date posted: October 14, 2019.  Answers (1)

  • Tenganisha mofimu katika neno lifuatalo kisha uonyeshe majukumu yake kisarufi. Onana (Solved)

    Tenganisha mofimu katika neno lifuatalo kisha uonyeshe majukumu yake kisarufi.
    Onana

    Date posted: October 14, 2019.  Answers (1)

  • Tumia neno ‘karibu’ katika sentensi kama: a) Kihusishi b) Kihisishi (Solved)

    Tumia neno ‘karibu’ katika sentensi kama:
    a) Kihusishi
    b) Kihisishi

    Date posted: October 14, 2019.  Answers (1)

  • Fafanua aina ya hali zilizotumika katika sentensi hizi. a) Mumo akacheka, akafurahia na akalala. b) Mtoto wa Maria hulia kila mara. c) Mwalimu aandika ubaoni....(Solved)

    Fafanua aina ya hali zilizotumika katika sentensi hizi.
    a) Mumo akacheka, akafurahia na akalala.
    b) Mtoto wa Maria hulia kila mara.
    c) Mwalimu aandika ubaoni.

    Date posted: October 14, 2019.  Answers (1)

  • Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli zilizo kwenye mabano. a) la (fanyia) b) suka (tendata)(Solved)

    Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli zilizo kwenye mabano.
    a) la (fanyia)
    b) suka (tendata)

    Date posted: October 14, 2019.  Answers (1)

  • Toa maana mbili za sentensi hii. Aliletewa ng’ombe na mtoto wake. (Solved)

    Toa maana mbili za sentensi hii.
    Aliletewa ng’ombe na mtoto wake.

    Date posted: October 14, 2019.  Answers (1)

  • Tofautisha sentensi hizi: a)Ningeondoka sasa ningefika mapema. b)Ningaliondoka sasa ningalifika mapema(Solved)

    Tofautisha sentensi hizi:
    a)Ningeondoka sasa ningefika mapema.
    b)Ningaliondoka sasa ningalifika mapema

    Date posted: October 14, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha aina za virai vilivyopigiwa mstari. Mjadala huo mzuri uliisha usiku wa manane. (Solved)

    Bainisha aina za virai vilivyopigiwa mstari.
    Mjadala huo mzuri uliisha usiku wa manane.

    Date posted: October 12, 2019.  Answers (1)

  • Mzizi ni nini? Toa mfano. (Solved)

    Mzizi ni nini? Toa mfano.

    Date posted: October 12, 2019.  Answers (1)

  • Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia jedwali. Kiongozi aliyeng’olewa mamlakani amekufa. (Solved)

    Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia jedwali.
    Kiongozi aliyeng’olewa mamlakani amekufa.

    Date posted: October 12, 2019.  Answers (1)

  • Andika kwa udogo.Chaka la Simba halilali paka. (Solved)

    Andika kwa udogo.
    Chaka la Simba halilali paka.

    Date posted: October 12, 2019.  Answers (1)

  • Yakinisha sentensi ifuatayo. Wanafunzi wasipopita mtihani huo mwalimu hatalaumiwa. (Solved)

    Yakinisha sentensi ifuatayo.
    Wanafunzi wasipopita mtihani huo mwalimu hatalaumiwa.

    Date posted: October 12, 2019.  Answers (1)

  • Weka shadda katika neno ‘nta’. (Solved)

    Weka shadda katika neno ‘nta’.

    Date posted: October 12, 2019.  Answers (1)

  • Andika neno ‘kuja’ katika hali ya kuamuru. (Solved)

    Andika neno ‘kuja’ katika hali ya kuamuru.

    Date posted: October 12, 2019.  Answers (1)

  • Andika kinyume cha sentensi hii. Mama alianika nguo zilizofuliwa na Kitwana. (Solved)

    Andika kinyume cha sentensi hii.
    Mama alianika nguo zilizofuliwa na Kitwana.

    Date posted: October 12, 2019.  Answers (1)

  • Andika sifa bainifu za /d/ na /f/. (Solved)

    Andika sifa bainifu za /d/ na /f/.

    Date posted: October 12, 2019.  Answers (1)

  • Ponografia ni tendo, maandishi, picha au mchoro unaoonyesha au kueleza uchi wa mtu au vitendo vya ngono kwa ajili...(Solved)

    Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali

    Ponografia ni tendo, maandishi, picha au mchoro unaoonyesha au kueleza uchi wa mtu au vitendo vya ngono kwa ajili ya kuchochea ashiki ya kuifanya. Mambo haya machafu huwasilishwa ana kwa ana kupitia sinema, video, magazeti, vitabu, muziki, televisheni. DVD, n.k.

    Ponorafia imekuwepo tangu jadi, hasa katika nchi za magharibi. Lakini sasa limekuwa tatizo sugu. Hii ni kwa sababu imeenea ulimwenguni kote mithili ya moto katika mbuga wakati wa kiangazi. Uenezi umechangiwa na mambo kadha wa kadha. Mchango mkubwa zaidi umetokana na kuimarika kwa vyombo vya teknolojia ya habari na mawasiliano. Matumizi ya tarakilishi, mdahilishi na viungambali vya picha yamesambaza ponografia ilivyoanza. Hata hivyo, hubuniwa au kutengenezwa na makundi mbali mbali ya watu. Miongoni mwa hawa ni watu wasiojali maadili. Pili, kuna wale wenye matatizo ya kisaikolojia na kijamii. Wao hutengeneza na kueneza uchafu huu kwa lengo la ama kuvuruga maadili katika jamii au kuchukiza wanajamii waadilifu. Kundi lingine ni lile la wanaoichukulia ponografia kama nyenzo ya kutosheleza ashiki zao. Hivi sasa, kundi kubwa ni lile la wanotumia matusi haya kama njia ya kuchuma. Kwa mfano, wanamziki ambao hutumia ponografia kuvutia wateja na hivyo kuzidisha mauzo yao.

    Kushamiri kwa wimbi na uonyeshaji ponografia kuna athari kubwa kwa jamii na hasa watoto. Ingawa watu wengine hudai picha hizi haziwaathiri, upo ushahidi kuonyesha kuwa wanaotazama picha za ngono hupata matatizo. Lazima ieleweke kuwa kinachoonekana na jicho au kusikika kwa sikio huathiri fikira au hisia. Picha za matusi zinachangia kwa kiasi kikubwa kuharibu akili. Badala ya kuzingatia mambo muhimu kama masomo watu huanza kutafakari mambo machafu.

    Vijana wengi ni kama bendera. Hivyo basi huanza kuiga wanayoyaona na kusikia. Hili ni tatizo linalowafanya kuacha mkondo wa maadili. Kutokana na uchafu huu, watu wengi hushawishiwa kuingilia shughuli za ngono mapema kabla hawajakomaa kimwili, kiakili na kihisia. Matokeo yake ni mengi. Haya ni pamoja na ukahaba, utendaji mbaya shuleni, mahudhurio mabaya darasani na mimba zisizotarajiwa. Vijana wengi huacha shule kabisa. Wengine nao huambukizwa magonjwa ya zinaa ambayo huwaletea mauti.

    Inasemekana kuwa akili za binadamu hunata zaidi mambo yanayowasilishwa kwa picha. Si ajabu vijana huyadumisha matusi haya katika kumbukumbu zao na kuyasanya sehemu ya maisha yao. Wengi huanza kuandama tabia mbovu kama ushoga, ubasha na usagaji. Kuna wale ambao huanza kujichua. Kujichua ni hali ya mwanamke au mwanaume kumaliza haja za kimaumbile bila kufanya mapenzi na mtu mwingine. Ponografia imechangia pakubwa kuenea kwa haya.

    Jambo hili limegeuza mielekeo ya vijana. Wanaiga mitindo mibaya ya mavazi yanayoanika uchi wao. Hali kadhalika, huiga lugha, ishara na miondoko inayohusiana na ngono. Yote haya yanapingana na desturi za Mwafrika. Si ajabu visa vya ubakaji vinaongezeka kila kukuchapo.

    Utazamaji wa picha chafu aghalabu huandamana na maovu mengine kama unywaji pombe, matumizi ya dawa za kulevya, uvutaji sigara na utumiaji wa dawa za kuchochea uchu wa ngono. Mambo haya huwapa vijana kutazama tabia za unyama.

    Jambo hatari ni kuwa kuendelea kutazama picha hizi huzifanya nishai na hisia za watu kuwa butu, yaani huondoa makali. Hata katika utu uzima, mtu atapoteza mhemko wa kawaida na kugeuzwa kuwa mtegemezi wa ponografia. Tatizo hili linaenea kwa vishindo mijini na vijijini. Ipo haja ya dharura kuikinga jamii kutokana na maenezi haya yasio na kizuizi.

    Jambo la kwanza ni kuongeza ufahamu wa umma wote kuhusu uovu wa picha hizi. Kwa namna hii itawezekana kupunguza mahitaji na uuzaji wa ponografia. Tatizo hili linaenea kwa vishindo mijini na vijijini. Ipo haja ya dharura kuikinga jamii kutokana na maenezi haya yasiyo na kizuizi.

    Tatizo la kuenea kwu ponografia limeendelea kuwepo kwa sababu ya udhaifu wa sheria. Kilichoko basi ni kuweka sheria za kuzuia utengenezaji wa upujufu huu. Kuambatana na haya, hatua kali zichukuliwe kwa wanaovunja sheria hizi. Hali kadhalika, ushirikiano wa karibu baina ya wadau uimarishwe katika ulimwengu mzima. Serikali na wanaohusika wakabiliwe ipasavyo. Jamii ingependa kuona michakato ya kuharamisha utengenezaji, usambazaji na utangazaji wa ponografia ikiwekwa.

    Wazazi nao wasijipweteke tu bali nao wasaidie. Ni muhimu washikilie kwa sharti juhudi zao za kuwaelekeza na kuwashauri watoto kuzingatia uongofu na kukwepa picha hizi najisi. Watoto lazima waeleweshwe kuwa haifai kutazama picha au michoro michafu. Itikadi na imani za kidini na utamaduni wa Kiafrika unakataza vikali mtu kuona uchi wa mtu mwingine. Matokeo ya kuasi makatazo haya yana madhara makubwa kwa watu na jamii.

    Maswali
    a)Fupisha ujumbe wa aya ya pili na ya tatu kwa maneno 20 – 25
    Matayarisho
    Nakala safi
    b)Kwa kutumia maneno 55 – 60, eleza mambo muhimu yanayojitokeza katika aya ya nne hadi ya tisa
    kuhusu athari za ponografia .
    Matayarisho
    Nakala safi

    Date posted: October 12, 2019.  Answers (1)