U-i
A – wa
Kavungya answered the question on October 16, 2019 at 13:51
- Andika sentensi hii katika msemo halisi
Mwalimu alimuambia mwanafunzi amalize kazi hiyo haraka
(Solved)
Andika sentensi hii katika msemo halisi
Mwalimu alimuambia mwanafunzi amalize kazi hiyo haraka
Date posted: October 16, 2019. Answers (1)
- Taja sifa tatu kuu za sauti /k/(Solved)
Taja sifa tatu kuu za sauti /k/
Date posted: October 16, 2019. Answers (1)
- Nidhamu ni kitu cha maana sana maishani mwa binadamu. Kila mwanafunzi anapaswa kuwa na nidhamu ya hali ya juu...(Solved)
Soma kifungu kisha uyajibu maswali yanayofuata.
Nidhamu ni kitu cha maana sana maishani mwa binadamu. Kila mwanafunzi anapaswa kuwa na nidhamu ya hali ya juu sana.Akiwa na nidhamu hiyo, atakuwa mtu mwadilifu, anayeweza kustahiwa na kusadikika katika mambo, shughuli na hali tofauti.
Kwanza, mtoto mwenye nidhamu huwa kama anga au nuru nyumbani mwao, shuleni na pia katika jamii.Watu wote wanampenda na kumheshimu. Wazee kwa vijulanga wote wanamtegemea kama msimamizi wa mambo nyeti ya maisha yao. Kwa hivyo, ni dhahiri shahiri kwamba mwadilifu hunufaika sana, kinyume na mkaidi ambaye wahenga walimwambia kwamba atakosa kufaidi hadi siku ya Idi.
Pili, huwadia nyakati ambapo huwa kuna jambo la busara, mathalani jukumu ama dhima fulani ambayo huhitaji tu mwakilishi mmoja darasani, shuleni au katika jamii. Watu hapana shaka watamteua yule mwadilifu kuchukua nafasi kama hiyo. Ndio maana viranja wanaoteuliwa shuleni, huwa ni wanagenzi ambao tayari wamekwisha tiliwa katika mizani na kupigwa msasa madhubuti.
Vile vile, mwadalifu daima atajiepusha na shutuma na majanja yote yanayoweza kuchipuka. Kuna msemo maarufu, kwa busara yake iliyobusarisha mwadilifu kwamba “aliye kando haangukiwi na mti.”Pia waliambiwa kwamba, “ pilipili usiyoila yakuwashiani?”
Ni bayana kutokana na misemo hiyo miwili kwamba mwenye nidhamu hawezi kuhusishwa na majanga hatari yanayoweza kuyakumba watu.
Walakini ni vyema kujiuliza, je, nidhamu huanzia wapi, na kwa nini kuna baadhi ya ‘watoro’ ambao ni utovu wa nidhamu? Utovu wa nidhamu huanzia awali sana maishani mwa mja. Mtoto anapozaliwa, anategemea miongozo na mielekeo ya watu wazima ambao wakomazingirani mwake.Ndipo wakale wale waliokaramka walisema kwamba mtoto akibebwa, hutazama kisogo cha nina.
Hivi ni kusema kwamba, nidhamu au utovu wa nidhamu huanzia nyumbani hadi shuleni, kisha hupanuka hadi kufikia kiwango ambapo mja anatangamana na watu wote katika maisha yake.Ikiwa sehemu moja ya ukuaji wa nidhamu maishani mwa mja itasambaratika, basi hawezi akawa mkamilifu kinidhamu maishani mwake.
Kwa vile ni bayana kwamba mabaya yote ayatendayo duniani hulipwa na Mola papa hapa duniani,watovu wa nidhamu wote huishia kuangamia, ama kujuta mno kwa amali zao potovu.Ni kheri mja kujihidi mwenyewe, kwani uhalifu haulipi chochote.
a) Nini umuhimu wa nidhamu? (maneno kati ya 50-55)
Matayarisho
Jibu
(b) Bila kubadilisha maana, fupisha aya nne za mwisho. (tumia maneno 55-60)
Matayarisho
Jibu
Date posted: October 16, 2019. Answers (1)
- Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanoyofuatia.
Malengo ya maendeleo ya Milenia
Malengo ya maendeleo ya Milenia (yajulikanayo kwa kimombo kama Millenium Development Goals (MDG), Ni...(Solved)
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanoyofuatia.
Malengo ya maendeleo ya Milenia
Malengo ya maendeleo ya Milenia (yajulikanayo kwa kimombo kama Millenium Development Goals (MDG), Ni malengo manane ya nchi wanachama wa umoja wa mataifa, ambayo nchi hizi zilikubaliana kujitahidi kutimiza kufikia mwaka wa 2015.Azma ya kufikia malengo haya ilizinduliwa rasmi mnamo septemba 2000 katika azimio la millennia la umoja wa mataifa.Wakati wa uzinduzi, mataifa yote 189 wanachama wa umoja wa mataifa yalihusika.Kwa sasa, mataifa wanachama yameongezeka na kufikia 193 na yote yanajizatiti kutekeleza azma hii.
Azma ya kwanza ni kukomeza au kupunguza umaskini uliokithiri kwa asili 50 miongoni mwa watu ambao kipato chao ni chini ya dola moja kwa siku.Aidha lazima hii inalenga kupunguza kwa kiasi hicho idadi ya watu wanaokumbwa na dhiki ya njaa kufikia mwaka wa 2015.Kwa kielelezo, kwa mfano vijiji viitwavyo ‘vijiji vya milenia’vilianzishwa katika nchi sahara,ambazo ni Uhabeshi, Ghana, Kenya, Malawi, Rwanda, Nigeria, Senegal, Tanzania na Uganda vilichaguliwa.Wakazi hawa wanapookolewa kutoka kwa ulitima, hatua zilichukuliwa vijijini humu yanaonyesha athari chanya.Kunayo matumaini.
Lengo la pili lilikuwa kutimiza elimu ya msingi kwa wote chini ya wito ‘Elimu kwa wote’, yaani kwa kingereza Eduction for All (EFA) kufika mwaka wa 2015.Nchini Kenya, elimu ya msingi ilifafanuliwa upya katika katiba mpya ya 2010, ikawa yaanzia shule ya chekechea hadi kidato cha nne. Aidha imetajwa kuwa ya lazima, kwamba mtoto sharti ahudhurie masomo.Ina maana kuwa mzazi analazimika kumpeleka mtoto shuleni. Lengo pia lipo, kuhakikisha watoto wote wa jinsia za kike na kiume wanahitimu.
Lengo jingine ni kuwania usawa wa kijinsia kwa kuhakikisha kuna nafasi sawa kwa wote.Katika janibu nyingi za wanachama wa umoja wa mataifa, wanawake kwa miaka ya ayami walionekana kuwa chini ya wanaume kutokana na taasubi ya kiume, mwanamke alifaa kuwa chini ya mwanamume.Hatua ya kwanza ya malengo ya maendeleo ya millennia inanuia kuondoa tofauti ya uwiano wa wasichana na wavulana katika elimu ya msingi hadi sekondari ifikapo mwaka 2005; na katika ngazi zote za elimu ifikapo 2015. Kuondoa utoro miongoni mwa wahudhuriao masomoni hutahakikisha usawa huu.
Lengo la nne ni kupuuza vifo vya Watoto wa umri chini ya miaka mitano kwa theluthi mbili kufikia mwaka wa 2015. Jitihada zinatiwa kuhakikisha kuwa kina mama waja wazito hawazai njiti wala watoto wao hawaagi punde baada ya kuzaliwa.Changamoto imekuwa kwamba watoto wengi katika nchi zinazoendelea hufa kabla kufikia umri wa miaka mitano. Mapambano dhidi ya magonjwa kama vile kifaduro, polia na malaria yaliyosababisha vifo hivi pamoja na jitihada za kujizatiti za kufikia lengo hili.
Kunayo azma ya kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za uzi ili kupunguza kwa robo tatu vifo vya uzazi kufikia 2015. Kua kwa wajawazito kunaashiria huduma duni wakati wa kuhimili.Kina mama wengine katika nchi zinazoendelea hawahudhurii kliniki wakati wakati wa kulea mimba.Kwingineko, huduma hizi huwa mbali sana, huku namna za usafiri zikiwa duni.Kina mama huishia ama kuhudumiwa na ‘wakunga’ wasiohitimu au hata kujifungua pweke .Mataifa wanachama wanahimiza kuongezea zahanati na vituo vingine muhimu vya afya.Kadhalika jitihada zinatiwa kuwaelimisha kina mama na jamii kwa jumla kuhusu umuhimu wa kuhudhuria kliniki wakatiwa ujauzito na kuhakikisha mama yu salama wakati wa kujifungua.
Magonjwa sugu yanayotishia kuwamaliza walimwengu ni kikwazo cha jitihada za walimwengu kujiendeleza.Ndiyo maana lengo la sita ni kupambana na Ukimwi, malaria na magonjwa mengineyo.Kampeni zinaimarishwa katika jumuiya hii kuzuia kabisa na kupunguza maambukizo mapya ya Ukimwi.Jitihada zinatiwa kupunguza au kuzuia kabisa ugonjwa wa malaria au magonjwa mengine hatari. Vyombo vya habari, vituo tamba vilivyo na maafisa wa nyanjani vinatumiwa nyanjani katika mataifa wanachama ili kufaulisha kampeni hii.
Aidha wanachama wanalenga kuhifadhi mazingira kwa kujumuisha misingi ya maendeleo endelevu katika sera na program za nchi.Zinalenga kuzuia upotevu wa rasilimali ya mazingira kama vile miti na maji.Lengo lipokuhakikisha kuwa katika kipindi hiki wanachama watapunguza kwa asilimia 50 idadio ya watu wanaoshindwa kupata maji safi na salama – hii ni moja wapo ya malengo ambayo, kwa mujibu ya tovuti ya umoja wa mataifa www.un.org/milleniumgoals, kuna matumaini ya kutimiza zaidi ya 2015.
Mwisho kuna lengo la kujenga mshikamano wa maendeleo duniani, kwanza kwa kuboresha zaidi mfano wa Fedha na biashara duniani kuhakikisha ni wa usawa, unafuata sheria na kamwe hauna ubaguzi.Utawala bora; kushughulikia mahitaji ya kipekee ya nchi changa kama vile kuziondolea ushuru wa bidhaa muhimu,kuzipunguzia au kuziondolea madeni; kutoa misaada zaidi kwa nchi maskini zinazotia jitihada kutoa umaskini kushughulikia mahitaji muhimu, ya visiwa vidogo na nchi zisizo na bandari miongoni mwa nchi zinazoendelea; kuwapa vijana ajira bora; kushirikiana na sekta za kibinafsi ili kuimarisha teknolojia ya kisasa hasa katika habari na mawasiliano ni baadhi ya yanayozingatiwa kulenga kutimiza mshikamano huu.
MASWALI.
1. Malengo ya maendeleo ya milenia ni nini?
2. Ni wachochole wa kiwango gani wanaolengwa kuinuliwa na hatua za malengo ya maendeleo ya milenia?
3. Taja vipengele viwili muhimu kuhusu elimu katika katiba mpya ya Kenya vinavyo changia kufikia
malengo ya maendeleo ya milenia?
4. Gusia changamoto tano zinazowakabili kina mama wajawazito katika ulimwengu wa tatu.
5. Kampeni dhidi ya magonjwa sugu inafanywa kwa namna gani.
6. Hali ya maji inatarajiwa kuwaje kufikia 2015.
7. Eleza maana ya vifungu hivi.
a) Hawazai njiti
b) Vifo vya uzazi.
Date posted: October 16, 2019. Answers (1)
- a. Eleza maana ya lakabu.
b. Huku ukitoa mifano mwafaka, taja asili tano za lakabu.
c. Eleza sifa saba za lakabu.
d. Eleza umuhimu wa lakabu...(Solved)
a. Eleza maana ya lakabu.
b. Huku ukitoa mifano mwafaka, taja asili tano za lakabu.
c. Eleza sifa saba za lakabu.
d. Eleza umuhimu wa lakabu katika jamii
Date posted: October 15, 2019. Answers (1)
- Soma Shairi kisha ujibu maswali.(Solved)
Soma Shairi kisha ujibu maswali.
(a) Kwa kuzingatia mishororo miwili ya mwisho kila ubeti, eleza bahari ya shairi hili.
(b) Onyesha kero zinazosababishwa na mvua.
(c) Eleza kanuni zilizofuatwa kutunga shairi hili.
(d) Onyesha namna mshairi alivyotumia idhini yake.
(e) Andika ubeti wa kwanza kwa lugha ya nathari.
(f) Taja mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika shairi hili.
(g) Andika maana za maneno haya kulingana na muktadha wa shairi.
(i) kutwa na kucha
(ii) kuicha mvua
Date posted: October 15, 2019. Answers (1)
- Eleza jinsi mwandishi alivyofanikisha mbinu ya kisengere nyuma.(Solved)
Eleza jinsi mwandishi alivyofanikisha mbinu ya kisengere nyuma.
Date posted: October 15, 2019. Answers (1)
- Akifisha sentensi hii:
Lo ni nani huyo anayeshambulia mwanangu jirani yangu aliuliza kwa hasira nyingi.(Solved)
Akifisha sentensi hii:
Lo ni nani huyo anayeshambulia mwanangu jirani yangu aliuliza kwa hasira nyingi.
Date posted: October 15, 2019. Answers (1)
- Eleza matumizi ya ‘kwa’ katika sentensi ifuatayo:
Moja kwa tano ya watu waliosafiri kwa gari la moshi walikula wali kwa mchuzi.(Solved)
Eleza matumizi ya ‘kwa’ katika sentensi ifuatayo:
Moja kwa tano ya watu waliosafiri kwa gari la moshi walikula wali kwa mchuzi.
Date posted: October 15, 2019. Answers (1)
- Unda Nomino kutokana na vitenzi vifuatavyo:
Dhulumu
Tubu(Solved)
Unda Nomino kutokana na vitenzi vifuatavyo:
Dhulumu
Tubu
Date posted: October 15, 2019. Answers (1)
- Andika visawe vya maneno yaliyopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo:Lupita ndiye alitakadamu upelelezi wa shamba hili.(Solved)
Andika visawe vya maneno yaliyopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo:
Lupita ndiye alitakadamu upelelezi wa shamba hili.
Date posted: October 15, 2019. Answers (1)
- Changanua sentensi ifuatayo kwa mishale:
Magaidi waliochoma kanisa ni maadui wakubwa sana.(Solved)
Changanua sentensi ifuatayo kwa mishale:
Magaidi waliochoma kanisa ni maadui wakubwa sana.
Date posted: October 15, 2019. Answers (1)
- Andika sentensi ifuatayo katika hali ya udogo wingi.
Mvulana mkorofi alimkata mbuzi sikio kwa kisu kikali(Solved)
Andika sentensi ifuatayo katika hali ya udogo wingi.
Mvulana mkorofi alimkata mbuzi sikio kwa kisu kikali
Date posted: October 15, 2019. Answers (1)
- Tunga sentensi ukitumia kihusishi cha wakati.(Solved)
Tunga sentensi ukitumia kihusishi cha wakati.
Date posted: October 15, 2019. Answers (1)
- Tambua yambwa katika sentensi ifuatayo na ueleze ni za aina gani.
Wazazi waliwanunulia wanafunzi bora zawadi nyingi kwa hundi.(Solved)
Tambua yambwa katika sentensi ifuatayo na ueleze ni za aina gani.
Wazazi waliwanunulia wanafunzi bora zawadi nyingi kwa hundi.
Date posted: October 15, 2019. Answers (1)
- Andika katika usemi wa taarifa.
"Mkishinda timu hii leo nitamtuza." Mkufunzi akatwambia.(Solved)
Andika katika usemi wa taarifa.
"Mkishinda timu hii leo nitamtuza." Mkufunzi akatwambia.
Date posted: October 15, 2019. Answers (1)
- Eleza maana tatu za sentensi hii.
Chakula kingine kimeliwa na wageni(Solved)
Eleza maana tatu za sentensi hii.
Chakula kingine kimeliwa na wageni
Date posted: October 15, 2019. Answers (1)
- Tumia kiunganishi seuze/sembuse katika sentensi.(Solved)
Tumia kiunganishi seuze/sembuse katika sentensi.
Date posted: October 15, 2019. Answers (1)
- Unda sentensi yenye muundo ufuatao:
KN(N+V), KT (t+V+E)(Solved)
Unda sentensi yenye muundo ufuatao:
KN(N+V), KT (t+V+E)
Date posted: October 15, 2019. Answers (1)
- Andika mifano mine ya vitenzi vya silabi moja katika kauli ta kutendesha.(Solved)
Andika mifano mine ya vitenzi vya silabi moja katika kauli ta kutendesha.
Date posted: October 15, 2019. Answers (1)