Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Kama kiswahili si lahaja ya kiarabu,Basi ni lugha mseto.Taathmini madai haya

      

Kama kiswahili si lahaja ya kiarabu,Basi ni lugha mseto.Taathmini madai haya

  

Answers


Faith
Kiswahili si lahaja ya kiarabu bali ni lugha mseto.Kutokana na kuingiliana kwa lugha za kigeni ,maneno yalichukuliwa na vizalia vya mazingira hayo.Wageni walioana na wenyeji wanawake wabantu na hivyo lugha zao zilitumiwa kuunda kiswahili.Wafuasi wa nadharia hii Kama vile steere, Taylor, Bloomfield na Johnson.Wanadai kuwa kiswahili ni mchanganyiko wa lugha za kiafrika na lugha za kigeni Kama vile kiarabu ,kituruki n.k wao wanatoa ushahidi ufuatao:
• Johnson anadai kwamba maneno ya kiarabu na kiajemi ambayo watoto hao walijifunza kutoka kwa baba zao yalihusu Vita,ubaharia,usafiri na vyombo vya ufundi.Lakini maneno ya kibantu waliyojifunza kutoka kwa mama zao yalihusu kilimo,ufugaji,vyakula na maisha ya Kila siku.
• Bloomfield Naye anadai kwamba kilikuwa na haja ya waarabu kuwasiliana na watumwa wa kibantu.Kwa hivyo ilibidi wachanganye maneno ya lugha ya kibantu na Yale ya kiarabu ili waweze kuelewana wakati walipokuwa wakifanya kazi za utumwa.Kutokana na mseto huowa maneno hivyo basi lugha ya kiswahili ikachimbuka .Hii inatuonyesha kuwa kiswahili si kiarabu Kama vile Chimerah (1998:3) Anasema sarufi ya kiswahili haifanani na sarufi ya kiarabu Wala za lugha zingine za kigeni bali inafanana kwa ukaribu na kibantu.Pili ni kuwa watafiti wameeleza kuwa takriban asilimia 60% ya maneno yote ya kiswahili ni ya asili ya kibantu,30% ni kiarabu na 10% ni lugha nyingine.

Titany answered the question on December 6, 2021 at 08:17


Next: Huku ukidondoa ushahidi wa kiisimu jadili madai kwamba kiswahili ni lugha asili ya kiafrika
Previous: Eleza kwa nn wafanya biashara waarabu walfanikiwa sana kueneza Kiswahili nchini Tanganyika kuliko Kenya

View More Historical Development of Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions