Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Eleza matatizo mbalimbali yanayowakumba watafiti wanapojaribu kuhesabu na kuainisha lahaja za lugha

      

Eleza matatizo mbalimbali yanayowakumba watafiti wanapojaribu kuhesabu na kuainisha lahaja za lugha

  

Answers


Faith

1) Kwanza kutokuwa na asasi moja inayowaunganisha wataalamu wote wa lugha kusimamia usanifishaji kwa nchi zote za Afrika mashariki. Hali Hii ni tofauti na ilivyokuwa wakati wa kamati ya lugha ya Afrika Mashariki. Wajumbe walipatikana kwa utaratibu unaofanana. Mwaka wa 1939 lilitolewa pendekezo kwamba mjumbe mmoja kutoka nchi awe mtu ambaye lugha yake ya Kwanza ni kiswahili.Hii ilikuwa ya kurahisisha katika usanifishaji wa kiswahili lakini hapo awali ilishindikana wanakamati wote hawakuwa wazungumzaji wa kiswahili.
2) Kukinzana kimsimamo kwa wataalamu wa lugha kuhusu istilahi zinazofaa kutumika katika uandishi wa taansifu.Kumekuwa na visawe vingi katika matumizi ya istilahi ya kiswahili inayopaswa kutumika.kwa mfano
Mareo/rejea/marejeleo (references)
• Changamoto ya kutoshirikishwa kwa wazungumzaji wa lahaja za Kiswahili.Baada ya kuanzishwa kwa kamati ya lugha na kupewa pamoja na mambo mengine jukumu la kusimamia usanifishaji wa lugha ya Kiswahili, wajumbe wa kamati walijiwekea mikakati ya kutekeleza majukumu yao ikiwa ni pamoja na kupokea maoni kutoka kwa wadau wa lugha ya Kiswahili. Utafiti ulipewa msisitizo (Whitley 1969). Akiunga mkono katika kufanya utafiti TEMU(1980) anasema kwa kuchunguza kwa makini anapata lahaja zinazotumika, maneno mengi hayatumiki katika kiswahili. Baada ya kupata uhuru, Afrika Mashariki, kila nchi ilikuwa huru na sera zake kuhusu lugha ya kiswahili.
• Kuna tofauti ya matumizi ya lugha baina ya jamii moja na nyingine. Licha ya tofauti ya mitazamo ya wataalamu wa Kiswahili kuhusu usanifishaji wa Kiswahili kama tulivyoeleza ,kuna tofauti pia ya matumizi ya lugha baina ya nchi moja. Hivi sasa kumekuwa na juhudi kubwa ya kuchapisha vitabu vya lugha.
Nchini Tanzania pia Kuna tofauti ya matumizi ya lugha baadhi ya maneno kati ya Tanzania bara na Zanzibar. Ukichunguza matumizi ya maneno kama mfereji, tungule, hoho, nyanya, mshumaa utagundua kwamba maana za maneno hayo ni tofauti Kati ya Tanzania bara na Zanzibar. Mara nyingi wataalamu wa Tanzania bara hukuza kiswahili kwa kutumia lugha za kibantu . Kwani ndio lugha zao za kwanza. Kwa upande wa Zanzibar kwa kuwa watu wanaohusika na ukuzaji wa Kiswahili walio wengi, lugha zao za kwanza ndizo hizi tunazoziita lahaja za Kiswahili. Msamiati wao mwingi unatokana na lahaja nyingine.Hivyo basi kusanifisha Kiswahili huwa changamoto sababu lugha yao ni lahaja.

Titany answered the question on December 6, 2021 at 09:26


Next: Taja lahaja zinazopatikana katika lugha yako iwapo zipo kisha eleza jinsi zilizuka
Previous: Huku ukitoa mfano mwafaka bainisha tofauti za kifonolojia na kimofolojia katika lahaja za kimvita ,kivumba na kiswahili sanifu

View More Historical Development of Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions