Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.
Kusudi la waingereza nchini nchini Kenya ilikuwa kudidimiza Kiswahili tangu mwanza wa utawala wao (Ndongo na Mwai1991:145)walitatiza maenezi ya Kiswahili kwa njia zifuatazo.
Kwanza walitumia Kiswahili kuendesha shughuli zao za kawaida k.m kuwekeana mikataba uliowekwa miongoni mwa kampuni ya Imperial British East Africa (I.B.E.A) na kutunga kiongozi wa ukambani mnamo mwaka wa 1887 uliandikwa katika Kiswahili na bwana Bashir Mchangamwe.
Pili waingereza waliwatawala wenyeji kimabavu huku wakitumia waswahili hivyo Kiswahili kilihusishwa na utawala wa dhuluma kwa sababu hii, watu wengi wa bara walianza kupinga Kiswahili na kukizuia kuenea. Wenyeji wa bara waliwaona waswahili kama watu wadanganyifu waliotumiwa na waingereza kama vigaragosi au vibaraka ili kuimarisha utawala wa kikoloni kufika leo kuna baadhi ya watu wanaoamini kwamba mswahili ni mtu asiyeaminika pamoja na lugha yake eti asili yake haijulikani , lugha yake hutumika kuwadangaya watu na hivyo basi mtu yeyote anayezungumza lugha hii haaminiki. Hii ndio sababu anapozungumza na mtu haamini ukweli wa yale anayosema, huenda akakuambia kuwa “wewe ni mswahili” au “usiniletee uswahili chako” kwa hivyo waingereza walitatiza kuenea na kukua kwa Kiswahili
Tatu, katika elimu waingereza walisisitiza matumizi ya kingereza na lugha za kwanza huku wakipuuza Kiswahili sera hii iliimarisha Zaidi. Hasa baada ya vita vikuu vya pili ambapo serikali ya kikoloni cha kuwaunganisha dhidi ya wakoloni kwa hivyo walianza kuhimiza matumizi ya lugha ya kwanza shuleni ili kuwagawanya wakenya katika misingi ya kikabila ndipo waweze kuwatawala bila shida kulingana na Chache Nyoigol Cheche (2001) waingereza walikuwa maadui wakubwa wa kiswahili kwa sababu sera zao hazikuwa na mwelekeo mzuri hasa nchini Kenya walifurahia kuwaona watalii
Titany answered the question on December 6, 2021 at 08:24
- Eleza kwa nn wafanya biashara waarabu walfanikiwa sana kueneza Kiswahili nchini Tanganyika kuliko Kenya(Solved)
Eleza kwa nn wafanya biashara waarabu walfanikiwa sana kueneza Kiswahili nchini Tanganyika kuliko Kenya
Date posted: December 6, 2021. Answers (1)
- Kama kiswahili si lahaja ya kiarabu,Basi ni lugha mseto.Taathmini madai haya(Solved)
Kama kiswahili si lahaja ya kiarabu,Basi ni lugha mseto.Taathmini madai haya
Date posted: December 6, 2021. Answers (1)
- Huku ukidondoa ushahidi wa kiisimu jadili madai kwamba kiswahili ni lugha asili ya kiafrika(Solved)
Huku ukidondoa ushahidi wa kiisimu jadili madai kwamba kiswahili ni lugha asili ya kiafrika
Date posted: December 6, 2021. Answers (1)
- Ushahidi was kihistoria ni muhimu katika kujadili swala la chimbuko la kiswahili.Jadili kauli hii kwa kurejelea Ushahidi huo(Solved)
Ushahidi was kihistoria ni muhimu katika kujadili swala la chimbuko la kiswahili.Jadili kauli hii kwa kurejelea Ushahidi huo
Date posted: December 6, 2021. Answers (1)
- Kwa kutoa mifano fafanua vipengele vitano vya kiisimu vinavyothibitisha kwamba kiswahili ni lugha ya kibantu(Solved)
Kwa kutoa mifano fafanua vipengele vitano vya kiisimu vinavyothibitisha kwamba kiswahili ni lugha ya kibantu
Date posted: December 6, 2021. Answers (1)
- Eleza upungufu wa nadharia inayodai kwamba Kiswahili ni lugha ya mseto(Solved)
Eleza upungufu wa nadharia inayodai kwamba Kiswahili ni lugha ya mseto
Date posted: December 6, 2021. Answers (1)
- Orodhesha maneno mengine ya Kiswahili yakiyokopwa kutoka lugha mbalimbali za kigeni na uzitaje lugha hizo(Solved)
Orodhesha maneno mengine ya Kiswahili yakiyokopwa kutoka lugha mbalimbali za kigeni na uzitaje lugha hizo
Date posted: December 6, 2021. Answers (1)
- Je kwa maoni yako, unafikiri asili ya neno 'Kiswahili' ni nini?(Solved)
Je kwa maoni yako, unafikiri asili ya neno 'Kiswahili' ni nini?
Date posted: December 6, 2021. Answers (1)