Fafanua mambo manne yaliyochochea usanifishaji wa Kiswahili wakati wa ukoloni nchini.

      

Fafanua mambo manne yaliyochochea usanifishaji wa Kiswahili wakati wa ukoloni nchini.

  

Answers


Maurice
(i) Kuondoa utata wa kutumia lahaja tofauti katika mawasiliano.

(ii) kuhitajika kwa lugha moja ya uandishi wa vitabu vya masomo katika nchi zote za Afrika Mashariki.

(iii) palihitajika lugha ambayo ingetumiwa katika shughuli za kufundishia katika nchi zote za Afrika Mashariki.

(iv) Kutaka kusawazisha hati za Kirumi kwa matumizi ya Kiswahili badala ya hati za Kiarabu.

(v) Palihitajika usawazisho wa maendeleo ya lugha hii ili kuwe na sarufi moja inayokubalika.

(vi) Haja ya lahaja moja ambayo ingetumika kutafsiri vitabu vilivyokuwa vimeandikwa tayari.
maurice.mutuku answered the question on November 20, 2019 at 11:23


Next: a) Complete the table below for y = x3 + 2x2 - 5x - 4 b) On the grid provided, draw the graph of y =...
Previous: Toa sababu nne zinazosababisha watu kufanya makosa katika matumizi ya lugha.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions