Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Wajerumani na Wamishonari walikuwa marafiki wakubwa wa Kiswahili? Jadili kauli hii uku ukieleza jinsi walivyochangia maenezi ya lugha hii katika afrika mashariki

      

Wajerumani na Wamishonari walikuwa marafiki wakubwa wa Kiswahili? Jadili kauli hii uku ukieleza jinsi walivyochangia maenezi ya lugha hii katika afrika mashariki

  

Answers


Faith
Wajerumani na wamishonari walichangia maenezi ya Kiswahili nchini Kenya, Tanzania na Uganda kwa njia zifuatazo.
Katika Tanganyika wajerumani walipokuja, walikuta kwamba lugha ya Kiswahili ilikuwa imeenea sana nchini humo kutokana na misafara ya waarabu. Badala ya kuchagua Kiswahili kama lugha ya utawala, waliamua kutumia kijerumani katika shule walizoanzisha lakini juhudi hizo hazikufua dhafu kwa sababu Kiswahili kilikuwa kimeenea zaidi nchini Tanganyika. Punde si punde iliwabidi wabadili nia yao na kutumia Kiswahili katika utawala wa elimu. Tunaelezwa kwamba walifanya hivyo kwa maslahi yao wenyewe wala si kwa maslahi ya wananchi wa Tanganyika. Hata hivyo, wajerumani walisaidia katika kukuza na kueneza Kiswahili kwa njia zifuatazo:

Waliwalazimisha wafanyikazi wote wa serikali kujifunza kiswahli, yeyote ambaye hangemudu Kiswahili hakuruhusiwa kuhajiriwa katika serikali ya wajerumani. Hali hii iliwatia moyo waafrika wengi ambao walianza kujifunza Kiswahili ili wapate ajira.
Wajerumani walilazimika kujifunza Kiswahili ili watumie katika utawala wao. Walipotoka ujerumani walishauriwa kijifunza Kiswahili huko kabla ya kuja Tanganyika na hali hii ilisaidia Kiswahili kuenea sana. Hata hivyo, baadhi ya waafrika walikipinga Kiswahili kwa sababu walikihusisha na utawala wa kidhuluma wa wajerumani.
Watawala wajerumani waliwateua wawakilishi wao yaani Okida, (mjumbe au liwali) katika sehemu mbalimbali za nchi na wawakilishi hao pia kujifunza Kiswahili . Aidha, ripoti zote walizotoa kwa uongozi wao ziliandikwa kwa lugha ya Kiswahili.
Wafanyi kazi wengine kama vile makuhani walikuwa wakihamishwa kila muda kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa minajili ya kukuza Kiswahili. Wafanyikazi walipokelewa kwa lugha ya wenyeji. Wajerumani walianzisha shule kwa madhumuni ya kuwafunza waafrika ambao wangetumika kufanya kazi ndogo ndogo za ofisini na ulinzi.
Wajerumani walianzisha mashamba makubwa na kupanda majani chai. Katika shamba hizo wafanyikazi walikuwa wa pwani na bara . Walikitumia Kiswahili kikazidi kuenea na kukua.
Nao wanasheria pia walisaidia kwa kuenea kwa Kiswahili katika Afrika Mashariki nchini Tanganyika na Uganda
-Walifanyia lugha ya Kiswahili utafiti na wakaandika vitabu kwa mfano. Askofu Edward Steve wa dhehebu la universities Mission to central Africa. (L.M.C.A) aliandika kitabu kiitwacho ; A Handbook of the Swahili language as spoken in Zanzibar mnamo mwaka wa 1870 katika lahaja ya Kiunguja.

Nchini Kenya
Baada ya mabishano makali kati ya watawala, wamishenari na walowezi, maoni ya walowezi yalichukuliwa na hivyo basi Kiingereza kikapigwa marufuku katika shule zote za Waafrika kutumia kiswahili. Pia vyama vya waafrika vya kisiasa vilitumia Kiswahili Kama lugha ya kupigania uhuru. Kama vile mnamo mwaka 1992, Harry Thuku alitumia kiswahili Kama chombo cha kuwaunganisha wafanyi kazi Waafrika ili wapinge ubaguzi wa rangi na sheria za kikoloni zilizowalazimisha Waafrika kubeba vitambulisho (Ndungo & Mwai, 1991:63)

Nchini Uganda
Wamishenari walikitumia Kiswahili kueneza dini ya kikristo kwa mfano mnamo mwaka 1878 mzungu mmoja alisema:
"Kwa bahati nzuri Kiswahili kinafahamika sana nami nakijua vizuri na nina vipande vingi vya Agano la Kale na Jipya kwa lugha ya Kiswahili. Basi ningeweza kuwasomea Neno la Mungu mfalme na Baraza lake lote"

Titany answered the question on December 6, 2021 at 08:50


Next: Sera ya lugha ya uingereza ilitatiza kukua nakuenea kwa Kiswahili nchini Kenya “ jadili kauli hii kwa tafsili
Previous: Fafanua sababu zilizotatiza kukua na kuenea kwa lugha ya Kiswahili nchini Uganda kabla ya uhuru

View More Historical Development of Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions