Siku ya Alhamisi tarehe 4 Disemba 2014 Umoja wa Mataifa ulitoa ripoti ukitahadharisha juu yakuongezeka vitendo vya ghasia na mauaji...

      

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali

Siku ya Alhamisi tarehe 4 Disemba 2014 Umoja wa Mataifa ulitoa ripoti ukitahadharisha juu ya
kuongezeka vitendo vya ghasia na mauaji nchini Kenya. Ripoti hiyo inasema kuwa katika kipindi cha
miaka miwili iliyopita watu zaidi ya 300 wameuawa na wengine takribani 220,000 kulazimika kuishi kama
wakimbizi kutokana na ghasia hizo. Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu wa Umoja huo amesema kuwa
ukame mkubwa na mivutano inayotokana na siasa za kuhamishia madaraka mashinani ni baadhi ya
mambo yanayochangia kuongezeka vitendo vya ghasia na mapigano katika maeneo ya kaskazini na ya
mbali nchini Kenya. Ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa wizi wa mifugo na mauaji ya kulipiza
kisasi kati ya jamii hasimu za wafugaji katika maeneo hayo ni jambo la kawaida na kwamba silaha
ndogondogo zinapatikana kwa wingi kati ya jamii hizo. Ugomvi wa kuwania ardhi, malisho, vyanzo vya
maji na madaraka ya kisiasa mwaka huu umewafanya raia wengi katika maeneo ya kaskazini mwa Kenya
kuwa wakimbizi katika nchi yao wenyewe. Kwa kadiri kwamba idadi ya wakimbizi hao imeongezeka
mara nne zaidi ikilinganishwa na ya mwaka uliopita wa 2013.
Mbali na matatizo ya ndani yanayotokana na ukame na ugomvi wa kikabila, mashambulio ya kundi
la kigaidi la al- Shabaab ni jambo jingine ambalo linahatarisha usalama wa Kenya. Kundi hilo Jumapili
iliyopita lilitangaza kuhusika na bomu lililolipuka katika soko moja huko mjini Garissa, mashariki mwa
Kenya karibu na mpaka wa nchi hiyo na Somalia. Kundi hilohilo lilihusika na mauaji ya abiria 28
waliokuwa kwenye basi moja la shirika la usafiri la Makka lililokuwa njiani kutoka mjini Mandera
kaskazini mwa nchi kuelekea mji mkuu Nairobi. Siku 10 baadaye kundi hilo hilo la kigaidi lilivamia na
kuwafyatulia risasi kinyama wafanyakazi 36 wa machimbo ya mawe katika kijiji cha Koromey kilicho nje
kidogo ya mji huo wa Mandera.
Katika tukio jingine la mashambulio ya kundi la al- Shabaab katika maeneo yanayopakana na
Somalia, siku ya Jumatatu iliyopita kundi hilo lilishambulia klabu ya Ngamia mjini Wajir na kuwafatulia
risasi kiholela watu waliokuwa katika klabu hiyo ambapo waliua mmoja kati yao na kuwajeruhi wengine
13. Visa hivyo vya machafuko na ukosefu wa usalama vilimpelekea Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
Jumanne iliyopita kuwafuta kazi Waziri wa Mambo ya Usalama wa Ndani pamoja na Inspekta Mkuu wa
polisi ya nchi hiyo. Kufuatia matukio hayo, vyombo vya usalama vya Kenya vimezidisha hatua za
kiusalama nchini ili kuzuia kukaririwa kwa matukio kama hayo ya utovu wa nidhamu na usalama. Mbali na
hayo mwaka uliopita kundi la al- Shabaab lilishambulia na kusababisha maafa na hasara kubwa katika
jengo la maduka ya kibiashara la West Gate mjini Nairobi. Al- Shabaab linapigana na kikosi cha askari wa
kulinda amani cha Umoja wa Afrika kinachohudumu huko Somalia AMISOM na limekuwa likitekeleza
mashambulio ya kigaidi nchini Kenya kama alama ya kulalamikia ushiriki wa nchi hiyo katika kikosi
hicho, ili hatimaye liilazimishe iondoe askari wake katika radhi ya nchi hiyo.

1. Yape makala haya kichwa mwafaka.
2. Taja matatizo manne ya ndani kwa ndani ambayo yanahatarisha usalama wa Kenya.(alama 2)
3. Taja matukio matatu yaliyomfanya rais awapige kalamu waziri na inspekta mkuu wa polisi (alama 3)
4. Eleza sababu wanayotoa wana al-Shabaab ya kutekeleza ukatili dhidi ya Wakenya. (Alama 2)
5. Eleza dhamira ya kikundi cha al-Shabaab
6. Kwa maoni yako mwenyewe, Eleza mambo matatu ambayo anayevamiwa na kundi la al-shabaab
anaweza kufanya ili kujiokoa na kuokoa wengine.
7. Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika kufungu.
a) Radhi
b) Wakimbizi

  

Answers


Kavungya
1.Ugaidi/ visa vya mauaji. Mwalimu atathmini jibu la mwanafunzi
2.Ukame
Mivutano ya kisiasa
Wizi wa mifugo
Mauaji ya kulipiza kisasi
Kupatikana kwa silaha ndogo ndogo
Ugomvi wa kuwania ardhi, malisho, vyanzo vya maji na madaraka.
3.Kulipuliwa kwa soko moja Garrissa
Mauaji ya abiria
Kuuliwa kwa wafanyikazi wa machimbo 36
Ushambulizi wa klabu ya Ngamia mjini Wajir
Ushambulizi wa West- gate
4.Ushiriki wan chi hiyo katika kikosi cha AMISOM
5.Kuondoa Askari wa Kenya katika ardhi ya somalia.
6.Kujificha
Kukimbia
Kupigana
7.(a) radhi - Baraka
(b) Wakimbizi – watu waliohamishwa kwao.
Kavungya answered the question on October 31, 2019 at 06:06


Next: Cheptoo set-up some apparatus as shown in the diagram below:-
Previous: The diagram below shows a Zinc –copper cell.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions