(a) (i) Sekta za umma humu nchini zina uzembe mwingi katika kutoa huduma.
(ii) Uzembe wa wafanyakazi wa sekta hii hotukana na ukosefu wa motisha.
(iii) Visa vya ufisadi ni sifa kuu inayopambanua huduma za umma.
(iv) Baadhi ya wafanyakazi hupatikana katika maeneo yao ya kazi kwa nadra sana.
(v) matendo haya yamesababisha kukokota kukua kwa uchumi.
(b) (i) Sekta za kibinafsi zimetambulika kuwa muhimu sana.
(ii) Uchumi wa mataifa yanayopendelea mfumo huu umekua kwa kasi sana.
(iii) Mashirika ya kibibafsi yana udhaifu wa aina yake.
(iv) Serikali inaposhirikiana na setka hii ustawishaji wa hali za kikazi utajiri.
(v) Mashirika ya kibinafsi huwafanyiza wanfanyikazi wao kazi nyingi ili kujizolea faida kemkem.
(vi) Mshahara wa sekta ya kibinafsi ni bora kuliko wa umma.
(vii) Baadhi ya sera za sekta hii ni kandamizi kwa wafanyakazi.
(viii) Ushirikiano wa serikali na mashirika ya kibinafsi yana uwezo wa kustawisha uchumi.
maurice.mutuku answered the question on November 20, 2019 at 08:18
- Takwimu za tafiti za umaskini kila mara huonyesha kuwa bara la Afrika ndilo bara maskini kabisa kote duniani. Takriban wakaazi kiasi cha asilimia...(Solved)
Takwimu za tafiti za umaskini kila mara huonyesha kuwa bara la Afrika ndilo bara maskini kabisa kote duniani. Takriban wakaazi kiasi cha asilimia themanini hawawezi kumudu kutumia dola moja kwa siku. Toka kaskazini hadi kusini. mashariki hadi magharibi mwa bara, makaazi ya vibanda yametamalaki. Wakaazi wengi hulala njaa kutokana na ukosefu wa chakula. Watu wa mitaani waliovaa mararuraru wamejaa katika miji ya bara hili. Swali ni: Je, kwa nini umaskini umeliganda bara la Afrika hivi mithili ya kupe? Kwa nini bara huselelea katika lindi la uchochole?
Ili kuelewa sababu za umaskini kuganda barani Afrika, yampasa mtu ima fa ima kurejelea historia ya bara hili. Kwa kipindi cha karne nyingi, Afrika ilidhibitiwa na walowezi pamoja na mabeberu. Wanawake ambao wangelistwawisha bara hili kiuchumi walitwaliwa kimabavu na kupelekwa, huku wamefungwa minyororo, kustawisha uchumi wa mabara mengine. Afrika ikaporwa nguvu ambayo ni rasilmali kuu katika ustawishaji wa uchumi. La kusikitisha ni kuwa Afrika haikufidiwa kutokana na wizi huu. Badala yake iliongezewa mizigo mingine.
Baada ya kipindi cha biashara ya utumwa kumalizika, Afrika ilijipata katika janga jingine. Wakoloni wakaliingilia bara kwa pupa. Wakaligawanya katika koloni mbalimbali miongoni mwao. Wakaingiwa na wendawazimu kuiba malighafi ya bara hili. Wakaiba mashamba, madini, miti na chochote cha maana walichokipata. Badala ya malighafi haya kutumika kunawirisha bara la Afrika, yalitwaliwa kustawisha chumi za walikotoka wakoloni. Afrika ikaachwa kuzidi kudidimia katika lindi la umaskini.
Wakoloni walipotoka barani Afrika na kuzipa dola nyingi za Afrika ‘uhuru’, waliacha mkururo wa madhila. Madhila haya hayangeikubalia Afrika kujikomboa kutoka katika biwi la uchochole. Tatizo la kwanza na kubwa zaidi ni wakoloni kugawanya na kukatakata Afrika katika mataifa mengi. Mgawanyo huu ukawa haukufuata utaratibu wowote. Kwa sababu hii, watu wa nasaba moja wakawekwa katika nchi tofauti. Mathalani , watu wa nasaba ya Kisomali waligawanywa na kuwekwa chini ya nchi huru ya Somali, wengine chini ya dola la Uhabeshi, huku wengine wakiwa nchini Kenya na Jibuti. Watu kama hawa hawakutaka mpango huu. Waliokuwa Kenya na Uhabeshi wakachukua silaha na kupigana ili warejeshwe chini ya himaya moja ya taifa huru la Somali. Watu kama hawa wakatumia muda mwingi kupigana; muda ambao ungetumika kuinua Afrika kiuchumi. Mapigano haya ya wenyewe kwa wenyewe yamekithiri kote katika bara la Afrika.
Halikadhalika, mkoloni hakufanya juhudi zozote za kuanzisha viwanda ambavyo vingenyanyua uchumi wa Afrika na kuwatoa Waafrika katika biwi la ufukara. Palipokuwa na ari yoyote ya kuanzisha kiwanda, kilipoanzishwa hakikusaidia Afrika kiuchumi. Vilikuwa viwanda vya kupunguza zigo la bidhaa na kuzifanya kuwa nyepesi ili zisafirishwe kwa ajili ya viwanda vya nchi walizotoka wakoloni.
Kwa kipindi cha muda ambao mkoloni amekuwa na maingiliano na wakaazi wa Afrika, amehakikisha kuwa mwafrika amekuwa mtegemezi wake. Malighafi ya Afrika yalipelekwa kutayarishiwa viwanda vya wakoloni. Kisha mwafrika alirudishiwa zikiwa bidhaa kamili za kutumiwa. Mwafrika akaonyeshwa kuwa chochote kilichotoka kwa wakoloni ni bora zaidi ya chake alichozalisha. Hii ikawa ni mbinu moja ya wakoloni kuwafukarisha Waafrika. Hata sasa, kilichotoka Ulaya, hata kama ni cha hali ya chini, huonekana bora zaidi kuliko alichozalisha Mwafrika
Kwa upande mwingine, inadhihirika kuwa wakoloni hawajawahi kuondoka na kuwaachia Waafrika jukumu kamili la kuendesha uhuru wao kisiasa, kijamii na kiuchumi. Waliondoka kupita mlango mmoja na kurudi kwa wa pili. Mlango wa pili ukawa ni ukoloni kuchukua sura nyingine, sura ya ukoloni mamboleo. Kupitia ukoloni huu, wakoloni hudhibiti uchumi na maendeleo ya Afrika kupitia asasi mbili walizozianzisha, yaani Benki Kuu ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani. Ili kupata mikopo ya maendeleo, asasi hizi hutoa masharti ambayo hukwamiza badala ya kuchangia kuleta maendeleo barani Afrika.
Sasa hivi pana haja ya wana wa Afrika kufanya vikao vya dhurura ili kujadiliana kuhusu suluhisho la tatizo hili sugu la umaskini barani. Lazima wawahimize Waafrika wote kujikomboa kiakili na kung’amua kuwa maendeleo ya bara lazima yaongozwe na yadhibitiwe na Waafrika wenyewe. Wawahimize kuacha hulka za kukimbilia mataifa yaliyowafanya watumwa na kuwakalia kikoloni kwa misaada ya maendeleo. Misaada hii si ya dhati bali ni ya chati na hailengi kuondoa umaskini barani bali kuuendeleza.
Pana haja pia Waafrika kuwa na miungano ya kiuchumi. Miungano hii husaidia katika uteteaji wa soko pamoja na bei za bidhaa zao ikilinganishwa na taifa moja kuyaendeleza mambo haya. Halikadhalika, Waafrika wanapaswa kutambua kile wanachotaka na kupanga mikakati ya kufikia mahitaji ya kimsingi kwa wananchi wake. Kwa mfano, uimarishaji wa mbinu msingi ambazo zitachangia kuimarisha uchumi wa mataifa wahitaji kuwa mstari wa mbele badala ya ununuzi wa magari na ndege za hadhi za kuwabebea viongozi.
(a) Ipe taarifa uliyoisoma anwani mwafaka.
(b) Kutamalaki kwa umaskini barani Afrika kunadhihirishwa na nini.
(c) Onyesha jinsi ambavyo wakoloni wameendeleza umaskini barani Afrika.
(d) Thibitisha kwa kutoa hoja tatu, dhana ya kuwa “Waafrika wenyewe ndio wamechangia kuwepo kwa umaskini wa bara la Afrika.”
(e) Umaskini barani Afrika unaweza kukabiliwa vipi kwa mujibu wa makala haya?
(f) Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika taarifa:
(i) kuselelea……………
(ii) mabeberu…………
Date posted: November 20, 2019. Answers (1)
- Halleluyah… Mungu asifiwe sana… shetani ashindwe…
Tambua na utoe sifa za sajili hii.(Solved)
Halleluyah… Mungu asifiwe sana… shetani ashindwe…
Tambua na utoe sifa za sajili hii.
Date posted: October 31, 2019. Answers (1)
- Eleza dhima ya sentensi hii.
Rudi ulikotoka.(Solved)
Eleza dhima ya sentensi hii.
Rudi ulikotoka.
Date posted: October 31, 2019. Answers (1)
- Kanusha.
Mwanafunzi alikuwa akilia alipojikwaa.(Solved)
Kanusha.
Mwanafunzi alikuwa akilia alipojikwaa.
Date posted: October 31, 2019. Answers (1)
- Onyesha aina ya vishazi katika sentensi hii.
Isipokuwa ni kulewa kwake angeenda Kitui.(Solved)
Onyesha aina ya vishazi katika sentensi hii.
Isipokuwa ni kulewa kwake angeenda Kitui.
Date posted: October 31, 2019. Answers (1)
- Kosoa sentensi ifuatayo kwa njia mbili tofauti.
Ningelima shamba langu kwa wakati ufaao ningalivuna sawasawa.(Solved)
Kosoa sentensi ifuatayo kwa njia mbili tofauti.
Ningelima shamba langu kwa wakati ufaao ningalivuna sawasawa.
Date posted: October 31, 2019. Answers (1)
- Tunga sentensi kutofautisha maana ya majina haya.
Nadhari
Nathari(Solved)
Tunga sentensi kutofautisha maana ya majina haya.
Nadhari
Nathari
Date posted: October 31, 2019. Answers (1)
- Onyesha shamirisho katika sentensi ifuatayo.
Kakubwa alimjengea mama yake nyumba kwa mawe.(Solved)
Onyesha shamirisho katika sentensi ifuatayo.
Kakubwa alimjengea mama yake nyumba kwa mawe.
Date posted: October 31, 2019. Answers (1)
- Badilisha sentensi ifuatayo iwe katika kauli ya kutendwa.
Simba mwenda pole alimla swara mnono sana.(Solved)
Badilisha sentensi ifuatayo iwe katika kauli ya kutendwa.
Simba mwenda pole alimla swara mnono sana.
Date posted: October 31, 2019. Answers (1)
- Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi.
Anampenda wake sana lakini alimpiga sana(Solved)
Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi.
Anampenda wake sana lakini alimpiga sana
Date posted: October 31, 2019. Answers (1)
- Tumia neno msomi kama nomino na kama kivumishi katika sentensi.(Solved)
Tumia neno msomi kama nomino na kama kivumishi katika sentensi.
Date posted: October 31, 2019. Answers (1)
- Andika kinyume cha sentensi hii.
Mama alienda sokoni jana asubuhi.(Solved)
Andika kinyume cha sentensi hii.
Mama alienda sokoni jana asubuhi.
Date posted: October 31, 2019. Answers (1)
- Andika sentensi hii kwa udogo wingi.
Mti ulikatwa ukatengeneze kiti.(Solved)
Andika sentensi hii kwa udogo wingi.
Mti ulikatwa ukatengeneze kiti.
Date posted: October 31, 2019. Answers (1)
- Tunga sentensi moja ukitumia kiunganishi cha kuongeza.(Solved)
Tunga sentensi moja ukitumia kiunganishi cha kuongeza.
Date posted: October 31, 2019. Answers (1)
- Tumia kiambishi ndi- pamoja na kiwakilishi huru cha nafsi ya kwanza wingi.(Solved)
Tumia kiambishi ndi- pamoja na kiwakilishi huru cha nafsi ya kwanza wingi.
Date posted: October 31, 2019. Answers (1)
- Thibitisha kuwa neno moja linaweza kuwa katika ngeli mbili tofauti.(Solved)
Thibitisha kuwa neno moja linaweza kuwa katika ngeli mbili tofauti.
Date posted: October 31, 2019. Answers (1)
- Onyesha mofimu mbalimbali katika neno kikikipikia.(Solved)
Onyesha mofimu mbalimbali katika neno kikikipikia.
Date posted: October 31, 2019. Answers (1)
- Eleza kanuni ya kutia shadda katika lugha ya Kiswahili.(Solved)
Eleza kanuni ya kutia shadda katika lugha ya Kiswahili.
Date posted: October 31, 2019. Answers (1)
- Toa mfano wa maneno mawili ambayo yana sauti mwambatano mbili.(Solved)
Toa mfano wa maneno mawili ambayo yana sauti mwambatano mbili.
Date posted: October 31, 2019. Answers (1)
- Taja sifa mbili za irabu /e/ na /i/ ambazo zinafanana.(Solved)
Taja sifa mbili za irabu /e/ na /i/ ambazo zinafanana.
Date posted: October 31, 2019. Answers (1)