Historia na fasihi zina uhusiano wa karibu sana hasa fasihi ya kihistoria. Hata hivyo fasihi siohistoria na historia si fasihi kwa...

      

UHUSIANO WA FASIHI NA HISTORIA

Historia na fasihi zina uhusiano wa karibu sana hasa fasihi ya kihistoria. Hata hivyo fasihi sio
historia na historia si fasihi kwa sababu hizi ni taaluma mbili ambazo zina uhusiano tu. Hata hivyo, fasihi
na historia zina mambo ambayo yanafana na yale ambayo hayafanani.
Kati ya mambo ambayo yanafanana ni kwamba fasihi na historia wakati mwingine huweza kuwa
na wahusika ambao wanafanana kitabia, kimaumbile na hata wakati mwingine matendo ya kukumbukwa
waliyofanywa. Mfano ni katika shairi la “Hongera Rais Moi” katika diwani ya ' Malenga wa ziwa kuu'
ambapo mhusika ni rais Moi na mhusika kama yule pia aliishi katika kipindi Fulani katika nchi ya Kenya.
Jambo jingine ambalo linapatikana katika fasihi na pia kinaoana na historia ni mandhari. Wakati
mwingine, mandhari ambayo ni ya kihistoria yanakaribiana sana na ya kifasihi na hata wakati mwingine
kufanana. Mandhari ya shamba la bwana Delamon katika 'kilio cha haki' yanaweza kuwa shamba lolote na
mabwanyenye kama hata ni ya Bwana Dalamere.
Wakati mwingine matukio katika fasihi huwa karibu sawa na yale ambayo yanapatikana katika
historia ya kawaida. Mfano katika shairi la ' wasifu wa baba Kenyatta', mhusika mkuu yasemekana
alipigania uhuru wa nchi ambayo aliiongoza. Matukio kama kufungwa jela ambayo mhusika huyu
anapitia katika kujaribu kukomboa nchi ni sawa na yale ambayo mhusika wa kihistoria ambaye ni rais wa
kwanza wa nchi ya Kenya.
Pia, wakati mwingi historia na fasihi huwa na maudhui na dhamira sawa. Tamthilia kama 'Mstahiki
Meya' ambayo nia yake ni kuonyesha jinsi waafrika ambao walichuukua uongozi baada ya ukoloni
walivyowanyanyasa waafrika wenzao yaweza kuwa sawa na historia ambapo waafrika ambao
walichukua uongozi waliwanyanyasa waafrika wenzao.
Uhusiano mwingine wa karibu ni kwamba wakati mwingine fasihi huchota kutoka kwa historia na
inapofanya hivyo fasihi hiyo inakuwa ya kufanana sana na historia yenyewe.Mfano ni kitabu cha
mzalendo kimathi ambapo matukio mengi katika kitabu hicho kinadhihirisha kwamba kimechota kutoka
kwa historia. Pia baada ya kipindi Fulani, fasihi husika inakuwa historia.
Uhusiano mwingine ni kwamba zote huandikwa kwa lugha na zinapoandikwa fasihi hufufua majina
ya wale ambao majina yao hayakuweza kuingia katika vitabu vya historia.
Mwisho, historia na fasihi hufanya jukumu la kumjuza mwanadamu kuhusu mazingira yake hasa
yale ya zamani na kumuwezesha kuweza aidha kuyarekebisha au kuyakubali. Mfano ni katika tamthilia ya
kidagaa, Mtemi Nasaba Bora anawapokonya waafrika wezake mashamba kwa kutumia nguvu. Fasihi hii
pia inaoana na jinsi ambavyo historia inafunza ambavyo viongozi wa kwanza walivyojipatia vipande
vikubwa vikubwa vya ardhi.Fasihi na historia pia zinakaribiana sana kutokana kwamba mwanahistoria na
mwanafasihi ni wanajamii wote. Wale ambao huchunguza matukio ya kihistoria na wale ambao huandika
fasihi pia ni wanajamii.
Mojawapo wa tofauti ya historia na fasihi ni tofauti ya kiwakati. Historia imefungika kiwakati hivi
kwamba upeo wake ni sasa. Mwanahistoria akitaka kujuza kuhusu nchi Fulani anaeleza ilikoanza hadi
ilikofika lakini mwanafasihi anaweza kueleza mahali nchi fulani ilikoanza, iliko sasa na itakavyokuwa
baada ya miaka mingi baada ya sasa. Mwanafasihi anaweza kuandika kuhusu nchi ya kesho peke yake na
fasihi iwe imekamilika. Mfano mwema ni George Orwell ambaye alikiandika kitabu mwaka wa 1978 na
akakiita 1984. Pia Riwaya ya 'Walenisi' ni riwaya ambayo inazungumza kuhusu dunia ambayo ni ya kesho
jambo ambalo historia haiwezi.
Tofauti nyingine ni kwamba historia hutegemea ithibati ili iweze kufahamisha. Kama
inazungumzia kuhusu tukio Fulani, lazima iwe na dhibitisho sahihi na hamna nafasi ya ubunifu. Kwa
upande mwingine, fasihi ina nafasi ya ubunifu na sio lazima mwanafasihi adhibitishe yale ambayo
ameandikia yalifanyika. Hata kama Mstahiki Meya ni jina ambalo ni la kihalisia katika masikio ya
Wakenya, mwandishi wa tamthilia ya Mstahiki hana jukumu la kutoa idhibati za kuonyesha kwamba aliishi
na pia cheneo ni mojawapo wa miji ya nchi fulani.
Tofauti nyingine ni kwamba kila mwanafasihi huwa na itikadi yake lakini mwanahistoria huweka
mambo jinsi yalivyo na kumwachia msomaji awe wa kuamua. Mwandishi kama wa tamthilia ya 'Mstahiki
Meya' ana itikadi kwamba viongozi dhalimu wanastahili kuondolewa mamlakani kwa nguvu lakini
mwanahistoria hawezi kuwa na msimamo kama huo.
Tofauti nyingine ni kwamba fasihi hujikita sana kwa wahusika na maisha yao lakini jambo kuu na
ambalo historia huzingatia sana ni matukio na wakati ambao matukio hayo yalitokea. Hili hufanya takriban
fasihi zote kuwa na mhusika mkuu lakini kipindi fulani cha historia chaweza kosa hata mhusika mmoja
mkuu.
Jambo jingine ni kwamba historia na fasihi hutofautiana kiwakati, mahali na mandhari ambamo
matukio fulani yanatokea. Tamthilia kama ya ‘Mstahiki Meya’ ina uwezakano kwamba inazungumza
kuhusu Kenya na viongozi wa baada ya uhuru lakini mahali ambapo matukio ya tamthilia yanafanyikia ni
cheneo ala sio wa mji kama Nakuru au Nairobi.
Tofauti nyingine ni kwamba hamna nafasi ya ubunifu katika historia lakini fasihi huwa ni zao la
ubunifu. Mambo ambayo wanahistoria huwa wamekosa katika historia yanaweza yakawa wazi kupitia
ubunifu wa mwandishi. Fasihi pia inaweza ikaumba wahusika au hata dunia ambayo haiwezi ikapatikana
katika ulimwengu wa kawaida.

Maswali.
a. Fupisha aya tatu za kwanza kwa maneno 20-30.
Nakala safi
b. Fupisha aya tano za mwisho kwa maneno kati ya 60-70
Matayarisho

  

Answers


Kavungya
i.wahusika
ii.mandhari
iii.matukio
iv.maudhui
v.Dhamira
vi.Kupasha kuhusu mazingira
vii.Fasihi huchota kutoka kwahistoria.

a.Tofauti ya kiwakati
b.Historia hutegemea idhibati lakini fasihi hutegemea ubunifu.
a.Kila mwanafasihi ana itikadi yake lakini kila mwanahistoria huweka mambo jinsi yalivyo.
c.Fasihi hujikita kwa wahusika na maisha yao lakini historia ni matukio
d.Hutofautiana kiwakati, mahali na mandhari.
e.Hamna nafasi ya ubunifu katika historia kama ilivyo katika fasihi.
Kavungya answered the question on October 31, 2019 at 06:16


Next: The diagram below shows a Zinc –copper cell.
Previous: Taja sifa mbili za irabu /e/ na /i/ ambazo zinafanana.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions