Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Fafanua sababu tatu zilizochochea usanifishaji wa lugha ya Kiswahili kabla ya uhuru .

      

Fafanua sababu tatu zilizochochea usanifishaji wa lugha ya Kiswahili kabla ya uhuru .

  

Answers


Kavungya
1)Haja ya Kiswahili kutumika katika shughuli rasmi za kielimu katika ngazi za kitaifa na kimataifa.
2)Haja ya kutumia Kiswahili katika idhaa za kupeperusha matangazo katika BBC, Avoa, Radio China na idhaa za hapa maeneo ya Afrika mashariki.
3)Haja ya kutumia Kiswahili katika shughuli za kibiashara na kisiasa katika Afrika mahsariki na kote duniani.
4)Kwingine kama Tanzania Kiswahili kilihitajika kutumika kuendesha shughuli bungeni.
5)Katika uandishi wa majarida, magazeti na vitabu.
6)Kiswahili kilihitajika kama lugha rasmi katika muungano wa Afrika mashariki.
Kavungya answered the question on October 29, 2019 at 10:08


Next: Eleza mambo manne yaliyochangia kuenea kwa lugha ya Kiswahili kabla ya uhuru wa mataifa ya Afrika mashariki .
Previous: Study carefully the information given below and answer the questions that follow:-

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • Eleza mambo manne yaliyochangia kuenea kwa lugha ya Kiswahili kabla ya uhuru wa mataifa ya Afrika mashariki .(Solved)

    Eleza mambo manne yaliyochangia kuenea kwa lugha ya Kiswahili kabla ya uhuru wa mataifa ya Afrika mashariki .

    Date posted: October 29, 2019.  Answers (1)

  • Tambua hali na nyakati katika sentensi ifuatayo Atakuwa ameondoka utakapofika. (Solved)

    Tambua hali na nyakati katika sentensi ifuatayo
    Atakuwa ameondoka utakapofika.

    Date posted: October 29, 2019.  Answers (1)

  • Geuza sentensi ifuatayo kwa kutumia kirejeshi ‘AMBA’ Mti uzaao matunda mengi ulikatwa jana (Solved)

    Geuza sentensi ifuatayo kwa kutumia kirejeshi ‘AMBA’
    Mti uzaao matunda mengi ulikatwa jana

    Date posted: October 29, 2019.  Answers (1)

  • Unda sentensi yenye muundo ufuatao. T+E+H+N+T+E (Solved)

    Unda sentensi yenye muundo ufuatao.
    T+E+H+N+T+E

    Date posted: October 29, 2019.  Answers (1)

  • Ainisha vitenzi vilivyopigiwa mstari Niliwahi kumwona kifaru. Niliwahi gari hilo la asubuhi. (Solved)

    Ainisha vitenzi vilivyopigiwa mstari
    Niliwahi kumwona kifaru.
    Niliwahi gari hilo la asubuhi.

    Date posted: October 29, 2019.  Answers (1)

  • Toa visawe viwili vya ‘uchochole’ (Solved)

    Toa visawe viwili vya ‘uchochole’

    Date posted: October 29, 2019.  Answers (1)

  • Kanusha sentensi ifuatayo: Aimbapo vizuri mtuze (Solved)

    Kanusha sentensi ifuatayo:
    Aimbapo vizuri mtuze

    Date posted: October 29, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha maana mbili zinazojitokeza katika sentensi hii Mshikie mtoto. (Solved)

    Bainisha maana mbili zinazojitokeza katika sentensi hii
    Mshikie mtoto.

    Date posted: October 29, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi ifuatayo katika hali ya ukubwa Paka huyu aliguguna mfupa wa mtoto huyu. (Solved)

    Andika sentensi ifuatayo katika hali ya ukubwa
    Paka huyu aliguguna mfupa wa mtoto huyu.

    Date posted: October 29, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi mbili kudhihirisha matumizi ya virai vifuatavyo na uvipigie mstari a)Kirai Nomino b)Kirai kivumishi (Solved)

    Tunga sentensi mbili kudhihirisha matumizi ya virai vifuatavyo na uvipigie mstari
    a)Kirai Nomino
    b)Kirai kivumishi

    Date posted: October 29, 2019.  Answers (1)

  • Tambua kiima na kiarifa katika sentensi hii(Solved)

    Tambua kiima na kiarifa katika sentensi hii

    Taa yake inatoa moshi mwingi

    Date posted: October 29, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi ifuatayo katika hali ya kutenda Alikatwa mkono na jizi lile (Solved)

    Andika sentensi ifuatayo katika hali ya kutenda
    Alikatwa mkono na jizi lile

    Date posted: October 29, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi ukitumia neno katika ngeli ya YA-YA. (Solved)

    Tunga sentensi ukitumia neno katika ngeli ya YA-YA.

    Date posted: October 29, 2019.  Answers (1)

  • Andika katika usemi halisi Mwelekezi alimwambia Loisi kuwa safari yao ingekamilika siku iliyofuata. (Solved)

    Andika katika usemi halisi
    Mwelekezi alimwambia Loisi kuwa safari yao ingekamilika siku iliyofuata.

    Date posted: October 29, 2019.  Answers (1)

  • Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi . Mtoto alipoumia alitibiwa haraka sana. (Solved)

    Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi .
    Mtoto alipoumia alitibiwa haraka sana.

    Date posted: October 29, 2019.  Answers (1)

  • Yakinisha katika nafsi ya pili wingi sitakusomea kitabu hicho (Solved)

    Yakinisha katika nafsi ya pili wingi
    sitakusomea kitabu hicho

    Date posted: October 29, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha shamirisho katika sentensi hii Mpishi alikatiwa kuni kwa shoka na mpasua kuni. (Solved)

    Bainisha shamirisho katika sentensi hii
    Mpishi alikatiwa kuni kwa shoka na mpasua kuni.

    Date posted: October 29, 2019.  Answers (1)

  • Taja mfano mmoja kwa kila aina ya sauti zifuatazo; Kipasuo-kwamizo – Irabu ya nyuma wastani - (Solved)

    Taja mfano mmoja kwa kila aina ya sauti zifuatazo;
    Kipasuo-kwamizo –
    Irabu ya nyuma wastani -

    Date posted: October 29, 2019.  Answers (1)

  • Ukeketaji wa mwanamke ni hali ya kudhuru sehemu ya uzazi ya mwanmke...(Solved)

    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali

    Ukeketaji wa mwanamke ni hali ya kudhuru sehemu ya uzazi ya mwanmke kwa sababu zisizo za kimatibabu. Barani Afrika, ukeketaji ni jinamizi ambalo licha ya kampeni za kulimaliza limekuwa ndumakuwili.
    Sababu kadha wa kadha zimetolewa na wanaoendeleza uhalifu huu kutetea hatua yao. wengi wao wanadai kwamba lengo la zoezi hilo huwa ni kudhibiti hisi za kimapenzi za mwanamke. Hii ni kutokana na thamani ya ubikira kabla ya ndoa au haja ya kudhibiti huba la ibana katika ndoa, hali ambazo huwafanya wadai kuwa ukeketaji humpunguzia mwanamke hamu ya kufanya mapenzi.
    Yapo pia masuala ya kiitikadi, kwamba ukeketaji ni kigezo kikuu cha kumwingiza msichana katika kundi la wanawake na kuamua majukumu ambayo mwanamke husika atapewa katika maisha ya baadaye na maisha ya ndoa. Wengine wao waniendeleza shughuli hii kwa misingi ya itikadi za kidini.
    Mbali na visingizio – ni visingizio kwa kuwa havina mashiko – vinavyotolewa na jamii zinazoeendeleza uhalifu huu dhidi ya mwanamke, yapo madhara mengi san yanayotokana na kitendo cha kumkeketa mwanamke. Moja ni kwamba mhusika huweza kufariki kwa kupoteza damu nyingi au kupatwa na maumivu makali yanayoweza kuathii mfumo wake wa mwili. Aidha, anaweza kupatwa na ugonjwa wa anemia.
    Mwathiriwa wa ukeketaji anaweza pia akakubwa na matatizo ya kwenda haja ndogo, hasa kwa kubana mkojo kwa kuogopa uchungu. Hali hii inaweza kusababisha maradhi katika kibofu na sehemu za kupitsha mkojo.
    Pamoja na hayo, matumizi ya kijembe au kisu kichafu, tena kwa zaidi ya mtu mmoja katika mazingira machafu kunaweza kusababisha maambukizi ya maradhi mengine kama vile, virusi vinavyosababisha ukimwi au magonjwa mengine ya kuambukiza. Magonjwa kama hayo yanaweza pia kusababisha matatizo katika mfupa wa uzazi na baadaye kusababisha kusumishwa kwa damu. Hali hiyo ikikosa kupata tiba (isipokuwa ukimwi ambao hauna tiba), mhusika anaweza kuishia kufa.

    Maswali
    a)Fupisha kwa maneno 64 – 69 ujumbe wa aya tatu za kwanza
    Matayarisho
    Jibu
    b)Kwa maneno 40 – 45, eleza madhara ya ukeketaji kwa wanawake.
    Matayarisho
    Jibu

    Date posted: October 29, 2019.  Answers (1)

  • Nilianza kusikia habari za ugonjwa wa ukimwi mnamo mwaka wa 1984. Wakati huo nilikuwa nimemaliza masomo yangu ya kidato...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali

    Nilianza kusikia habari za ugonjwa wa ukimwi mnamo mwaka wa 1984. Wakati huo nilikuwa nimemaliza masomo yangu ya kidato cha sita na kujiunga ia chuo cha walimu kilichoko wilayani Nyeri kiitwacho Kagumo. Nilihofu sana maradhi hayo hasa nilipowaona walioambukizwa wakikondeana mthili ya ng’onda. Baada ya waathiriwa kufariki, jamaa zao hawakuruhusiwa kuwazika. Wizara ya afya ilitoa amri kali kuwa wale wore waliofariki kutokana na maradhi ya ukimwi wazikwe na kikundi maalum cha madaktari ma wauguzi wa hospitali za wilayani. Kulikuwa na kasisi mmoja tuliyehusiana kiukoo aliyefariki kutokana na maradhi ya ukimwi. Sisi hatukuruhusiwa hata kumsongea karibu marehemu alipoletwa nyumbani.
    Madaktari na wauguzi walivalia majoho meupe ungedhani ni malaika. Mikononi walivaa glovu nyeupe ambazo zilitutisha machoni.
    Mara nyingi nimeshangazwa na athari za ugonjwa huu. Inasemekana kuwa kuna njia kadha za usambazaji wa ugonjwa wa ukimwi. Njia moja ni kuhusika katika kitendo cha mapenzi na mtu ambaye ameambukizwa virusi vya ugonjwa huo. Njia nyingine nimeelezwa kuwa ni kwa kutumia kwa pamoja vifaa vyenye makali na mtu aliyeambukizwa virusi vya ukimwi. Inasemekana kuwa kugusa damu ya mtu aliyeambukizwa ugonjwa huo pia kunaweza kukutia mashakani.
    Mama mja mzito aliyeambukizwa ugonjwa huu anaweza kumwambukiza mtoto aliye tumboni anapojifungua na hati baadaye anapomnyonyesha mtoto wake mchanga. Kisha kuna kupokea damu kutoka kwa mtu ambaye tayari ameambukizwa virusi hivyo. Yote hayo yanachangia pakubwa katika kututumbukiza kwenye janga hili la ukimwi.
    Lakini nimewahi kusikia watu wakisema kuwa ukimwi si maradhi. Yaani ni
    upungufu tu wa kinga ya kukabiliana na magoniwa katika mwili wa binadamu. Maadamu ukiweza kuimarisha kinga ya magonjwa katika mwili wako basi unaweza kuishi kwa miaka ma mikaka. Anachohitajika mtu ni apate chakula na lishe bora, afanye mazoezi ya kutosha, na kujiepusha na mahusiano ya kimapenzi na watu wenine ambao huenda wakamwambukiza aina tofauti tofauti za virusi vya ukimwi. Hayo yakifanyika mwathiriwa huwa na matumaini ya kuishi kwa muda mrefu kwani hatazidiwa na maradhi hayo na mwishowe kwenda jongomeo. Kuna haja kubwa ya kujilinda na kuepukana kabisa na janga hili lililotuzingira. Wengi tayari wameshapoteza roho zao. Wengine walioambukizwa wanaugua mahospitalini ma na majumbani mwao kisirisiri. Mungu atujalie heri na shari, kwani utafiti wote ambao umefanywa kuhusu tiba ya uwele huu haujafua dafu hata kidogo. Hata hivyo Mola hamtupi mja wake.

    Maswali
    a) Ipe habari hii anwani ifaayo.
    b) Kwa nini mwandishi ana hofu sana ya maradhi ya ukimwi?
    c)Hapo awali watu waliwachukulia vipi walioambukizwa maradhi ya Ukimwi?
    d)Eleza njia mbalimbali zinazomfanya mtu kuambukizwa maradhi ya ukimwi .
    e)Je, tunawezaje kuepukana na janga hili la ukimwi?
    f)Eleza maana ya vifungu hivi vya maneno kama vilivyotumika katika taarifa.
    i)Wauguzi
    ii)Makali
    iii)Virusi
    iv)Uwele
    v)Janga

    Date posted: October 29, 2019.  Answers (1)