Taja mfano mmoja kwa kila aina ya sauti zifuatazo; Kipasuo-kwamizo – Irabu ya nyuma wastani -

      

Taja mfano mmoja kwa kila aina ya sauti zifuatazo;
Kipasuo-kwamizo –
Irabu ya nyuma wastani -

  

Answers


Kavungya
Kipasuo – Kwamizo = /ch/
Irabu ya nyuma wastani = /o/
Kavungya answered the question on October 29, 2019 at 08:52


Next: Ukeketaji wa mwanamke ni hali ya kudhuru sehemu ya uzazi ya mwanmke...
Previous: Study the standard electrode potential for the half-cells given below and answer the questions that follow.(The letter do not represent the actual symbols of the...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions


  • Ukeketaji wa mwanamke ni hali ya kudhuru sehemu ya uzazi ya mwanmke...(Solved)

    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali

    Ukeketaji wa mwanamke ni hali ya kudhuru sehemu ya uzazi ya mwanmke kwa sababu zisizo za kimatibabu. Barani Afrika, ukeketaji ni jinamizi ambalo licha ya kampeni za kulimaliza limekuwa ndumakuwili.
    Sababu kadha wa kadha zimetolewa na wanaoendeleza uhalifu huu kutetea hatua yao. wengi wao wanadai kwamba lengo la zoezi hilo huwa ni kudhibiti hisi za kimapenzi za mwanamke. Hii ni kutokana na thamani ya ubikira kabla ya ndoa au haja ya kudhibiti huba la ibana katika ndoa, hali ambazo huwafanya wadai kuwa ukeketaji humpunguzia mwanamke hamu ya kufanya mapenzi.
    Yapo pia masuala ya kiitikadi, kwamba ukeketaji ni kigezo kikuu cha kumwingiza msichana katika kundi la wanawake na kuamua majukumu ambayo mwanamke husika atapewa katika maisha ya baadaye na maisha ya ndoa. Wengine wao waniendeleza shughuli hii kwa misingi ya itikadi za kidini.
    Mbali na visingizio – ni visingizio kwa kuwa havina mashiko – vinavyotolewa na jamii zinazoeendeleza uhalifu huu dhidi ya mwanamke, yapo madhara mengi san yanayotokana na kitendo cha kumkeketa mwanamke. Moja ni kwamba mhusika huweza kufariki kwa kupoteza damu nyingi au kupatwa na maumivu makali yanayoweza kuathii mfumo wake wa mwili. Aidha, anaweza kupatwa na ugonjwa wa anemia.
    Mwathiriwa wa ukeketaji anaweza pia akakubwa na matatizo ya kwenda haja ndogo, hasa kwa kubana mkojo kwa kuogopa uchungu. Hali hii inaweza kusababisha maradhi katika kibofu na sehemu za kupitsha mkojo.
    Pamoja na hayo, matumizi ya kijembe au kisu kichafu, tena kwa zaidi ya mtu mmoja katika mazingira machafu kunaweza kusababisha maambukizi ya maradhi mengine kama vile, virusi vinavyosababisha ukimwi au magonjwa mengine ya kuambukiza. Magonjwa kama hayo yanaweza pia kusababisha matatizo katika mfupa wa uzazi na baadaye kusababisha kusumishwa kwa damu. Hali hiyo ikikosa kupata tiba (isipokuwa ukimwi ambao hauna tiba), mhusika anaweza kuishia kufa.

    Maswali
    a)Fupisha kwa maneno 64 – 69 ujumbe wa aya tatu za kwanza
    Matayarisho
    Jibu
    b)Kwa maneno 40 – 45, eleza madhara ya ukeketaji kwa wanawake.
    Matayarisho
    Jibu

    Date posted: October 29, 2019.  Answers (1)

  • Nilianza kusikia habari za ugonjwa wa ukimwi mnamo mwaka wa 1984. Wakati huo nilikuwa nimemaliza masomo yangu ya kidato...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali

    Nilianza kusikia habari za ugonjwa wa ukimwi mnamo mwaka wa 1984. Wakati huo nilikuwa nimemaliza masomo yangu ya kidato cha sita na kujiunga ia chuo cha walimu kilichoko wilayani Nyeri kiitwacho Kagumo. Nilihofu sana maradhi hayo hasa nilipowaona walioambukizwa wakikondeana mthili ya ng’onda. Baada ya waathiriwa kufariki, jamaa zao hawakuruhusiwa kuwazika. Wizara ya afya ilitoa amri kali kuwa wale wore waliofariki kutokana na maradhi ya ukimwi wazikwe na kikundi maalum cha madaktari ma wauguzi wa hospitali za wilayani. Kulikuwa na kasisi mmoja tuliyehusiana kiukoo aliyefariki kutokana na maradhi ya ukimwi. Sisi hatukuruhusiwa hata kumsongea karibu marehemu alipoletwa nyumbani.
    Madaktari na wauguzi walivalia majoho meupe ungedhani ni malaika. Mikononi walivaa glovu nyeupe ambazo zilitutisha machoni.
    Mara nyingi nimeshangazwa na athari za ugonjwa huu. Inasemekana kuwa kuna njia kadha za usambazaji wa ugonjwa wa ukimwi. Njia moja ni kuhusika katika kitendo cha mapenzi na mtu ambaye ameambukizwa virusi vya ugonjwa huo. Njia nyingine nimeelezwa kuwa ni kwa kutumia kwa pamoja vifaa vyenye makali na mtu aliyeambukizwa virusi vya ukimwi. Inasemekana kuwa kugusa damu ya mtu aliyeambukizwa ugonjwa huo pia kunaweza kukutia mashakani.
    Mama mja mzito aliyeambukizwa ugonjwa huu anaweza kumwambukiza mtoto aliye tumboni anapojifungua na hati baadaye anapomnyonyesha mtoto wake mchanga. Kisha kuna kupokea damu kutoka kwa mtu ambaye tayari ameambukizwa virusi hivyo. Yote hayo yanachangia pakubwa katika kututumbukiza kwenye janga hili la ukimwi.
    Lakini nimewahi kusikia watu wakisema kuwa ukimwi si maradhi. Yaani ni
    upungufu tu wa kinga ya kukabiliana na magoniwa katika mwili wa binadamu. Maadamu ukiweza kuimarisha kinga ya magonjwa katika mwili wako basi unaweza kuishi kwa miaka ma mikaka. Anachohitajika mtu ni apate chakula na lishe bora, afanye mazoezi ya kutosha, na kujiepusha na mahusiano ya kimapenzi na watu wenine ambao huenda wakamwambukiza aina tofauti tofauti za virusi vya ukimwi. Hayo yakifanyika mwathiriwa huwa na matumaini ya kuishi kwa muda mrefu kwani hatazidiwa na maradhi hayo na mwishowe kwenda jongomeo. Kuna haja kubwa ya kujilinda na kuepukana kabisa na janga hili lililotuzingira. Wengi tayari wameshapoteza roho zao. Wengine walioambukizwa wanaugua mahospitalini ma na majumbani mwao kisirisiri. Mungu atujalie heri na shari, kwani utafiti wote ambao umefanywa kuhusu tiba ya uwele huu haujafua dafu hata kidogo. Hata hivyo Mola hamtupi mja wake.

    Maswali
    a) Ipe habari hii anwani ifaayo.
    b) Kwa nini mwandishi ana hofu sana ya maradhi ya ukimwi?
    c)Hapo awali watu waliwachukulia vipi walioambukizwa maradhi ya Ukimwi?
    d)Eleza njia mbalimbali zinazomfanya mtu kuambukizwa maradhi ya ukimwi .
    e)Je, tunawezaje kuepukana na janga hili la ukimwi?
    f)Eleza maana ya vifungu hivi vya maneno kama vilivyotumika katika taarifa.
    i)Wauguzi
    ii)Makali
    iii)Virusi
    iv)Uwele
    v)Janga

    Date posted: October 29, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana ya istilahi zifuatazo za isimu jamii. i)Lugha ya taifa (ii)Lugha ya ishara (iii)Lugha mwiko (iv)Sajili za lugha (v)Uchanganyaji msimbo.(Solved)

    Eleza maana ya istilahi zifuatazo za isimu jamii.
    i)Lugha ya taifa
    (ii)Lugha ya ishara
    (iii)Lugha mwiko
    (iv)Sajili za lugha
    (v)Uchanganyaji msimbo.

    Date posted: October 21, 2019.  Answers (1)

  • ISIMU JAMII Ali: Wee kuja hapa. Wewe ni nani? Sema haraka! Ebo: Mimi … ni … afande ni Ebo Ali: Unatoka wapi sa ii? Hapa hakuna sheria? Ebo:...(Solved)

    ISIMU JAMII
    Ali: Wee kuja hapa. Wewe ni nani? Sema haraka!
    Ebo: Mimi … ni … afande ni Ebo
    Ali: Unatoka wapi sa ii? Hapa hakuna sheria?
    Ebo: Samahani mkubwa. Mimi niku…
    Ali: Mkubwa wa nani? Wakubwa wako ofisini.
    Ebo: Pole mzee.
    Ali: Mzee gani? Hii mtu lazima niiwekwa store. Yaani self-contained.
    Toa viatu.
    Ebo: Tafadhali Bwana Askari, nilichelewa …
    Ali: Mimi sitaki hadithi! Hizo pelekea nyanya yako, eh. Fanya haraka!
    Ebo: Naomba mkubwa …
    Ali: Hapa si kanisani. Unaomba! Hata …

    Fafanua sifa tano za sajili hii.

    Date posted: October 21, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana ya nomino.(Solved)

    Eleza maana ya nomino.

    Date posted: October 21, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana tatu zinazopatikana katika sentensi hii. Alikuwa amenijuza kuwa angefika kwao.(Solved)

    Eleza maana tatu zinazopatikana katika sentensi hii.
    Alikuwa amenijuza kuwa angefika kwao.

    Date posted: October 21, 2019.  Answers (1)

  • Eleza matumizi ya kwa katika sentensi hii. Kwa nini umeishi kwao kwa miaka mingi?(Solved)

    Eleza matumizi ya kwa katika sentensi hii.
    Kwa nini umeishi kwao kwa miaka mingi?

    Date posted: October 21, 2019.  Answers (1)

  • Tumia kivumishi kionyeshi cha karibu pamoja na nomino katika ngeli ya I-ZI kisha utunge sentensi katika ukubwa - wingi.(Solved)

    Tumia kivumishi kionyeshi cha karibu pamoja na nomino katika ngeli ya I-ZI kisha utunge sentensi katika ukubwa - wingi.

    Date posted: October 21, 2019.  Answers (1)

  • Onyesha aina tofauti za shamirisho katika sentensi hii. Ali alimnunulia Asha viatu kwa pesa zake. (Solved)

    Onyesha aina tofauti za shamirisho katika sentensi hii.
    Ali alimnunulia Asha viatu kwa pesa zake.

    Date posted: October 21, 2019.  Answers (1)

  • Eleza dhana ya shamirisho.(Solved)

    Eleza dhana ya shamirisho.

    Date posted: October 21, 2019.  Answers (1)

  • Nyambua kitenzi ja katika kauli ya kutendewa kisha utunge sentensi.(Solved)

    Nyambua kitenzi ja katika kauli ya kutendewa kisha utunge sentensi.

    Date posted: October 21, 2019.  Answers (1)

  • Weka kirejeshi ‘O’ tamati kwenye kitenzi chunga kisha ukitungie sentensi.(Solved)

    Weka kirejeshi ‘O’ tamati kwenye kitenzi chunga kisha ukitungie sentensi.

    Date posted: October 21, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi moja kubainisha matumizi ya ‘na’ kama. (i)Kihusishi cha ‘na’ ya mtenda. (ii)Kiunganishi(Solved)

    Tunga sentensi moja kubainisha matumizi ya ‘na’ kama.
    (i)Kihusishi cha ‘na’ ya mtenda.
    (ii)Kiunganishi

    Date posted: October 21, 2019.  Answers (1)

  • Tumia mzizi –w- katika sentensi kama: (i)Kitenzi kisaidizi. (ii)Kitenzi Kishirikishi.(Solved)

    Tumia mzizi –w- katika sentensi kama:
    (i)Kitenzi kisaidizi.
    (ii)Kitenzi Kishirikishi.

    Date posted: October 21, 2019.  Answers (1)

  • Sahihisha sentensi ifuatayo. Mtu ambaye aliyechukua kitabu chenye kilikuwa hapa arudishe. (Solved)

    Sahihisha sentensi ifuatayo.
    Mtu ambaye aliyechukua kitabu chenye kilikuwa hapa arudishe.

    Date posted: October 18, 2019.  Answers (1)

  • Onyesha vishazi katika sentensi ifuatayo kisha uelezee ni vya aina gani. Ajapo tutamlaki kwa shangwe.(Solved)

    Onyesha vishazi katika sentensi ifuatayo kisha uelezee ni vya aina gani.
    Ajapo tutamlaki kwa shangwe.

    Date posted: October 18, 2019.  Answers (1)

  • Andika kwa msemo wa taarifa: Askari: Ulikuwa unaelekea wapi uliposhambuliwa? Jirani: Nilikuwa nikienda sokoni jana. (Solved)

    Andika kwa msemo wa taarifa:
    Askari: Ulikuwa unaelekea wapi uliposhambuliwa?
    Jirani: Nilikuwa nikienda sokoni jana.

    Date posted: October 18, 2019.  Answers (1)

  • Neno lifuatalo liko katika ngeli gani? Matukio (Solved)

    Neno lifuatalo liko katika ngeli gani?
    Matukio

    Date posted: October 18, 2019.  Answers (1)

  • Viambishi vilivyopigiwa mstari vinawakilisha dhana zipi za kisarufi? i)Udhaifu ii)Walani? (Solved)

    Viambishi vilivyopigiwa mstari vinawakilisha dhana zipi za kisarufi?
    i)Udhaifu
    ii)Walani?

    Date posted: October 18, 2019.  Answers (1)

  • Eleza ni kwa nini neno umma ni la asili ya kigeni.(Solved)

    Eleza ni kwa nini neno umma ni la asili ya kigeni.

    Date posted: October 18, 2019.  Answers (1)