Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Liandike ubeti ufuatao katika kiswahili sanifu Kisha itaje lahaja aliyotumia mtunzi.

      

Liandike ubeti ufuatao katika kiswahili sanifu Kisha itaje lahaja aliyotumia mtunzi.
"Malimwengu yote yawatiile
na dunia yao iwaokele
wachenenda zitea zao zilele
mato matumizi wayatumbiye"
Jawabu;
"Ulimwengu wote uwatii
na dunia yao iwaokoe
Wataenda Vita vyao vile macho yaliyofumbwa wayafumbue"
Hii ni lahaja ya kiamu.

(b) Kwa kutoa mifano kutoka ubeti huo na kwingineko ,zibainishe sifa Tisa zinazotofautisha lahaja hiyo na kiswahili sanifu.

  

Answers


Faith
Kiamu ilikuwa lahaja ya usomi na ushairi katika Karne zilizopita.Tofauti za kifonolojia Kati ya kiamu na kiswahili ni:
Kiambishi (-le) hutumiwa Kama kiishio cha kitenzi katika baadhi ya maneno ya mashairi yaliyoandikwa zamani kwa kiamu.
Kiamu - Kiswahili sanifu
Iwaokele - iwaokoe
Sauti (v) na (vy) hutamkwa Kama (z) kwa mfano
Zao - vyao
Vyombo - zombo
Sauti (ch) hutamkwa Kama (t) kwa mfano
Wachenenda - wataenda
Kicheko- kiteko
Macho - mato
Sauti (nj) hutamkwa Kama (nd) kwa mfano
Njia - ndia
Nje - nde

Titany answered the question on December 6, 2021 at 09:31


Next: Huku ukitoa mfano mwafaka bainisha tofauti za kifonolojia na kimofolojia katika lahaja za kimvita ,kivumba na kiswahili sanifu
Previous: Eleza ni kwa nini lahaja ya kiunguja ilichaguliwa kwa msingi wa kusanifisha lugha ya kiswahili na wala sio kimvita au kiamu

View More Historical Development of Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions