Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Takwimu za tafiti za umaskini kila mara huonyesha kuwa bara la Afrika ndilo bara maskini kabisa kote duniani. Takriban wakaazi kiasi cha asilimia...

      

Takwimu za tafiti za umaskini kila mara huonyesha kuwa bara la Afrika ndilo bara maskini kabisa kote duniani. Takriban wakaazi kiasi cha asilimia themanini hawawezi kumudu kutumia dola moja kwa siku. Toka kaskazini hadi kusini. mashariki hadi magharibi mwa bara, makaazi ya vibanda yametamalaki. Wakaazi wengi hulala njaa kutokana na ukosefu wa chakula. Watu wa mitaani waliovaa mararuraru wamejaa katika miji ya bara hili. Swali ni: Je, kwa nini umaskini umeliganda bara la Afrika hivi mithili ya kupe? Kwa nini bara huselelea katika lindi la uchochole?

Ili kuelewa sababu za umaskini kuganda barani Afrika, yampasa mtu ima fa ima kurejelea historia ya bara hili. Kwa kipindi cha karne nyingi, Afrika ilidhibitiwa na walowezi pamoja na mabeberu. Wanawake ambao wangelistwawisha bara hili kiuchumi walitwaliwa kimabavu na kupelekwa, huku wamefungwa minyororo, kustawisha uchumi wa mabara mengine. Afrika ikaporwa nguvu ambayo ni rasilmali kuu katika ustawishaji wa uchumi. La kusikitisha ni kuwa Afrika haikufidiwa kutokana na wizi huu. Badala yake iliongezewa mizigo mingine.

Baada ya kipindi cha biashara ya utumwa kumalizika, Afrika ilijipata katika janga jingine. Wakoloni wakaliingilia bara kwa pupa. Wakaligawanya katika koloni mbalimbali miongoni mwao. Wakaingiwa na wendawazimu kuiba malighafi ya bara hili. Wakaiba mashamba, madini, miti na chochote cha maana walichokipata. Badala ya malighafi haya kutumika kunawirisha bara la Afrika, yalitwaliwa kustawisha chumi za walikotoka wakoloni. Afrika ikaachwa kuzidi kudidimia katika lindi la umaskini.

Wakoloni walipotoka barani Afrika na kuzipa dola nyingi za Afrika ‘uhuru’, waliacha mkururo wa madhila. Madhila haya hayangeikubalia Afrika kujikomboa kutoka katika biwi la uchochole. Tatizo la kwanza na kubwa zaidi ni wakoloni kugawanya na kukatakata Afrika katika mataifa mengi. Mgawanyo huu ukawa haukufuata utaratibu wowote. Kwa sababu hii, watu wa nasaba moja wakawekwa katika nchi tofauti. Mathalani , watu wa nasaba ya Kisomali waligawanywa na kuwekwa chini ya nchi huru ya Somali, wengine chini ya dola la Uhabeshi, huku wengine wakiwa nchini Kenya na Jibuti. Watu kama hawa hawakutaka mpango huu. Waliokuwa Kenya na Uhabeshi wakachukua silaha na kupigana ili warejeshwe chini ya himaya moja ya taifa huru la Somali. Watu kama hawa wakatumia muda mwingi kupigana; muda ambao ungetumika kuinua Afrika kiuchumi. Mapigano haya ya wenyewe kwa wenyewe yamekithiri kote katika bara la Afrika.

Halikadhalika, mkoloni hakufanya juhudi zozote za kuanzisha viwanda ambavyo vingenyanyua uchumi wa Afrika na kuwatoa Waafrika katika biwi la ufukara. Palipokuwa na ari yoyote ya kuanzisha kiwanda, kilipoanzishwa hakikusaidia Afrika kiuchumi. Vilikuwa viwanda vya kupunguza zigo la bidhaa na kuzifanya kuwa nyepesi ili zisafirishwe kwa ajili ya viwanda vya nchi walizotoka wakoloni.

Kwa kipindi cha muda ambao mkoloni amekuwa na maingiliano na wakaazi wa Afrika, amehakikisha kuwa mwafrika amekuwa mtegemezi wake. Malighafi ya Afrika yalipelekwa kutayarishiwa viwanda vya wakoloni. Kisha mwafrika alirudishiwa zikiwa bidhaa kamili za kutumiwa. Mwafrika akaonyeshwa kuwa chochote kilichotoka kwa wakoloni ni bora zaidi ya chake alichozalisha. Hii ikawa ni mbinu moja ya wakoloni kuwafukarisha Waafrika. Hata sasa, kilichotoka Ulaya, hata kama ni cha hali ya chini, huonekana bora zaidi kuliko alichozalisha Mwafrika

Kwa upande mwingine, inadhihirika kuwa wakoloni hawajawahi kuondoka na kuwaachia Waafrika jukumu kamili la kuendesha uhuru wao kisiasa, kijamii na kiuchumi. Waliondoka kupita mlango mmoja na kurudi kwa wa pili. Mlango wa pili ukawa ni ukoloni kuchukua sura nyingine, sura ya ukoloni mamboleo. Kupitia ukoloni huu, wakoloni hudhibiti uchumi na maendeleo ya Afrika kupitia asasi mbili walizozianzisha, yaani Benki Kuu ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani. Ili kupata mikopo ya maendeleo, asasi hizi hutoa masharti ambayo hukwamiza badala ya kuchangia kuleta maendeleo barani Afrika.

Sasa hivi pana haja ya wana wa Afrika kufanya vikao vya dhurura ili kujadiliana kuhusu suluhisho la tatizo hili sugu la umaskini barani. Lazima wawahimize Waafrika wote kujikomboa kiakili na kung’amua kuwa maendeleo ya bara lazima yaongozwe na yadhibitiwe na Waafrika wenyewe. Wawahimize kuacha hulka za kukimbilia mataifa yaliyowafanya watumwa na kuwakalia kikoloni kwa misaada ya maendeleo. Misaada hii si ya dhati bali ni ya chati na hailengi kuondoa umaskini barani bali kuuendeleza.

Pana haja pia Waafrika kuwa na miungano ya kiuchumi. Miungano hii husaidia katika uteteaji wa soko pamoja na bei za bidhaa zao ikilinganishwa na taifa moja kuyaendeleza mambo haya. Halikadhalika, Waafrika wanapaswa kutambua kile wanachotaka na kupanga mikakati ya kufikia mahitaji ya kimsingi kwa wananchi wake. Kwa mfano, uimarishaji wa mbinu msingi ambazo zitachangia kuimarisha uchumi wa mataifa wahitaji kuwa mstari wa mbele badala ya ununuzi wa magari na ndege za hadhi za kuwabebea viongozi.

(a) Ipe taarifa uliyoisoma anwani mwafaka.

(b) Kutamalaki kwa umaskini barani Afrika kunadhihirishwa na nini.

(c) Onyesha jinsi ambavyo wakoloni wameendeleza umaskini barani Afrika.

(d) Thibitisha kwa kutoa hoja tatu, dhana ya kuwa “Waafrika wenyewe ndio wamechangia kuwepo kwa umaskini wa bara la Afrika.”

(e) Umaskini barani Afrika unaweza kukabiliwa vipi kwa mujibu wa makala haya?

(f) Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika taarifa:
(i) kuselelea……………
(ii) mabeberu…………

  

Answers


Maurice
(a) Umaskini / umaskini barani Afrika

(b) -Takwimu kuonyesha kuwa wakaazi wengi wa Afrika hawawezi kuishi kwa dola moja kwa siku
- Hali za maisha kote barani – makazi mavazi na chakula vinaashiria hali ya umaskini inayolikabili bara.

(c) -Kuporwa kwa nguvu za Afrika bila fidia katika kipindi cha biashara ya utumwa.
-Nguvu hii ambayo ingetumika kustawisha bara la Afrika ilitwaliwa kwenda kustawisha chumi za mabara mengine.
-Uporaji wa rasilmali na malighafi ya Afrika na kwenda kunufaisha mabara mengine.
-Kutoanzisha viwanda ambavyo vingesaidia kustawisha uchumi wa Afrika.
-Wakoloni walikatakata bara la Afrika katika dola ambazo hazina manufaa kiuchumi.
-Watu wa nasaba moja kugawanywa na kuwekwa chini ya mataifa mbalimbali. Baadaye watu hawa kuzusha vita na kutumia muda mwingi ambao ungetumika kustawisha uchumi badala ya mapigano.
-Mkoloni kuanzisha ukoloni mamboleo kupitia kwa asasi kama Benki Kuu ya dunia na Shirika la Fedha Duniani. Hizi zimechangia kuendeleza umaskini barani.

(d) - Wafrika kuwa wategemezi. Hununua vya watu wengine na kudharau walivyozalisha kwa hivyo bidhaa zao hukosa soko. Hili haliwezi kustawisha uchumi bali kuendeleza umaskini.
-Waafrika kukosa kujikomboa kiakili na kujua kuwa maendeleo ya bara yanatakiwa kuanzishwa na kudhibitiwa na Waafrika wenyewe. Wao hukimbilia misaada ya maendeleo kwa njia ya mikopo kutoka kwa mataifa yaliyowafanya watumwa na kuwakalia kikoloni.
-Waafrika kukosa utaratibu mwafaka wa uwekezaji. Badala ya kutumia walichonacho kuanzisha mbinu msingi ambazo zitachangia uimarishaji wa uchumi, wao hununua magari na ndege za kifahari ili kubeba viongozi.


(e) -Waafrika kuelewa kuwa maendeleo ya bara lazima yaongozwe na kudhibitiwa na wao wenyewe.
-Waafrika waache kuombaomba misaada kutoka kwa wakoloni waliowafanya watumwa na kupora malighafi.
-Waafrika kuacha tabia ya utegemezi. Wajue kuwa wanapodharau kilicho chao na walichozalisha wanaendeleza umaskini barani.
-Waafrika kuunda muungano mmoja wa kiuchumi ambao utaweza kutafuta soko na kutetea bei za bidhaa kutoka Afrika. Hii itapunguza taifa moja kupunjwa kwani huwa halina nguvu ya kutetea haya.
-Waafrika kupanga mambo yao kwa kubainisha mahitaji yao na kuyapa kipaumbele. Mambo ambayo yataendeleza kustawisha uchumi wa bara yawe katika mstari wa mbele. Rasilmali zitumike kugharamia haya badala ya kutumiwa kwa mambo yasiyokuwa na umuhimu kiuchumi.
-Waafrika kuanzisha viwanda vitakavyotengeneza na kusindika bidhaa kikamilifu. Viwanda visiwe ni vya shughuli zinazohusisha kilimo tu bali shughuli mbali mbali.

(f) Kuselelea – kuishi hivyo daima
Mabeberu – wakoloni
maurice.mutuku answered the question on November 20, 2019 at 08:09


Next: Explain six negative effects of Trans Saharan trade on African communities.
Previous:  Sekta za umma humu nchini hazina kifani katika uzembe. Unapohitaji huduma za posta, umeme, maji, mawasiliiano, utayarishaji wa mishahara na malipo mengine, utalazimika...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • Halleluyah… Mungu asifiwe sana… shetani ashindwe… Tambua na utoe sifa za sajili hii.(Solved)

    Halleluyah… Mungu asifiwe sana… shetani ashindwe…
    Tambua na utoe sifa za sajili hii.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Eleza dhima ya sentensi hii. Rudi ulikotoka.(Solved)

    Eleza dhima ya sentensi hii.
    Rudi ulikotoka.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Kanusha. Mwanafunzi alikuwa akilia alipojikwaa.(Solved)

    Kanusha.
    Mwanafunzi alikuwa akilia alipojikwaa.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Onyesha aina ya vishazi katika sentensi hii. Isipokuwa ni kulewa kwake angeenda Kitui.(Solved)

    Onyesha aina ya vishazi katika sentensi hii.
    Isipokuwa ni kulewa kwake angeenda Kitui.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Kosoa sentensi ifuatayo kwa njia mbili tofauti. Ningelima shamba langu kwa wakati ufaao ningalivuna sawasawa.(Solved)

    Kosoa sentensi ifuatayo kwa njia mbili tofauti.
    Ningelima shamba langu kwa wakati ufaao ningalivuna sawasawa.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi kutofautisha maana ya majina haya. Nadhari Nathari(Solved)

    Tunga sentensi kutofautisha maana ya majina haya.
    Nadhari
    Nathari

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Onyesha shamirisho katika sentensi ifuatayo. Kakubwa alimjengea mama yake nyumba kwa mawe.(Solved)

    Onyesha shamirisho katika sentensi ifuatayo.
    Kakubwa alimjengea mama yake nyumba kwa mawe.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Badilisha sentensi ifuatayo iwe katika kauli ya kutendwa. Simba mwenda pole alimla swara mnono sana.(Solved)

    Badilisha sentensi ifuatayo iwe katika kauli ya kutendwa.
    Simba mwenda pole alimla swara mnono sana.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi. Anampenda wake sana lakini alimpiga sana(Solved)

    Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi.
    Anampenda wake sana lakini alimpiga sana

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Tumia neno msomi kama nomino na kama kivumishi katika sentensi.(Solved)

    Tumia neno msomi kama nomino na kama kivumishi katika sentensi.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Andika kinyume cha sentensi hii. Mama alienda sokoni jana asubuhi.(Solved)

    Andika kinyume cha sentensi hii.
    Mama alienda sokoni jana asubuhi.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi hii kwa udogo wingi. Mti ulikatwa ukatengeneze kiti.(Solved)

    Andika sentensi hii kwa udogo wingi.
    Mti ulikatwa ukatengeneze kiti.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi moja ukitumia kiunganishi cha kuongeza.(Solved)

    Tunga sentensi moja ukitumia kiunganishi cha kuongeza.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Tumia kiambishi ndi- pamoja na kiwakilishi huru cha nafsi ya kwanza wingi.(Solved)

    Tumia kiambishi ndi- pamoja na kiwakilishi huru cha nafsi ya kwanza wingi.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Thibitisha kuwa neno moja linaweza kuwa katika ngeli mbili tofauti.(Solved)

    Thibitisha kuwa neno moja linaweza kuwa katika ngeli mbili tofauti.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Onyesha mofimu mbalimbali katika neno kikikipikia.(Solved)

    Onyesha mofimu mbalimbali katika neno kikikipikia.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Eleza kanuni ya kutia shadda katika lugha ya Kiswahili.(Solved)

    Eleza kanuni ya kutia shadda katika lugha ya Kiswahili.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Toa mfano wa maneno mawili ambayo yana sauti mwambatano mbili.(Solved)

    Toa mfano wa maneno mawili ambayo yana sauti mwambatano mbili.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Taja sifa mbili za irabu /e/ na /i/ ambazo zinafanana.(Solved)

    Taja sifa mbili za irabu /e/ na /i/ ambazo zinafanana.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Historia na fasihi zina uhusiano wa karibu sana hasa fasihi ya kihistoria. Hata hivyo fasihi siohistoria na historia si fasihi kwa...(Solved)

    UHUSIANO WA FASIHI NA HISTORIA

    Historia na fasihi zina uhusiano wa karibu sana hasa fasihi ya kihistoria. Hata hivyo fasihi sio
    historia na historia si fasihi kwa sababu hizi ni taaluma mbili ambazo zina uhusiano tu. Hata hivyo, fasihi
    na historia zina mambo ambayo yanafana na yale ambayo hayafanani.
    Kati ya mambo ambayo yanafanana ni kwamba fasihi na historia wakati mwingine huweza kuwa
    na wahusika ambao wanafanana kitabia, kimaumbile na hata wakati mwingine matendo ya kukumbukwa
    waliyofanywa. Mfano ni katika shairi la “Hongera Rais Moi” katika diwani ya ' Malenga wa ziwa kuu'
    ambapo mhusika ni rais Moi na mhusika kama yule pia aliishi katika kipindi Fulani katika nchi ya Kenya.
    Jambo jingine ambalo linapatikana katika fasihi na pia kinaoana na historia ni mandhari. Wakati
    mwingine, mandhari ambayo ni ya kihistoria yanakaribiana sana na ya kifasihi na hata wakati mwingine
    kufanana. Mandhari ya shamba la bwana Delamon katika 'kilio cha haki' yanaweza kuwa shamba lolote na
    mabwanyenye kama hata ni ya Bwana Dalamere.
    Wakati mwingine matukio katika fasihi huwa karibu sawa na yale ambayo yanapatikana katika
    historia ya kawaida. Mfano katika shairi la ' wasifu wa baba Kenyatta', mhusika mkuu yasemekana
    alipigania uhuru wa nchi ambayo aliiongoza. Matukio kama kufungwa jela ambayo mhusika huyu
    anapitia katika kujaribu kukomboa nchi ni sawa na yale ambayo mhusika wa kihistoria ambaye ni rais wa
    kwanza wa nchi ya Kenya.
    Pia, wakati mwingi historia na fasihi huwa na maudhui na dhamira sawa. Tamthilia kama 'Mstahiki
    Meya' ambayo nia yake ni kuonyesha jinsi waafrika ambao walichuukua uongozi baada ya ukoloni
    walivyowanyanyasa waafrika wenzao yaweza kuwa sawa na historia ambapo waafrika ambao
    walichukua uongozi waliwanyanyasa waafrika wenzao.
    Uhusiano mwingine wa karibu ni kwamba wakati mwingine fasihi huchota kutoka kwa historia na
    inapofanya hivyo fasihi hiyo inakuwa ya kufanana sana na historia yenyewe.Mfano ni kitabu cha
    mzalendo kimathi ambapo matukio mengi katika kitabu hicho kinadhihirisha kwamba kimechota kutoka
    kwa historia. Pia baada ya kipindi Fulani, fasihi husika inakuwa historia.
    Uhusiano mwingine ni kwamba zote huandikwa kwa lugha na zinapoandikwa fasihi hufufua majina
    ya wale ambao majina yao hayakuweza kuingia katika vitabu vya historia.
    Mwisho, historia na fasihi hufanya jukumu la kumjuza mwanadamu kuhusu mazingira yake hasa
    yale ya zamani na kumuwezesha kuweza aidha kuyarekebisha au kuyakubali. Mfano ni katika tamthilia ya
    kidagaa, Mtemi Nasaba Bora anawapokonya waafrika wezake mashamba kwa kutumia nguvu. Fasihi hii
    pia inaoana na jinsi ambavyo historia inafunza ambavyo viongozi wa kwanza walivyojipatia vipande
    vikubwa vikubwa vya ardhi.Fasihi na historia pia zinakaribiana sana kutokana kwamba mwanahistoria na
    mwanafasihi ni wanajamii wote. Wale ambao huchunguza matukio ya kihistoria na wale ambao huandika
    fasihi pia ni wanajamii.
    Mojawapo wa tofauti ya historia na fasihi ni tofauti ya kiwakati. Historia imefungika kiwakati hivi
    kwamba upeo wake ni sasa. Mwanahistoria akitaka kujuza kuhusu nchi Fulani anaeleza ilikoanza hadi
    ilikofika lakini mwanafasihi anaweza kueleza mahali nchi fulani ilikoanza, iliko sasa na itakavyokuwa
    baada ya miaka mingi baada ya sasa. Mwanafasihi anaweza kuandika kuhusu nchi ya kesho peke yake na
    fasihi iwe imekamilika. Mfano mwema ni George Orwell ambaye alikiandika kitabu mwaka wa 1978 na
    akakiita 1984. Pia Riwaya ya 'Walenisi' ni riwaya ambayo inazungumza kuhusu dunia ambayo ni ya kesho
    jambo ambalo historia haiwezi.
    Tofauti nyingine ni kwamba historia hutegemea ithibati ili iweze kufahamisha. Kama
    inazungumzia kuhusu tukio Fulani, lazima iwe na dhibitisho sahihi na hamna nafasi ya ubunifu. Kwa
    upande mwingine, fasihi ina nafasi ya ubunifu na sio lazima mwanafasihi adhibitishe yale ambayo
    ameandikia yalifanyika. Hata kama Mstahiki Meya ni jina ambalo ni la kihalisia katika masikio ya
    Wakenya, mwandishi wa tamthilia ya Mstahiki hana jukumu la kutoa idhibati za kuonyesha kwamba aliishi
    na pia cheneo ni mojawapo wa miji ya nchi fulani.
    Tofauti nyingine ni kwamba kila mwanafasihi huwa na itikadi yake lakini mwanahistoria huweka
    mambo jinsi yalivyo na kumwachia msomaji awe wa kuamua. Mwandishi kama wa tamthilia ya 'Mstahiki
    Meya' ana itikadi kwamba viongozi dhalimu wanastahili kuondolewa mamlakani kwa nguvu lakini
    mwanahistoria hawezi kuwa na msimamo kama huo.
    Tofauti nyingine ni kwamba fasihi hujikita sana kwa wahusika na maisha yao lakini jambo kuu na
    ambalo historia huzingatia sana ni matukio na wakati ambao matukio hayo yalitokea. Hili hufanya takriban
    fasihi zote kuwa na mhusika mkuu lakini kipindi fulani cha historia chaweza kosa hata mhusika mmoja
    mkuu.
    Jambo jingine ni kwamba historia na fasihi hutofautiana kiwakati, mahali na mandhari ambamo
    matukio fulani yanatokea. Tamthilia kama ya ‘Mstahiki Meya’ ina uwezakano kwamba inazungumza
    kuhusu Kenya na viongozi wa baada ya uhuru lakini mahali ambapo matukio ya tamthilia yanafanyikia ni
    cheneo ala sio wa mji kama Nakuru au Nairobi.
    Tofauti nyingine ni kwamba hamna nafasi ya ubunifu katika historia lakini fasihi huwa ni zao la
    ubunifu. Mambo ambayo wanahistoria huwa wamekosa katika historia yanaweza yakawa wazi kupitia
    ubunifu wa mwandishi. Fasihi pia inaweza ikaumba wahusika au hata dunia ambayo haiwezi ikapatikana
    katika ulimwengu wa kawaida.

    Maswali.
    a. Fupisha aya tatu za kwanza kwa maneno 20-30.
    Nakala safi
    b. Fupisha aya tano za mwisho kwa maneno kati ya 60-70
    Matayarisho

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)