/ny/-hutamkiwa katika kaakaa gumu
/ng/-hutamkiwa katika kaakaa laini
marto answered the question on October 15, 2019 at 07:07
- UFUPISHO
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali uliyopewa.(Solved)
UFUPISHO
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali uliyopewa.
Kwa mujibu wa utafiti wa wanasayansi, binadamu ndiye kiumbe aliyepevuka zaidi katika fikra kuliko viumbe wengine. Anasemekana kuwashinda viumbe wengine kwa njia nyingi,hata kuweza kuwatala na kuwaratibia maisha yao. Binadamu amepewa uwezo wa kuyatawala mazingira na kukabidhiwa ufundi wa kuweza kuunda vifaa mbalimbali ili kuyakabili mazingira hayo. Uwezo huu ndio umemwezesha kukimu mahitaji ya kizazi kimoja hadi kingine kwa miaka na mikaka. Hata hivyo, kuna tofauti kubwa kati ya binadamu na wanyama. Tofauti hii inaweza kumvua binadamu sifa zake zote na kuuona ukwasi wa maarifa yake kama ishara ya maangamizi ya ulimwengu. Hii ni kutokana na hasara anayosababisha katika mazingira tulivu waliyoumbiwa viumbe wote na Muumba wao.
Lakini ifahamike kuwa mandhari ya ulimwengu tunamoishi humpendeza kila kiumbe, mathalan hewa safi itokayo miliamini, chemichemi za maji, mito na vijito mnamotiririka maji safi, vilele vya milima vilivyofunikwa kwa theluji daima dawamu, yakiwemo mabonde na tambarare zinazohimili uhai wa viumbe wengi.
Vilevile ibainike kuwa uzuri huu wa kiasili hauwezi kufikia kilele bila vichaka na misitu inayoipamba ardhi hii huku ikileta mvua. Mapambo yote haya ni kwa nguvu za maumbile; nguvu ambazo hazisababishwi na kuwa hatari kwa uhai wa binadamu na viumbe wenzake kwa sababu anayaharibu maumbile kwa kiasi kikubwa kinachomtisha binadamu mwenyewe.
Sababu mojawapo ni uchafuzi wa maji kama rasilmali muhimu ya kiasili. Uchafuzi huu umeathiri viumbe na mimea pakubwa, yakiwemo maradhi mbalimbali. Kwa kweli bila maji, uhai utatoweka duniani. Uharibifu mkubwa wa maji machafu yenye sumu hasa kutoka viwandani na kuingia kwenye mito na bahari, huwadhuru viumbe wengine wenye makao majini. Maji huleta madhara sit u kwa mimea bali hata kwa binadamu kupitia kwa ulaji wa vyakula.
Binadamu ameharibu misitu kwa ukataji wa miti kihoela hasa kwenye sehemu za chemichemi. Hali hii husababisha uhaba wa mvua ambao huleta kiangazi kinachokausha mimea na visima vya maji.
Ujenzi wa viwanda hasa katika nchi zilizostawi unaelezwa na wanasayansi wanaohusika na hali za anga kuwa umesababisha taharuki na wasiwasi mwingi. Hii ni kwa sababu umeonyesha kuharibu utandu unaozuia miale ya jua kupenya moja kwa moja kwenye sayari hii na hapo kuhatarisha uhai. Hii ni kutokana na hewa chafu itokayo viwandani. Kadri binadamu anavyochangia pakubwa katika kuondoa polepole uhai wa viumbe wote ulimwenguni.
Warsha nyingi zimefanywa ili kutahadharisha ulimwengu dhidi ya uharibifu wa mazingira na maliasili.‘Ajenda’ za mikutano hiyo hasa zinalenga nchi zilizostawi kwani hizi ndizo zinazochafua mazingira kwa kasi zaidi kuliko zile zinazostawi.
Mapendekezo mengi yametolewa katika vikao hivyo ili kusulihisha tatizo hili lakini ni hatua chache mno zinazochukuliwa kurekebisha mambo haya. Itakuwa bora zaidi ikiwa watu watajipa jukumu la kusafisha mazingira yao. Watoto wafunzwe jinsi ya kuhifadhi mazingira yanapochafuliwa. Wakumbuke kuwa
utumwa si karaha kwa sababu afya zetu na viumbe wengine zimo hatarini ikiwa mazingira yatachafuliwa. Kwa hivyo, ni jukumu la kila mmoja wetu kutunza mazingira anamoishi kwa manufaa ya leo na kesho. Viongozi wanaohudhuria kongomano la kila mwaka maarufu kama ‘KYOTO PROTOCAL’wahakikishe kuwa maazimio yote ya kulinda mazingira yametekelezwa, na sheria kali kuidhinishwa dhidi ya raia wao, la sivyo, siku zijazo kutakuwa na mafuriko mengi ambayo yatasababisha visiwa na sehemu zote za Pwani kufunikwa na maji.
a) Eleza kwa ufupi hasara zinazoweza kusababishwa na uharibifu wa mazingira. (Tumia maneno 45- 55)
b) Eleza hatua ambazo mwanadamu anapaswa kuchukua ili kupunguza madhara ya upanuzi wa viwanda. (Tumia maneno 45)
Date posted: October 15, 2019. Answers (1)
- Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuatia:
Shule yangu ya upili(Solved)
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuatia:
Shule yangu ya upili
Majio yangu katika shule hii ya upili hayakutokea kwa bahati nasibu bali kwa mipango kabambe niliyoianza tangu nikiwa shule ya vichekechea. Nikiwa sitetereki hata kwa wazazi wangu waliponisihi nijiunge na shule nyingine za karibu nikawa sisikii la mwadhini wala la mteka maji msikitini. Nikawa na ragba ya mkanja nikingoja siku ya kujiunga na shule yenyewe. Kweli majuto ni mjukuu na huja kinyume.
Nilizaliwa katika aila yenye nafasi iliyotopea na kubobea katika ukwasi uliodhihirika kutokana na mitaa tulikoselelea kwa muda kabla ya baba kuaamua kununua nyumba yake mwenyewe huko upande wa Karen hivyo tukagura kutoka Runda. Wakati wa likizo tukawa tunaruka hadi pwani ambako mama yangu alikuwa amemiliki jumba lililokuwa katika ufuo wa bahari lililojengwa katika kipande kisichopungua ekari tatu alilotunukiwa wakati wa nikahi yao na wakwe wa baba yangu.
Wavyele wangu wakawa wanaendesha magari meusi ya kifahari ingawa sikuwahi kumwona mama akichangamka kuendesha magari yake ya maana, kila macheo ya siku za kazi gari lililoendeshwa na dereva ambaye alimstahi mama hadi akawa anamfungulia mlango wa gari na kuufunga baada ya mama kujitoma katika tumbo la gari lilimjia na kumrejesha kwa wakati. Nikajiunga na shule ya msingi ya kibinafsi ambako nilishughulikiwa kama kikembe. Wengi wa wale tuliosoma nao walikuwa wa tabaka langu na walikuwa wametoka katika kila sehemu nchini Kenya.
Hayawi hayawi huwa na siku ya kuripoti ikafika. Alfajiri, dereva mmoja akatumwa kwenda hadi Kisumu ili atulaki na kutusafirisha kutoka uwanja wa ndege hadi shule ya upili ambayo ilikuwa yangu ya rohoni. Nasi tukaelekea hadi uwanja wa ndege ili turuke hadi Kisumu. Safari yetu kutoka kitongoji cha kifahari hadi Airport ilikuwa njema, safari yetu tulipoabiri ndege ilikuwa bila bughudha, safari yetu kutoka Kisumu mjini haikuwa na kasoro na tulienda kulingana na mpango. Safari yetu ilikuwa mufti hadi tulipofika katika lango la shule ya kitaifa!
Tulipotia ozi tu!!....jamani......jamani nikafa moyo. Labda mama aliweza kubaini mabadiliko ya hisia zangu, nilitamauka, nikawa mchege na kusema kweli niliyoyaona sikuamini. Mvua iliyokuwa imepasua hapo awali ilikuwa imeacha vitua vya maji kwenye vijia vya kutembea vilivyochakaa na kubomoka bila yeyote kujali kuvikarabati. Majengo yalikuwa makongwe yaliyojengwa miaka mia moja iliyopita na yalistahili kuitwa makafadhi badala ya pahali pa kumkaribishia mwanafunzi aliyepita kwa alama mia nne na thelathini na tano.
Asiye na wake ana Mungu, nikapiga moyo konde lazima nisajiliwe katika shule ya ndoto langu. Ningewezaje kughairi wazo langu baada ya siku hizo zote za maandalizi tena mbele ya wanuna walioniona kama kielelezo chao tangu walipozaliwa. Nikasajiliwa!
Sikujua, hakika sikujua, sikujua shule ya upili ya kitaifa yaweza kuwa hivi. Kweli mwanafunzi aweza kukosa viatu na hata kushindwa kununua rangi ya kupaka viatu hivyo iwapo amenunuliwa na wahisani? Nilimlaumu ninamaana hakunieleza kuwa mtu anaweza kula chakula ambacho mbwa wetu hawezi hata kukiangalia. Nilipoingia katika ukumbi wa chakula nilihisi kitefutefu nusura nichafukwe na moyo, makapi ya mboga na uchafu usioelezeka ulinikumba, kisha nikapewa kisahani cha plastiki na kupakuliwa kipande cha ugali ambacho bado kilikuwa na unga na kuachiwa hiari ya kukila au kukitupa. Wenzangu wakawa wanakirambatia chakula kwa kasi
huku mmoja wao alipoona jinsi nilivyokiangalia changu akanihisi nimpe chote na kukimaliza fyu. Wote walikuwa na furaha kemkem na kuajabia utukufu wa shule iliyotukuka ya kitaifa ila mimi.
Baada ya mlo ‘rojo rojo’, tukaelekea darasani nilikopigwa na mghuma mkubwa. Tulikuwa wanafunzi hamsini na watano katika darasa moja tu! Mwalimu mmoja akaja na kutukaribisha shuleni kisha akatuarifu kuwa atakuwa mwalimu wa darasa letu. Nilipomsikia akinena nusura niishiwe na stahamala, kimombo chake kilinishangaza, hasa matamshi yake yalipungukiwa na kudhirisha athari za lugha ya asili. Nilihisi kana kwamba ningemrekebisha lakini sikudhubutu.
Tukafululiza hadi bweni na nikajilaza kitandani chembamba huku mwingine nisiyemjua lakini asiyejua kuwa kuna nguo maalum za kulala akalala uchi katika ghorofa ya juu ya kitanda chetu. Mgeni njoo mwenyeji apone maana baada ya muda wadudu ambao sikuwahi kuwaona aushini mwangu wakanza kunishambulia. Nikaamka baada ya kumnasa mmoja wa wadudu hawa na kuuliza mmoja wa wenzangu ni wepi wadudu hawa na kwa kutojali hata kidogo, akanieleza kuwa hawana neno bali ni kunguni tu, sikujua na kwa kweli mama hakuniambia kuwa kuna wadudu wanaotafuna mtu na hunuka fye! Sikulala kwa hofu huku wenzangu wakiforota kwa njia ya kunighasi. Sikuwahi kudhani kuwa watu wengi wanaweza kulala chumba kimoja huku changu kikiwa na hamamu na vifaa vyote muhimu kikibaki bila mtu!
Tulisomeshwa na walimu wasiojali kana kwamba tunaelewa au la. Hawakushughulika iwapo tulifanya kazi za ziada au la, ndio, hakujali chochote. Kilichonishangaza ni kuwa wanafunzi waliojiunga nasi kutoka shule za umma wenye alama duni waliwapenda na kuelewa haraka walichosomeshwa na hawakujali matamshi yao, labda hawakuyatambua.
Hatimaye tukafanya mtihani wa mwisho wa muhula wa kwanza. Nilishangaa ghaya iliponibainikia kuwa aliyetuongoza alikuwa ghulamu mmoja mshamba niliyempuuza tu mvulana kutoka kijijini ambacho singetambua katika ramani ya nchi ambaye hata vitu vya kimsingi vilimpiga chenga. Nikafanya uchunguzi nikatambua mwenzangu alikuwa na alama mia mbili hamsini na tatu akitoka katika darasa la nane, nilifanikiwa kuwa nambari mia mbili hamsini na tatu kwa jumla ya wanafunzi mia tatu!
Tulipofunga kwa likizo ya Pasaka nikaamua kuchukua hatua nyingine sitawahi kuhama kutoka shule hii ya upili wala kuwa zaidi ya nambari kumi!
Maswali
a) Thibitisha kauli kuwa msimulizi ana msimamo dhabiti.
b) Tofautisha jinsi mwandishi alivyofunzwa katika shule ya kibinafsi na shule ya upili.
c) Taja mambo matatu yanayotuonyesha kuwa msimulizi alilelewa katika aila ya kikabaila kulingana na aya ya pili.
d) Andika masuala matatu yaliyomshangaza katika shule ya upili.
e) Andika tamathali mbili zilizotumika katika kifungu.
f) Eleza maana ya msamiati huu kama ulivyotumika katika kifungu.
i) alimstahi
ii) kughairi
iii) kunighasi
Date posted: October 15, 2019. Answers (1)
- Fafanua sifa za sajili ya matanga. (Solved)
Fafanua sifa za sajili ya matanga.
Date posted: October 14, 2019. Answers (1)
- Eleza wajibu wa lugha ya Kiswahili kama lugha ya taifa nchini Kenya.(Solved)
Eleza wajibu wa lugha ya Kiswahili kama lugha ya taifa nchini Kenya.
Date posted: October 14, 2019. Answers (1)
- Tumia kivumishi kionyeshi cha mbali pamoja na nomino katika ngeli ya I - I.(Solved)
Tumia kivumishi kionyeshi cha mbali pamoja na nomino katika ngeli ya I - I.
Date posted: October 14, 2019. Answers (1)
- Bainisha yambwa katika sentensi hii.
Simu aliyonunuliwa Ali na mjombake imepotea.
(Solved)
Bainisha yambwa katika sentensi hii.
Simu aliyonunuliwa Ali na mjombake imepotea.
Date posted: October 14, 2019. Answers (1)
- Tenganisha mofimu katika neno lifuatalo kisha uonyeshe majukumu yake kisarufi.
Onana
(Solved)
Tenganisha mofimu katika neno lifuatalo kisha uonyeshe majukumu yake kisarufi.
Onana
Date posted: October 14, 2019. Answers (1)
- Tumia neno ‘karibu’ katika sentensi kama:
a) Kihusishi
b) Kihisishi (Solved)
Tumia neno ‘karibu’ katika sentensi kama:
a) Kihusishi
b) Kihisishi
Date posted: October 14, 2019. Answers (1)
- Fafanua aina ya hali zilizotumika katika sentensi hizi.
a) Mumo akacheka, akafurahia na akalala.
b) Mtoto wa Maria hulia kila mara.
c) Mwalimu aandika ubaoni....(Solved)
Fafanua aina ya hali zilizotumika katika sentensi hizi.
a) Mumo akacheka, akafurahia na akalala.
b) Mtoto wa Maria hulia kila mara.
c) Mwalimu aandika ubaoni.
Date posted: October 14, 2019. Answers (1)
- Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli zilizo kwenye mabano.
a) la (fanyia)
b) suka (tendata)(Solved)
Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli zilizo kwenye mabano.
a) la (fanyia)
b) suka (tendata)
Date posted: October 14, 2019. Answers (1)
- Toa maana mbili za sentensi hii.
Aliletewa ng’ombe na mtoto wake.
(Solved)
Toa maana mbili za sentensi hii.
Aliletewa ng’ombe na mtoto wake.
Date posted: October 14, 2019. Answers (1)
- Tofautisha sentensi hizi:
a)Ningeondoka sasa ningefika mapema.
b)Ningaliondoka sasa ningalifika mapema(Solved)
Tofautisha sentensi hizi:
a)Ningeondoka sasa ningefika mapema.
b)Ningaliondoka sasa ningalifika mapema
Date posted: October 14, 2019. Answers (1)
- Bainisha aina za virai vilivyopigiwa mstari.
Mjadala huo mzuri uliisha usiku wa manane.
(Solved)
Bainisha aina za virai vilivyopigiwa mstari.
Mjadala huo mzuri uliisha usiku wa manane.
Date posted: October 12, 2019. Answers (1)
- Mzizi ni nini? Toa mfano. (Solved)
Mzizi ni nini? Toa mfano.
Date posted: October 12, 2019. Answers (1)
- Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia jedwali.
Kiongozi aliyeng’olewa mamlakani amekufa.
(Solved)
Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia jedwali.
Kiongozi aliyeng’olewa mamlakani amekufa.
Date posted: October 12, 2019. Answers (1)
- Andika kwa udogo.Chaka la Simba halilali paka. (Solved)
Andika kwa udogo.
Chaka la Simba halilali paka.
Date posted: October 12, 2019. Answers (1)
- Yakinisha sentensi ifuatayo.
Wanafunzi wasipopita mtihani huo mwalimu hatalaumiwa.
(Solved)
Yakinisha sentensi ifuatayo.
Wanafunzi wasipopita mtihani huo mwalimu hatalaumiwa.
Date posted: October 12, 2019. Answers (1)
- Weka shadda katika neno ‘nta’. (Solved)
Weka shadda katika neno ‘nta’.
Date posted: October 12, 2019. Answers (1)
- Andika neno ‘kuja’ katika hali ya kuamuru. (Solved)
Andika neno ‘kuja’ katika hali ya kuamuru.
Date posted: October 12, 2019. Answers (1)
- Andika kinyume cha sentensi hii.
Mama alianika nguo zilizofuliwa na Kitwana.
(Solved)
Andika kinyume cha sentensi hii.
Mama alianika nguo zilizofuliwa na Kitwana.
Date posted: October 12, 2019. Answers (1)