Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata: Katika safu yangu hii sina lengo la kuzishambulia dini zetu na namuomba Mungu sana asiniandikie dhambi kutokana na ninayotaka...

      

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata:

Katika safu yangu hii sina lengo la kuzishambulia dini zetu na namuomba
Mungu sana asiniandikie dhambi kutokana na ninayotaka kuyaandika. Lakini nashawishika kuikumbusha jamii yangu ambayo inatufanya watu tuzione dini zetu zinamkandamiza mwanamke. Dini zetu kubwa kama Uislamu na Ukristo zinatuelekeza mwanamke kumheshimu mumewe na kumsikiliza anachosema, lakini kwa yeye
kufuata maadili ya dini na si kukuambia uue ukakubali.
Wakati dini inasema utekeleze amri ya mumeo na wao wameelezwa mambo
ya kuwafanyia wanawake, ikiwa ni pamoja na kuwaheshima na kuwaridhisha kadri
ya uwezo wao.
Kutokana na hilo la amri, wanaume wengi ndio wamechukua kama tiketi ya kunyanyasa mwanamke na hata kumnyima fursa ya kujiendeleza kielimu na hata kufanya shughuli za kuongeza kipato. Unakuta familia ni ya kimaskini, baba hana fedha za kutosha kuihudumia familia yake, lakini baba huyo anataka kujishughulisha
na shughuli yoyote ya kumuingizia kipato kinachoweza kuwasaidia wote na matokeo yake kuendelea kuwepo, kwenye dimbwi la umasikini. Wengine kwa hofu ya kupata changamoto kutoka kwa wake zao wanawakatalia wanawake walio wao kujiendeleza kielimu au kutafuta mwanamke asiyeelimika ili asiweze kuhoji mambo kadhaa ndani
ya nyumba.
Hili limebainishwa hivi karibuni na shirika moja lisilo la kiserikali huko
kigoma ambapo katika utafiti wao asilimia 90% ya wanawake wa vijijini wanashindwa kutoa hoja kutokana na uelewa wao duni na kutoa sababu ya kuwa hiyo ni kutokana
na ukosefu wa elimu, masuala ya kidini yanayomwelekeza mwanamke kufuata amri
za mumewe, mila na desturi kadhaa.
Dini zote zinaeleza wazi umuhimu wa mtu kupata elimu bila kubagua kama
ya kiislamu inavyosema; mtu anapata thawabu anapotafuta elimu na anatakiwa
aitafute popote bila kujali umbali na hata ikiwezekana kufika China ambapo
inaaminika ni mbali.
Sijawahi kuona wala kusikia dini ikisema mwanamke asipate elimu lakini
baba zangu na kaka zangu wanaume wanalipotosha hili kutaka kuendelea kumkandamiza mwanamke bila kufikiri kuwa mwanamke ni msaada mkubwa
kwao na kwa maendeleo ya taifa lote; ikiwa leo tupo katika harakati za kupata maendeleo na nchi hii hivi kweli tutafanikiwa?
Mapambano ya kuleta maendeleo yaanze katika ngazi ya familia kwa
kuondoka kwa ujinga wa kumkandamiza mwanamke ili naye aelimike, aweze
kujenga hoja, aweze kujitafutia kipato na mwisho kusaidia katika maendeleo ya
familia ambayo kwa njia nyingine ndiyo maendeleo yenyewe ya taifa hili.

(a)Fupisha aya tano za kwanza. (Maneno 70).
Matayarisho
Jibu.
(b)Mwanamke anaweza kuendelezwa vipi. Rejelea aya mbili za mwisho. (Maneno 50).
Matayarisho
Jibu.

  

Answers


Kavungya
a)(a)Sina lengo la kuzishambulia dini zetu na namuomba mungu asiniandikie dhambi.
(b)Dini za uislamu na ukristo zinatuelekeza mwanamke kumheshimu mumewe na
kumsikiliza anachosema.
(c)Dini imewapa wanawake jukumu la kufuata amri ya mumeo.
(d)Wanaume wengi wamechukua amri hii kunyanyasa na kuwanyima fursa ya elimu na hofu
ya kupata kipato.
(e)90% ya wanawake hawatoi hoja kwa sababu wao wameiamini kuwa dini.
(f)Wanaume huwa na hofu ya kupata changamoto kutoka kwa wake waliojiendeleza kielimu.
(g)Dini zinaeleza umuhimu wa mtu kupata elimu bila kubagua.

(b)- Kwa kupata elimu.
-Asikandamizwe kwa vyovyote.
-Tutambue umuhimu wa mwanamke katika ujenzi wa taifa.
-Atafute kipato cha familia.
-Aweze kutoa maoni ya ujenzi wa nchi.
-Imani potovu za kidini zitupiliwe mbali.
Kavungya answered the question on October 18, 2019 at 13:44


Next: Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata. Ni fedheha kuona taifa ambalo halijakuwa likitambua msamiati wa shibe kwa zaidi ya miongo miwili sasa limeacha chakula kiharibike...
Previous: Taja maneno yenye miundo ifuatayo ya silabi. (i)KKKI (ii)Irabu pekee (II)

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata. Ni fedheha kuona taifa ambalo halijakuwa likitambua msamiati wa shibe kwa zaidi ya miongo miwili sasa limeacha chakula kiharibike...(Solved)

    Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.

    Ni fedheha kuona taifa ambalo halijakuwa likitambua msamiati wa shibe kwa zaidi
    ya miongo miwili sasa limeacha chakula kiharibike mashambani kutokana na ukosefu wa soko. Taarifa kuwa ni zamu ya wakulima wa mahindi kukadiria hasara baada
    ya wenzao wa maziwa ni za kuhuzunisha. Inasemekana wakulima wa zao la mahindi katika mikoa ya pwani, mashariki, kati na Bonde la ufa wanendelea kuhesabu hasara kutokana na ukosefu wa soko la mahindi kutoka kwa serikali.

    Hii ni hata baada ya serikali kuwapatia na kuwauzia pembejeo kwa bei nafuu kama
    njia mojawapo ya kuimarisha uzalishaji wa chakula nchini. Kinachovunja moyo
    zaidi ni habari kuwa serikali iyo hiyo ilitoa ahadi ya kununua mazao yote ya
    wakulima hao kama njia mojawapo ya kuwatia moyo katika kazi yao.

    Kando na wakulima wa kibinafsi, ilitumia mamilioni ya pesa za umma kuzindua
    miradi ya kilimo cha mahindi kwa kunyunyizia mashamba maji na mazao yake
    pia yanaharibikia. Wakulima wa mradi wa kilimo cha kunyunyizia mashamba wa
    Hola, kwa mfano, wameathirika pakubwa kutokana na ukosefu wa soko la mazao
    yao. Imekuwa ikijikokota kutokana na sababu kadhaa ikiwemo ukosefu wa fedha
    za kununua mahindi.

    Hii ni hata baada ya uchunguzi kuonyesha kuwa usalama wa chakula nchini
    umedorora kutokana na kiangazi cha muda mrefu. Mbali na kutokuwepo kwa
    utaratibu wa kununua mahindi kutoka kwa wakulima hao halmashauri ya nafaka
    haina uwezo wa kuwashughulikia wakulima wote nchini.

    Hii ni kwa sababu wakulima wengi hawapati huduma za halmashauri hiyo ambayo imejikita katika maeneo yaliyokuwa yakizalisha chakula kwa wingi miaka iliyopita. Eneo la Hola, kwa mfano, liko mbali kutoka kwa kituo cha halmashauri hiyo kwa sababu eneo hilo ni kame.

    Ni kutokana na muktadha huu serikali inapaswa ichukue hatua za haraka kuepusha
    kuharibika kwa zao la mahindi nchini. Serikali inapaswa kutenga fedha zaidi za kununua mahindi kutoka kwa wakulima. Inakisiwa kuwa hasara zaidi inatarajiwa kutokea ikiwa pesa zaidi hazitatengwa kwa sababu idadi ya wakulima wanaovuna mahindi inatarajiwa kuongezeka.

    Maswali
    (a)Kwa nini chakula kinaharibikia mashambani?
    (b)Serikali ilichangia vipi katika kuimarisha uzalishaji wa chakula?
    (c)Eleza vile halmashari ya nafaka haijaweza kuepushia wakulima wa mahindi hasara.
    (d)Kwa nini wakulima wa maeneo kame hawajashughulikiwa na halmashuri ya nafaka?
    (e)Kutokana na taarifa hii serikali inaweza kutatua tatizo la wakulima kwa njia gani?
    (f)Pendekeza namna taifa linaweza kuepuka na kupambana na uharibifu wa chakula mashambani.
    (g)Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika taarifa.
    (i)Miongo
    (ii)Pembejeo
    (iii)Umedorora

    Date posted: October 18, 2019.  Answers (1)

  • Taja mambo yoyote manne yanayofanywa na serikali yetu kuimarisha lugha ya Kiswahili (Solved)

    Taja mambo yoyote manne yanayofanywa na serikali yetu kuimarisha lugha ya Kiswahili

    Date posted: October 17, 2019.  Answers (1)

  • Kanusha katika ukubwa Mwizi huyu aliiba kisu na ng’ombe wa mwanamke yule. (Solved)

    Kanusha katika ukubwa
    Mwizi huyu aliiba kisu na ng’ombe wa mwanamke yule.

    Date posted: October 17, 2019.  Answers (1)

  • Eleza tofauti iliyopo kati ya sentensi hiziTulipofika hotelini tulipewa soda na chupaTulipofika hotelini tulipewa soda kwa chupa(Solved)

    Eleza tofauti iliyopo kati ya sentensi hizi
    Tulipofika hotelini tulipewa soda na chupa
    Tulipofika hotelini tulipewa soda kwa chupa

    Date posted: October 17, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana ya sentensi hii Ningalikuwa na pesa ningalinunua gari na ningalistarehe. (Solved)

    Eleza maana ya sentensi hii
    Ningalikuwa na pesa ningalinunua gari na ningalistarehe.

    Date posted: October 17, 2019.  Answers (1)

  • Andika neno lenye maana sawa na Hawala Katani(Solved)

    Andika neno lenye maana sawa na
    Hawala
    Katani

    Date posted: October 17, 2019.  Answers (1)

  • Onyesha matumizi ya kiimbo katika sentensi hii Ondoka hapa! (Solved)

    Onyesha matumizi ya kiimbo katika sentensi hii
    Ondoka hapa!

    Date posted: October 17, 2019.  Answers (1)

  • Eleza sifa mbili za vishazi tegemezi.(Solved)

    Eleza sifa mbili za vishazi tegemezi.

    Date posted: October 16, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha aina za vitenzi katika sentensi ifuatayo. Walimu ni watu wasiopendwa wanaposema ukweli kuhusu wanafunzi (Solved)

    Bainisha aina za vitenzi katika sentensi ifuatayo.
    Walimu ni watu wasiopendwa wanaposema ukweli kuhusu wanafunzi

    Date posted: October 16, 2019.  Answers (1)

  • Onyesha virai katika sentensi zifuatazo na ueleze ni vya aina gani. i) Anachukia kusoma riwaya yenye masuala ya kisiasa. ii) Watoto wa kike hudunishwa katika jamii...(Solved)

    Onyesha virai katika sentensi zifuatazo na ueleze ni vya aina gani.
    i) Anachukia kusoma riwaya yenye masuala ya kisiasa.
    ii) Watoto wa kike hudunishwa katika jamii nyingi

    Date posted: October 16, 2019.  Answers (1)

  • Yakinisha katika nafsi ya tatu wingi Sijasafiri kwenda marekani (Solved)

    Yakinisha katika nafsi ya tatu wingi
    Sijasafiri kwenda marekani

    Date posted: October 16, 2019.  Answers (1)

  • Changamua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha jedwali Omondi anaazimia kuwa mhasibu Lakini hatii bidii masomoni (Solved)

    Changamua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha jedwali
    Omondi anaazimia kuwa mhasibu Lakini hatii bidii masomoni

    Date posted: October 16, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi ifuatayo kwa wingi, wakati uliopita hali ya kuendelea Mwalimu humuadhibu mwanafunzi mwenye hatia. (Solved)

    Andika sentensi ifuatayo kwa wingi, wakati uliopita hali ya kuendelea
    Mwalimu humuadhibu mwanafunzi mwenye hatia.

    Date posted: October 16, 2019.  Answers (1)

  • Weka nomino hizi katika ngeli zake Mbalungi Mturuki(Solved)

    Weka nomino hizi katika ngeli zake
    Mbalungi
    Mturuki

    Date posted: October 16, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi hii katika msemo halisi Mwalimu alimuambia mwanafunzi amalize kazi hiyo haraka (Solved)

    Andika sentensi hii katika msemo halisi
    Mwalimu alimuambia mwanafunzi amalize kazi hiyo haraka

    Date posted: October 16, 2019.  Answers (1)

  • Taja sifa tatu kuu za sauti /k/(Solved)

    Taja sifa tatu kuu za sauti /k/

    Date posted: October 16, 2019.  Answers (1)

  • Nidhamu ni kitu cha maana sana maishani mwa binadamu. Kila mwanafunzi anapaswa kuwa na nidhamu ya hali ya juu...(Solved)

    Soma kifungu kisha uyajibu maswali yanayofuata.

    Nidhamu ni kitu cha maana sana maishani mwa binadamu. Kila mwanafunzi anapaswa kuwa na nidhamu ya hali ya juu sana.Akiwa na nidhamu hiyo, atakuwa mtu mwadilifu, anayeweza kustahiwa na kusadikika katika mambo, shughuli na hali tofauti.

    Kwanza, mtoto mwenye nidhamu huwa kama anga au nuru nyumbani mwao, shuleni na pia katika jamii.Watu wote wanampenda na kumheshimu. Wazee kwa vijulanga wote wanamtegemea kama msimamizi wa mambo nyeti ya maisha yao. Kwa hivyo, ni dhahiri shahiri kwamba mwadilifu hunufaika sana, kinyume na mkaidi ambaye wahenga walimwambia kwamba atakosa kufaidi hadi siku ya Idi.

    Pili, huwadia nyakati ambapo huwa kuna jambo la busara, mathalani jukumu ama dhima fulani ambayo huhitaji tu mwakilishi mmoja darasani, shuleni au katika jamii. Watu hapana shaka watamteua yule mwadilifu kuchukua nafasi kama hiyo. Ndio maana viranja wanaoteuliwa shuleni, huwa ni wanagenzi ambao tayari wamekwisha tiliwa katika mizani na kupigwa msasa madhubuti.

    Vile vile, mwadalifu daima atajiepusha na shutuma na majanja yote yanayoweza kuchipuka. Kuna msemo maarufu, kwa busara yake iliyobusarisha mwadilifu kwamba “aliye kando haangukiwi na mti.”Pia waliambiwa kwamba, “ pilipili usiyoila yakuwashiani?”
    Ni bayana kutokana na misemo hiyo miwili kwamba mwenye nidhamu hawezi kuhusishwa na majanga hatari yanayoweza kuyakumba watu.
    Walakini ni vyema kujiuliza, je, nidhamu huanzia wapi, na kwa nini kuna baadhi ya ‘watoro’ ambao ni utovu wa nidhamu? Utovu wa nidhamu huanzia awali sana maishani mwa mja. Mtoto anapozaliwa, anategemea miongozo na mielekeo ya watu wazima ambao wakomazingirani mwake.Ndipo wakale wale waliokaramka walisema kwamba mtoto akibebwa, hutazama kisogo cha nina.

    Hivi ni kusema kwamba, nidhamu au utovu wa nidhamu huanzia nyumbani hadi shuleni, kisha hupanuka hadi kufikia kiwango ambapo mja anatangamana na watu wote katika maisha yake.Ikiwa sehemu moja ya ukuaji wa nidhamu maishani mwa mja itasambaratika, basi hawezi akawa mkamilifu kinidhamu maishani mwake.

    Kwa vile ni bayana kwamba mabaya yote ayatendayo duniani hulipwa na Mola papa hapa duniani,watovu wa nidhamu wote huishia kuangamia, ama kujuta mno kwa amali zao potovu.Ni kheri mja kujihidi mwenyewe, kwani uhalifu haulipi chochote.

    a) Nini umuhimu wa nidhamu? (maneno kati ya 50-55)
    Matayarisho
    Jibu
    (b) Bila kubadilisha maana, fupisha aya nne za mwisho. (tumia maneno 55-60)
    Matayarisho
    Jibu

    Date posted: October 16, 2019.  Answers (1)

  • Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanoyofuatia. Malengo ya maendeleo ya Milenia Malengo ya maendeleo ya Milenia (yajulikanayo kwa kimombo kama Millenium Development Goals (MDG), Ni...(Solved)

    Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanoyofuatia.

    Malengo ya maendeleo ya Milenia

    Malengo ya maendeleo ya Milenia (yajulikanayo kwa kimombo kama Millenium Development Goals (MDG), Ni malengo manane ya nchi wanachama wa umoja wa mataifa, ambayo nchi hizi zilikubaliana kujitahidi kutimiza kufikia mwaka wa 2015.Azma ya kufikia malengo haya ilizinduliwa rasmi mnamo septemba 2000 katika azimio la millennia la umoja wa mataifa.Wakati wa uzinduzi, mataifa yote 189 wanachama wa umoja wa mataifa yalihusika.Kwa sasa, mataifa wanachama yameongezeka na kufikia 193 na yote yanajizatiti kutekeleza azma hii.

    Azma ya kwanza ni kukomeza au kupunguza umaskini uliokithiri kwa asili 50 miongoni mwa watu ambao kipato chao ni chini ya dola moja kwa siku.Aidha lazima hii inalenga kupunguza kwa kiasi hicho idadi ya watu wanaokumbwa na dhiki ya njaa kufikia mwaka wa 2015.Kwa kielelezo, kwa mfano vijiji viitwavyo ‘vijiji vya milenia’vilianzishwa katika nchi sahara,ambazo ni Uhabeshi, Ghana, Kenya, Malawi, Rwanda, Nigeria, Senegal, Tanzania na Uganda vilichaguliwa.Wakazi hawa wanapookolewa kutoka kwa ulitima, hatua zilichukuliwa vijijini humu yanaonyesha athari chanya.Kunayo matumaini.

    Lengo la pili lilikuwa kutimiza elimu ya msingi kwa wote chini ya wito ‘Elimu kwa wote’, yaani kwa kingereza Eduction for All (EFA) kufika mwaka wa 2015.Nchini Kenya, elimu ya msingi ilifafanuliwa upya katika katiba mpya ya 2010, ikawa yaanzia shule ya chekechea hadi kidato cha nne. Aidha imetajwa kuwa ya lazima, kwamba mtoto sharti ahudhurie masomo.Ina maana kuwa mzazi analazimika kumpeleka mtoto shuleni. Lengo pia lipo, kuhakikisha watoto wote wa jinsia za kike na kiume wanahitimu.

    Lengo jingine ni kuwania usawa wa kijinsia kwa kuhakikisha kuna nafasi sawa kwa wote.Katika janibu nyingi za wanachama wa umoja wa mataifa, wanawake kwa miaka ya ayami walionekana kuwa chini ya wanaume kutokana na taasubi ya kiume, mwanamke alifaa kuwa chini ya mwanamume.Hatua ya kwanza ya malengo ya maendeleo ya millennia inanuia kuondoa tofauti ya uwiano wa wasichana na wavulana katika elimu ya msingi hadi sekondari ifikapo mwaka 2005; na katika ngazi zote za elimu ifikapo 2015. Kuondoa utoro miongoni mwa wahudhuriao masomoni hutahakikisha usawa huu.

    Lengo la nne ni kupuuza vifo vya Watoto wa umri chini ya miaka mitano kwa theluthi mbili kufikia mwaka wa 2015. Jitihada zinatiwa kuhakikisha kuwa kina mama waja wazito hawazai njiti wala watoto wao hawaagi punde baada ya kuzaliwa.Changamoto imekuwa kwamba watoto wengi katika nchi zinazoendelea hufa kabla kufikia umri wa miaka mitano. Mapambano dhidi ya magonjwa kama vile kifaduro, polia na malaria yaliyosababisha vifo hivi pamoja na jitihada za kujizatiti za kufikia lengo hili.

    Kunayo azma ya kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za uzi ili kupunguza kwa robo tatu vifo vya uzazi kufikia 2015. Kua kwa wajawazito kunaashiria huduma duni wakati wa kuhimili.Kina mama wengine katika nchi zinazoendelea hawahudhurii kliniki wakati wakati wa kulea mimba.Kwingineko, huduma hizi huwa mbali sana, huku namna za usafiri zikiwa duni.Kina mama huishia ama kuhudumiwa na ‘wakunga’ wasiohitimu au hata kujifungua pweke .Mataifa wanachama wanahimiza kuongezea zahanati na vituo vingine muhimu vya afya.Kadhalika jitihada zinatiwa kuwaelimisha kina mama na jamii kwa jumla kuhusu umuhimu wa kuhudhuria kliniki wakatiwa ujauzito na kuhakikisha mama yu salama wakati wa kujifungua.

    Magonjwa sugu yanayotishia kuwamaliza walimwengu ni kikwazo cha jitihada za walimwengu kujiendeleza.Ndiyo maana lengo la sita ni kupambana na Ukimwi, malaria na magonjwa mengineyo.Kampeni zinaimarishwa katika jumuiya hii kuzuia kabisa na kupunguza maambukizo mapya ya Ukimwi.Jitihada zinatiwa kupunguza au kuzuia kabisa ugonjwa wa malaria au magonjwa mengine hatari. Vyombo vya habari, vituo tamba vilivyo na maafisa wa nyanjani vinatumiwa nyanjani katika mataifa wanachama ili kufaulisha kampeni hii.

    Aidha wanachama wanalenga kuhifadhi mazingira kwa kujumuisha misingi ya maendeleo endelevu katika sera na program za nchi.Zinalenga kuzuia upotevu wa rasilimali ya mazingira kama vile miti na maji.Lengo lipokuhakikisha kuwa katika kipindi hiki wanachama watapunguza kwa asilimia 50 idadio ya watu wanaoshindwa kupata maji safi na salama – hii ni moja wapo ya malengo ambayo, kwa mujibu ya tovuti ya umoja wa mataifa www.un.org/milleniumgoals, kuna matumaini ya kutimiza zaidi ya 2015.

    Mwisho kuna lengo la kujenga mshikamano wa maendeleo duniani, kwanza kwa kuboresha zaidi mfano wa Fedha na biashara duniani kuhakikisha ni wa usawa, unafuata sheria na kamwe hauna ubaguzi.Utawala bora; kushughulikia mahitaji ya kipekee ya nchi changa kama vile kuziondolea ushuru wa bidhaa muhimu,kuzipunguzia au kuziondolea madeni; kutoa misaada zaidi kwa nchi maskini zinazotia jitihada kutoa umaskini kushughulikia mahitaji muhimu, ya visiwa vidogo na nchi zisizo na bandari miongoni mwa nchi zinazoendelea; kuwapa vijana ajira bora; kushirikiana na sekta za kibinafsi ili kuimarisha teknolojia ya kisasa hasa katika habari na mawasiliano ni baadhi ya yanayozingatiwa kulenga kutimiza mshikamano huu.

    MASWALI.
    1. Malengo ya maendeleo ya milenia ni nini?
    2. Ni wachochole wa kiwango gani wanaolengwa kuinuliwa na hatua za malengo ya maendeleo ya milenia?
    3. Taja vipengele viwili muhimu kuhusu elimu katika katiba mpya ya Kenya vinavyo changia kufikia
    malengo ya maendeleo ya milenia?
    4. Gusia changamoto tano zinazowakabili kina mama wajawazito katika ulimwengu wa tatu.
    5. Kampeni dhidi ya magonjwa sugu inafanywa kwa namna gani.
    6. Hali ya maji inatarajiwa kuwaje kufikia 2015.
    7. Eleza maana ya vifungu hivi.
    a) Hawazai njiti
    b) Vifo vya uzazi.

    Date posted: October 16, 2019.  Answers (1)

  • a. Eleza maana ya lakabu. b. Huku ukitoa mifano mwafaka, taja asili tano za lakabu. c. Eleza sifa saba za lakabu. d. Eleza umuhimu wa lakabu...(Solved)

    a. Eleza maana ya lakabu.

    b. Huku ukitoa mifano mwafaka, taja asili tano za lakabu.

    c. Eleza sifa saba za lakabu.

    d. Eleza umuhimu wa lakabu katika jamii

    Date posted: October 15, 2019.  Answers (1)

  • Soma Shairi kisha ujibu maswali.(Solved)

    Soma Shairi kisha ujibu maswali.

    shairi104410152019.png

    (a) Kwa kuzingatia mishororo miwili ya mwisho kila ubeti, eleza bahari ya shairi hili.

    (b) Onyesha kero zinazosababishwa na mvua.

    (c) Eleza kanuni zilizofuatwa kutunga shairi hili.

    (d) Onyesha namna mshairi alivyotumia idhini yake.

    (e) Andika ubeti wa kwanza kwa lugha ya nathari.

    (f) Taja mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika shairi hili.

    (g) Andika maana za maneno haya kulingana na muktadha wa shairi.

    (i) kutwa na kucha

    (ii) kuicha mvua

    Date posted: October 15, 2019.  Answers (1)