Maana ya hadithi na sifa zake

      

Maana ya hadithi na sifa zake

  

Answers


Isacko
Hadithi ni masimulizi yanayowasilishwa kwa lugha ya nathari kuhusu watu, matukio na mahali mbali mbali, nayo sifa za hadithi ni;
Huwa na wahusika wa aina mbali mbali,binadamu,wanyama,mazimwi, miti,mawe,miungu.
Huwa na ploti sahili au nyepesi-hueleza matukio kwa mpangilio wa moja kwa moja.
Hutumia lugha ya kimaelezo.
Huwa na mtendaji au fanani.
Husimulia matukio ya kweli au ya kubuni yenye maadili.
Huwa na wakati maalum na mahali maalum pa kutolewa.
Huwasilishwa kwa hadhira hai.
Huwa na mgogoro au tukio la kueleza, mara nyingi mgogoro huwa kati ya wema na uovu.
Huwa na fomula maalum ya kuanzia na kumalizia.




Mohaissack answered the question on September 27, 2017 at 19:20


Next:  5 men have enough food for 36 weeks. How long would the same food last for 15 men?
Previous: Describe one method of determining the diameter of the oil drop

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions