Ukeketaji wa mwanamke ni hali ya kudhuru sehemu ya uzazi ya mwanmke...

      

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali

Ukeketaji wa mwanamke ni hali ya kudhuru sehemu ya uzazi ya mwanmke kwa sababu zisizo za kimatibabu. Barani Afrika, ukeketaji ni jinamizi ambalo licha ya kampeni za kulimaliza limekuwa ndumakuwili.
Sababu kadha wa kadha zimetolewa na wanaoendeleza uhalifu huu kutetea hatua yao. wengi wao wanadai kwamba lengo la zoezi hilo huwa ni kudhibiti hisi za kimapenzi za mwanamke. Hii ni kutokana na thamani ya ubikira kabla ya ndoa au haja ya kudhibiti huba la ibana katika ndoa, hali ambazo huwafanya wadai kuwa ukeketaji humpunguzia mwanamke hamu ya kufanya mapenzi.
Yapo pia masuala ya kiitikadi, kwamba ukeketaji ni kigezo kikuu cha kumwingiza msichana katika kundi la wanawake na kuamua majukumu ambayo mwanamke husika atapewa katika maisha ya baadaye na maisha ya ndoa. Wengine wao waniendeleza shughuli hii kwa misingi ya itikadi za kidini.
Mbali na visingizio – ni visingizio kwa kuwa havina mashiko – vinavyotolewa na jamii zinazoeendeleza uhalifu huu dhidi ya mwanamke, yapo madhara mengi san yanayotokana na kitendo cha kumkeketa mwanamke. Moja ni kwamba mhusika huweza kufariki kwa kupoteza damu nyingi au kupatwa na maumivu makali yanayoweza kuathii mfumo wake wa mwili. Aidha, anaweza kupatwa na ugonjwa wa anemia.
Mwathiriwa wa ukeketaji anaweza pia akakubwa na matatizo ya kwenda haja ndogo, hasa kwa kubana mkojo kwa kuogopa uchungu. Hali hii inaweza kusababisha maradhi katika kibofu na sehemu za kupitsha mkojo.
Pamoja na hayo, matumizi ya kijembe au kisu kichafu, tena kwa zaidi ya mtu mmoja katika mazingira machafu kunaweza kusababisha maambukizi ya maradhi mengine kama vile, virusi vinavyosababisha ukimwi au magonjwa mengine ya kuambukiza. Magonjwa kama hayo yanaweza pia kusababisha matatizo katika mfupa wa uzazi na baadaye kusababisha kusumishwa kwa damu. Hali hiyo ikikosa kupata tiba (isipokuwa ukimwi ambao hauna tiba), mhusika anaweza kuishia kufa.

Maswali
a)Fupisha kwa maneno 64 – 69 ujumbe wa aya tatu za kwanza
Matayarisho
Jibu
b)Kwa maneno 40 – 45, eleza madhara ya ukeketaji kwa wanawake.
Matayarisho
Jibu

  

Answers


Kavungya
a)
i) Ukeketaji ni hali ya kudhuru sehemu ya uzazi ya mwanamke kwa sababu zisizo za kimatibabu.
ii) Ukeketaji ni jinamizi barani Afrika licha ya kampeni za kulimaliza.
iii) Ukeketaji unadaiwa kulenga kudhibiti hisia za kimapenzi za mwanamke na kuzuia kuwa na huba la ibana.
iv) Kiitikadi ukeketaji unadaiwa kuwa kigezo cha kumwingiza msichana katika kundi la wanawake.
v) Ukeketaji unachangia maamuzi ya majukumu anayopewa mwanamke.
vi) Ukeketaji pia unaendelezwa kwa misingi ya kidini.

b)
i) Mhusika huweza kufariki kwa kupoteza damu nyingi.
ii) Maumivu makali yanayoweza kuathiri mfumo wa mwili.
iii) Ugonjwa wa anemia
iv) Matatizo ya kwenda haja ndogo na maradhi ya kibofu
v) Ukimwi au magonjwa ya kuambukiza
vi) Matatizo katika mfupa wa uzazi.
vii) Kusumishwa kwa damu
viii) Kifo
Kavungya answered the question on October 29, 2019 at 08:38


Next: Consider the cell diagram below
Previous: Taja mfano mmoja kwa kila aina ya sauti zifuatazo; Kipasuo-kwamizo – Irabu ya nyuma wastani -

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions