Linganisha na ulinganue fasihi simulizi na fasihi andishi.

      

Linganisha na ulinganue fasihi simulizi na fasihi andishi.

  

Answers


KOMBO
Fasihi simulizi na fasihi andishi zinahusiana katika vipengele mbalimbali kama ifuatavyo:
(i)Fasihi simulizi huweza kuwasilishwa kupitia maandishi na fasihi andishi huweza kutumia ala za fasihi simulizi kunogesha kazi yake na kufikisha ujumbe wake. Hivyo maandishi sio kigezo cha kuitenganisha kabisa fasihi simulizi na fasihi andishi.
(ii) Ukichunguza kazi mbalimbali za fasihi andishi utabaini kila mwandishi ameathiriwa na fasihi simulizi kwa namna fulani. Wapo walioathiriwa kifani na wengine kimaudhui.
(iii) Zote mbili ni kazi za sanaa zinazotumia lugha ili kufikisha ujumbe kwa hadhira yake.
(iv) Fasihi simulizi na fasihi andishi zote mbili zinaundwa kwa fani na maudhui.
(v) Zote ni kazi za kisanaa zitumiazo maneno teule kufikisha ujumbe.
(vi) Zote maudhui yake humhusu mwanadamu na maisha yake katika kumletea maendeleo katika nyanja zote.
Tofauti kati ya FasihiAndishi na Fasihi Simulizi
1.Fasihi simulizi huwasilishwa kwa njia ya mdomo na/au matendo ilhali andishi huwasilishwa kwa njia ya maandishi.
2.Fasihi simulizi ni mali ya jamii ilhali fasihi andishi ni mali ya mwandishi (mchapishaji).
3.Fasihi simulizi msimulizi anaweza kubadilisha sehemu fulani ilhali fasihi andishi kitabu kilichoandikwa hakiwezi kubadilishwa.
4.Fasihi simulizi huhifadhiwa akilini ilhali huhifadhiwa vitabuni .
5.Fasihi simulizi hubadilika nawakati ilhali fasihi andishi haibadiliki na wakati.
6.Fasihi simulizi huhitaji msimulizi na hadhira yake wawe mahali pamoja wakati wa masimulizi ilhali fasihi andishi msomaji anaweza kusoma kitabu cha hadithi peke yake, mahali popote, wakati wowote.
7.Fasihi simulizi mtu yeyote anaweza kutunga na kusimulia ilhali ni lazima mwandishi na
msomaji wawe na uwezo wa kusoma.
8.Fasihi simulizi hutumia wahusika changamano (wanyama,watu, mazimwi n.k) ilhali fasihi andishi utumia wahusika wanadamu.




hepto answered the question on October 2, 2017 at 15:12

Winnie
Kulinganisha fasihi simulizi na fasihi andishi

-Zote ni lugha ya sanaa

-Zote ni kazi ya kisanii

-Kwa zote, maudhui humhusu mwanadamu na maisha yake katika kumletea maendeleo katika nyanja zote

-Zote huundwa kwa fani na maudhui


Kulinganua fasihi simulizi na fasihi andishi


-Fasihi simulizi huwasilishwa kwa njia ya mdomo pamoja na vitendo ilhali fasihi andishi huwasilishwa kwa njia ya maandishi bila vitendo

-Fasihi simulizi ni ya watu wote katika jamii ilhali fasihi andishi ni ya wale wanaojua kusoma na kuandika

-Fasihi simulizi simulizi ilhali fasihi andishi huwa hai kidogo ukilinganisha na fasihi andishi

-Fasihi simulizi huhifadhiwa kwa kichwa ilhali fasihi andishi huhifadhiwa kwa maandishi

-Fasihi simulizi hutungwa kwa muda mfupi ilhali fasihi andishi hutungwa kwa muda mrefu
Wincate 1 answered the question on October 12, 2017 at 15:21

Next: Explain how orthographic rain is formed
Previous: Despite the introduction of the ATM cards, human resource is still necessary in banks. Give four reasons why human beings are still needed.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions