Nilianza kusikia habari za ugonjwa wa ukimwi mnamo mwaka wa 1984. Wakati huo nilikuwa nimemaliza masomo yangu ya kidato...

      

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali

Nilianza kusikia habari za ugonjwa wa ukimwi mnamo mwaka wa 1984. Wakati huo nilikuwa nimemaliza masomo yangu ya kidato cha sita na kujiunga ia chuo cha walimu kilichoko wilayani Nyeri kiitwacho Kagumo. Nilihofu sana maradhi hayo hasa nilipowaona walioambukizwa wakikondeana mthili ya ng’onda. Baada ya waathiriwa kufariki, jamaa zao hawakuruhusiwa kuwazika. Wizara ya afya ilitoa amri kali kuwa wale wore waliofariki kutokana na maradhi ya ukimwi wazikwe na kikundi maalum cha madaktari ma wauguzi wa hospitali za wilayani. Kulikuwa na kasisi mmoja tuliyehusiana kiukoo aliyefariki kutokana na maradhi ya ukimwi. Sisi hatukuruhusiwa hata kumsongea karibu marehemu alipoletwa nyumbani.
Madaktari na wauguzi walivalia majoho meupe ungedhani ni malaika. Mikononi walivaa glovu nyeupe ambazo zilitutisha machoni.
Mara nyingi nimeshangazwa na athari za ugonjwa huu. Inasemekana kuwa kuna njia kadha za usambazaji wa ugonjwa wa ukimwi. Njia moja ni kuhusika katika kitendo cha mapenzi na mtu ambaye ameambukizwa virusi vya ugonjwa huo. Njia nyingine nimeelezwa kuwa ni kwa kutumia kwa pamoja vifaa vyenye makali na mtu aliyeambukizwa virusi vya ukimwi. Inasemekana kuwa kugusa damu ya mtu aliyeambukizwa ugonjwa huo pia kunaweza kukutia mashakani.
Mama mja mzito aliyeambukizwa ugonjwa huu anaweza kumwambukiza mtoto aliye tumboni anapojifungua na hati baadaye anapomnyonyesha mtoto wake mchanga. Kisha kuna kupokea damu kutoka kwa mtu ambaye tayari ameambukizwa virusi hivyo. Yote hayo yanachangia pakubwa katika kututumbukiza kwenye janga hili la ukimwi.
Lakini nimewahi kusikia watu wakisema kuwa ukimwi si maradhi. Yaani ni
upungufu tu wa kinga ya kukabiliana na magoniwa katika mwili wa binadamu. Maadamu ukiweza kuimarisha kinga ya magonjwa katika mwili wako basi unaweza kuishi kwa miaka ma mikaka. Anachohitajika mtu ni apate chakula na lishe bora, afanye mazoezi ya kutosha, na kujiepusha na mahusiano ya kimapenzi na watu wenine ambao huenda wakamwambukiza aina tofauti tofauti za virusi vya ukimwi. Hayo yakifanyika mwathiriwa huwa na matumaini ya kuishi kwa muda mrefu kwani hatazidiwa na maradhi hayo na mwishowe kwenda jongomeo. Kuna haja kubwa ya kujilinda na kuepukana kabisa na janga hili lililotuzingira. Wengi tayari wameshapoteza roho zao. Wengine walioambukizwa wanaugua mahospitalini ma na majumbani mwao kisirisiri. Mungu atujalie heri na shari, kwani utafiti wote ambao umefanywa kuhusu tiba ya uwele huu haujafua dafu hata kidogo. Hata hivyo Mola hamtupi mja wake.

Maswali
a) Ipe habari hii anwani ifaayo.
b) Kwa nini mwandishi ana hofu sana ya maradhi ya ukimwi?
c)Hapo awali watu waliwachukulia vipi walioambukizwa maradhi ya Ukimwi?
d)Eleza njia mbalimbali zinazomfanya mtu kuambukizwa maradhi ya ukimwi .
e)Je, tunawezaje kuepukana na janga hili la ukimwi?
f)Eleza maana ya vifungu hivi vya maneno kama vilivyotumika katika taarifa.
i)Wauguzi
ii)Makali
iii)Virusi
iv)Uwele
v)Janga

  

Answers


Kavungya
a) Anwani – Hatari za ugonjwa wa Ukimwi.

b) Hofu – Kukonda sana kwa waathiriwa.
Awali waliofariki kutokana na ukimwi hawakuwa wakizikwa na jamaa zao

c) -Awali watu waliwaona wagonjwa hao kama waasi au wahalifu waliojiletea balaa.
- Walistahili kuepukwa kabisa kwa hofu ya kuwaambukiza wengine viini vya maradhi ya ukimwi.

d) - Kuhusika katika ngono na mtu aliyeambukizwa virusi vya ukimwi.
- Athari ya kuwa na wapenzi wengine.
- Matumizi ya vifaa vyenye makali na watu wenye virusi vya ukimwi.
- Mama mtu aweza kuzambaza viini hivyo kwa mtoto wake wakati anapojifungua na kumnyonyesha.
- Mtu anapotiwa damu yenye virusi vya ukimwi huambukizwa mara moja.

e)- Kutofanya mapenzi kiholela bila kutumia kinga yoyote.
-Kutoshirikiana na watu wanaougua ugonjwa huu katika matumizi ya vifaa vyenye makali.
-Kuwa waaminifu na kumcha Mwenyezi Mungu.

f)i ) Wauguzi – wanaowahudumia na kuwaangalia vizuri wagonjwa katika hospitali au zahanati.
ii)Makali – sehemu ya kifaa k.m kisu inayoweza kukata.
iii)Virusi – viini vinavyosababisha ugonjwa kama ukimwi.
iv)Ndwele – ugonjwa, maradhi
v)Janga – balaa, shida, tabu, matata.
Kavungya answered the question on October 29, 2019 at 08:18


Next: The reaction blow is a redox reaction
Previous: Consider the cell diagram below

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions