Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Ushahidi was kihistoria ni muhimu katika kujadili swala la chimbuko la kiswahili.Jadili kauli hii kwa kurejelea Ushahidi huo

      

Ushahidi was kihistoria ni muhimu katika kujadili swala la chimbuko la kiswahili.Jadili kauli hii kwa kurejelea Ushahidi huo

  

Answers


Faith
Ushahidi wa kihistoria unatueleza mengi kuwa kiswahili ni mojawapo ya lahaja za kibantu.Wafuasi was nadharia ya kuwa kiswahili ni kibantu wametoa madai haya;
• Maandishi ya kale.Maandishi ya kale yaliyoandikwa kwa kiswahili yanapatikana katika mashairi.mashairi haya Yana maneno ya kale sana na pia wa maandishi yenyewe inafanana kimuundo na lugha ya kibantu.Maandishi haya ya kale Kama vile utenzi was Hamziya Ina maneno ya kingozi,utenzi wa Al-Inkishafi Ina maneno ya kiamu.Kwa hivyo hii inatuonyesha kuwa kiswahili ilitumiwa mwanzoni hata kabla kuja kwa waarabu na wamishenari wengine.
• Historian simulizi ya Uswahilini.Historia ya miji ya Lamu,kilwa na Pate inapatikana kwa Tarihi iliyoandikwa Karne ya 16.Tarihi ni kumbukumbu ya historia ya kale yaliyopangwa kulingana na nyakati.Tarihi ya Lamu unatueleza kuwa Koo zinazounda jamii zote za Lamu inajulikana kwa majina ya kiswahili Kama vile kina Mfamao,kina mti na Ungwana was Yumbe.Tarihi ya kilwa unatueleza kuwa Sultani was kilwa alipewa lakabu 'nguo mingi'naye mwanawe aliyeongoza mafia alijulikana 'mkoma mtu' kwa vile haya ni maneno ya kiswahili yaliyotumika katika miji ya zamani ya uswahilini,Hadi tunaweza kusema kuwa kiswahili kilikuwa yangu zamani.
• Wasafiri wa zamani- Wasafiri was zamani walioutembelea mwambao was Afrika Mashariki waliona na kuandika kuhusu Mambo mbalimbali.Wanasema waliona miji iliyostawi yenye watu weusi na pia pia lugha yao.Tutaweza kujadili Kila msafiri na alichoeleza.
Al-Masud-Alizuru Pwani ya Afrika mashariki Karne ya 10.Alieleza kuhusu nchi ya 'Zanj' yaani watu weusi ambao walikuwa na wafalme na mungu aliyeitwa 'mkulungu' vyakula Chao kilikuwa ndizi na mtama.Pia alitaja neno kilazi.Kulingana na watafiti na wanaisimu maneno hayo yalibadilika na kuwa 'Mulungu' na 'kiazi'.
Al-Idris - Alizuru Pwani ya Afrika Mashariki Karne ya 12.Alitaja miji ya malindi na Mombasa.Akasema zamani Zanzibar ilikuwa ikiitwa Unguja.Pia aliandika majina ya ndizi Kama vile kisukari,mkono wa tembo,kikonde na kadhalika.
Ibn-Batuta -Alizuru mnamo Karne ya 14.Alisema watu wa Mombasa walikuwa wakinunua vyakula kutoka nchi ya waswahili nap watafiti wanasema huenda nchi hiyo ilikuwa katika eneo la mto Ozi.Pia alipofika Kilwa wenyeji walikuwa wakiandika mashairi kwa kutumia lugha ya kiswahili.
Pia Mgiriki aliyeandika kitabu 'The periplus of the Erythraean sea' Nate aliandika mjini Alexandria mnamo mwaka wa 100 baada ya Kristi.Alitaja bandari mbalimbali na eneo la Afrika Mashariki.Pia kitabu kinazungumza utamaduni wa Waswahili Kama vile mitepe,ngalawa na madema ya kuvulia samaki.Kutokanq na madai ya Wasafiri hawa no kweli kuwa wao walipata kiswahili na si lugha ya kuletwa.
• Msamiati na methali za kiswahili.Tunaposoma methali na kuangalia msamiati was maneno yaliyotumiwa na Waswahili Basi tunaweza kuelewa kuhusu utamaduni na mazingira ya waswahili.Msamiati umejaa Mambo ya kibaharia na uundaji was vyombo vya bahari Kama vile day,mtumbwi,ngalawa n.k.Mfano ni mwenda tezi na omo marejeo ni nyamani,Nazi mbovu harabu ya nzima.Ushahidi huu unatuonyesha kuwa kiswahili kilizuka katika mazingira ya Pwani na yenye wazungumzaji wake asili.

Titany answered the question on December 6, 2021 at 08:15


Next: Kwa kutoa mifano fafanua vipengele vitano vya kiisimu vinavyothibitisha kwamba kiswahili ni lugha ya kibantu
Previous: Huku ukidondoa ushahidi wa kiisimu jadili madai kwamba kiswahili ni lugha asili ya kiafrika

View More Historical Development of Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions